Bosi wa idhaa ya Kiswahili ya BBC Solomon Mugera Omollo (kulia) akikaribishwa Kiluvya Pub na Mzee wa Kiluvya wakati mwanahabari huyo alipokaribishwa usiku wa kuamkia leo kwenye tafrija maalumu aliyoandaliwa yeye na  mtangazaji Charles Hillary kwenye kiota hicho cha maraha kilicho Kiluvya kwa Kawawa kama kilomita 25 toka katikati ya jiji la Dar barabara ya Morogoro rodi. Walikuwa wakitokea Butiama ambako waliwakutanisha watoto wa Mwalimu Nyerere na Iddi Amin juzi
Mzee wa Kiluvya alitumia nafasi kumkabidhi nanihii fulanazzz ya gemu za ugenini ya Bwawa la Maini aliyomletea toka Ukerewe
Nanihii akifurahia zawadi yake huku Mzee wa Macharanga Charles Hillary na Mzee wa Kiluvya wakimshangilia
Wakazi wa Kiluvya kwa Kawawa wakiwakaribisha wageni kwa vifijo 
uongozi wa Kiluvya Pub katika picha ya pamoja na bosi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Solomon Mugera Omollo (wa pili shoto) na Charles Hillar (wa pili kulia) na nanihii (shoto)
mambo ndani ya Kiluvya Pub kabla ya shughuli kuanza
mapatroni wa Kiluvya Pub wakisubiri shughuli ianze
meneja wa Kiluvya Pub (shoto) akiwa na DJ Muddy wakiweka mambo sawa. Muziki wa hapo ni wa bakulutu kwa sana pamoja na vibao vya nyumbani vya kale na vya leo. yaani raha tupu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Marko MwipopoApril 11, 2009

    ISSA BIN MICHUZI,
    NAKUSHUKURU SANA KWA KAZI NZURI! KWANZA NAMSALIMIA SANA MZEE WA KILUVYA PUB HAPO PAMOJA NA TIMU YAKE YOTE (WAZEE WA MITAA HIYO) AKINA MWAKIPESILE, MZEE KIMORI, MWALIMU JUMA HAMAD NCHIMBI (MWENYE TAI KULIA KABISA). HESHIMA YAKO JUMA. NAONA KAMA KAWAIDA YAKO MAMBO YA TAI UNAENDELEZA.

    NIMEFURAHI SANA KUKUMBUSHWA VIWANJA VYA NYUMBANI HIVYO. AKINA HASSAN MGALA, MJEMA, FRANCO NA WENGINE MPOOOOO??? INAONEKANA MAMBO YAKO VILEVILE SAFI SIKU ZOTE. MZIKI, NYAMA CHOMA, SUPU, NDIZI NA VINGINE VINGI. MZEE WA KILUVYA HONGERA KUTUONYESHA MAMBO YA HAPO KILA UNAPOREJEA TOKA UKEREWE.

    WASALAAM,

    MARKO J. MWIPOPO ( Ticha )
    UNIVERSITY OF OREGON,
    EUGENE, OREGON STATE
    U.S.A

    ReplyDelete
  2. duh umenikumbusha mbali sana yaani mwaka mpya wa 2003 nilijirusha sana disko la home la Kiluvya Pub... naona sasa kumekucha zaidi... will pay you a visit.

    pamekucha

    ReplyDelete
  3. Mzee Hillay umeowa kama huna mke niko. nimekumaind ile mbaya, bado unadai kaka.kama una mke nawatakia Pasaka njema pamoja na familia yako. MADAME

    ReplyDelete
  4. Mkuu wa nanihii,hiyo jezi amekupa wakati muafaka kwani utaivaa next wiki ijayo tutakapowakandamiza The Blues bao 4 pale kwao darajani.Kama ningekuwa home ningekutafuta uniuzie huo UZI wa Ugenini wa VIJOGOO wa Jiji!
    TIKA(THE KOP)
    ST-JEAN
    CANADA

    ReplyDelete
  5. Tatizo la michuzi hata umpe nini bado atavaa ule mfulanazz wake ningekuwa na uwezo ningeichoma moto na kuitupilia mbali unanikera mnooooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...