'salamaleko....' askari wa trafiki 'akisalimiana' na dereva wa daladala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Hakuna salam hapo, afande anapokea sumu hapo. kwa utaratibu huu atufiki, mshikaji anapokea mrungula hadharani

    ReplyDelete
  2. Kaka unaharibu kazi za watu hapo live..Watoto watakula nini kakaaa!

    ReplyDelete
  3. anachukuwa hongo huyo

    ReplyDelete
  4. Huyu anachukua kitu kidogo, hakuna cha kusalimiana hapo!

    ReplyDelete
  5. Wanasalimiana au wanapeana karanga kiasi cha huyo abiria kunusa harufu ya karanga zenyewe zilizokaangwa?

    ReplyDelete
  6. Hapo mbona kama askari anapokea kitu kidogo au macho yangu!!

    ReplyDelete
  7. RUSHWA waziwazi kweli bongo soo yaani askari hapo anapokea mshiko wake bila ya noma, swali langu ni kwako wewe Michuzi au mtu aliyepiga hii picha, je umefanya nini kuhakikisha huyu askari anafikishwa kwenye vyombo vya sheria?? au hata mkimpeleka kwenye vyombo vya sheria hatochukuliwa hatua zozote?

    ReplyDelete
  8. Yani anapokea rushwa hadharani tena mbele ya watoto, mungu ainusuru hii nchi, halafu unaweza kukuta huyo askari bado yupo huru akiendelea na mchezo huu huu!

    ReplyDelete
  9. Michuzi! Je unajua ni watu wangapi wamepoteza maisha?

    ReplyDelete
  10. yaani huyu Afande back yupo mwenye kazi yake? Hana aibu kabisa. Yaani happo ni kweupe mno

    Tanzania rushwa aiishi yaani hata tufanyeke

    ReplyDelete
  11. Huo mkono lazima aulambe....Si unajua mkono mtupu haulambwI! Michuzi kulikoni?

    ReplyDelete
  12. Mkono mtupu hausalimiwi yakhe. Hawa ndiyo wanaendekeza uvunjaji wa sheria barabarani kwa njaa zao.

    Hebu serikali sasa ifikirie kuwalipa na hawa jamaa wanaobeba dhamana ya kusimamia sheria angalau hata robo ya watunga sheria, huenda watapata moyo wa kuzisimamia vizuri badala ya kuzivunja

    ReplyDelete
  13. Huyo afande vp? hapo wala hawasalimiani bali anachukua pesa ya vocha kama 1000/= au 2000/=hv, ndo rushwa zao hawa jamaa. hawapendi dereva mwenye makosa kumwandikia faini ambayo ni 20,000/= kwa kila kosa, na pesa kwenda serikalini.

    ReplyDelete
  14. Kesho utamkuta barabarani kama kawa na aibu wala ethics hamna...

    ReplyDelete
  15. Ninayeandika ni mimi mwenyew traffic polisi ninayepokea anwani ya huyu dereva, jamaa yangu ambaye tunatoka kijiji kimoja, ananipatia namba yake ya simu. Ndugu yangu kwa nini uwe na mawazo ya kuwuawa katika nchi yetu ta Taznaia ya uwazi na ukweli. Kama nikiona unanione kwa uzushi nami si nakuvuruta mahakani ninadai fidia ya shilingi moja.. Jamani tupendane watanzania!

    ReplyDelete
  16. kwa taarifa yenu huyo jamaa alikuwa akipewa hongo.icho ni kitu cha kawaida huwa wanajifanya kusalimiana kumbe anafinyanga noti na kumpa,ilikuwa hongo ile mkae mkijua

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 01, 2009

    Afu bado unabisha.Bongo we acha tuuuuuu

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 01, 2009

    ni mimi naona vibaya au/ hiyo body language....mhhhhh ...naona kama anakatiwa kitu kidogo vile.

    I hope I'm so wrong

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 01, 2009

    Mh alikuwa anapewa leseni?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 01, 2009

    Hivi wananchi wa kawaida tunatoa wapi ujasiri au haki ya kulalamika kama sisi wenyewe tutatoa au kupokea rushwa? Hakika dereva huyu akifanikiwa siku moja kuwa na mabasi yake ndiye atakaehonga kupindisha kesi ya basi lake litakaloua watu 30 na kujeruhi wengi wengine kwenye ajali Kitonga, na huyo traffic wa kawaida wa barabarani ndiye atakaekuwa Regional Traffic Officer (RTO)mkoa wa Iringa atakaemsaidia wakati huo na siku moja huyo RTO atapenda cheo taratibu hadi kuwa IGP- na atakayoweza kuyafanya huko kwa ukubwa wa madaraka atakayokuwa nayo yanatisha. Isitoshe huyo dereva atafanikiwa siku moja kuwa na mabasi mengi tu ambayo atayaingiza nchini kinyemela bila kuyalipia ushuru.Wakifika ngazi hizo tutaanza kulalamika 'Oh mafisadi'. Lakini ufisadi umeshaanza katika tabia zao sasa.Kila mmoja wetu ana wajibu kupigana na ufisadi kwa kujichunguza kwanza kabisa yeye mwenyewe.Hivi haiwezekani watanzanai tukafanya mgomo wa wiki moja tu ya kukataa kutoa rushwa popote pale (barabarani, mahakamani, polisi, TAKUKURU, ofisi ya ardhi n.k)kwa wiki moja alafu tuangalie mambo yanakuaje? Vinginevyo mnawalalamikia Manji, Rostam na wengine nini wakati wanchokifanya ni kile kile ambacho na sisi tunafanya kwa ngazi zetu za chini kwa kutumia udhaifu wetu? Michuzi itisha mgomo wa kutoa rushwa wa walau wiki moja kwa kutumia blog hii na vyombo vingine vya habari vitakavyokuunga mkono, tuone itakuwa vipi.

    ReplyDelete
  21. Hivi wabongo mnajua kusoma na kuandika?

    Michuzi ameweka alama za nukuu kwenye maneno "salimiana" akiwa ana maanisha kwamba sio kusalimiana. Wao ndio wanajifanya wanasalimiana.

    Kwa hiyo wadau wote hapo juu mliong'ang'ania kutueleza kwamba jamaa anachukua rushwa, that is obvious, hakuna aliyesema wanasalimiana. Hebu eleweni Michuzi mwenyewe alivyoiandika hivyo "wanasalimiana." Duuuu kaazi kweli....

    ReplyDelete
  22. Ndo ile wagosi walisema 'MKE WANGU BANDIKA UGALI, MBOGA NALETA SASAIVI'

    SamChom InTheMixx

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 01, 2009

    Wacha wachukue hongo MSHAHARA ni mdogo. Serikali imeshindwa kuwahudumia wafanyakazi wake. Sioni tatizo hii ni kama njia nyingine ya kujipatia kipato hana tofauti na mtu anayefanya biashara huku akiwa ni mtumishi wa serikali.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 01, 2009

    Tunaweza tukafikiri labda anapewa mchango wa harusi au kitu kama hicho. LAKINI body language za askari na dereva zinawasuta. Kijana aliye dirishani ni shahidi. Nimesikia hizi rushwa lazima upeleke mgawo kwa bosi, naye napeleka kwa wajuu yake mpaka JUU kabisa zinafika. Usipotoa ushirikiano unahamishwa kituo, au kunyang'anywa gari/pikipiki.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 01, 2009

    Hii sasa kali yaani mchana kweupe hata haogopi!!! huku Arusha bwana mihuzi trafic anakusimamisha anatafuta kosa kwenye gari lako akikosa utasikia "nipe basi hata ya chai tu sijaamka kabisa leo" sijui kama watu wengine walishakutana na hili ila ukweli jeshi la polisi tanzania linahitaji marekebisho makuba sana!!!

    HONGERA SANA BWANA MICHUZI KWA PICHA HII NAAMINI UMEFIKISHA UJUMBE,LAITI KUNGEKUWA NA BLOG TATU ZIAMUE KUREKEBISHA SERIKALI NAAMINI INGESHTUKA

    mdau nkya
    a-town

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 01, 2009

    Kama maoni ni haya na watu wanamfikiria vibaya,itafika mahali maaskari waogope kusalimiana na raia hata kama ni kwa nia nzuri.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 01, 2009

    Kwani trafiki haruhusiwi kusalimiana kwa mkono na dreva?

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 01, 2009

    Dah michuzi kiboko,umeitaimu vipi hyo,duu noma

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 01, 2009

    Sisi tulivyofunzwa udogoni unapomsalimia mwezio lazima umpe mkono hata kama wewe ni askari.Acheni roho mbaya.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 01, 2009

    Nimemuomba Mkuu wa Wilaya ya nanhii aitishe mgomo wa'kusalimiana'lakini matokeo yake amegoma kuitisha mgomo! Eti anasema yeye akale wapi, maana mgomo ukiitikiwa vizuri atapata wapi picha tamu kama hii? Basi next time Mkuu wa wilaya tupatie na namba zao wanazovaa kwenye magwanda- zoom in kwenye kale kasilva badge kale alafu kachang!

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 02, 2009

    ivi nyie watu askari na driver hawaruhusiwi kusalimiana??????
    au km ni mshkaji wake,majirani,ndugu uko mtaani??na anampa ujumbe au simu??

    acheni kufikiria watu vibaya,yaangalieni ya MAPAPA MAFISADI NCHI HII

    mwenyezi atusaidie

    ReplyDelete
  32. ex AfandeMay 02, 2009

    Kwa uchunguzi wangu ndani ya jeshi la polisi kitengo cha usalama makao makuuu hii picha ilikuwa ktk gazeti la mwanachi kwa mara ya kwanza na huyu afande mhusika hapa alikuwa anatoa risiti ya faini alio mpa huyu dereva wa daladala kwa makosa alio tenda kinyume cha sheria za barabarani na askari huyu baada ya uchunguzi anaendelea na kazi yake kama kawaida mimi nipo nje ya nchi lakini kawaida yangu sitoi maelezo bila uchunguzi asante wananchi mdau stellenbosch western cape SA

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 02, 2009

    Sofia Simba upo hapo , sio mpaka Mengi aseme!

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 02, 2009

    Ths is too much, what is the IGP doing? Yikes

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...