Baadhi ya wazee wasiojiweza wa Kambi ya wazee ya Funga Funga, Manispaa ya Morogoro wakiwa na majozi baada ya juzi ( Aprili 5) kutokea kwa vifo vya wezao wawili , Alfonce Amon (90) na Mohamed Said ( 70) inaodaiwa waliuawa Mzee mwenzao Afred Kategule ( 75)
Picha na habari na mdau John Nditi
WAZEE wawili, Mohamed Said ( 70) na kikongwe Alfonce Amon, (90) wa kambi ya wazee wasiojiweza ya Funga Funga, Manispaa ya Morogoro, Mkoani hapa wameuawa kikatili kwa kuchomwa na kisu tumboni na mwezao, Afred Kategule ( 75).

Muuaji huyo anayeishi pia kambini hapo kwa zaidi ya miaka mitatu alidai kuwa amekifanya kitendo hicho kwa lengo kupiga kitendo cha baadhi ya wazee wenzao kudiriki kula njama ya kutaka kumwondoa kuendelea kuishi kambini hapo wakati wakitambua hana uwezo wa kuishi nje ya kambi hiyo.


Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo jana ( Aprili 6) mjini hapa kuwa tukio hilo lilitokea juzi ( Aprili 5) majira ya saa sita usiku.

Alisema kuwa mzee wa kawanza aliyeuawa usiku huo alikuwa ni Alfonce Amon ( 90) mmoja wa watu wawili waliokuwa wakiishi na muuaji chumba kimoja na kwamba mwingine alikuwa amesafiri kitambo.

Kwa mujibu wa Ofisa Ustawi wa Jamii hiyo, muuaji huyo pia usiku huo alifanikiwa kuchoma kisu tumboni mzee mwingine Mohamed Said na alifariki dunia wakati lipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro, katika kurupishani hizo za kutekeleza mauaji hayo, Kategule alifanikiwa kuwajeruhi wengine wawili ni Sebastiani Ligoha sehemu ya kifuani na tumbano, wakati Mwanahamisi Saidi, mlemabu wa viungo kuchimwa kisu tumboni ambapo wote wamelazwa katika Hosipitali ya Mkoa wa Morogoro.

Akizungunmza kwa niaba ya wazee wenzake Kambini hapo, Joseph Kaniki, alisema usiku huo wa majira ya saa sita, mwenzao Mwanahamaisi Said alipiga kelele kuwa ameshambuliwa na mtu kwa kuchomwa kisu na kamba ya kutahamaki mtu aliyemchoma kisu naye aliamua kupika kelele za kuitia mwizi.

Alisema wakati kelele za wizi zikiwa zinaendelea, mmoja wa wazee Sebastiani aliamua kutoka ndani ya chumba chake kwa ajili ya kwenda kutoa msaada na ndipo akipochumwa kisu naye tumboni na mtu aliyemfahaamu wadhania wameingiliwa na wizi,



Alisema baada ya kuomba msaada kwa wasimamizi wa kituo hicho na kutoa taarifa Polisi, walipofika eneo hilo waliwachukua majeruhu watatu ambao ni Mohamed, Ligoha na Mwanahamisi kwa ajili ya kupelekwaa Hosipitali ya Mkoa kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa Mzee huyo, baada ya kitambo Polisi walairejea tena kambini hapo kwa ajili ya kufanya upekuzi ndani ya jengo ambalo baadhi ya wazee hao wamejeruhiwa kwa kuchomwa visu na walipogonga moja ya chumba alikutwa Kategule akiwa amekachini chumbani humo.

Hata hivyo alisema Polisi mara baada ya kuiongia chumbani humo waliukuta mwili wa mzee Alfonce Amon mwenye umri wa miaka 90 ukiwa umechinwana kisu shingoni na kupasuliwa tumboni.

“ alipoulizwa kisa cha kufanya mauaji hayo…mtuhumuwa alidai kuwa baadhi ya wazee wa kambini hapo walikula njama ya kutaka kumfukuza na ndiyo ameamua kufanya mambo hayo kwa sababu akiondoa eneo hilo hana mahali pakuishi na yeye ni mzee” alisema Kiongizi huyo wa wazee kambini hapo

Naye mfanyakazi wa kituo hicho, Kwangu Bakari, alisema walifika kuamushwa usiku hiyo na mmopja wa majeuhi Mwanahamisi Said kuwa kunamtu amewajeruhi kwa akuwachuma kisu wazee akiwemo na yeye.

Kwa mujibu wa mfayakazi wa Kambi hiyo, kuwa abaada ya kupokea taarifa hizo waliwasilaina na Ofisa wa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Polisi ambao walifika eneo la tukio mara moja kwa ajili ya kuchukua hatua zinazostahiki.

Hata hivyo alisema wamesikitishwa na tukio hilo ambalo si la kawada kutokea katika kambi za wazee wasiojiweza kwa kushambuliana na hadi kusababisha vifo vya watu hao wawili.


Naye, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Marko Nkya , alisema majeruhi hao wawili Sebastoani na Mwanahamisi wanaendelea kupatiwa matibabu ya kina kutokana na majeraha waliyoyapaata.


Polisi imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mwaba inamshikiria mtuhumiwa aliyefanya mauaji hao kwa ajili ya upelelezi zaidi ili sheria iwezekuchukua mkondo wake.

Kambi ya Funga Funga yenye majengo matatu ilianzishwa mwaka 1970 na inauwezo wa kupokea watu wasiojiweza 56, na ina jumla ya watu wasiojiweza 45 kati ya hao watoto wawili wenye umri wa miaka 12 na 14 na idadi ya wazee wasiojiweza wanaume ni 30 na wanawake ni 13.
waombolezaji wakiwa wamekusanyika nje ya
bweni lililotokkea maafa hayo kambini hapo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hizi nursing homes naona zimechachamaa manake kule NC wamepiga risasi sasa na hii nursing home ya Moro wamecharanga wazee wa watu. Hii recession itauwa wengi, naona hii recession inaanza kwenda kwenye depression back to 1930s sio mchezo mwana!

    ReplyDelete
  2. Hawa wazee wasiruhusiwe kuwana silaha, their minds are like kids sometimes

    ReplyDelete
  3. Jamaniiiiii, lakini inawezekana AMECHANGANYIKIWA, maana uzee unakuja na mengi,wachunguze kwa kina na Afya yake hasa AKILI.Poleni Wafiwa.Waelimishwe na hao wazee wengine ili kuepuka vitendo vya namna hii na vinavyofanana na hivi. Amani kwa wote.Mungu tubariki.Naipenda nchi yangu nasikitika kuona na kusikia haya.

    ReplyDelete
  4. Hao wa mika ya 70 wanafanya nini kwenye hiyo kambi 70's still young wana nguvu sana. Wakalime wakukaa hapo waanzie 80's and up...

    na kuuwa ndio itamsaidia nini saa atakaa hapo kweli tena au ataishia jela sasa....poor him

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...