juu ni uzi wa simba na chini ni wa yanga ambao utaonekana leo kwa mara ya kwanza kwenye gemu la watani hao wa jadi Washington DC
Kisebusebu na kiroho papo...walete.... walete....tumewaona....Hayo ndio mambo yatakayojili leo katika kusherehekea sikuu ya Muungano Washington Dc wakati mahasimu wawili Simba na Yanga watakapo pimana ubavu huku Simba wakijaribu kulipiza kisasi ilikipata june 15 mwaka jana 4-1 dhidi ya Yanga
Tofauti na mwaka jana, mwaka huu timu zote za Yanga na Simba zitaingia uwanjani zikiwa na uzi mpya zilitolewa na mfadhili ambae hakutaka kutajwa jina lake. Mgeni wa heshima katika mpambano huo ni msaidizi balozi Mh. Switebert Mkama.
Mbali na hiyo mechi inayosubiliwa na mashabiki wa kabumbu washington Dc na majirani zao,kutakuwepo na nyama choma ikiwa ni moja ya shamla shamla za muungano
Hadi tunaingia mitamboni kambi zote zilikuwa shwari na tayari kwa mpambano. Kocha mchezaji wa Simba Libe (Germany defence) amesema washabiki wategemee ushindi kwani walipiga kambi Brazil na Juzi walilijipima nguvu na Vasco Da Gama na kutoka nao 0-0.
"Sisi tutaingia Dc jumapili saa 9 mchana na kuelekea uwanjani moja kwa moja", alisema Libe ila alipoulizwa kikosi gani kitashuka dimbani alikataa kutaja na kusema Yanga wasubili kipigo kitakatifu. "Wapenzi wetu muwe watulivu tutawapa kandanda safi yenye ushindi..."
Kwa upande wa Yanga, kambi yao imekua kimya kutokana na kuwa na majeruhi wengi. Dedy Luba golikipa namba moja ameumia mkono baada ya kugongana na Kheri Kheri na mchezaji wa Seif Ndossa kiungo huenda asicheze mechi hiyo kutokana na kusumbuliwa na nyonga.
Mshambuliaji wao hatari Hussein hataweza kuichezea timu hiyo ya jangwani kutokana na kufungiwa kwa muda usiojulikana kwa madai ya utovu wa nidhamu.katika mechi ya mwaka jana Hussein aliifungia Yanga mabao 3 kati ya 4 yaliyofungwa kwenye mechi hiyo.
Kocha wa Yanga, Meya, alipoulizwa kikosi gani kitashuka dimbani jumapili hii alikataa kutaja kwa kisingizio ana majeruhi wengi. "Yaani mpaka sasa hivi sijui nani atacheza itategemea tutakavyo amka...."aliiamwabia ripota wa globu ya jamii.
katika dodosa dodosa ya ripota wetu inasemekana timu zote zinaogopana ndio maana inakua vigumu kutaja kikosi kitakacho shuka dimbani.
Watabiri wanaipa nafasi kubwa Simba kuibuka mshindi lakini kwa kuzingatia Yanga ni timu bora na inayotandaza kabumbu la kisasa, mechi itakua ngumu,mshindi ni dakika 90
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...