Mahojiano na Watanzania wanaofundisha Kiswahili London. 
Kati ni Amina Waziri Richards (mjukuu wa gwiji Shaaban Robert) shoto ni Dora Gwao na kulia ni Freddy Macha wa AiL-TV
Mwanzilishi wa AiL-TV JJ Otieno akiwa kazini 

...Kwa miaka lukuki Waafrika tumeonyeshwa shaghala baghala ndani ya runinga na vyombo vya habari duniani. Mtazamo ulioenea ni kuwa tunasota njaa, unyang’anyiro (na vita vya wenyewe) ; taswira zenye watoto wenye makamasi na mainzi usoni, wanawake wenye matiti yaliyoanguka wanaobeba mizigo; kina baba miguu mitupu, majeshi katili na viongozi wenye vitambi wasiojali maslahi ya wananchi...

Naam... ndiyo sababu ya kuanzishwa Africans in London TV  (AiLTV), Uingereza , kujaribu kuachana na maono haya muflis...Bahati mbaya kama hutumii mtandao au iwapo kompyuta yako haina Media Player si rahisi kuiona runinga hii. Kwa sasa bado ni televisheni ya mtandaoni. Lakini haitakuwa hivyo muda mrefu...kila kunapokucha teknolojia inazidi kuwa karibu ya wananchi wa kawaida.

AiL-TV  imeanzishwa na Mkenya, Joseph Adamson, akishirikiana na baadhi ya wanamuziki Waafrika tunaoishi mjini hapa nikiwemo mwandishi wa kipande hiki.

Bwana JJ ( kama anavyojulikana) mwanamuziki, fundi mitambo na  mwendeshaji mkuu anafafanua katika kurasa nne nzima za mahojiano na jarida maarufu la televisheni TV-BAY karibuni  kuwa lengo letu kuu ni kuitumia teknolojia vyema. Kaeleza pia kwenye barua kwa vyombo vya habari iliyotolewa na makao makuu ya runinga za mtandaoni mjini Brighton Uingereza, IPTV Chanell :

“...Vipindi vyote vya AiL-TV vitatengenezwa na watu wenye asili ya Kiafrika, kuhusu watu wenye asili ya Kiafrika, au kuonyesha maslahi na utamaduni  wa watu wenye asili ya Kiafrika.”    

[youtube=http://www.youtube.com/watch?v=zQB2AoXGX0g]  

AiLTV ilivyoanza rasmi ilikuwa hivi mwaka 2007...  

Kutokana na juhudi zetu, moja ya kampuni bab kubwa zinazotangaza urembo nchini Uingereza Brand Design Agency (BDA) imeahidi kuisaidia AIL-TV (inayofanya kazi bila pesa na kwa kujitolea), kusimama dede... 

Hebu angalia baadhi ya vipindi hapa; uwe na subira kama picha zitakwama au pole pole kutegemea na kompyuta unayotumia:

http://ailtv.gdbtv.com/player.php?rand=853&h=a431593a04b99572ab390b80e596b75e&TID=05defa40f8aa04e24ce986554fca7684  

Je unataka kutengeneza vipindi vya runinga? Je unayo sinema? Jaribu kufanikisha ndoto zako kwa kuwasiliana nasi. Tutumie video fupi (demo) isiyozidi dakika tano kuonyesha mfano. Tuko pamoja. 

Tuwasiliane:

josephadamson62@yahoo.com

Simu: +44-7595 040-952

+44-7986375-992

Au

kitoto2004@yahoo.co.uk

+44-7961 833040         

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wow!!! nice. Macha, KWA WALE WA ZAMANI KIDOGO WATAMJUWA KATIKA MAGAZETI YA SERIKALI, I LOVED TO READ HIS STORIES, THEN I WAS A SECONDARY SCHOOL STUDENT, THEN ALIPOTEA NA KUANZA KU-HIT THE GROUNG RUNNING, BRAZIL, USA, CANADA NA KUANGUKIA UK SASA, HE IS A LEGEND NO UBISHI ABOUT THAT

    ReplyDelete
  2. mkuu habari za kazi? maoni yangu hayahusiani na picha ya hapo juu ila napenda kukuarifu kuwa london marathon imeisha muda si mrefu na mshindi wa kwanza ni s.wanjiru kutoka kenya ambae ametumia 2:05 wa pili t.kebede kutoka ethiopia na watatu ni j.gharib kutoka morocco.mdau uk

    ReplyDelete
  3. Braza mithupu japo hii haihusiani na picha ila naomba umfikishie ujumbe huyu mwalafyale adam huu ujumbe. Kuna watu tunazimii sana articles zake maana zimeenda shule sasa tukichangia kwa ustaarabu wote hatuoni kitu yaani kunakuwa hakuna mjadala. Nisichoelewa ni je mpaka tufanye registration kama vile tunataka kuaangalia mitandao ya ngono au ni aje? Haiwezekani blog kama ile ikakosa wachangiaji makini. Kama hajajiandaa kutembelea tovuti yake mara kwa mar afunge asubiri atakpokuwa tayari. (Waosha vinywa msije mkasema nifungue ya kwangu) ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  4. AILTV imenipa mwanga kuwa ukiwa 'mwafrika' jijini London waweza kuwa na 'PhD' lakini ni 'korokoroni', mwosha sufuria n.k kama clip ya youtube ya Mh mbunge wa borough ya London anavyohojiwa na Freddy Macha.

    Mie najiuliza Marcus Gavey (mtu mweusi pyuwaa)aliwezaje kuwa ana miliki taxi karibu ya mia moja mwanzoni mwa miaka ya 1900 hapo jijini London.

    lakini kipindi hiki na karne hii hasa hasa Uingereza wenye PhD, Masters na degree wanashindwa kujipenyeza na kufanya shughuli zinazolingana na viwango vyao vya elimu, hii inakuwaje hasa hasa wadau wa Uropa na Marekani mwaweza kutuambia, ni kwa nini????

    Mdau
    Kindamba Kiparamoto
    Kongowe DSM.

    ReplyDelete
  5. Mdau Kindamba sababu ni moja tuu UBAGUZI lakini wao (takataka na matapeli)wakija kwetu TUNAWAABUDU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...