Mazishi ya hayati Beatrice

Katika hali iliyoshangaza wengi inasemekana marehemu Vicky Goerge Makanya na Beatrece Costantine ambao walifariki papo hapo baada ya Bajaj walilokuwa wakisafiria kugongwa na gari la Mh. Andrew Chenge walikuwa hawatumii majina yao halisi.

Habari zinasema kwa upande wa Vicky yeye alikuwa akitambulika kama Halima kwao lakini kazini kwake alikuwa akitambulika kama Vicky. Hata katika Ibada ya mazishi alizikwa kwa heshima ya dini ya Kiislamu katika makaburi ya Lumala 'B' kwa jina la Halima.

Inasemekana  Vicky alikuwa muigizaji wa filamu na alitumia jina hilo katika maigizo  na kwamba jina hilo la Vicky lilipata nguvu pale alipozaa  mtoto aliyeitwa jina la Innocent(5). Inaemekana kwamba aliyezaa naye ni Mkristo.

Kwa upande wa Beatrece Costantine naye pia mambo yalikuwa hivyo kwani amezikwa kwa jina la Paskazia badala ya lile la Beatrice na kaka yake ameeleza kuwa jina hilo la iilikuwa ni jina la nyumbani na kwamba  jina lake la Ubatizo ni Paskazia hivyo amezikwa kwa jina lake la dini. Hayati Beatrice alikuwa ni mkristo wa madhehebu ya Roman Katoliki.

Picha na habari na 
Frederick M. Katulanda
Cell:+255 (0)784 642620
+255 (0)754 642620

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. sentensi za kiswhaili ngumu kweli kweli, sasa ikiwa mtu kishakuwa marehemu atafariki vipi tena?

    ReplyDelete
  2. hiyo mbona ni kawaida kuwa na majina tofauti mf.jina la shule/kazi na jina la nyumbani. na pia kuna watu wengine hawapendi majina waliyopewa na wazazi wao hivyo kuamua kubadilisha. kwahiyo sioni ajabu kwa hao marehemu kuwa na majina tofauti.

    ReplyDelete
  3. msaada tutani, mheshimiwa anashtakiwa kwa kusababisha ajali ya kina nani? Vicky& Beatrice au Halima na Paskazia? Mh RIP

    ReplyDelete
  4. mbona ni kawaida watu kujulikana/kutumia mtaani jina tofauti na lile lililozoeleka majumbani mwao. hii haimaanishi kwamba hilo jina la mtaani halijulikani nyumbani la hasha ni kwamba tu halijazoeleka nyumbani

    ReplyDelete
  5. Ahsante kwa info.Lakini sioni tatizo liko wapi hapo. Kuna watu wengi wanatambulika kwa majina yasiyo rasmi(kisheria/kuzaliwa).Baadhi ya waigizaji maarufu wanatambulika kwa majina waliyotumia katika filamu/ucheshi nk.

    ReplyDelete
  6. Sasa kama walibadilisha majika kikazi au kimapenzi inahusuje ajali yao? Watu wa watuwamefariki na kuacha mtot/watoto bado wadogo kwa ajili ya greed people ambao wanaachia hivi vibajaji tu kabla ya kufanya utafiti jinsi vitakavyosafiri mitaani....Jiji kubwa sana hili na bado vibajaji tu mitaani. Hivi hao wakubwa wameshavipanda hivyo wakajua usalama wake?

    Na hao wafiwa wataweza kusue jiji au waliosababisha ajali? owner wa kibajaji na mr Chenge once wakishajua nani mwenye kosa muhimu kulipa hapa.....watu wakishachukuliwa mali zao basi na wengine watakua more careful kuendesha au kuajiri madereva wazuri

    ReplyDelete
  7. HAYATI???
    UNAUHAKIKA MWANDISHI???????

    POLENI WAFIWA DUNIANI TU WAGENI MAKAO YETU YA UKWELI NI MBINGUNI

    ReplyDelete
  8. Huo ni mchezo wa watu wengi kutumia majina ya watu especially watu wanaojaribu kuja marekani na walipata division 4.wanaiba jina la mtu aliyefaulu vizuri .nitatizo kubwa

    ReplyDelete
  9. Kweli maisha ya binadamu ni sawa na hua,Marehemu Beatrece Costantine enzi za huai wake alikuwa ni mpangaji wetu miaka miwili iliyopita. Nilipo julishwa juu ya kifo chake nilishtushwa sana. Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi AMIN.

    ReplyDelete
  10. Anon 12:10Am nani kakudanganya Marekani wanajali Division uliyoipata bongo?
    Watu wengine bwana.
    Kwanza ukija marekani sijui una ki-division 1,2 or 3 cha form 4 or form 6 ukija marekani unaonekana kama umemaliza form four ambayo ni sawa na yule aliyepata division four uliyemwacha bongo.
    Kwa vile ww umekuja kusoma unafikiri Marekani kusoma unadhani wote wanakuja kusoma.Kuna wengine tumepata Green Cards kabla hatujatoka bongo.

    ReplyDelete
  11. Hapo lipo jambo!Baba Mkwe kafumwa Suruali imemdondoka magotini,Lahaula System yote nje nje!La kufanya hana!Wema mtendee Mbuzi Binadamu atakudhuru!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...