*Je Unajua Kwamba Kundi la Taarabu la
Malindi lina Miaka 104 na Limetoa Nyimbo 3,000?
*Je unalifahamu kundi kongwe la muziki wa taarabu Malindi?
*Je ulikuwa unafahamu kwamba sasa limetimiza miaka 104?
* Unajua kuwa Malindi wana jumla ya albamu 200 na jumla nyimbo 3000?
*Je unajua kwamba lina wanamuziki wake barani ulaya na Asia,
Ufaransa pekee wako 50?
Ukitaka majibu ya yote hayo
bofya linki hiyo hapo chini
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=1714958&&Cat=8
Nikiwa mpenzi mkubwa wa malindi na mzazi wangu kuwa miongoni mwa wanamuzi wa malindi wakati wa uhai wake, napenda kupinga vikali baadhi ya taarifa hii.
ReplyDeleteMalindi haikuwa ikitowa albamu za nyimbo zake, mambao ya albamu yameanza miaka ya hivi karibuni. kwa hivyo kusema malindi katika miaka yake 104 imetowa albamu 200 na nyimbo 3000 ni upotoshaji.
Kama kulikuwepo na albamu ningelipenda muandishi na huyo mtu mzima anaejiita cholo watutajie majina ya albamu kumi tu ambazo zilitolewa kabla 1990.
Malindi miaka yote ilikuwa ikiburudisha katika maharusi, siku za eid na baadhi ya wakati katika sherehe za serikali, nyimbo zao zote zilikuwa zikirikodiwa na kupigwa na radio zanzibar, na tvz ilipoanza nao walikuwa wakirikodi na kuonyesha nyimbo zao. malindi mapato yao yalikuwa ni kutoka katika maharusi na sherehe za eid na vunja jungu. HAPAKUWEPO uuzaji wa albamu.
Nakubaliana na mchangiaji wa mwanzo, nimesoma taarifa katika hiyo link na nimesikitishwa sana kwa namna ya taarifa potofu kuhusu akhwan safa (malindi).
ReplyDeleteMalindi taarab haikuwa ikitowa albamu kwa nyimbo zake, infact mambo ya albamu yameanza baada ya kuingia musiki wa kisasa (rap na r&b) tanzania
Hadi naondoka visowani miaka ya 90 malindi haikuwa ikitowa ajira kwa wanamuziki wake, miaka yote taarab ya malindi ilikuwa ni past time activities, ni hobby wanamuziki wote walikuwa na ajira zao nje ya taarab.
Huyo jamaa anaejiita cholo anaonyesha haijui historia ya malindi, na ameonyesha hayo zaidi pale aliposhindwa kutaja majina ya waimbaji na pia nyimbo za miaka ya nyuma zaidi ya 1980.