Brother Michuzi,
Habari za kazi, Nomba msaada uniwekee hili suali langu katika blog yako. Mimi nimewasili hapa uk muda sio mrefu sana na nipo katika mji wa london - willesden green (north west). Ninachotaka kujuwa kwa wadau wenzangu waliopo katika mji huu ni haya:-
1) natafuta kazi part time (wakati wa masomo) na full time (wakati wa likizo) tatizo kila agency ninapojiandikisha sifanikiwi kapata kazi, jee ndugu zangu ni agency gani mnzotumia na ziko sehemu gani? au ni company gani mnazozijuwa zinazoajiri? sijali umbali (zone 1 - 4)
2) mko wapi? nataka kujuwa kama kuna watanzania wowote ambao huwa wanajikusanya na kupiga ball wakati wa week end, ningelipenda kujiunga nao. Pia kama kuna mahali ambapo huwa mnakutana kupiga stori, kutizama mechi na mengine (sio mikutano ya siasa) ningelipenda kujuwa ili nami nijumuike na watanzania wenzangu email yangu ni
shukrani
Mohammed (Fish)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. Mr shabbanApril 03, 2009

    Mbeba box huyo kaja. karibu sana kwenye chama kubwa Habari za nyumbani,Vipi foleni,Vipi umeme wa mgao,vipi waalimu na Viboko,Vipi Mwakei na Rosthamu,Vipi Vumbi la Kweneye meno,Vipi foleni kweneye ATM,Vipi vibaka kwa mtogole, Vipi mafuriko msasani, Vipi rushwa kila sehemu hadi Mochwari,Vipi maDc wapya,Vipi Maandalizi ya 2010.Karibu sana.

    ReplyDelete
  2. KWANI WEWE KAMA NI MGENI INAMAANA HUANGALII NEWS??
    NA KAMA UNAANGALIA HUKUONA WATU JUZI KTK MKUTANO WA G.20 WALIVYOANDAMANA KWAAJILI YA UKOSEFU WA KAZI
    HAKUNA AJILA HIVI SASA NA KAMA HUNA ADA YA KUTOSHA ULITEGEMEA KUPIGA BOX ILI UJILIPIE UTAKUWA UMEFIKIA PABAYA KWANI RECESSION IMEHARIBU KILA KITU

    ReplyDelete
  3. Kacheki McDonald,hukosi kazi,labda ukatae mwenyewe.Jifunze kupiga deki! Ukishindwa huko nenda Care! Kutunza vibabu na vibibi. Shift za kumwaga.

    Na mpira huku,hatuna muda, ni kusaka pound 24/7.

    Hilo ndio box!!!!!

    ReplyDelete
  4. ULAYA HAKUNA UMBEYA NA HAKUNA KUKAA KIJIWENI UNAULIZA WABONGO WA NINI MBONA UMEWAACHA BONGO??
    TAFUTA WAZUNGU ILI UJUWE LUGHA ACHA USHAMBA WABONGO UTAPATA WASIOKUWA NA KIPINDI WATAKUYEYUSHA TU. HUO NDIYO UKWELI KAMA UNATAFUTA UMBEA

    ReplyDelete
  5. ndugu yangu kama huna kaakiba hali itakuwa ngumu,kwasababu habari ya leo 8.3% ni rate ya unemployement,na aijawahi kutokea tangia 1983..ma box yote wanachukua wazawa sasa hivi.

    ReplyDelete
  6. Ushauri wangu
    1.tanua uwigo usione noma kuvamia watu wengine zaidi mfano toka congo, pakistani, peru, brazil ,kenya , nigeria, india n.k
    2. Kazi za box wakikuuliza 'una experience' wewe jibu 'tena sana hata kama hujawahi kusugua masufuriana au kupiga deki kwa kutumia vifaa maalumu, maana kazi za 'box' lazima 'uwongo mwingi karibu ya kweli' maana hutashindwa kupata experience baada ya dakika 30 ukiianza.
    3. Ukipewa miadi ya taimu ya kuanza uwe unawahi na kufanya 'box' kwa bidii.
    4. Nenda ubalozi wetu karibu na bond street tube station. kila alhamisi ni siku ya wabongo 'kuzuka' bila miadi, hapo utapata mawili matatu ya wapi utakutana wa wabongo wengine.

    Mpiga Box Mstaafu
    Aliyerejea Bongo baada ya 'Kuwini'.

    ReplyDelete
  7. we, shabban, sura mbaya!

    ReplyDelete
  8. nenda paddington kamata great western kituo cha kwanza reading ni zone 8 lol outside london. ukitoka uliza mtu yeyote oya salaama awe mzungu mchina au mwarabu wote watakujibu kwa kiswahili then the ball start fro there. waambie wakulete palmer park kwa sunday football. kuhusu mpira wapigie sky hd paundi 29 tu you are home and dry.

    ReplyDelete
  9. sasa we jamaa ni waajabu sana! mwenzio kafika hapo baada ya kumpa mchongo we unaanza kuulizia oh eti nyumban vp

    ReplyDelete
  10. wewe hapo juu habu acha upuuzi wako msaidie mwenzio. Kiroboto wewe.

    ReplyDelete
  11. Wewe, yaani kifupi ni hivi: Watu kila siku waachishwa kazi. Ina maana hujui hilo? Mwajiri gani ataajiri agency wakati watu wanapiga miyao kutwa kucha? Wewe soma urudi ukawe fisadi bongo. Halafu huku weekend watu ni siku ya mapumziko sio siku ya kuongea ufisadi! Umenielewa? Michuzi wewe upo current mweleze huyo juba anayeficha jinale. Nasema soma ukawe fisadi maana ndo wabongo mawazo yao. halafu ukipata nondo kwenye email yako chini kabisa unatangaza hizo nondo utakazozipata.

    ReplyDelete
  12. Jaribu: www.reed.co.uk
    kinachotakiwa ni kwamba ujiandikishe kila agency ambayo unaiona, shala mungu atakusaidia
    niliwahi kuishi huko miaka ya 70s and 80s sijui siku hizi kukoje nasikia ningumu sana kupata kazi!
    lazima uwe na NI number kabla hujapata kazi, je hiyo unayo?

    wee anon wa juu acha utani msaidie mwezio kama wewe uko UK

    P.E.D

    ReplyDelete
  13. karibu sana mdau. sisi tupo.
    ushauri wangu ni kwamba kwenye maswala ya kazi si kwamba unaomba tu na kupata na pia nikitu cha kutafuta wewe jiandikishe kote na kwa maagency wote. na usisahau kuwa kipindi hiki cha credit crunch kazi ni tabu kidogo, ila usife moyo.
    na pia zingatia sana lililokuta, wengi hubadilika.

    ReplyDelete
  14. DOGO UKITAKA COMPANY NJOO EAST LONDON KWA WAJANJA,KUNA PUB KIBAO ZA WAKENYA,KAMATA TRAIN MPAKA BARKING STATION,UKIFIKA BARKING STATION ULIZIA PUB YA WAKENYA YAITWA "BUZZ"HAPO WABONGO KIBAOOOOO,WAKENYA WA KUMWAGA,POMBE NA MADEMU BWELELEE,LAKINI ANGALIA USIJE ACHA SHULE BUREE,JUMBA BOVU SIKU HIZI HAWATAKI MCHEZO,.

    ReplyDelete
  15. sasa wewe unamkaribisha mwenzio lakini unashindwa kumjibu alouliza, sasa ndio ufahamike nini?
    kijana anaonyesha ana malengo na pia anataka kuwa karibu na wabongo wenzake kwa nini hamumpokei kwa hima, au kuna uchoyo katika kubeba box?

    ReplyDelete
  16. karibu baba boksi linakusubiri tu. shule na boksi mtaka yote hukosa yote.

    ReplyDelete
  17. mtaka yote hukosa yote hahahah shule na box haah ahaha aha aha aha ah
    acha namba yako sya simu humu nitakutafuta nikupe mchongo
    hakuna stoli huku watu tuko bise babangu

    ReplyDelete
  18. hey kwanza pole!! pili Njoo zako Reading makazi ya kumwaga wewe tu, lakini ni neppi kwa kwenda mbele au kucheka na mataira kwa sana. Agency Mac caring, uk opportunity, The Mount care home, St Lukes (wabongo tele), Austin House, Beacher hall, blue arrow,crowthorn village, GOOGLE TYPE IN U WIL GET CONTACT DETAILS. 90%YA WABONGO WANALIPA ADA KWA BOX WASIKUTISHE!! KARIBU FANYA KILICHOKULETA UTAFANIKIWA!!!

    ReplyDelete
  19. wasiliana na www.tanzaniaone.co.uk au www.tzuk.com
    ukumbi wanaokutana watanzania ni Club Africa ya mtanzania Jesse.
    kituo cha karibu cha train ni Canning Town train hiyo hiyo inayotoka kwako-jubilee line.

    Leyton kuna club nyingine.

    Mpira kuna sehemu zifuatazo.East Ham,leyton nyuma ya uwanja wa timu ya mpira ya leyton orient.Makocha ni said John na Juma skrub.

    Edmonton kuna uwanja wa mpira na club ya Sai sai eneo la watanzania.

    woolwch nako kuna timu ya watanzania.

    ReplyDelete
  20. bro mithupu, nakwambia wabongo wanaoshi nje,akili kidogo,unagoam kupost maelezo yangu.kuuliza si ujinga,soma coment zote hapo juu,ni kumkatisha tamaa mtanzania mwenzao, kisa wivu,usenene, na kwanini apate. watanzania acheni hizo.mwelekezeni mwenzenu, ulaya haitofautiani, wala hajakurupuka kuuliza hayo kwani anajua yapo,kuanzia baa,sehemu za mpira na makutano.
    AU mnaogopa kwa kuwa kaja na shule atachukua kazi zenu,mwelekezeni wanavyouza magazeti na kazi hizo nyingine.
    ushauri wangu kwako ,kama unamdhamini ,piga buku ,rudi bongo,utajiaaibisha tu,kama wanavyoaibika wenzetu ambao hawajasoma.

    ReplyDelete
  21. Jamani msimkatishe tamaa huyo mdogo wetu wakati sisi sote hizo ndio kazi zetu.

    ReplyDelete
  22. Pooooooooooooooooole lakini kazi bado zinapatikana. karibu

    ReplyDelete
  23. ndugu mimi nitakusaidia kuhusu kucheza mpira kama hutoona mbali njoo hapa heston maeneo ya hounslow karibu na hoteli ya ya thornclif kuna park kubwa huwa kila week end tunacheza mpira lakini kuhusu kazi kwa kweli ni kipindi kigumu kupata maana hata hao wanaokwenda job centre kusign basi wanaambiwa hakuna kazi asante mdau hounslow.

    ReplyDelete
  24. kijana jaribu kujiandikisha kwenye agency ya BLUE ARROW,utagawa gawa gazeti nje ya tube stations lakini mkono utaenda kinywani.otherwise kasome course fupi ya care then uombe kazi kwenye care homes mbali mbali. karibu sana London...

    ReplyDelete
  25. Mr ShabbanApril 04, 2009

    Pole sana ndugu yangu,mwingi hapo ni utani,japo kuna vichembechembe vya ukweli, lakini ukweli huku huwa tunafurahi sana kuona mwenzetu amechomoka bongo kwakuwa kufika huku tayari tunakuhesabu ni mjanja.Usihofu wala kukata tamaa kuja uk. Ila mi nafikiri ugejaribu sweden nasikia huko ni fresh zaidi kuzidi uk. Waombe na wadau waliopo uswidi wakupe data,japo wadau wa uswidi ni wabinafsi kupita kiasi. Karibu sana uk. Mdau Shebby

    ReplyDelete
  26. Hili ndilo tatizo la wabongo!! Yaani baadala ya kumsaidia mzalendo mwenzao wanaongea pumba tu!! Mbongo habadiliki..ndio maana nyumbani hatuendelei!! Utafikiri tumelaaniwa! Haki ya mungu! Mdau tutawasiliana kupitia kwenye email yako mi niko North London na sio kila mtu anapiga boksi nchi hii! Usifanye kosa la kuacha masomo!!

    ReplyDelete
  27. babu karibu sana Ulaya bonge la experience hakuna tena, ishu zote ulizokuwa unaona kwenye ma Tv zote uzushi kucheza na akili zetu tu, huku kila mtu ndani tu hakuna ku socialize kama ki bongo bongo, hata mi wakati nakuja nilidhani ntapata sehemu ya kucheza Mpira au kukaa kupiga stori mbili tatu lakini hamna ishu hizo na wabongo wengi wanaokaa huku ndo kama ulivyoona hapo juu ma wivu na akili kama wamerogwa usijali, we keep ur head up na baada ya miezi 3 tu utakuwa ushapata elimu kuliko uliyoifuata, kazi ndo hivyo sasa hivi ishu sio mchezo lakini kila mtu na zali lake unaweza ukapata komaa kichwa tu mwisho wa siku Mungu yupo na hauwezi kufa, mi mpira napenda ila sichezi kwa sababu ya baridi, make u learn somthing out of this experience, thats all i can tell u brah, naitwa Twali-kii.

    ReplyDelete
  28. Kaka umejionea wabongo walivyo almost 90% ya hayo wame kudiscourage hiyo tabia ya wabongo wameshindwa hao wanadhani wote watakua ni failures.Mfano mzuri watu wa west walivyo na ushirikiano sio sisi wabongo.kaka ushauri wangu rudi home ujipange waaulize wote hao walio nje nini nani mwenye maendeleo jibu nizero kaka mimi nimekaa viwanja kibao anzia kwa O,kuja kwa Brown wabongo woote wlikua wananikimbia kwa jinsi walivyo choka kaka rudi home ujipange uzimiaje it is a old time fashion!ZOMBA ZAPATERO

    ReplyDelete
  29. Twali-kii una ushauri mzuri sana ndugu yangu, kama ni mbeba box uko more advanced.

    ReplyDelete
  30. SIKILIZA MGENI, UKIMTAFUTA MBONGO LONDON BASI KALAGABAHO...WOTE WAINGEREZA KWA URAIA NA TABIA. USHAURI WA BURE HATA KAMA HUUPENDI NI TAFUTA NJIA W/END NENDA READING KAMA MSHAURI MMOJA ALIVYO KUAMBIA.HUWAPENDI CCM SAWA LAKINI WATAKUA MSAADA WA 1 KWAKO BILA HAYA. NENDA READING STATION TEMBEA HADI OXFORD RD,ULIZA SOLMAR(KILIMANJARO)RESTAURANT.USIRINGE. MDAU-LONDON.

    ReplyDelete
  31. KWELI KABISA MICHU HAWA WABONGO WA SWEDEN NAUNGANA NA SHABBAN HAPO JUU WANAJIDAI SANA,SIJUI KWANINI WAKATI HUKO USWIDI HATA BOX HAZIBEBEKI WANASHINDIA SLESI MOJA NA JUISI WAKO CHOKA VIBAYA MDAU US

    ReplyDelete
  32. daa kama ni mdogo wangu marahaba,kama ni kaka basi shikamoo,ndugu yangu kwanza nakupa hongera ya kuja ulaya mpaka hapo wewe ni mjanja sio wote wanaweza,kuja ulaya either wewe ni fighter katika maisha aka hustler kama sio hivyo basi wewe ni msomi,bab kubwa,ee bwana wangu kusema ukweli hiyo experince unayo pata sasa hata sisi tumetoka huko huko,ni kweli umekuja kipindi kibaya ila usikate tamaa Mungu ni kubwa na kila mtu ana ridhiki yake.ila nakupa pole sana kufikia hapo london hapo ni kama kariakoo wangu nahisi mwenyewe umeshaona,kuwa makini sana na wapopo,wapakii,wa congo n.k,usiwe muwazi sana kwa watu kwani hapa hasa sana hapo lond kuna machoko wengi sana,kwanza wanaunguzana wenyewe kwa wenyewe sio wa bara wala wa visiwani aka wapemba.ushauri wangu tuliza ball kama ezi 2 usihangaike kwani kwenye maisha ni subira,wasenge ndio wanakuwa na papara,tulia wangu,usiwe na tamaa ya haraka jitahidi kufanya mambo yako ukiwa na tamaa watakubebesha unga sasa hivi,bi mkubwa queen kawa mbaya sana hapo kipawa,angalia kama ni shule basi soma then,kama utaona mambo magumu hapo nakushauri uondoke hapo faster kwani wabongo wengi wenye maisha na wanaosoma hawapo hapo wengi wapo nje ya lon,simaanishi kwamba lond hamna wasomi la hasha ila ukweli ni kwamba watafuta maisha ambao hawasomi wapo lond,na wengi wa hapo ni waburundi wa kuchonga na wapemba hao watakushauri uoe na wewe uwe na nyekundu sio kitu kibaya ila usiache shule.sasa kazi kwako huo ndio ushauri wangu,kuhusu mpira nakushauri utafute tv yako uangalie ndani tu,mambo ya ushirika utajuta wangu.lastly usichague kazi box ndio lenyewe hao wote walio comment hapo juu ni waosha vyombo,waosha vibabu/vibibi nk,wasikutishe kaza buti.otherwise karibu ulaya ingawa picha uliyokuwa nayo kabla ya kuja huku sio unayo iona.
    cao.
    mimi mzalendo

    ReplyDelete
  33. YANI ATOKE LONDON AENDE READING?????/HAHAHAHAHAA = UNATOKA DAR UNAENDA MOROGORO!!!!!!!!KUWAFATA WABONGO TUUU??????AU STORY?AU KAZI???

    ReplyDelete
  34. NI KWELI WABONGO WA STOKHOLM WANAJITENGA SANA SIJUI NI KWANINI. AU NDIYO UPEMBA NA UUNGUJA. KAZI KWELIKWELI. MDAU CALF US

    ReplyDelete
  35. WANAFIKI WAMEANZA HUKU USWIDI SISI KAZI HATUJUI UMBEA.MDAU UKISHINDWA UK NJOO ULE KUKU STOKH KARIBU UMEKI EUR HADI USHANGAE. HAPO UK MICHOSHO TU WASHIKAJI HAWANA KITU HATA POUD 2 KUMEK SHUGHULI WANACHO JUA WAO KUCHONGA TU, MARA USWIDI HIVI MARA HONGKONG VILE, MTACHONGA SANA LAKINI UKWELI UNABAKI PALEPALE TUNAWASHINDA KWA KILA KITU MLIOKO UK. Mjanja wa Stokholm.

    ReplyDelete
  36. MIMI NINGEKUSAIDIA KUHUSU KAZI, LAKINI ITAKUWA SHIDA KWA VILE HAPA WANATAKA MTU FULL TIME NO PART TIME KAZI NI YA KUMWAGA NA KAMPUNI YETU KIDOGO INAUBAVU WA KUPAMBAMBANA NA CREDIT CRUNCH, NA HIYO RECESSION, HADI SASA HAKUNA MTU AMEFUKUZWA KAZI N WANAAJIRI KILA KUKICHA. LONDON NI KUBWA NA INACHANGANYA KAMA MGENI WEWE CHA KUFANYA JIFANYE KAMA KICHAA HIVI JIANDIKISHE KILA AGENCY INGIA KILA JOB CENTRE SOMA MAGAZETI YOTE HATA METRO LA BURE UTALIPAT UNDREGROUND STATIONS, EVENING STANDARDS, NA MAGAZETI MENGI YA BURE HAPA LONDON, PIA KUNA KOZI ZA SECURITY GUARDS FANYA HIZO, KOZI ZA CARE FANYA HIZO USIONE AIBU MWAMZO MGUMU, HATA MIE ALIKUWA HIVYO HIVYO BAADA YA NONDO YANGUYA MBA MAMBO SAFI SASA. PIA KAMA HUKUJA NA BARUA YA POLISI KUTOKA TANZANI FANY HIVYO UAGIZIE NYUMBANI UPELE FINGER PRINT ZAKO WAKULETEE INASAIDIA KUPATA KAZI PI SEHEMU ZINGINE NYETI AMBAZO WANATAKA POLISI REPORT. WEWE ULIZIA KILA MTU HABARI Y KZI HATA HAO WAZUNGU WAULIZE TENA WAZURI TU WATAKUSIDA. ONDOA AIBU KABISA JIFNYA KAM ZIMERUKA, AT CLEANING JOBS FANYA UKIENDA HUKO UTAKUTANA A LINK ZINGINE, NETWORKING.

    ReplyDelete
  37. Mpwa njoo Reading. Kwanza kuna CCM, watakupa kazi,nao ni kama Agency. Mpira utacheza sana, wabongo tupo wa kumwaga, kuna college za nguvu,home office zinatambulika.

    Kuna impact college,utc,london college of professional studies. Hapo utaongeza visa uchoke mwenyewe.

    Kazi za care,zipo bwerere. Tunapiga shift balaa. Masaa 80 kwa wiki. Kila mwezi kontena bongo.

    ReplyDelete
  38. Naungana na wadau walio-comment kuhusu Wabongo walio Sweden, yaani ni Wabinafsi sijapata ona! Wabongo wa Sweden zero kabisa!!!

    ReplyDelete
  39. MDAU UNEFANYA KAZI MASAA 80 KWA WIKI NAMBIE NI KAZI GANI UNAFANYA NA UNALIPWA KIASI GANI KWA SAA. NIJE LEOLEO KAMA SIYO KUMDANGAYA MSHIKAJI,JARIBUNI KUSEMA UKWELI, HALAFU TUKISEMA OOO WABONGO WA SWEDEN OOOOMARAHIVI OOOMARAVILE JARIBUNI KUWA WAWAZI MWAMBIENI NDUGUYETU, NENDA SEHEMU HII KUNA KAZI HII NA HII WANALIPA KIASI HIKI NENDA SEHEMU INAITWA HIVI PALE KUNA KAZI HII NA HII WANALIPA HIVI NA HIVI KWA SAA, HAPO MTAKUWA MMEMSAIDIA KWA KIASI KIKUBWA SANA TENA SANA.TAMBUENI MWENZENU NI MGENI HIVI HAMUELEWI MAANA YA MTU KUWA MGENI,JAMANI VIPI NYIE. NA MWISHO WOTE MLOTUSEMA WABONGO WA SWEDEN TAFADHALINI ACHENI MARA MOJA, SIYO KUJENGA HUKO NI KUBOMOA, KAMA TUNA KOSEA TUAMBIENI TUNACHOTAKIWA KUFANYA NININI SIO KUTUNANGA. TUNAWAKARIBISHA WA UK NJOONI SWEDEN MSHANGAE. NAOMBA KUWAKILISHA MDAU SWEDEN.

    ReplyDelete
  40. MWAMBIENI NENDA SEHEMU FULANI,UTALIPWA POUND KIASI FULANI KWA SAA, KAZI YENYEWE NI FULANI,KAWAIDA HUWA INAKWISHA SAA FULANI UKIMALIZA HAPO KAMA BADO UNA UWEZO WAKUENDELEA KWA MAANA YA NGUVU, UNAWEZA KWENDA KUUNGANISHA SEHEMU FULANI HAPO KAZI HUANZA MUDA FULANI NANI KAZI FULANI NA UTALIPWA KIASI FULANI KWA SAA, SASA MNA KALIA USIFEMOYO USIFEMOYO USIFEMOYO ASIFE MOYO WAKATI BADO HAMUMPI MAELEKEZO TOSHELEZI?. HALAFU MNA SEMA WABONGO WA USWIDI WABINAFSI,WABONGO WABINAFSI WAPO HUKO,NIHADITHI NDEFU NIKIAMUA KUWAHADITHIA. MDAU HONGKONG.

    ReplyDelete
  41. sasa nyie watu wa ulaya mwenzenu kaomba msaada mnamzingua,rafiki yangu ujue huko uk hakuna mbongo watu ni wasomali na waburundi na wanyarwanda.kila mtu hapo uk na sweden kasaidiwa kujiripua na hao waliofika kabla yenu sasa na yeye mpeni mwelekeo na akajiwashe acheni roho mbaya wajinga wakubwa nyie kila mtu alikwenda na gea ya kusoma kuna nani huko mtz anaweza kujilipia shule?kama sio ulimbukeni wa maisha,mnazani maisha ni rahisi,watu hamna hata huruma je mnajua kama nauli zenyewe zinatoka wapi? hakuna mtz wa kawaida tunayemjua na tena mzalendo akawa na nauli yake otherwise ni mwizi yeye baba yake au fisadi kama mwl.nyerere alivyosema nadhan matokeo mnayaona kina lowasa,Hii ndio taabu ya ku-overtake maisha hamyajui mmetoka kibada mpaka uk sasa mnashindwa kuwasaidia wenzenu sababu maisha hamyajui ulimbukeni tu,mpeni tafu mshikaji shenzi zenu,na pumbavu sana nyie ,au ndio pesa za mvuto pou.55 per week zinawazingua nyoooooo!!!!!
    wadau JPN.Dozo baga

    ReplyDelete
  42. walio wema mpelekeeni mawazo katika email yake. Hivi kwa mlioko uk (londo) ni kwa nini mnaona shida kumsaidia mwezenu? kwani akipata naye kazi ndio atakuzibieni riziki zenu? saidianeni huko mliko!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...