madansa wa kundi la intergrated promotions wakiwajibika wakati wa uzinduzi wa malta guiness street dancing competition leo katika ukumbi wa hellenic club jijini dar.
warembo wa kampuni maarufu ya intergrated promotions wakisubiri kuwakaribisha wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi huo.

Malta Guiness, kilaji kisicho na kilevi, leo kimezindua shindano la uchezaji dansi wa mitaani, yaani malta guiness street dance africa, ambalo ni shindano la aina yake linalotarajia kuibua vipaji lukuki vya uchezaji dansi hapa nchini.

Hapo atatafutwa mshindi atakayewakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia, ikiwa ni baada ya kuchuana na mabingwa wengine wa mabara mengine. Kwa mara ya kwanza katika historia, mashindano haya ya kumpata bingwa wa dunia yatafanyika nairobi, kwa watani wa jadi mwezi agosti mwaka huu. Pia hili ni shindano la pili barabni africa na la kwanza afrika mashariki.

Kuanzia tarehe 14/04/2009 wale wote wenye nia ya kushiriki wanaweza kujiandikisha kwenye vituo kibao vitavyotangazwa. Washindi watapata zawadi kibao ikiwa ni pamoja na kujifunza kucheza dansa nma wataalamu wa kimataifa pamoja pesa taslimu ambapo washindi wa kanda watavuta laki 6.

Ratiba kamili ya mashindano ni kama ifuatavyo.

09/04/2009 usahili Mt Uluguru Hotel, Morogoro
23/04/2009 usaili Villa Park, Mwanza
06/06/2009 usaili Tanga hotel, Tanga
20/06/2009 usaili Ngome Kongwe, Zanzibar
04/07/2007 Usaili Matongee Club, Arusha
19/04/2009 Usaili Ccoco Beach, Dar
01/08/2009 Fainali Kitaifa Diamond Jubilee Hall, Dar




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wamenuuuuuuna

    -----JOOMEK------

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli watu wamenuna hivyo halafu unikaribishe mimi unadhani nitakubali?afadhali huyo wa 2 toka mbele ana katabasamu na anaweza kumkaribisha mgeni.waandaaji tuwe tunaangalia watu wa kuweka mapokezi/promotion kwani hao hutoa picha nzima ya tukio lenyewe.Ajabu ni kuwa hiyo picha sio ya kushtukisha bali ya kujiandaa.

    ReplyDelete
  3. Sura nzuri ila kwa nini wanune,hawakupewa posho au.ila tutakuja tu

    ReplyDelete
  4. halafu kama wanaona aibu vile.....tanzania tukipata kazi tunaona aibu kuifanya.....enjoy ur job....ilimradi inalipa usijali lolote...mimi nilishavaa pizza suit summer moja hivi mbele ya restaurant summer moja hivi......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...