

wadau wa nmb wakishangilia bwawa la maini kumdungua fulham jana

mapaparazi kibao walikuwapo
Chid Benz akiwa ameshikilia Tuzo yake aliyoshinda kama masanii bora wa kiume mara baada ya kukabidhi wa na mwanamuziki Chingy kutoka Marekani aliyekuwepo kutumbuiza pia

Hamie B. akipokea tuzo yake ya mtayarishaji bora wa nyimbo kutoka kwa Ilunga wa kampuni ya Push Mobile akiwa amesindikiza na msanii AY.

TID akihojiwa baada ya kumwaga lazi kwenye tuzo za kili awards


bosi wa masoko wa tbl david minja (kulia) akimkabidhi mwakilishi wa msanii Tunda Man tuzo ya wimbo bora wa reggae

ssebo wa eatv (kulia) na wasanii ay, kundi la blue 3, nameless pamoja na dj bush baby

mpiga tumba bingwa wa twanga pepeta MCD pamoja na mpiga ngoma martin kibosho wakipiga sebene


mmoja wa mamodo waliokuwa wakiipeleka tuzo jukwaani

washereheshaji jokate na dj ncha kali walifanya kazi nzuri sana

malenga mahiri mrisho mpoto 'mjomba' (kulia) akichill na babana zorro

mtunzi bora karama legesu (kulia) na mwenzie

mbunge wa kinondoni mh. iddi azzan (shoto) katika meza ya twanga pepeta ambapo kuna mwenyekiti wa african stars entertainment wamiliki wa twanga, papaa msiilwa baraka, asha baraka na sauda simba kilumanga

kiongozi wa vibration sound elyson angai (shoto) na khalid chokoraa wa twanga pepeta

banana zorro na bendi yake wakitumbuiza

mwenyekiti wa yanga akimpa tuzo dogo mfaume ya muziki bora wa asilia (kazi ya dukani). madega pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia mchezo safi walioonesha yanga dhidi ya al ahly pamoja na kufungwa 1-0 na pia alitangaza jihad dhidi ya watani wao simba sc ambao amesema watakona cha mtemakuni watapokutana kwenye mechi yao ya ligi kuu kwa vile walikuwa wakishangilia al ahly.

nameless toka kenya akipokea tuzo ya muziki bora wa afrika mashariki toka kwa hoyce temu

che mundugwao na mwenzia wakifurahia baada ya kutangazwa kwamba 'deladela' ni albamu bora ya muziki asilia.

mwasiti akijidai na tuzo yake ya wimbo bora wa zouk (nalivua pendo)

mzee yusuf (shoto) akipokea tuzo ya albamu bora ya taarab (VIP) alinyakua pia mwimbo bora wa taarabu kwa kibao hicho hicho cha VIP

keisha akiwa na tuzo ya kili awards ya mwimbaji bora wa kike 2008/2009
msanii keisha (pichani) usiku huu ameibuka kidedea baada ya kupata tuzo ya kuwa mwanamuziki bora wa kike kwa mwaka 2008/2009 wa kili music awards katika ukumbi wa diamond jubilee hall, dar. wengine waliojinyakulia tuzo ni kama ifuatavyo:
1. mwimbaji bora wa kike - keisha
2 mwimbaji bora wa kiume - Mb Dogg
3. albamu bora ya taarab - VIP (Jahazi Modern Taarab)
4. wimbo bora wa taarab - VIP (Jahazi Modern Taarab)
5. wimbo bora wa mwaka - Anita (Matonya ft, Lady Jd0
6.wimbo bora wa Kiswahili - Fm Academia (Heshima kwa Mwanamke)
7. albamu bora ya Kiswahili - Akudo Impact ( Pekecha pekecha)
8. wimbo bora wa R&B - Natamani (Q-Jay na Makamua ft. Josilin)
9. albamu bora ya asilia - Che Mundugwao (DelaDela)
10. wimbo bora wa Hip Hop - Chid Benz (Ngoma itambae)
11. Wimbo bora wa reggae - Tunda man ( Ripoti)
12. msanii bora wa rap - Mangwea
13. Wimbo bora wa Afrika mashariki - Nameless toka Kenya ( Salary)
14. Mtunzi bora wa muziki - Karama Legesu
16. Mtayarishaji bora wa muziki - Hammie B
17. Mwandikaji Bora wa muziki - Profesa J
18. Wimbo bora wa zouk - Mwasiti (Nalivua pendo)
19. Mtayarishaji bora wa video - Kallaghe production
20. wimbo bora wa kolabo - Matonya ft. Lady Jd (Anita)
21. wimbo bora wa asilia - Dogo Mfaume (Kazi ya dukani)
22. mtayarishaji bora wa nyimbo - Hammie B
hi mr misoup hii imekaa sawa sio mbaya kama ya mwaka jana, sisi ambao hatuna umeme tukienda intent cafe tunaona yale ambayo yametokea usiku mzima Ubalikiwe kaka.
ReplyDeleteoyaa vp ngosha asipate kitu wakati inajulikana wazi kabisa ni bingwa wa kuchana. Big up fid q, yote uzalendo ndugu yango, i know you are the best.
ReplyDeleteSpartans rattled our men, see full story New York Times
ReplyDeletekwa utaji huo wa tuzo,wimbo wa temba kwa jina ENZI ZETU, unakuwa na maana zaidi. kwani utoaji umekuwa siasa. hata hivyo hongereni wachukua tuzo. naona madega hakuwa na raha pia baada ya mpira wake wa magazeti kutozaa mtoto.
ReplyDeletehivi waandaaji wa tuzo Adam Juma wa visual Lab kawafanya nini? yeye ndio best video producer. kallaghe kaja juzi na video mbili tatu eti kachukua! achen chuki na siasa!!!
ReplyDeleteUshauri kwa Keisha
ReplyDeleteBibie Hongera sana mimi huwa nakufagilia mno na sauti yako.
Naomba chunga sana vipodozi vinaharibu ngozi yako. Tafuta ushauri kwa daktari bingwa wa ngozi. usifanye mchezo na vipodozi vina chemical mbaya sana kwa ngozi
Hivi vitu ndio nchi yetu na wananchi wanaviona ni maendeleo!!!!Na ndio maana hatuendelei tunapiga mark time tuuu wakati wenzetu wanapiga mguu.
ReplyDelete........ndo hiyo!
Aliyetoa ushauri kwa Keisha hajui kwamba Keisha ni albino?
ReplyDeleteHawa watu ngozi zao ni sensitive sana hata kama hawatumii vipodozi.
Keisha nilijua tu utashinda.
Sauti yakumtoa nyoka pangoni
Tuzo ya mwimbaji bora wa kiume imekwenda kwa MB DOGG na nyimbo iliyomuezesha ni "Natamani" , produced by Ambrose Dunga , Mangwea amevuma na nyimbo "nipe deal " na akashinda tuzo ya msanii bora wa rap , produced by Ambrose Dunga.Wimbo bora wa kushirikiana amepewa Matonya na Lady Jaydee na nyimbo 'Anita" , produced by Ambrose Dunga .Wimbo wa mwaka ilikua Anita , produced by ...yes Ambrose Dunga .Sasa ni maajabu kabisa kwamba mtayarishaji bora wa nyimbo imekwenda kwa Hamie B, kwa hit yake moja " Habari ndio hii". Nakaaya alikuwa top of the charts kwa miezi 6 na mr politician ( produced by Dunga) , Matatizo na Shame na hivi sasa ana haki ya kutamba kwa sababu ya kazi yake nzuri mwaka jana, kwamba ni muimbaji wa kwanza wakiTanzania kupewa mkataba/ufadhili wa Sony !!! and yet jina lake lilikua noticably absent kwenye Tuzo hizi za Kili ...Jamani kulikoni au ni seme kilikoni??????
ReplyDeleteUnacheza wewe, Mr Minja akiweka ngumu hata uwe nomminated mara billioni hupiti ..Michuzi bana na hii!
ReplyDeletethere is something wrong na hizi tuzo mheshimiwa mkuu wa wilaya....we huwezi ukampa tuzo ya reggae tunda ukawaacha akina jhiko man na wenzie wengi tu wanaopiga reggae kweli...
ReplyDeletekweli unamnyima tuzo ambrose dunga wakati pini zake kibao ndo zilikuwa nominated na nyingine kushinga!!? mi sielewi jamani...
siko biased but kwa mtindo huu hatufiki popote...ebu imagine jamani adam wa visual lab kafanya kazi ngapi zimesimama?
then kituko kikaja pale kwenye ile category aliyoshinda che mudugwao...sasa mtu yuko peke yake mnategemea asishinde? na kwa nini awe yake? saida karoli na wanne star wanaimba nini? bongo fleva au?
jamani nyie watu wa kili awards acheni mambo ya ajabu coz am sure dandu angekuwepo mwenyewe mambo haya yasingetokea...dilinga unatuyeyusha mzazi...
nina mengi ya kuongea hapa but mkuu wa wilaya na nanihii ambaye juzi muisrael kawaokoa naomba uipost kwanza hii mengine yanakuja
bado kuna matatizo sana kwenye hizi tunaziita tuzo.hami b hakustahili kumshinda dunga,fid q alitakiwa kupata ya msanii bora wa rap na sio mangwea,kama ambavyo chidi benzi hakustahili kuipata ya wimbo bora wa hipihop kwa ile ngoma itambae yake kwa kuishinda bado nipo nipo ya fa,ni vitu vya wazi kabisa.adam wa visualab pia ameporwa tuzo yake akapewa kalage,na bila kuunganisha na maamuzi ya kisiasa keisha amepewa tuzo ya lady jd
ReplyDeleteThere is something wrong with a 'national' awards program where a 'committee' regardless of clear nomination preferences can unilaterally 'decide' that an artist is out of the running, or that an underground or up-and-coming artist/producer/video producer should get an award because 'they hadn't yet got one, and 'that other' artist got it last year'.
ReplyDeleteEvent planners... are TBL the only game in town? BASATA... no comment.. The artists belong to the citizens of this country, they are the voice of the people and opinion leaders... why shut them down by holding awards that reward mediocrity and bias?
Why does business reward undertalented and underperforming industry pawns rather than INDEPENDANT CREDIBLE JURIES using a strict criteria for both qualification and selection. In fact the country needs 2 separate awards.. an awards campaign based on sales and popular votes, and another based on MUSICAL TALENT AND INTEGRITY OF PRODUCT.
Finally, business should be calamoring for the few opportunities to sponsor such events, rather than the sponsor running the show. I do not want to take away how much brands can push musicians into the spotlight, and support the industry, that has happened.. but using an entire budding industry of hardworking talented people as a promotional tool is shallow and short sighted.
SPEAK OUT PEOPLE!!!