Heshima yako mkuu wa nanihii ya nanihii,
Namuuliza mheshimiwa Makongoro Mahanga mbunge wa Ilala amefikia wapi kuhusu ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni iliyopita kwamba ataimarisha barabara za mitaa ya TABATA na atajenga barabara ya Tabata Dampo - Kigogo kwa kiwango cha lami? Uchaguzi unakaribia na hatujaona maandalizi ya kuweka lami katika njia ya dampo.
 
Barabara kubwa ya Tabata ni nzuri sana na ina mifereji mikubwa hatuna tatizo kabisa. Barabara za mitaa hazitamaniki na hiyo ya Dampo ndio usiseme, tena angeanza hata angalau kidogokidogo ingetusaidia sana sasa hivi wakati ujenzi wa barabara ya Mandela unaendelea kwa sababu kuna foleni kubwa sana kutoka Tabata Relini - Buguruni.
 
Asante
Mdau Mnyarugusu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Heri sisi tusiseme, watu na barabara yetu ya Moshi Bar-Mombasa, labda kwenye kampeni tutasikia jipya

    ReplyDelete
  2. Shwari zuli sana,Lakini wapo wengi sana wa kuhulizwa Akiwemo Dr Remmy Ongala alimdanganya mkewe "nitakununulia gari nitakujengea nyumbakubwa kama mrima kilimanjaro..."

    ReplyDelete
  3. Watanzania lazima sasa tuamke.Mbunge hajengi barabara.Umeuliza JIJI? suala la ujenzi wa brbr ni comprehensive initiative ya sekta mbalimbali.
    Usimlaumu Makongoro Mahanga.
    Kwanza ameleta mabadiliko kuliko Rupia ambaye alikua hata haishi Jimboni.
    Mughaka wa Abhaiseki.

    ReplyDelete
  4. mahanga hana lolote ni aina ya viongozi wapenda sifa na kujinufaisha na familia yake tuuu. tangu awe mbunge hana la maana kwa wana ukonga zaidi ya kuendekeza kutafuta uwaziri ili ajinufaishe tuu

    ukonga ni jmbo lenye kila aina ya taabu za miundo mbinu kuanzia maji, barabara nk lakini hajafanya juhudi za kuwakutanisha pamoja wapiga kura na kuweka mkakati thabiti wa ufumbuzi wa kero hizooo.

    kazi kwenu wana ukonga kuendelea kusikia huduma ya maji ya bomba na kuendelea na bara bara mbovuuuuuuuuuuuuuuu....

    chagueni mabadilikoooooooooooooooo...

    mahanga jaribu kuwatembelea wapiga kura wako sio kushinda kwenye mabar tuuuuuuu

    ReplyDelete
  5. Anony no.3 kama mbunge hajengi barabara kwa nini kwenye kampeni anaahidi kuwa nitaawajengea barabara? kwa hiyo anawadanganya wananchi ili apate kura. sasa anatakiwa afahamu kuwa watanzania sio mabwege tena

    ReplyDelete
  6. jamae, viongozi wetu wakiwa na shahada feki mnategemea nini. ikiwa walisoma ni tofauti, ningependa baadhi ya hawa madktari kusema ni wapi wamekaa, vyuo vikuu ambako wamemaliza hata miaka miwili na hivyo vi phD's vyao

    matokeo yake ndo tunaona mabwawa za kuogelea katikati ya barabara zetu kwa maana akiwa na 4x4 anaona kama barabara ni nzuri kwa wote matokeo yake ni hela mfukoni

    ReplyDelete
  7. "MAKE POVERTY HISTORY"

    Watanzania wenzangu kwa kweli hali ya uchumi ulimwenguni zimekwamisha
    ahadi za viongozi kimaendeleo nchi nyingi katika bara la Africa.

    Tujaribu kuwazindua na kuwaelimisha
    "mataifa yaliyoendelea" kukumbuka
    ahadi walizoziweka kufanya mabadiliko ya uchumi na maendeleo kutokomeza "umasikini" katika bara la Africa,tatizo ambalo hata nusu yake hawakulitimiza.

    Tutajikuta tupo katika malumbano ya kubadilisha "viongozi na mikataba" wakati hata viongozi wengine wakichaguliwa hawatofanya mabadiliko ya maendeleo ya haraka

    Nchi za kimataifa zilizoendelea zinafanya jitihada za kurekebisha uchumi wa nchi zao na kusahau kabisa ahadi za bara la africa,mojawapo ya kurudisha maendeleo ya ujenzi si barabara pekee hata matibabu na elimu.

    Mickey Jones
    mickey@mail-online.dk
    DENMARK

    ReplyDelete
  8. Duu! Hii noma.
    Watajificha wapi wabunge wetu na ahadi zao. Globu ya jamii sasa hivi inawafikishia ujumbe wa kuwakumbusha mara moja tena basi moja kwa moja.
    Wabunge wengine mpooo? Tunaanza kuulizia kabisa utekelezaji wa ahadi kabla hamjaja kuomba kura.

    ReplyDelete
  9. anon wa kwanza umenigusa, tena alituahidi kuwa atakuja na greda huku yeye binafsi akiwa na bukta wakati kazi hiyo ya ujenzi barabara ikifanyika......thubutuuuu...namuona na suti yake tu akipepea, natamani kweli kumuona akirudi, sijui atarudi na sera gani!

    ReplyDelete
  10. ANONY WA TATU. LICHA YA JIJI MBUNGE ANAWEZA KUTAFUTA VYANZO VINGINE VYA MAPATO, MISAADA HATA HARAMBEE KUJENGA BARABARA. MBONA TUMEONA HATA VIKUNDI TU VIMESAIDIA UJENZI WA BARABARA? MFANO MKUBWA NI MFUKO WA MAENDELEO TABATA, UNAFAHAMU WAMEFANYA MAMBO MANGAPI, NAKUPA HOMEWORK. UTASHANGAA.

    MBUNGE ANA KILANGO ANGESEMA UBUNIFU WA KUWATAFUTIA WAPIGA KURA WAKE NAMNA YA KUJIIINUA KIUCHUMI KWA MRADI WA TANGAWIZI NA UPATIKANAJI WA MAJ LEO WANANCHI WA SAME WANGEKUWA WAPI KATIKA KILIMO CHA TANGAWIZI? JAPO NDIO MWANZO LAKINI INATIA MOYO.

    MSUYA ALIPOSAIDIA MWANGA KUPATA UMEME UNAKUMBUKA?

    NAAMINI HATA SERIKALI INAWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKISHA MALENGO YAKO KAMA UTAONYESHA NIA.

    ASANTE.
    MDAU
    NGOSHA

    ReplyDelete
  11. Hii habari yote imepotoka, japo nawachukia sana wanasiasa lakini kwenye hili nadhani huyo msanii mahanga anashutumiwa bure. Nasema hivyo kwa sababu kama ni kweli maeeneo yaliyotajwa yako jimbo la Ilala basi mahanga siyo mbunge wake. Mbunge wa Illala ni somebody Zungu. Mahanga ni mbunge wa Ukonga, kama vingunguti na tabata viko ukonga basi ni sawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...