
Honda cr-v 2.0
Wadau naombeni msaada wenu.
Nafahamu ya kwamba hapa ni jungu kuu. Gari aina ya Honda cr-v 2.0 auto, kwa kiwango gani inafaa kutumika katika nchi zetu za kiafrika.
Kwa mtu ambaye anatumia gari ya aina hii au mtu anayeifahamu gari hii anaweza kutoa picha kamili, kama gharama za uendeshaji na maintainance, uimara wa gari, upatikanaji wa spare, nk. Ushauri wenu utanisaidia sana katika kufanya maamuzi!
Ahsante
Mdau Dan, Belgium
Thanks Mr Michuzi in Advance!
Utalia na vipuri!!! Kuna mtu namfahamu analo kama hilo. Ameliegesha kwa sababu mpaka aagize vipuri kutoka ng'ambo.
ReplyDeleteTafuta Rav-4 au Harrier. Utalia na spea.
ReplyDeleteI own a crv since 2005 it had abt 54000km and it is not expensive to maintain. The only major repair i have done to the car is to change stabiliser bushes, stabiliser links..as you know the condition of our roads. The only thing i can advice you is to follow maintance schedule and to use unleaded petrol. You will enjoy it more when you travel long distances..it response to the pedal very well...
ReplyDeleteHello, ninapenda kukuambia kuwa HONDA CR-V ni moja ya chaguo langu, kwa maana kuwa inapenda kuwa family car. Japo sina hakika na upatikanaji wa spare parts zake, nimeshawahi kuambiwa kuwa spare parts za HOND CR-V ni kazi kupatikana Tz.
ReplyDeletePamoja na hayo nimeona watu wengi wakiendasha Honda CR-V sasa sijui wanazipata wapi hizo spare parts.
Kila gari inategemea na matumizi na udereva vyote vinachangia kuwa na gari kwa muda mrefu na ktk ununuzi wa spare pia kwa maana hiyo unakuja kutumia mwenyewe na itakuwa ndio gari mmoja kwa kila safari au?/hapo ukiweza jibu hayo maswali utapata mamna ya kuona gari yako itakuwaje,ila kwa aina ya gari hiyo ni nyanya(kimeo)haifai kwa maana hiyo achana nayo kwa ushauri wa bure.
ReplyDeleteNDUGU YANGU HIZO HONDA HUKU ZIMEJAA KAMA YEBO YEBO NOW UKIRUDI NA KITU NYUMBANI USIDHANI KAMA UTAKUTA HAKIJAINGIA.
ReplyDeleteWEWE RUDI NA GARI LAKO SPEAR PART ZA KUMWAGA TU
spare au spear parts sio kazi. vijana wa kuzichomoa kutoka gari moja na kuwauzia watu wengine au kutoka kwenye gari mwenyewe na kuuziwa sio kazi kubwa hapa kwetu bongo. we leta mchuma tu tuongeze idadi ya kugawana utajiri na umaskini.
ReplyDeleteKweli utalia na vipuri LAKINI ukifunga vinachukua muda kabla ya kuchakaa.
ReplyDeleteUshauri: Jaribu TOYOTA, pamoja na kwamba Honda CR-V na Nissan X-Trail ziko daraja moja lakini bei na upatikanaji wa HONDA ni mgumu!
Sasa wadau wenzangu huu ushauri wa upatikanaji wa spare za Honda DR-V ni kwa hiyo model ya 2.0 au ni kwa zote? Kwa kweli mmenifungua macho sana kwani nami nilikuwa na wazo la kuvuta Honda CR-V. Sasa wadau gari gani 4WD ni bora kwa TZ kwa wakati huu. Natanguliza shukurani zangu kwa ushauri wenu.
ReplyDeleteMdau U.S.
Kwa uzoefu wangu mdogo ni kuwa kwa Tanzania bado suala la spare ni tatizo kwa magari ya aina zote ukiachilia mbali TOYOTA. Haya magari ya aina nyingine watu wanaendesha tu kwa ku-"cross fingers" matatizo yasitokee. Na wengine wanayagharamia saana kwa kuagiza spare Japan (Hapa ninamifano ya mtu alieagiza spare Japan za Honda-Odyssey).Na nadhani kinachofanya watu wanunue aina nyingine za gari ni bei zilivyokuwa ndogo ukilinganisha na Toyota makes. Unaweza ukaona aina za mitsubishi,Nissan,SUbaru,Daihatsu, Honda yaana bei ndogo ya kutupa ukilinganisha na Toyota (Hapa nikifananisha model zinazoshabihiana kwa kila manufacturer).
ReplyDeleteUshauri wangu ni nunua Toyota achana na aina nyingine za magari "pasua kichwa" kwa Tanzania. Ukiwa Japan, na nchi nyinginezo hamna tabu gari lolote ni sawa tu.
Umasikini wa akili ni kitu kibaya sana.
ReplyDeletemtu maeuliza upatikanaji wa spea , wewe unajibu honda bongo zipo nyingi sana.
nijibu swali, spea za honda bongo si nyingi kama toyota .
HAO WOTE WALIOANDIKA KWAMBA SPARE ZA CRV HAZIPATIKANI AU SIO GARI LA UHAKIKA HAWA-OWN CRV...PROBABLY NI MANENO YA MTAANI TU. HUKU BONGO ZIMEJAA KIBAO UKITAKA MPYA NA USED. NA UZURI MPAKA SASA HIVI SPARE ZA CRV HAZIJAWA FAKE ZA KICHINANA KAMA ZILIVYO ZA TOYOTA. MIMI NINA RAV NA PIA CRV...I CAN TELL U RAV4 INAHITAJI MAINTANCE MARA KWA MARA KULIKO CRV...NA SPARE ZAKE FAKE NI NYINGI SANA MPAKA NIMEAMUA NIWE NANUNUA USED TU...
ReplyDeletecrv siku hizi zinanunuliwa na baadhi ya wizara. hiyo ni indication kwamba ni ya uhakika. Spare zake zipo nyingi tu na kama kuna mtu amekosa spare ya crv aseme ni spare ya chombo gani. Ila ukweli spare zake ni ghari na hasa kwa sababu sio fake kama za magari mengine. Pls bring ur crv we will soon start crv owners club...
ReplyDeleteNimekuwa natumia honda miaka minne sasa, Kwa ujumla gari hizi ni nzuri sana hazina matengezo ya mara kwa mara na kama ukitengeneza ni stabilizer tu kwa ajili ya barabara zetu na zenyewe itakuchukua mda kubadilisha tena, Zinakimbia sana na ni stable barabarani nikilinganisha na Toyota rav 4 ambayo pia rafiki yangu anayo. Utumikaji wa mafuta ni wa kawada kwa wastani ni lita 1 kwa km 13. Zina space ya kutosha. Spare parts zipo maeneo ya Kitumbini kuna wataalam kule hawakosi kitu. Na ata hivyo kuagiza Japan kama utalazimika katika nyakati hizi sio jambo gumu kuna wadau wanafanya kazi iyo.
ReplyDeleteMimi ninakushauri kama mtumiaji wa Honda. Nimekuwa ninatumia gari za aina ya Honda kwa zaidi ya miaka 18 sasa na ninakuhakikishia kuwa ni gari nzuri yenye low maintenance cost ukilinganisha na ubora wa gari. Nimekuwa na aina tofauti za Honda form Civi to Accord na sasa hivi nina tumia CRV na Odyssey.
ReplyDeleteManunuzi yangu ya spare parts za honda si ya mara kwa mara kwani sifa kubwa ya watengenezaji wa Honda ipo kwenye engine na wanajivunia hilo ingia hapa www.honda.com or www.honda.jp
Huwa ni rahisi kwangu kununua spare parts online rather than kwenda kununua kariakoo kwani parts za honda zipo Kariakoo mtaa wa Msimbazi na duka lingine lipo mtaa wa Swahili. Lakini kwangu mimi ni convenient kununua online kwani sihitaji kuhangaika na ninapata kile hasa ninachokihitaji na ni Genuine Part.
Vinginevyo njia nyingiine ya kununua parts unaweza kununua kutoka Nairobi kwa kutuma message kupitia simu yako ya mkononi kwa kuwasiliana na Accord Ltd wa mtaa wa Kirinyaga. Kwa update ya namba zao angalia kwenye Yellow Pages ya Kenya.
Spare parts nyingi za magari hasa Toyota si genuine parts as a result ukifunga kwenye gari performance inapotea na hazi chukui muda matatizo yanajirudia.
Nunua mawili kabisa, ili moja uwe unachomoa spea! Halafu hizo CRV ni update tu ya 'Kitchen Party', Unazikumbuka? Zilikuwa Bwerere juzi tu, sasa zimekwenda wapi? Nakushauri ununue Toyota.
ReplyDeleteHonda CRV ni 4WD gari nzuri ambayo hata mimi naitamani, lakini katika kusoma maoni ya watu nimegundua kitu kimoja! Watu ambao wanamiliki CRV maoni yao wote wanaipa credit gari hili! Pengine kutokana na uzoefu halisi wanaoupata, Maoni mengi hasi ni ya watu wasiomiliki CRV. Fuata ushauri wa mtu anayeimiliki gari kuliko ule wa mtu aliyesikia tu. Jamaa yangu aliwahi kuniambia huwezi kusifia iphone wakati wewe unatumia Blackberry! Labda ajitokeze mtu ambaye imewahi kumsumbua gari hii atuambie!
ReplyDeleteMLETA MADA,NAOMBA UJUE HAKUNA KNACHOKOSEKANA TANZANIA SOEAR PARTS ZIPO,NA HIZO HONDA ZIMEJAA KIBAO KILA AINA YA HONDA,WASIKUTISHE WEWE HATA HAMMER LETE ZIPO TU,
ReplyDeleteJAMANI,na mimi nina swali langu kama la mdau naomba msaada,mimi nipo ughaibuni nataka na mimi nianguke bongo na mchuma na mchuma ninaofikiria ni grand vitara new model 2.0 engine,sasa nayo vipi hapo kuhusu vipuri?
ReplyDeleteGrand Vitara za kumwaga, gari iko reliable, inadumu, iko economical ila ni target No 1 ya wachomoa spear. As for Honda CRV ni 4X4 nzuri tafuta msaada zaidi kwa watalaamu kama yule jamaa wa top gear BBC, Uki google Honda CRV review BBC top gear jamaa atakupa pro and cons that hiyo gari!
ReplyDeleteUlieomba ushauri jaribu kuwasiliana hii blog watakushauri vizuri mimi nilikuwa na tatizo linalofanana na hilo,na walinisaidia
ReplyDeletemagaribeipoa.blogspot.com
HAKUNA CHA KUULIZA SPEA PARTS TZ ZIPO ZA KILA AINA NASHANGAA MTU ANAULIZA HATA YA SUZUKI WAKATI KUNA MAGARI YA BEI MBAYA LAKINI SPEA ZIPO,HUKOSI KITU TZ SASA DEALERS WAPO WANAOWAKILISHA MAKAMPUNI MAKUBWA KAMA NISSAN NA SUZUKI AGENT DT DOPBIE,TOYOTA KILA MAHALI ZIPO HIVYO WATANZANIA WALIOUGHAIBUNI TAMBUENI HAPA KUNA KILA KITU SASA TANGU FAKE PARTS UP TO GENUENE,NYINYI LETENI TU MIKOKORO IMEJAA HAPA ILA MAFOLENI TU YANATIHSA
ReplyDeleteTabu ya wabongo mnaokwenda nje ya nchi mnaondokaga washamba sana na sijui ni kwanini hamuamini kama Bongo siku hizi kuna changes. Dunia ya huku pia iko kwenye kiganja ni wewe na vijisenti vyako tu. Njoo hata na Hammer Petrol/Diesel mpaka Gas za kumwaga.
ReplyDeleteMtakuwa washamba hata HOME!
GJK
Mimi ni mtumiaji wa Honda toka 2002 na nina kuhakikishia katika gari ambazo zina space kubwa ndani na unakaa bila shaka ni honda huwezi kulinganisha na ufinyu wa RV4. Kuhusu suala la msingi juu ya spare, Dar spare za kumwaga sio kama zamani tulikuwa tunanunua toka Nairobi "Accord Spare" Nenda Ilala mtaa wa Uhuru kuna duka la wapemba bei yao ni nzuri sana nasikitika jina nimelisahau. Tanzania sio ya Toyota peke yake na mara utakapogundua uzuri wa Honda utajuta kuchelewa kuifahamu.
ReplyDeletesorry wadau nami pia napenda kujua kuhusu nissan teana 230jk na series nyingine za teana.sijaziona tz au ni kwamba sijabahatika kuziona.vip kuhusu spare parts,uimara wake nk.
ReplyDeletemdau
hongkong.
Mie nakushauri achana na honda, ni juzi kati tu nilikuwa naongea na mafundi nikawauliza kuhusu spea zake wakasema zipo ila bei ni kubwa sana hata wao wanapendelea kwenda dukani na mwenye gari akasikilizie mwenyewe bei asije sema anaibiwa, kazi kwako kipato na uwezo wako unaujua mwenyewe.
ReplyDeleteCha bei kubwa na vitu Adimu ndio Org
Deletekwanza angalia unakaa wapi hapo dar....lakini all in all ebwana achana na honda na hata mitsubishi hawa walishashindwa kutengeneza 4WD za ukweli...labda ni Trucks na Meli ndiyo wazuri.....sana sana kama una kahela hiyo CRV mnunulie mkeo manake ni Ladyish car ..awe anaeneda nayo saluni na kwenye kichen parties ,basi.....otherwise utaumia
ReplyDeleteNDUGU UNAACHA KUULIZA UBORA WA GARI UNAULIZA UPATIKANAJI WA VIPURI???NINI MAANA YA KUPATIKANA VIPURI IKIWA KILA BAADA YA MIEZI MIWILI UNAVIBADILISHA???JIULIZE NI NINI UNATAKA?,UBORA?,USALAMA?,UHAKIKA?,UIMARA WA BODI,SOCK UPS NK?SMOOTH HANDLING? JIBU NI RAHISI SANA...NUNUA HONDA.GOOGLE UINGEREZA NA MAREKANI MTENGENEZAJI INJINI BORA JIBU NI HONDA!!!NI RAHISI KUUA BODI YA HONDA LAKINI SIO INJINI!!!INGAWA WATU WENGINE HUWA HAWANA BAHATI, HATA WAKINUNUA NINI KINAPATA MITIHANI.MIMI NAMILIKI HONDA MBILI,CR-V MIAKA 3 SASA NA HR-V MIAKA 5 SASA NA SIJAJUTA KUZITUMIA NA SITOHAMA HONDA.KUNA UBAYA GANI KUNUNUA OIL FILTER TSH.80000/= IKIWA KAMA ITATUMIKA MWAKA MZIMA???ACHANA NA KASUMBA ZA KIENYEJI KUTOKA KWA WATU WANAOAMINI MANENO YA MADALALI NA MAFUNDI WANAOTENGENEZA MAGARI KWA MAZOEA NA KIMBUMBUMBU.HONDA NI ZAIDI YA GARI NA UKITUMIA NDO UTAJUA KWA NINI WAZUNGU HUWAAMBII KITU KUHUSU HONDA. USHAHIDI:
ReplyDelete1)THE 100 MOST RELIABLE CARS OF THE LAST DECADES, #1 HONDA ACCORD, #6 HONDA CIVIC, #8 HONDA CR-V CHANZO NI www.gizmag.com
2)WHO MAKES THE WORLD MOST RELIABLE ENGINES?, #1 HONDA, CHANZO www.gaadi.com
3)THE WORLD'S BEST AND WORST ENGINE MAKERS, #1 HONDA. CHANZO www.cardekho.com
4)CAR RELIABILITY INDEX TOP 100, #1 HONDA JAZZ, #8 HONDA HR-V. CHANZO www.reliabilityindex.com
HUU NI UTAFITI WA KISAYANSI KUTOKA KWA WATUMIAJI MAGARI DUNIANI NA SIO MANENO YA MADALALI WA MAGARI BONGO. SIKATAI HATA KIDOGO KWAMBA TOYOTA NI GARI NZURI SANA LAKINI UZURI WA TOYOTA HAUJALETWA NA UPATIKANAJI WA VIPURI KWA URAHISI BALI NI WELEDI WA KAMPUNI,JE IWEJE HONDA IWE MBAYA KWA SABABU TU VIPURI VYAKE NI GHALI SANA?JE HAO AMBAO HAWAJATUMIA HONDA WANAJUA SISI WATUMIAJI WA HONDA NAMNA AMBAVYO HATUNA PRESHA NA VIPURI TUNAVYOFUNGA KWA SASABU YA GENUINENESS ZAKE??NA AMBAVYO VINAKAA MPAKA MIAKA 5???, ALAFU TUJIULIZE NI MFANYA BIASHARA GANI AMBAE ATAHIMILI KUUZA KIPURI KILA BAADA YA MIAKA MITANO NA BADO ASIFE NJAA??,TUJIULIZE JE KAMA KUNGEKUWA NA VIPURI HALISI VYA TOYOTA TANZANIA JE WATUMIAJI WA TOYOTA WANGEVIMUDU??,HITIMISHO LANGU NI KUWA KAMA UNATAKA GARI LA KIMASIKINI (MAFUTA NA UIMARA WA VIPURI SABABU HAKUNA FEKI) NUNUA HONDA.ACHANA NA KASUMBA ZA WATU WANAOSIKIA NA KUAMINI.
kuba.
Ulaya na Marekani wazungu hutumia Honda kwa sababu ya kile wanachokiita "MOST RELIABLE CAR/HONDA RELIABILITY IS UNBEATABLE".ingawa inacost kidogo kufanya repair lakini kwao si tatizo kwa sababu wanafanya mara moja kwa kipindi kirefu sana,kumbuka Wazungu ni wabahili sana so Honda ni Mkombozi wao.mfano TIMING BELT ambayo mimi nilifunga katika HR-V yangu ina MIAKA MINNE sasa na nikiikagua hakuna hata dalili ya kunyambuka na zaidi ya yote Spark Plugs zake sikuzibadili toka niinunue kutoka UK na hakuna misses...mambo ya Honda hayo!.na ndo mana huko Duniani kuna mpaka klabu za CR-V,HR-V,ACCORD nk.Honda ni Gari ya Kimaskini na ndiyo sifa yake,inatumia mafuta vizuri na inaaminika kwa ubora na usalama.ingawa Marekani kwa sasa wanachochea ukuzaji wa soko la brand zao kama GMC, kuna propaganda za kutaka kupunguza soko la Honda USA so wao wanairank GMC #1 then TOYOTA #2 Honda #3 ili kuwafanya wamarekani wanunue GMC kuliko Honda kwa sababu wanajua hata wangesema Toyota ni #1 bado wamarekani wasingeshawishika kutumia Toyota na ndo mana Honda wakaanzisha Brand inayoitwa ACURA ambayo imefunguliwa USA.kama Tanzania vipuri vya Honda hakuna hilo si tatizo la Honda bali ni tatizo la soko,rejea falsafa za Kiuchumi.kama uliweza kununua gari kutoka Japan kwa unini ushindwe kununua Shock-ups kutoka Dubai au Kenya???.Watanzania tukumbuke kuwa maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua.kama watanzania tuliichagua TOYOTA hilo si chaguo baya pia sababu Laws of Nature/critique of pure reasons zinafundisha kuwa yote tunayoyajua yanatokana na Muda na Nafasi(Space and Time).Hivyo tisiiponde Honda wakati bado hatujaipa nafasi na muda wa kuitumia na ndo mana wauza vipuri bado hawawezi kuuza vipuri visivyo na soko.
ReplyDeleteMimi navutiwa sana na HONDA HR-V na cc 1600 kwahiyo nimepata jibu kwamba nikati ya gari bora sana ngoja nijipange
ReplyDelete