Heshima yako kaka,

Kuna habari hii nadhani wadau wa blogu yetu ya jamii watakuwa interested nayo inahusu mtangazaji mmoja wa Uturuki aliyejipaka rangi nyeusi uso wake ili kujifananisha na Obama ambaye alikuwa anatembelea Uturuki.

....................................................................
VIDEO - Mtangazaji wa Habari Aliyejipaka Rangi Nyeusi Kujifananisha na Obama

Mtangazaji huyo wa luninga alitangaza taarifa ya habari huku akiwa amejipaka rangi nyeusi uso wake katika kumuigizia rais Obama ambaye alikuwa nchini humo kwenye ziara yake ya siku mbili katika ziara yake ya siku nane barani Ulaya.

Link kwaajili ya habari kamili na video ya Mtangazaji huyo ni 

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=1721706&&Cat=2

Shukran kaka 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya, shukrani kwa taarifa hii. Nimeiona kwa mara ya kwanza hapa kwenye blogu ya jamii. Kilichonijia akilini, mara moja, ni kuwa kuna tatizo la tamaduni kugongana. Utafiti wangu mwingi uko katika masuala haya ya tofauti za tamaduni. Nilihisi kuwa kitendo cha huyu mtangazaji kingeleta sokomoko Marekani.

    Basi, baada ya kupaga hisia hiyo, nimeenda na kufanya utafiti kidogo, na hima nimegundua kuwa ni kweli, kitendo hiki kinavyoeleweka Uturuki ni tofauti na kinavyoeleweka Marekani. Na nimeangalia taarifa mbali mbali na kuona kweli kitendo cha mtangazaji kimeleta sokomoko Marekani. Na hapo ndipo Waturuki nao walipokuja kuamka, maana bila Wamarekani kuleta zogo, Waturuki hawakuona kama ni kitu cha ajabu.

    Hayo ndio masuala ninayoyatafiti, kwani naona kuwa tusipofanya juhudi ya kujielimisha kuhudu tamaduni mbali mbali, tutakuwa na migongano isiyoisha. Maandishi yangu mengi yamelenga huko, na warsha ninaendesha huku Marekani, na nimeanza kuzifanyia Tanzania pia. Nimewahi kufanyia Zanzibar, Pemba, na Arusha. Ujumbe wangu kwa waTanzania wenzangu ni kuwa sherti tujizatiti, maana dunia inazidi kuwa kijiji, na katika kijiji hicho tutakuwa tunagongana na watu wa tamaduni mbali mbali. Tusipowaelewa na wao kutuelewa, itakuwa ni matatizo juu ya matatizo.

    ReplyDelete
  2. That's racial discrimination, he does not need to do so because obama's skin colour looks like theirs, he is not black enough at all.

    ReplyDelete
  3. Hamna lolote huo ni ubaguzi tu

    ReplyDelete
  4. AFANDE MIDAKOApril 13, 2009

    hapo wakulalamika ni black indians coz jamaa 100% amejifananisha nao na si obama kwa wale msiowajua wahindi weusi ama wao wanavyojiita tamils ukimwita black indian panakuwa hapatoshi inaosemekana jamaa wamelaniwa wapo sana malaysia tz sijawahi kuwaona

    ReplyDelete
  5. chizi nini anafikili obama mwindi mweusi!

    ReplyDelete
  6. nimefurahi sana kuona mtu mweusi anakwenda chooni white house na anapika mihogo jikoni hahahaha!

    ReplyDelete
  7. Watu wenye inferiority complex utawajua tu! yaani hata kama mtu anafikiri nyie ni baab kubwa na kujaribu kujifananisha na nyie au kujaribu kuonekana kama nyie au kuwaiga nyie basi mnafikiri sijui vitu gani, sijui amewabagua nakadhalika, lakini nyie mkiiga mambo yao mnaona sawa tu, thats how it should be eti wao ndio wakuwaiga. wengine hata kujichubua hujichubua ili wawe weupe basi hiyo sawa tu, lakini mtu mweupe akijipaka rangi nyeusi kwa sababu ameizimia rangi nyeusi eti yeye mbaguzi. People wake up sisi watu weusi ni baab kubwa acha wajifananishe na sisi, we are not inferior, kwa hiyo acheni hiyo complex.

    ReplyDelete
  8. Huyo jamaa ni chizi kweli!!kwani Obama mweusi hivyo..majitu mengine bwana kwa ubaguzi wa rangi..sasa kuwa mweusi ndio nini!mbona wao wanalala kwenye jua wabadili rangi...

    ReplyDelete
  9. Mwalimu Mbele ila hujatueleza katika utafiti wako kuhusu hili sokomoto matokeo yake yalikuwa nini?
    Je unaposema Waturuki hawakuona jambo ya ajabu hiyo ni kutokana na nini?
    Je, ni utamaduni wao au huyu mwandishi alikuwa anaonyesha heshima kutokana na kitendo hicho?
    Ilikuwa maana ya nini kuhusu hiki kitendo?

    Naomba ueleweshe jamii kwa sababu umesema wewe umejikita zaidi kwenye hii taaluma na tunaomba kulishwa elimu muhimu kwenye hii jamaa inayoenda kuwa kijiji cha dunia.

    ReplyDelete
  10. Kwa mtoa maoni wa "April 13, 2009 9:38pm" napenda kutoa shukrani kwa kuniuliza masuali. Papo hapo, mimi hupenda kujitambulisha kwa jina, na ningefurahi zaidi iwapo ungetumia mtindo huo.

    Pamoja na hivyo, nimeguswa na moyo wako wa kutaka kuelimishana. Mimi kama mwalimu nawajibika kuzingatia zaidi hilo kuliko kujali kuwa mwulizaji hafahamiki. Ni vema kuzingatia hoja.

    Utafiti si kitu cha "chap chap," na hauwezi kumalizika. Utafifi wa hili suala la uso mweusi haumaliziki. Ni suala lenye mkabala na historia ndefu pande zote, yaani upande wa Waturuki na upande wa Wamarekani, na upande wetu sisi pia, na litaendelea kuwepo na kubadilika.

    Kama nilivyosema katika ujumbe wangu pale juu, nimefanya utafiti kidogo na kuona kuwa zogo linaloendelea baina ya Wamarekani na Waturuki wakati huu ni suala la tamaduni kugongana. Fikra za Waturuki kuhusu uso ule ni tofauti na fikra za Wamarekani.

    Jambo moja ambalo nimejifunza ni kuwa Waturuki wanaamini na wana usemi kwamba kuomba kitu ni kujipa uso mweusi. Kwa falsafa yao, unapoomba chochote unajidhalilisha. Wanatumia dhana ya uso mweusi kwa maana hii. Hapo nimejaribu kutafsiri dhana ya hao Waturuki ambayo haitafsiriki kwa kweli. Labda tukitaka kuielewa kidogo tutumie usemi wa kwetu "Mtaka cha uvunguni, sherti ainame." Lakini hii nayo haiipatii vizuri dhana ya Waturuki ya uso mweusi.

    Huu mfano moja tu unaonyesha jinsi lugha inavyoweza kuwa chanzo cha migongano, kwa sababu unachosema katika lugha moja, huwezi kukitafsiri katika lugha nyingine au ukitafsiri ile tafsiri inaweza kuleta maana tofauti au mbaya.

    Tofauti na watu wanavyoamini, lugha hazitafsiriki. Tunachofanya, kwa kiasi kikubwa, ni kubahatisha au kubabaisha. Kwa mujibu wa taaluma ya lugha na falsafa yake, kitu kinachoitwa tafsiri hakiwezekani.

    Kwa hivi, nikijifanya naweza kutafsiri sawa sawa wanachomaanisha Waturuki, nitakuwa najidanganya, na nitakuwa nawadanganya wengine.

    Kwa upande wa Wamarekani, mtu ambaye si mweusi kujipaka rangi nyeusi ni tusi zito sana, kutokana na historia ya ubaguzi wa rangi katika nchi hii, ulioanzia wakati wa utumwa na bado kiasi fulani unaendelea. Ndio maana Wamarekani walivyoona tu ile sura ya Mturuki, wamehemka.

    Nimesema kuwa utafiti hauishi. Na katika suala hili la uso mweusi ni hivi hivi. Hili zogo ambalo linaendelea baina ya Wamarekani na Waturuki huenda litachangia kuwapa Waturuki mtazamo tofauti kuhusu dhana ya uso mweusi, na Wamarekani nao huenda watagundua kuwa tafsiri yao ya kitendo kile si tafsiri ya walimwengu wote. Mtafiti anapaswa kufuatilia historia na mabadiliko ya kitu anachokitafiti. Ndio maana nasisitiza utafiti haumaliziki.

    Kama unapenda kufuatilia zaidi fikra zangu, unaweza kuona taarifa zangu mtandaoni, na unaweza pia kunisikiliza hapa.

    ReplyDelete
  11. Na nyie watu weusi mna nongwa .. nyie kuwaita wazungu whiteboy ..sawa!! na yeye akukuita blackman unakuwa mbogo ? unajua sio kosa letu sababu tumetoka kwenye utumwa ..hivyo tukisikia maneno yanayoendana na rangi zetu . tunajihisi . kama bado tunadhalilishwa na slave master

    ReplyDelete
  12. Wewe unayejiita mtaalam huna lolote ulilotafsiri hapo juu ya huyo mtu kujipaka rangi nyeusi. nafikili yalikuwa ni mawazo yako. hakuna mtafiti anayeficha yale aliyogundua na hata ukisoma ulivyoandika inaonekana huna utafiti wowote uliofanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...