kiongozi wa msondo ngoma music band muhidin maalim gurumo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu harambee iliyoanzishwa ya kila mljai wa safari lager kuchangia ili bendi hiyo ipate vyombo vipya. meneja wa safari lager, fimbo butala, yuko pembeni. jumla ya tshs. milioni 50 zinatarajiwa kukusanywa ili kuipatia bendi hii kongwe vyombo vipya.
Home
Unlabelled
harambee ya kusaidia msondo kupata vyombo vipya yazinduliwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuna mtu atapigwa risasi....ngoja nikacheki wakwangu..Lol....mmenitisha..!!
ReplyDeleteKila wakipiga musiki na kukusanya viingilio huwa wanasahau kuweka mbegu. Omba omba - utamaduni sasa.
ReplyDeletemkulima kala mbegu........anaomba kwa jirani sasa.muziki mmpepiga miaka yote hiyo hamna hata akiba...ebooooo.
ReplyDeleteUkienda kwenye shoo zao wanavyokutolea macho ulipe kiingilio, Utafikiri mjusi kabanwa na mlango,Wakitaka vyombo vipya wapolee, Nyooooooooo bin kudadeki.
ReplyDeleteMdau-Orlando,FL.
Wadau kumbukeni hii bendi kwa miaka mingi ya nyuma ilikuwa ni mali ya chama cha wafanyakazi kwa hiyo fedha zilizopatikana zilikuwa za mwenye bendi na wanamuziki walikuwa waajiliwa wakilipwa mshahara tu, hivi karibuni ndio wameanza kujitegemea na bendi kuwa mali ya wanamuziki kwa hiyo tusiwalaumu kwamba miaka yote walifanya nini. Ninawapongeza TBL kwa kuamua kuwasaidia msondo maana muziki wao ni bomba ila kwa umri wao hawawezi kukimbizana na bendi za vijana, ninashauri pia ingeanzishwa namna nyingine kwa ajili ya wanaopenda kuchangia bila kupitia kinywaji cha safari
ReplyDeletenadhani hata mimi naunga mkono ushauri wa anony. hapo juu ili kuisaidia bendi yetu ni kweli wangeanzisha na njia nyingine ya mchango,kwa njia hii ya safari beer inatubana kidogo wengine.
ReplyDelete