Mkaguzi na M dhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Mh. Ludovick Utouh akiwa katika mkutano na waandishi baada ya kuwasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka ulioishia June 30,2008 bungeni Dodoma leo asubuhi
Mdhibiti Utouh akibadilishana mawazo na wabubge, Ole Sendeka na Chrisant Mzindakaya nje ya bunge Dodoma
Baadhi ya maofisa wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, wakiwa nje ya uykumbi wa Bunge Dodoma, mara baada ya kuwasilishwa ripoti ya ukaguzi wa serikali leo asubuh iliyowasilishwa na CAG, Ludovick Utouh.
Picha na Paschal Mayala wa PPR
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema ukaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka 2007/08 unaonyesha kuwa hali imetetereka kulinganisha na mwaka uliopita.
Bw. Utouh aliyasema hayo kwa waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Habari wa Bunge jana mjini hapa, saa chache baada ya Bunge kupokea taarifa za ripoti zake za ukaguzi zinazoishia Juni mwaka jana, ambazo zinahusu Hesabu za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Serikali za Mitaa.
Kwa upande wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa hali imetetereka ingawa kuna uborekaji mkubwa wa hesabu hizo kwa Mashirika ya Umma, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Bunge liunde Kamati ya Kudumu ya Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. “Kwa hesabu za Serikali Kuu, hesabu zake zimetetereka, kuna wizara tatu zimepewa hati mbaya, wakati balozi mbili pia zina hati mbaya.
soma zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. NAMJUWA UTOUH TOKA ANAKUJA MZUMBE KUSOMEA ADVANCED DIPLOMA IN PUBLIC CERTIFIED ACCOUNTANCY AKITOKEA UALIMU WA PRIMARY, WAKATI HUO MIMI NILIKUWA MDOGO SANA NINASOMA MZUMBE PRIMARY SCHOOL, ALIPOMALIZA ALIAJIRIWA NA CHUO AKALETA MDOGO WAKE TULIKUWA TUNASOMA NAE MZUMBE PRIMARY SCHOOL, BAADAYE ALIENDA KUSOMA ULAYA, NA AKAFANYA CPA ALIKUWA MWEMBAMBA MARA HII AMEZEEKA SANA, ANYWAY NI ZAMANI NI MIKAKA TAKRIBANI 33 HIVI, THAT WAS 1976. KULIKUWA NA MABITOZ MZUMBE CHUO WAKATI HUO KARIBU WALIMU WOTE WALIKUWA WAZUNGU, PARTY KILA WEEKEND TULIKUWA TUNAZAMIA SANA TU.

    ReplyDelete
  2. MsemwakweliApril 28, 2009

    Hakuna report hapo, huo ni utapeli mtupu wa kimacho macho, kutoka kwa Mzee Utoh. mkaguzi mkuu gani huyu muongo tu -Umemfunga nani, umemsimamisha kazi nani, nani amewajibika kutokana na hii ripoti yako. Ndo kwanza mafisadi yanaongezeka. na huyo mbunge Kabwe zito pembeni yako mwenyewe hana hata CPA, wala CMA, wala CFA, wala MBA, wala Msc-accountacy , kihivyo wala hajui anasoma ninihapo. Maana kakaa kwa kulishangaa hilo kabrasha la pages 50,000 halielewi.
    Nyote waongo tupu.

    ReplyDelete
  3. Wanakagua nini wizi mtupu

    ReplyDelete
  4. NAMJUWA UTOUH TOKA ANAKUJA MZUMBE ......soooooo what!

    ReplyDelete
  5. Muzumbe again!!!!

    ReplyDelete
  6. huu uhandishi wa habari uliotukuka,eleza basi kiufupi yaliyojitokeza kwnye hiyo ripoti, au unaogopa? maana siku hizi story za EPA, mafisadi sizioni tena!

    ReplyDelete
  7. Wizi mtupuuuuu! Audit fee zimepanda zaidi ya 1000% yaani Otouh ume-inflate Audit fee kwa kiasi kikubwa sana inakaribia mfumuko wa bei wa Zimbabwe.Please watch out this year upunguze gharama za ukaguzi,maana duuh haijawahi kutokea!!!

    ReplyDelete
  8. wizi kabisa
    uyo mwenyekiti wala haelewi kitu apo,ao maoditaz ndo khaaaa kazi kweli wanagharama km nini!!!
    afu wanavitisho kuliko polisi adi unaogopa

    michuzi
    weka habari za MAFISADI APA NA KESI ZA ZOMBE,MAPAPA nk

    bana sasa!!

    ReplyDelete
  9. msemwakweliApril 30, 2009

    This guy is so stupid.
    watu kama hawa ndio wanafanya nchi ife kwa kuendekeza uongo.
    Nchi za wengine zilizoendelea mtu kama huyu(Utoh) huwa hakai katikati wakati anawakilisha ukaguzi wake kwa kamati ya bunge. Huwa wanamuweka mtu kama huyu kiti moto, chini ya meza kuu.
    Watu wanaotakiwa kukaa meza kuu ni wenyeviti wa kamati hizo za hesabu na wabunge wenzao katika kamati hizo. Kumuweka mtu kama huyu katikati ni kuruhusu yeye kuwadanganya tu kama watoto.
    waliunda mtindo huo wanajua ni kwa nini. Angalia jinsi Kabwe anavyomsikiliza , ikionyesha hata hajui kinachosemwa hapo.
    Kibaya zaidi eti CAG(utoh) alipendekeza vijengwe vituo vya Polisi, forodha na maduka upande wa TZ katika mpaka wa Msumbiji na TZ kabla ya ufunguzi wa daraja la umoja, eti raisi wetu ataabika pindi rais wa msumbiji akija upande wa TZ. Huoni huyu jamaa ni mpumbavu kabisa. Huyu ni mdhibiti wa fedha , halafu anaomba fedha zitumike bila faida kwa ajili ya kumfurahisha Rais atakapoenda kufungua daraja.
    Mzee naona umechoka , uondoke hapo, ili vijana waje nakazi na ari mpya na sio mbinu za kugombea uongozi wa ubunge baadaye.

    ReplyDelete
  10. Audit fee ni kubwa sana bwana Outouh! Punguzeni ufisadi au kuna 10% yako mzee?

    ReplyDelete
  11. Kha huyu bwana si lolote hizo Audit firm nyingine hewa hazina wataalamu kabisa eti mtu ana ATEC anakuwa Auditor tangu lini? Kazi kuomba hela la lunch na usafiri tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...