BWANA MICHUZI,

NDUGU YANGU NAOMBA USINIWEKE KAPUNI. NINA HOJA MOJA NZITO SANA NATAKA WADAU WACHANGIE KWA KINA HADI KIELEWEKE. MAANA HII SASA IMEZIDI.

HOJA YENYEWE NI KUHUSU SWALA LA OVERTIME MAKAZINI HAPA BONGO. YAANI KUFANYA KAZI HATA BAADA YA MUDA RASMI KUMALIZIKA. HAPA KWETU INAONEKANA KUNA UTAMADUNI WA KUBEZA UMUHIMU WA MTU KUFANYA KAZI KWA MUDA ULE AMBAO UMEAINISHWA KATIKA MKATABA AMA MAKUBALIANO NA KAZI. KWA MAANA INGINE NI KWAMBA WAAJIRI WENGI, KAMA SI WOTE, HAPA BONGO HAWALITHAMINI HILO ASILANI.

UTAKUTA MTU UNAKULA MZIGO HATA BAADA YA MUDA WA KAZI KUMALIZIKA, UKILETA UBISHI UNATISHIWA KWAMBA AJIRA YAKO INAWEZA KUOTA MBAWA. UKIDAI MALIPO YA ZIADA KWA KAZI HIYO YA MUDA WA ZIADA UNAWEZA KUTOLEWA KOROMELO.

SASA WADAU NAOMBA KUULIZA HII IMEKAAJE?  INA MAANA KITU OVERTIME HAKUNA BONGO? KWA NINI?

MDAU OMAR
CHANG'OMBE MADUKA MAWILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. POLE SANA KAKA KWA KUWA WEWE HILI UNALIJUWA SASA HIVI WAKATI SIKU NYINGI WATU TUNATESEKA SANA KUHUSIANA NA HILO SWALA,LABDA MAWAZO YANGU MIMI OVERTIME MI NAFIKIRI HAPA BONGO KWASABABU SIO KAMPUNI AU MBILI NASIKIA WAFANYAKAZI WAKE WANALALAMIKIA KUHUSIANA NA HILI SWALA.. NO OVERTIME NO KUZIDISHA MDA.MDAU ANG

    ReplyDelete
  2. Pole Mdau! Kama una muda maalumu wa kazi kwenye mkataba wako na mwajiri, halafu anakufanyisha kazi zaidi ya muda huo, unaweza kumchukulia hatua. Nionavyo mimi, tatizo sio mwajiri, kwani yeye lengo lake ni kuzalisha kwa sana, kwa gharama nafuu. Tatizo ni uoga wa waajiriwa kudai haki zao, hata pale wanapofahamu kwamba haki hizo zinabakwa na mwajiri kwa makusudi.

    ReplyDelete
  3. Tatizo hili ni kubwa sana Mdau, pole na kazi.

    Wafanyakazi wa nyumbani ndio wanabanwa sana na matajiri wao. Hawa wafanyakazi wengi wao wametoka shamba na hawajui haki zao. Inaniuma roho zaidi nikiona ni wazawa wenzangu wanaoabana hawa wafanyakazi wa nyumbani kwa kuwafanyisha kazi bila malipo bora.

    ReplyDelete
  4. pole sana mdau wa temeke,hilo ni tatizo kwa baadhi ya kampuni nyingi hasa za private,mimi naona hili swala liangaliwe kwa umakiniwafanyakazi waache uwoga na wafikishe malalamiko yao kwa vyombo husika hasa vile vinavyoshughulikia madai yao kwasabau ni haki ya mfanyakazi kudai overtime kama atafanya muda zaidi ya mkataba wake,mabosi waache kutunyonyaaaaaaa.TINA wa Tabata

    ReplyDelete
  5. Pole Mdau, lakini bongo tangu lini tukawa wastaarabu? Bongo hatuheshimiani kama binadamu, wala hatuthaminiana. Ukikaa huku nje unagundua wazungu wanajithamini na kujipenda sana, hivyo wanalipna vizuri na wanakuwa na moyo wa kazi. Sisi utafikiri tunafanyia kazi ngómbe, yaani hatulipani, matokeo yake watu hawafanyi kazi vizuri(productivity iko chini sana)na matokeo yake wote tuna loose!

    ReplyDelete
  6. Tatizo moja Bongo mnafikiri overtime ni kushinda kazini, Wengi mkifika kazini badala ya kufanya kazi mliyoajiriwa mnaanza kusoma emails zenu binafsi na kusoma blog za akina michuzi.
    Kumbukeni kwamba hamjaajiriwa kufanya kazi hiyo na mnapostuka muda mliofanya kazi mlioajiriwa inakuwa ni chini ya masaa halisi kwa hiyo mnabaki kujizungusha ofisini na kudai overtime bila kuzalisha chochote cha maana.
    Kumbukeni kuzalisha siyo uwingi wa masaa mnaokuwa kazini na wengi wenu mna katabia ka kuiba masaa ya kazi kwa kufanya kazi zenu binafs

    ReplyDelete
  7. pole mdau, hilo halikukumbi wewe tu, maana hata huku ulaya hasahasa kazi za 'white/blue' collar(yaani za maofisini na viwandani, waajiri wanasema ikibidi tufanye kazi za mpitilizo(extra mile) sababu kuna ushidani katika biashara/kutoa huduma/uzalishaji na wapinzani wao(waajiri wengine)

    Ila wabeba box tu ndo hufanya kazi kwa masaa ya makubaliano kwa vile malipo ni madogo.

    Hivyo jikwamue ufanye shughuli zako mwenyewe.

    ReplyDelete
  8. BIBI UMEMEApril 28, 2009

    The new labour laws 2004 sec 19 allows for maximum number of days or hours that an employee may be permitted or required to work, 6 days in a week, 45 hrs in any week and 9 hrs in any day employer shall not require or permit an employee to work overtime - EXCEPT FOR AGREEMENT and not more than 50hrs and employer shall pay an employee not less than 1.5 times the employee's basic wage for any OT worked

    ReplyDelete
  9. Ndugu mtoa mada,

    Pole sana kwa adha inayokukumba. Jibu langu linaweza lisikufurahishe sana lakini naamini ndio suluhu ya kudumu.

    Unapokuwa umeajiriwa unakuwa mtumwa wa mwajiri wako. Mwajiri wako ndio anacontrol muda wako. Na akijisikia kuchukua muda wako zaidi ya ule mliokubaliana ni jukumu lako sasa kusema no.

    Hata hivyo dynamics za soko haziko upande wako. Kutegemea na aina ya kazi unayofanya unaweza kuta kuna watu wengi zaidi ambao wako tayari kumpa mwajiri wako muda zaidi kuliko unavyotoa wewe.

    Ni kama kungekuwa na sukari nyiingi sokoni halafu duka fulani wanakupa kila moja kwa Tshs 1,200/- wakati ukienda kwingine unapata kilo moja na robo kwa bei hiyo hiyo.

    Kwa hiyo from the perspective of your employer you are just a resource for his consumption. Not you as a person, but your time. He is there to consume as much of your time as possible.

    Hivyo ni kazi kwako kujitetea, na katika hilo umoja unahitajika.

    Otherwise njia bora ni kujikita katika ujasiriamali ili badala ya kuuza muda uanze kuuza bidhaa.

    Uzuri wa kuuza bidhaa ni kwamba utaweza kuajiri watu, hivyo utakuwa katika nafasi ya kuanza kutumia muda wa watu wengine kama vile mwajiri wako anavyotumia muda wako.

    Siku njema.

    ReplyDelete
  10. Asante mdau kwakuleta mada hii.
    Naanza na hao mabosi, jamani wengi wao hawana muda maalum wakuingia ofisini.

    Wakifika tu ofisini la kwanza ni vibaraka wote nikukimbiakimbia tu. Halafu wao nikuanza kuongea na simu kukumbushana mambo walofanya siku ilopita au charting na kunywa chai.

    Usirogwe ukafanya appointment na hao watu jinsi walivyo waswahili! Utajuta kuwafahamu.

    Hii imepelekea hata kwa waajiliwa kutokuwa waaminifu.

    Hili suala ni kwa ofisi zote za private na selikari wote tabia zao moja ila ni baadhi ya ofisi, huu ni ukweli mtupu.

    Mfano secretary eti haruhusiwi kutoka kazini hadi bosi atoke ili afunge mlango, mabosi wengi wa bongo hawafungi milango eti hadhi itashuka.

    Huo ni unyanyasaji mkubwa, kama bosi ana kazi zake za ziada, nivema kumuacha secretary aendelee na ratiba zake, lakini mabosi wengi hawatoi nafasi.

    Haya basi mlipe overtime huyo unae mshindisha njaa, kwa mshahara wa kcc, hiyo ni ndoto. Sasa jamani tunakwenda wapi?

    Overtime mnalipana wenyewe tu, kapuku itachukua karne kupata utasikia sijui voucher imeenda kusainiwa, mara ooo kaenda kwenye kikao, upuuzi mtupu! Ndo maana mara nyingine wanaamua kuwatoka.

    Wenye madaraka waoneeni huruma waajiriwa au watu wa chini yenu, maana hao wote wana haki kama zenu.
    Jalini sana muda wa mtu a
    cheni uswahili wajameni.

    ReplyDelete
  11. NCHI YOYOTE DUNIANI INA MASAA YA KISHERIA YA KAZI KWA WATU WOTE, MFANO UK NI MASAA 40 KWA WEEK ZAIDI YA HAPO UNATAKIWA ULIPWE PESA YA OVERTIME, NA KUFANYA OVERTIME NI HIARI SI LAZIMA, UKILAZIMISHWA UNAWEZA KUKATAA NA UKIFUKUZWA KAZI UNAWEZA KUMSHITAKI MWAJIRI NA KUMSHINDA, TANZANIA SHIDA NI SERIKALI NA VYOMBO VYA SHERIA KUTO KAZIA SHERIA ZILIZOPO, PIA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NI DHAIFU VIKO TOO POLITICAL BADALA YA KUFANYA CORE BUSINESS YAO AMBAYO NI KUTETEA WAFANYAKAZI POPOTE PALE, CHA KUFANYA NI KUPELEKA ISSUE HII KWA BUNGE IFAFANULIWE VIZURI NA WAZI, LILIKUWA JAMBO LA KAWAIDA NZI ZA UJAMAA KUFANYA EXTENDED TIME HASA KWA PUBLIC JOBS KWANI KULIKUWA NA FAIDA ZAKE NYINGI ZIKIWEMO SHULE BURE, MATIBABU BURE, MAJI BURE NA VITU VINGI TU BURE, LAKINI SASA NI UBEPARI KILA MTU ANATAKIWA KUPATA HAKI YAKE. SO SIMAMENI PAMOJA KUTETEA HAKI ZENU. YES YOU CAN.

    ReplyDelete
  12. Nafikiri mada hii imeingia sehemu isiyo stahili maana hata baadhi ya wachangiaji wake wa awali wanaonesha hivyo. Na hii inaakisi tabia yetu watanzania ya kwamba tatizo alilonalo mwenzio basi shauri lake. Hii hali ipo kuanzia kwa viongozi hadi raia wa kawaida. Nadhani inatokana na ile hali ya kutopenda kuona mwenzio anaendelea i.e "Wivu". Kuna matatizo mengi sana kwenye sekta ya ajira hapa nchini, kuanzia kwa Wizara husika, vyama vya wafanyakazi mfano TUICO,hadi kwa waajiri. Ajira nyingi hasa za sekta binafsi zina matatizo mengi mno na wala hatujui lini serikali itayatatua. Serikali yenyewe inakasoro nyingi sana katika mfumo wa ajira hasa sekta binafsi kuanzia kweye suala la kodi ambalo hakika serikali inamnyanganya raia jasho lake bila huruma, kwani kodi ya PAYE ni kubwa mno hasa kwa wafanyakazi wa kati,huku makampuni makubwa yakilipa kodi yanavyojisikia.
    Suala la overtime ni mojawapo ya kasoro za mfumo wa ajira hapa nchini. Wafanyakazi wengine hasa wanaofanya kazi shifti ndio wanaoumia sana huku makampuni mengi yakishindwa au kutotaka kuwalipa shifti allowance kama sheria y kazi inavyosema.Wafanyaki hawa inashangaza kuona siku kama ya JUMAPILI YA PASAKA wakiambiwa waende kazini na hawalipwi overtime na serikali yenyewe ikiwa haiitambui siku hiyo kama ni PUBLIC HOLIDAYMdau sijui tufanyeje maana hatuna pa kusemea, maana hata ukinyanyaswa na mwajiri wako utasema kwa nani? ukienda vyama vya wafanyakazi mfano TUICO viongozi wake wapo currupted mno (kumbuka mgogoro wa NBC na TUICO dhidi ya menejimenti ya NBC).
    Inakatisha tamaa sana ndio maana tukipata nafasi ya kuwaibia waajiri wetu huwa hatulazi damu.

    ReplyDelete
  13. tatizo liko pale unapoona bongo hamna UNION. Sasa kam ahovyo vyama havipo basi unganikeni mteteee haki zenu

    Lakini cha muhimu ni kuchapa kazi mkifika makazini sio kuzogoa bila kufanya kazi mkijashtukia muda umeisha na kazi hujafanya hivyo inabidi ukae zaidi kuonyesha hata kitu ulichofanya siku hiyo halafu unakuja kudai overtime.

    Bongo watu wako kazini wanaandaa michango ya harusi zao na kuorganize harusi yote bila hata kuchukua a week off or something like that kweli kazi itafanyika saa ngapi? mchana unakuta mfanyakazi amesign in lakini yupo mtaani tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...