JK akiweka saini kitabu cha Maombolezo leo Nyumbani kwa marehemu bibi Asha Adam Sapi Mkwawa wakati Rais Kikwete alipokwenda kutoa heshima zake za mwisho na kuwafariji ndugu wa Marehemu. Bibi Asha alikuwa mke wa Marehemu Adam Sapi Mkwawa aliyekuwa spika wa Zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwili wa Bibi Asha ulisafirishwa baadaye kwenda Iringa kwa Mazishi
JK akiwafariji ndugu na jamaa wa Marehemu bibi Asha Adam Sapi Mkwawa leo wakati Rais alipokwenda kuwapa pole kufuatia kifo cha mke huyo wa spika wa Zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Inalilahi wainailahi rajiun. Poleni wote ndio wote tunaelekea njia moja. tuliokuwa Duniani tukumbuke Kusoma kuswali na Kuwaombea Dua waliopita. Abdu Pole kaka.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa wote mlioko Dar, Iringa( Kalenga), US na kwengineko.
ReplyDeleteMola aiweke pema roho ya marehemu Bi. Asha Mkwawa.
poleni sana watu wa iringa kokote mlipo mzee sapi aliliwakilisha vizuri sana bunge kwa kusimamia vema nidhamu ya wabunge na kuweza kuendeleza libeneke la maswali na majibu pamoja na mijadala mbalimbali kwa nidhamu ya hali ya juu bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe!!!!
ReplyDeleteheeeee bibi yangu umefariki??
ReplyDeleteyani naona apa ktk blogu??
ndugu zangu poleni sana,na mfike salama iringa-kalenga kwa mazishi ya mpendwa wetu
inguluvi itange!!
ndugu yenu
Pokeeni salaam za rambirambi wafiwa wote,hususan watoto wa marehemu na ndugu kwa karibu kabisa,polei wana wa Kalenga wote,wanyalukolo wote wa mkoa wa Iringa na popote ulimwenguni,kwa watanzania wote waishio mkoa wa Iringa,kwa ndugu watanzania wenzangu wote.Tuko nanyi katika wakati huu mgumu na wa majonzi makubwa.Lakini alochokiamua Mwenyezi Mungu hakuna mwenye uwezo wa kukitengua.Sote tulimpenda sana mama Asha Mkwawa,lakini yeye Muumba kampenda zaidi!Ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu,amina!
ReplyDeletePoleni sana majirani zangu. tupo pamoja kuomboleza msiba huu mzito. Safari njema ya Kalenga ya kumsindikiza mpendwa wetu ktk nyumba ya millele.
ReplyDeleteInna lillah wainna ilaihi rajiun. Poleni sana ndugu zetu kwa msiba huu wa mama yetu mpendwa. Inshaallah Mwenyeezi Mungu Subhanahu Wataala atawapa subira katika wakati huu mgumu na Inshaallah atampa marehemu kauli thabit na kumweka pema, Aamin.
ReplyDeletePole sana Eddie Sapi.
Tangaulia segito Asha, kamweleze Mwagito Mkwavi Sitta (samwel) ameharibu misingi yote aliyoweka.
ReplyDeletePoleni sana wanafamilia. Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Amen.
ReplyDelete