
Mdau Edgar Kaliboti (juu kulia) si jina geni hasa kwa waliowahi kupiga tizi katika dojo la Zanaki la Goju Ryu Karate miaka ya 80 na 90 chini ya Sensei nantambu Camara Bomani na Senpai Magoma Nyamuko.
Hivi sasa Kaliboti yuko Sydney, Australia, anakofanya kazi ya kufundisha sanaa mbali mbali za mapambano zikiwemo karate, boxing, kick boxing, stick fighting n.k.
Pia amekuwa anashiriki kwa mafanikio makubwa katika mapambano mbali mbali ya mara kwa mara. akiwa anajihusisha mara kwa mara kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa. Hivi sasa ana mkanda wa blue katika Grace jiu jitsu.
Katika hizi picha alikuwa katika mechi ya fainali ya Brazillian Jiu Jitsu katika New State Championship uzito wa juu (97kg +) hivi karibuni ambapo alikuwa wa pili. Kiu yake ni kurejea bongo na kufundisha wadau mbinu mpya ya sanaa za mapigano.
Akiongea na globu ya jamii kwa njia ya simu anasema sanaa hii sasa imepanuka sana na kwamba wengi sasa wanafanya mazoezi ya sanaa mchanganyiko inayochanganya aina kadhaa ya sanaa kwa mpigo kama vile karate, Jiu Jitsu, kickboxing, judo na stick fighting.

Fainaly hiyo kweli, mbona kama mazoezi tu na hakuna hata watazamaji mimi naona watu wachache wamesimama na wengine wakiendelea na mazoezi yao.
ReplyDeleteHongera Kaliboti,mafunzo hayana mwisho!!
ReplyDeleteKumbuka enzi zetutulipotoka na juhudi ya mazoezi?, ni contact kupitia Michuzi.
Sensei Rumadha.
" KARATE NI SENTINASHI" By Sensei Master Kanryo Higaonna.(Mafunzo ya sanaa ya mikono mitupu hayana mwisho)
hongera kaliboti.
ReplyDeleteGround fighting is way to go!It is most effective and efficient way to finish your opponent.
ReplyDeleteStudent from Machado School.