Bro Michu,
naomba wadau wa ughaibuni wanisaidie kwa ushauri katika hili.
Mimi nipo hapa Uswidi katika mji wa Trelleborg nina miaka mitatu sasa. Hapa uswidi nilikuja kwa msaada mkubwa wa jamaa yangu fulani.
Naomba nieleweke msaada alionipa ni wa namna gani nitaweza kufika huku uswidi kutokea huko hom bongo land.Japo hakunisaidia pesa hata senti,lakini msaada wa kunipatia data za hapa ughaibuni kulinirahisishia sana ujio wangu huku.
Yeye alikuwepo huku miaka zaidi ya minne. nilifanikiwa kufika na kumkuta mwenzangu tayari alikwisha jilipua. alinishauri nami nijilipue mimi nilikataa suala la kujilipua, hivyo basi mwenzangu kwa nama moja au nyingine uhusiano ukapungua kwa kiasi kikubwa.nilihangaika sana hatimae nikahamia katika mji unaitwa Trelleborg. Jamaa yangu yeye akawa yupo... (jina kapuni).
Kutokana na kukumbuka fadhila zake kwa kunipa mwanga wa kuja huku ughaibuni kweli nilionyesha kwake upendo wa hali ya juu na kumjali sana, lakini jamaa yangu yaonekana hakupendezwa na maisha yangu kwani mara baada ya kuhamia hapa Trelleborg nilipata mwanamke wa kiswidi (naombeni radhi niseme alinioa)nasema hivyo kwa sababu hakuna ninacho msaidia huyu mama zaidi ya mimi kuwa kula kualala na isitoshe amenizidi umri.
Kwakweli maisha yangu yakabadilika ghafla yakawa mazuri, kama zilivyo ndoto za wengi nimeweza kusaidia familia yangu kwa kiasi kikubwa sana huko bongo. Sasa jamaa yangu amekuwa ni kikwazo kila siku mara anashida hii, kesho ana tatizo hili namsaidia.
Yaani imekuwa kero na kwa bahati mbaya msaada ninaouzungumzia hapa ni pesa. Na sijui pesa anayopata yeye anaipeleka wapi kwa sababu kila wakati anasema nimsaidie hana pesa. Hivyo ikitokea ukamwambia ndugu yangu leo sina hapo atakata simu kwa ghadhabu.
Msaada ninaoomba wadau mnisaidie kwa sababu tayari keshaanza kumjaza huyu mama maneno ya uchonganishi na ananitangaza kuwa mimi sijui fadhila na mambo chungu mzima.
Halafu hivi waliojilipua hapa uswidi kwani wanapata pesa kiasi gani? kiasi kwamba ndugu yangu yeye pesa anayopewa tena bure haimtoshi.Je ni kweli waliojilipua wanalipwa pesa kidogo au ana matumizi kupita kiasi.
Wadau hebu nisaidieni huyu ndugu yangu hapo... (jina kapuni) yawezakuwa analipwa kiasi gani kwa wiki pamoja na pesa vitu gani pengine hupatiwa bure katika mahitaji ya kibinadamu.
MDAU wa trelleborg
Kwanza mwandishi wa hii habari akili yako haikutoshi na kwa bahati mbaya ukizaa watoto sijui hata akili watatoa au kurithi wapi!!!...na tunakuomba uache huu ujinga wa kutujazia blog ya jamii upupu wako huu.
ReplyDeleteUshauri wangu...tafuta waganga wa magonjwa ya akili wakusaidie ili uweze kutumia hata kiasi kidogo cha akili ulichobaki nacho.
Pole sana mtu wangu na hongera sana kwa kuolewa. Kwanza nataka nijue maana ya kujilipua kwani hili neno lina maana mbalimbali ikitegemea na jinsi lilipotumiwa. Kama ni ugaidi inakuwa ni kujilipua, kama ni mtuhumiwa ni kwamba ameamua kukiri aliyofanya, kama ni mapenzi inakuwa umebambwa na mke au demu mwingine n.k
ReplyDeleteVile vile mtu wangu ni jambo la aibu sana kuishi nchi ya watu kwa kutegemea mwanamke.Yaani hata kama ulikuwa msela wangu ukaniambia wewe ni mtu wa mapenzi ili uweze kuishi kwenye nchi za watu mmmhhhh!! ni aibu sana mtu wangu na wala hufai katika jamii ya kuitwa mwanaume.
Isitoshe mtu wangu umekaa miaka yote hiyo hata hujaweza kupata mwanga wa kujitegemea unataka upewe muda gani ili uweze kujitegemea??? Au utaolewa milele. Uliposema mambo yako yalikuwa mazuri nilidhani ulipata kazi nzuri kumbe uliamua kuwa kuku la kienyeji na eti hapa unataka ushauri wa jinsi gani ya kumtoka msela badala ya kuomba ushauri ni jinsi gani ya kujitegemea na kuacha kuolewa!!!!
Msela bora urudi tu Bongo kwani una nguvu nyingi sana na tunazihitaji mwanaume.
Kwa hapo huna ujanja jinsi msela alivyokubana kwa sababu wewe kama ulikuwa unajitegemea yaani una uwezo wa kusimamia miguu yako mwenyewe ungeweza kufanya kitu lakini hili halipo. Hapo ni kama kurusha kete tu. Msela alikupokea then mama akakupokea. Raundi ya tatu sijui ni nani atakkupokea...
Hivyo msela jitahidi kwanza uweze kujitegemea namaanisha kuishi bila kumtegemea mwanamke na then tutakushauri ni jinsi gani ya kumtoka huyo jamaa.
Kujilipua maana yake ni nini? I think you need to cut ties with the guy, sidhani kama anakutakia mema.
ReplyDeleteNawewe usitujazie blog yetu kwa umbea wako eboo.
ReplyDeleteKaka kama kuna kitu waficha si bure huyo ndugu haachi kukutafuta.We kitu muhimu cha kwanza mweleze huyo mwaname wako kila kitu bila kumficha na kwanini inafikia hapo mlipo na huyo kaka.Hayo mambo mengine ya kufuatilia anakula nini analipwa nini.Mweleze huyo mama ukweli bila kumficha lazima utajisikia amani na huta ogopa wala kutishwa na huyo ex mwenyeji.Kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua so let it not be you.I can sense you have already suffered enough and it is about time you face your demons.All the best sweetheart.kujilipua ndio nini?
ReplyDeletePole sana nimeusoma ujumbe wako wooote na nimeuelewa kwa makini... kwanza kabisaa lazima uelewa, ndugu wengine hata ungewapa damu, figo na firigisi hawatoshekiiii kabisaaa... na pili ningekushauri ukate mawasiliano naye kwasababu inaonekana kama anataka kukuvurugia na huyo mwanamke wako, nia yake kwako inanitia wasiwasi mkubwa sana..."kuvuja kwapakacha heri ya mchukuzi kijana" sasa najua utanijibu kusema nindugu na amekusaidia hivi na vile naelewa hiloo tena sitaki tena ulirudie kwakuwa nimeshaelewa hilo..Lakini lazima ujue kuwa ndugu wengine ni mzigo tu na tena ni waziba rizki heri uwakwepe....Kuwa jasiri hapa amasivyo utakosa vyoote, yaani Mke na Ndugu...Pia MWOMBE SANA MUNGU AKUFUNGULIE NJIA NA AKUPE UJASIRI KIJANA, MUNGU WETU NI MWAMINIFU SANA...ASANTE KILA LA KHERI..
ReplyDeletekujilipua maana yake nini sisi huku marekani hatujui mambo ya kujilipua.
ReplyDeleteKujilipua? Oh, hiyo imeanza lini, Watanzania kujilipua?
ReplyDeleteHollo mdau wa trelleborg ni hivi kujilipua sio kwasababu ya kupata fedha watu wanajilipua ili wapate karatasi za kuishi ktk hiyo nchi swala la kuwa na pesa ni lazima ufanye kazi sasa huyo jamaa yako kama hafanyi kazi ni kweli atakuwa na shida kwani atakuwa anapata pesa ya kula tu kutokana na kutokuwa na kazi, mimi mwanangu yeye amejilipua holland na anafanya kazi hizi ninavyo andika hapo uwani kwangu kuna trskta 2 na nina gari ya kutembelea nyumba nzuri japo ipo kisiju. ebu mshauri huyo swahiba wako atafute kazi. mimi naamini kabisa huyo swahiba wako hana kazi.
ReplyDeletemdau
kisiju pwani
Hivi kujilipua ni nini wadau? Huwa sielewi nmaana ya neno hili.
ReplyDeleteWee kijana yaani umekuwa changudoa wa kiume halafu unataka tukushaurui?
ReplyDeleteTukushauri nini zaidi ya kuiacha hiyo dhambi na urudi nyumbani kulima?
kujilipua maana yake ni kuukana uraia wako wa awali na kuchukua uraia wa nchi nyingine (hiyo unayotaka kuishi). wabongo wengi wamejilipua huko ughaibuni.
ReplyDeleteJAMANI WATANZANIA WENZANGU KAJILIPUA MAANA YAKE NI KUISHI MAISHA YA KUKATA TAMAA KAMA VILE KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA,BANGI,WIZI ,UJAMBAZI NK
ReplyDeleteKujilipua maana yake ni kuomba hifadhi ya ukimbizi katika nchi fulani kwa sababu za kisiasa, usalama,uabuzi, dini, au jinsia. kingereza maana yake ni seeking asylum, mfano taksin shinawatra (aliyekuwa waziri mkuu wa thailand), ameomba hifadhi ya ukimbizi uingereza kwasababu za kisiasa...
ReplyDeleteWatu wengi sana huomba ukimbizi katika nchi wanazoamini ni salama na zinaendana na matakwa yao. USHAURI: Maswala haya si ya kuzungumza mtandaoni kwani networks are monitored, mtaharibia watu maisha yao, kwani kuna wakimbizi feki na wa kweli. Ieleweke kuwa Uchumi si sababu thabiti ya kuomba ukimbizi, sasa ili uqualify kuwa mkimbizi kwenye nchi unayoomba hifadhi, inabidi uwe na vithibitisho vya kutosha, Inategemea na Kamba utakazowapiga wazungu/wana uhamiaji wa nchi lengwa..
Nadhani nimeeleweka.
Pili Ndugu muomba ushauri, wanaume hukaa chini na kuzungumza matatizo ili yatatuliwe... kaa chini na huyo mshkaji wako, mzungumze yaliyojiri, na muweze kufikia itifaki. Elezeaneni maswala mbali mbali na nadhani ukimwambia nafasi yake moyoni kwako ni ipo ataelewa kama binadamu,sasa kama ataendelea kukughasi na kuleta fitina katika maisha yako huyo zi mtu wa kuwa na uhusiano naye, kwani ni mshari na mtafuta chokochoko.
Kama mshkaji wako hajapata makaratasi basi elewa kuwa kipato chake ni cha kubangaiza sana, mvumilie kwa hilo,kwasababu kisheria haruhusiwi kufanya kazi ya aina yoyote bila kibali. Lakini asisahau ubinadamu na kuleta fyoko fyoko zake kwa Mama watoto wako...
NB: Mwanaume hasifiwi kukaa ndani,Tafuta kazi acha kumtegemea mwanamke huyo... Halaf panua mawazo na fikra, ulaya mapambano...mpaka leo hujui mambo kibao na unaishi nchi iliyoendelea,info ulizouliza zimejaa online kwenye tovuti za serekali ya nchi uliyopo.
Kama hujasoma tafuta elimu ya watu wazima ujiendeleze...
Nadhani Nimeeleweka vilivyo.
Mdauz
"Kujilipua" ni kuukana uraia wa TZ na kukumbatia wa nchi nyingine.
ReplyDeleteKujilipua ni hivi= Unaingia katika nchi ya watu aidha kihalali au kwa njia za panya kisha unaukana utaifa wako,utajiita vyovyote ujuavyo ili mamlaka husika katika nchi hiyo zifikirie utaratibu wa kukupatia mahitaji muhimu,kwa maana makazi bora,chakula kizuri,maji safi na salama,huduma bora tena za uhakika za afya,mavazii elimu,pamoja na pesa ya kujikimu nk. Aina nyingine ya kujiwasha unafika nchi za watu unazamia street unaendelea kuishi bila vibali vyovyote vinavyokuruhusu kuishi katika nchi husika.Ninavyo fahamu mimi hiyo ndiyo maana ya neno kujilipua, kwa maana hiyo huyo mdau ana haki ya kusema hiyo kwa kuwa huyo jamaa yake anapatiwa kila kitu na serikali sasa iweje kila kitu amuombe jamaa yake.hata kama ndiye aliyempa data. Wadau wenyewe wa kujilipua wakirudi kutoka kwenye box utawasikia hapa muda si mrefu. MDAU WA SLOVAKIA
ReplyDeleteTAFADHALINI WADAU ANEELEWA MAANA YA KUJILIPUA TUNAOMBA AOKOE JAHAZI,,,,,PLEASE mdau wa kalemie-congo drc
ReplyDeleteAtakae tuelezea maana ya kijiwasha basi na atuambie na kupiga box. msinitukane tafadhali maana nawajua kwa ghadhabu... Mdau Gongolamboto.
ReplyDeletehuyo ndio mbongo halisi,atakuda hadi uzeeni.wabongo kazi kulea mikono tu.angalia atakulipua na wewe.
ReplyDelete...kujilipua ni kukana uraia wa asili (kwa kutumia vielelezo vya udanganyifu) ili upate uraia wa nchi uliyohamia. Mfano, kwa kuwa nchi nyingi za Scandnavia zinaruhusu watu watokao nchi zenye vita kuwa raia wake, hivyo mhamiaji toka Kenya anaweza kudanganya ametoka Somalia na hivyo kupata uraia.
ReplyDeleteKwa upande wa mwandishi wa habari hii, kwanza pole sana kwa yaliyokukuta maana hayo ndo majaribu ya maisha. Kwa kuwa huyu jamaa yako alikusaidia basi tegemea kuwa atakusumbua mpaka pale atakapomudu gharama za maisha yake (hata kama ni lifist). Usidhani kwamba kutangulia hapo Uswidi au kujilipua kumemsaidia sana, la hasha, bado atakuwa na matatizo pengine kuliko wewe ambaye umekuja yeye akiwa ameshajilipua. Naungana na Anony wa 7.56AM kukushauri ukae nae chini kujua kulikoni na ikiwezekana umshauri apige box kukidhi maisha yake. Kama umeshapata ujanja zaidi yake (maana kutangulia si kufika) msaidie hata kama ni kupitia mkeo ili apate kazi.
Lakini kama hizo approach zikishindikana then hachana naye maana maisha ni kupigana. Wee piga box zako na angaika na mambo yako maana wakati mwingine jamaa wa karibu anaweza kukusababishi umasikini hasa kama hashauriki.
Kujilipua ni kitendo cha kuoa mwenyeji wa nchi husika/ujanja wowote ili kupata uraia wa nchi hiyo.Neno hili linatumika sana kiwanja "marekani".Kwa kifupi wewe ndugu yetu uliolewa ni kaza kamba tafuta ways za kujitegemea.Its obvious jamaa has done some demage kwenye uhusiano wako na huyo "bibi"
ReplyDeletekiasi cha wewe kuwa ngumu kujilipua through her.Pole sana,i think jamaa yako ni mteja au shoga anaye-miss company yako.just stay away from that mess.Angalia life yako bro!
mdau kiwanja...
"kujilipua" mana yake ni kusema wewe ni mkimbizi kwahio nchi unayoishi huko ughaibuni wanakua wanakupa haki zote wanazopewa wakimbizi
ReplyDeleteMWANANGU KAZA BUTI KWA SANA KWANZA NAKUPA HONGERA KWA KUWEZA KUFIKA KATIKA HATUA NZURI,HUYO JAMAA YAKO ANA WIVU KWANIANAONA UTAENDA MBALI NA HUYO MAMA NA ISITOSHE POSSIBILITIES YA KUCHUKUA MKWAJU LABDA ZIPO JUU ILE ILE SO ANA TAKA KUKUBANIA,USIMPE NAFASI HATA KIDOGO NA KAMA VIPI KAMA NOMA NA IWE NOMA MAISHA YA BEACH NI MBWA KALA MBWA SO KAZA BUTI,NA NYIE WAJINGA WAJINGA WA BONGO MSITOE COMMENTS ZENU NA KUULIZA MASWALI YA KIPUUZI NINI MAANA YA KIJILIPUA SIJUI NINI,KAENI KWA BINTI ATHUMANI HAPO MLE UGALI NA MAHARAGE,MWENZENU ANATAFUTA MAISHA KIWANJA.
ReplyDeleteUMEOLEWA!!!
ReplyDeletetobaaaa
nimeishi nje miaka lkn nlikuwa sijui maana ya kujilipua,nlikuwa najua kujilipua ni kutumia sigara kubwa..
ReplyDeletehii mada ya kujilipua imenivutia sasa mimi nataka kujitoa muhanga kbs..,
na ni nchi gani ambazo ni nzuri kwa kujilipulia?
na je nikijilipua halaf nikafa nikafufuka bongo watanikubali tena? coz naskia kuna jamaa walichoma passport za tz i think it waz in UK dili likabuma JK akawatema BONGO.
NA KAMA BONGO WATANIKANA NITAENDA KUISHI WAPI?
wabeba maboxi mna mambo kweli. sasa inaonesha unaogopa huyo jamaa atamwambia mumeo na atakutimua.
ReplyDeleteachana nao wote mkeo na huyo jamaa we piga kazi uwanze maisha yako na uowe mke umpendaye.
na usaidie wandengeleko wenzako huku kwenu. jitahidi kutuonesha kuwa wewe ni mkubwa na unamaamuzi yako.
mdau wa
k'koo shimoni.
Mdau wa trelleborg, una matatizo makubwa kuliko ya huyo mshikaji wako aliyekupatia mchongo.
ReplyDeleteWatu wengi weusi wakienda kichwa kichwa huambulia wenza wa kike walio 'reject'au 'junkies', yaani walevi wa kupitiliza, watumiao unga, vokongwe wenye dementia syndrome n.k
Hivyo tatua matatizo yako kabla ya kutuelezea matatizo ya mbongo mwenzio, maana kuishiwa pesa inaweza kumtokea yeyote hata wewe unaweza kutimuliwa na huyo mamsapu wako mzungu.
Suala ongea na rafiki yako mpange mikakati ya kujikwamua kiuchumi maana nyote mna matatizo na yako ni makubwa zaidi.
kijana pole sana,wewe huyo jamaa kwanzia sasa wala usimpe kipao mbele kwani kinachofuata ni kukuharibia kwa jimama.
ReplyDeleteKujilipua=Nikujifanya mkimbizi na kupata misaada yote ya ukimbizi,kwani huwa watu walio kata tamaa hufanyahivyo.Faida ni kula na kuishi katika mahema ya kikimbizi.
Wewe wala usijilipue ishi maisha yako achana na mambo ya kitanzania kwani huyo jamaa kinachofuata atahamia nae kwajimamam lako.
Hayahaya kumekucha, vijana wakibongo `wanajilipua, na wengine wanataka kujitoa mhanga' Hii yote ni kuchoka na maisha ya Bongo.
ReplyDeleteMwenzenu kaolewa na mwanamke, haina shidakama anawakumbuka wenzake home,na sio kumbeba mwenzako, wasaidie wale wanaostahili, jamaa zakohuku Bongo,ili kudhalilikakwako huko kuwe na manufaa.
Hali kama hii tutabakia na vijana majivu tu!
Ndiyo huyo mtu amekusaidia, lakini kisiwe kigezo cha kukuomba pesa kila siku. Unapomsaidia mtu hapa duniani unasahau kama ulishamsadia. Mungu tu ndo atamlipa fadhila. Kwa ufupi achana na huyo mtu. Ulichomsadia kinatosha. Nia yake alisadia ili ufike hapo na wewe uangaike kivyako vyako. Kwa hiyo endelea na maisha yako. Anataka kukuvurugia uhusiano ulikuwa nao na huyo mtu anayekusadia. Achana na huyo jamaa yako. Asikutumie eti kwa sababu alikupa njia za kufika hapo. Hata asingewa yeye ungefika hapo ulipo siku. Kila kitu ni mipango ya Mungu. Ila endelea na maisha yako. Na yeye aliletwa, sahau kabisa kama alikuleta. Asikutumie.
ReplyDeleteMbona NDUGU ATAJUTA KUZALIWA, KUULIZA KOSAAA, POLE MWAYEGO.Halafu kwa taarifa yenu MAREKANI MICHEZO YA KUJILIPUA HATUFANYI, Mambo hayo yako Europe.
ReplyDeleteHuyu jama alouliza swali ana matatizo na baadhi ya wadau wanaochangia mada pia wana matatizo ya kuelewa. Jamaa ameandika "kwa walio ughaibuni tu". Sasa inashangaza kuona mtu anaandika comment eti yuko K`koo shimoni, matokeo yak wamekazana kuuliza kujilipua ndio nini. Waacheni walengwa wamshauri.
ReplyDeletenijuavyo mimi ni kwamba kwa muhusika aliye bongo,kujilipua ni kujikita ktk matumizi ya bangi/unga kupindukia.
ReplyDeletena kwa aliye ughaibuni,kujilipua ni kuukana utaifa/urai wake halali ili apate hifadhi ktk nchi nyingine kama mkimbizi.
kwanza nyie mnaechangia mada hamsomi vizuri auswali jingine nyie mmekazana kujilipua maanayake nini kama unakalia kigogo ndo utakua ujui,,mwaya hao wanaokuponda wanafki wanataka sana nafasi kama yako wanakosa wamebaki wivu tu mi nipo ulaya nawaona sana wamejaa kibao wanaotaka makaratasi.hongera mkaka,cha msingi kaa chini ikiwezekana toka nae out uyo mzungu wako atakama analipa yeye haijalishi,
ReplyDeletemueleze ukweli toka upo bongo mpaka umefika apo na msaada gani umepewa na uyo ndg yko,,na why anataka kukuaribia kwake atakuelewa tu wenzetu wanaelewa
WENYE WIVU MFEEEEEEEEEEEEEEEEE
MAANA RAHISI NA WAZI YA KUJILIPUA NI PALE UNAPOKWENDA KWENYE NCHI UNAYOPENDA KUISHI AMA UMEKWENDA KIHALALI AU KWA NJIA ZA PANYA NA UKIFIKA KULE UNASEMA MIMI SI MTANZANIA KWA MFANO NA UNASEMA WEWE NI MSOMALI NIMEKIMBIA MACHAFUKO HUKO NAHITAJI HIFADHI JAMANI, UNAPIGWA INTERVIEW UNASHINDA UNAPEWA MAKAZI YA KUDUMU HADI HAPO NCHI ULIYOJIITA UNATOKA ITAKAPOKUWA SHWARI UTARUDI, LAKINI KUNA NCHI ZINGINE KAMA UK UKIKAA KWA MUDA FULANI UNARUHUSIWA KUOMBA KUISHI MOJA KWA MOJA UKIKUBALIWA TENA UNAWEZA KUISHI KWA KIPINDI KINGINE UKAOMBA URAIA, NA TENA BAADAYE UKAOMBA PASSPORT. SASA KAMA MTU NI KWELI ANATOKA SOMALI NA KUJA KWA MFANO UK NA KUOMBA UKIMBIZI HUKO SI KUJILIPUWA KWA VILE YEYE NI KWELI MSOMALI, AU UNAPOKWENDA NCHI YA WATU KAMA UK NA KUOA AU KUOLEWA NA KUISHI MOJA KWA MOJA HUKO SI KUJILIPUA, AU UMEENDA KUSOMA NA UKAAMUA KUKAA MOJA KWA MOJA SI KUJILIPUA. KUJILIPUA NI PALE TU UNAPOHUSISHA UONGO WA SABABU ZAKO ZA KUTAKA KUISHI NCHI ULIYOKWENDA, HATA KAMA UNATOKA TANZANIA NA KUDAI KUWA MIMI NYUMBANI TANZANIA NINATESWA NA SERIKALI NIKIRUDI TU NITAULIWA AU KUFUNGWA SASA NAOMA HIFADHI ZA KISIASA NIENDLEA KUWEPO HAPA, KAMA UNASEMA UONGO NI KUJILIPUA PIA.
ReplyDeleteklwa nini usimuombe mjaidina ukajilipua au amia iraq kwa saadam ujilipue make naona wa bongo mnapenda kujilipua
ReplyDeleteWenye kisa kama cha mshikaji,tupo wengi sana huku ughaibuni sema tunaogopa kujitaja, Pia wengi kati ya wabeba box wamejiwasha iwe us uk na popote kule ughaibuni, tuliojilipua ni wengi sana tena sana sanaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
ReplyDeletesasa tofauti yako na yake ni ipi? yeye kajilipua wewe umeolewa ouch!!!!!!! mimi nadhani ni the same thing kwanza yeye roho yake inalala usiku wewe si ajabu umeacha kidemu au mke wako bongo na hujamwambia huyo bibi wa watu. Siku akigundua talaka unayo.
ReplyDeleteSema asante kwa huyo aliyekukaribisha. hata kama ulijilipia lakini hamna kitu kigumu hizi nchi kama kuweka makazi. kama huna mahali pa kushukia na huna mwenyeji japo akuhifadhi siku tano tu it's so damn hard. I know it.....kwa hiyo hata kama ni kumlamba miguu huyo mtu mlambe sana. usingekua hapo ulipo wewe.
Yaani kumbe ndio siri ya wabeba maboksi, mnarejea huku na magari ya kuhongwa, halafu mnajidai kuwa mumetoka ulaya,au ughaibuni, kumbe umetoka kuwekwa kimada na vibibi vya huko
ReplyDeleteMi nadhani kwa kuwa mdau jamaa alikusaidia na ukatoka , sasa ni zamu yako na wewe kutupa michongo sisi wamatumbi wa hapa kariakoo shimoni.
ReplyDeleteMimi pia kama ulivyokuwa wewe kitambo kile nina kila kitu ila naomba unipe mchongo wa kufika huko. nina kaelimu ka degree ya business , nataka exposure niweze kujipanga vizuri hapa bongo. email yangu ni kanange10@gmail.com.
Thanks.
Bro usione soo, sema na ''mkeo'', usijali maneno ya ''wakaanga ubuyu'' wa bongo. sema naye mpe data kamili kuhusu huyo fisadi kiwembe. Tena usimpatie pesa yako bure. Kumbuka wewe ''unanya kazi'' kupata hiyo pesa wakati yeye anasubiri kukinga pesa za bure (huku Ufini inaitwa KELA Money)
ReplyDeleteEndeleza maisha yako, haijalishi kupewa pesa na mwanamke, kwanza huku scandnavia wanawake ndo wenye maamuzi makubwa kwenye familia. Hata walioowa wazungu kwa ndoa za kawaida bado wanamsoto tu kama wewe, mbona hilo linajulikana? Hata weye wajua! JIPE RAHA, ACHANA NA HICHO KIROBA KILICHOUKANA URAIA WAKE WA BONGO!!!!
Pole mshkaji,
ReplyDeleteKwa jinsi ulivyoelezea kama ni kweli, mimi nafikiri inatosha ulivyomsaidia jamaa, iliyobaki sasa utamsaidia pale unapoona pana ulazima wa kufanya kama nduguyo aliye ughaibuni.Pia kaa chini na mkeo umueleweshe ukweli wa mambo lazima atakuelewa.
Usijali maneno yanayorushwa na watu ya kukukatisha tamaa kila mtu anahangaikia maisha yake ili mradi asivunje sheria.
Napenda kukushauri kuwa usikae na kubweteka hapo si kwenu kuna siku utarudi nyumbani, angalia usiende home na aibu tupu.
GJK