mdau akikatiza pembezoni mwa uwanja maarufu wa kidongo chekundu jijjini dar. umaarufu wa uwanja huu umefifia mno toka wazee wa jiji walipoamua kuupa mgongo, ikizingatiwa kwamba awali ulikuwa hai kila kukicha kwa michezo na hata matamasha wakati wa sikukuu kama vile idd na maulidi.  hapo ndipo hata JK alikuwa akicheza basketball na mpira wa miguu enzi za mwalimu. sijui kifanyike nini kuwaamsha wazee wa jiji ambao inaonekana wana mtindio wa ubunifu. hata sijui kodi za wananchi wanazifanyia nini endapo wanashindwa kuendeleza miundombinu. kama hela hakuna basi hata kuhamasisha makampuni nako ni shida? ah! inatia hasira wallahi!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Nadhani ifufuliwe ile kampeni ya uwajibikaji ya wakati wa Mzee Mwinyi alipokabidhiwa fagio la chuma kufagia wazembe, ikishindikana uongozi wote wa jiji ufukuzwe kazi. Hili ni tatizo sugu kwa nchi nzima, mpaka Waziri Mkuu au Rais atishie kumwaga radhi ndiyo viongozi waamke toka usingizini, akinyamaza nao wanarudi kulala usingizi.

    ReplyDelete
  2. Nani abuni. If only mngejua ukija upande wa Meya Abuu Jumaa na madiwani wenzie hawana lolote zaidi ya maslahi yao binafsi. Mkurugenzi Nyundo ni mgonjwa kila siku na ni mtu aliyekata tamaa. In short Ilala imelala. Wenye mawazo mazuri ni Kandoro na Mkuu wake wa Ulaya ambaye nae juzi juzi tu kaondolewa. Hawa wana mawazo mazuri ambayo Abuu Jumaa na wenzie hawataki hata ya kuyasikia. Na kisheria unfortunately there is not much the RC and DC can do. Jawabu ni kuirudisha tume ya jiji au JK aanzishe wizara ya kushughulikia jiji la Dar. Basi.

    ReplyDelete
  3. Hakuna kinachosaidia bongo!! Mimi kaka Michuzi nimeshindwa!!!

    ReplyDelete
  4. Hapo panasubiri vikwangua anga tuuuuuu!!! Hamjui wabongo tunavyokwenda wa wakati? hizi ni zama za vikwangua anga, achana na hizo habari zilizopitwa na wakati za viwanja vya michezo, sijui bustani za burudani!!

    ReplyDelete
  5. Wakati mnalalamika kuhusu kidongo chekundu mbona Mh Membe ametangaza kujengwa Mwl JK Nyerere conference center kwenye viwanja vya Gymkhana! Hii inaonyesha ni jinsi gani watu walivyo na masihara na sera zao za kukuza michezo

    ReplyDelete
  6. BONGO TAMBARAAAAAAAAAAAAAAAAARE... MAENDELEO MCHEZO WAKATI MEYA WA JIJI AMEKULIA KIPARANG'ANDA

    ReplyDelete
  7. hapo wanapanyamazia tu unaweza ukakuta pameshauzwa watu wanasubiri hali ya hewa ya EPA itulie lijengwe ghorofa hapo!!!

    balozi usiache kutupa habari ya hii sehemu!!!

    ReplyDelete
  8. Upumbavu wEtu tunAsifia vikwaNgua anga nA hApO tuNawaPa MafiSadi nafasi ya kuMaliza Open sPece zOtE

    ReplyDelete
  9. JK akicheza enzi hizo nani alikua anautunza huu uwanja? Ina maana hata yeye haukumbukia tena huu uwanja au haoni umuhimu wa kizazi hiki nacho kufaidi uwanja huo?

    ReplyDelete
  10. Utakuta mayor wa jiji anaishi oyster bay au mbezi huku atakuona saa ngapi?

    ReplyDelete
  11. Du, nakumbukia enzi zangu nasoma Kisarawe primary school( nasikia siku hizi ni sekondari)..Kidongo chekundu ilikuwa maarufu kwa michezo na sherehe za idd. Ukishuka mnazi mmoja unakutana na bustani safi tukipumzika mchana kwa kula mihogo ya kukaanga, juice ya ukwaju au bulga...by the way pale karibu kulikuwa na co-cabs offices (imeishia wapi?)..Dar-es-salaam bookshop unaikumbuka??..

    ReplyDelete
  12. Michuzi wazee wote wameshakufa ni juu yenu nyinyi sasa vijana kufanya hiyo kazi sababu viongozi wengi wa sasa hawajui chochote kuhusu kidongo chekundu na umuhimu wake au umaarufu wake kwao ni sehemu tu kama sehemu nyingine yoyote ukizingatia walivyotawaliwa na rushwa tena hiyo bado siku moja mtaona washauza hiyo sehemu watu wamejenga maghorofa na njaa zao na hakika kabisa sasa hivi wanapatafutia kamba ya kupauza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...