Baadhi ya wachezaji nyota wa Bongo United fc kwenye Lunch ya Usiku baada ya mazoezi jana:kutoka kushoto,Simon,Harry,Hamfrey,Libe na Evans

Na Ripota wetu Washington DC

Timu kabambe ya Bongo United imeingia kambini jana tayari kwa mpambano wao na Houston stars siku jumamosi may 23.

Pambano linalo subiliwa kwa hamu na mashabiki wa soka Watanzania waishio Unyamwezini,hasa wale watakao kuja kwenye WABONGO MEMORIAL REUNION EXTRAVAGANZA ya kwanza na aina yake,Timu kapteni Liberatus Mwang'ombe (Germany defence) amesema wachezaji wenzagu wana ari wa ushindi,mazoezi yanaendelea vizuri,chini ya supa kochi Gharib Latto.
 
Wachezaji ambao wameanza kambi ni Liberatus Mwan'gombe,Kheri Yahaya,Simon Marco,Hamfrey Owen,Shawn shaban,Denis Godfrey,Remy Mhando,Aristot Maruma,Evans Shangalai,Adam Tenga,Adam Jongo,Henry Kente,Vicent Ndusilo,Innocent Godfrey,Yasin Manyoka,Seif Ndosa,Aloyce Mbulu,Marco Mbulu,Ray Abraham,Dedi Luba,David Mbosi,Victor Kileo,Khasim Khamis,Patrick Kajale,Richard Mawenya,Rasheed Beach boy,Ismail Bana,Steav Majumbo Boas,Dulah na malilo.
 
Wachezaji Lucas "Kinyang'anyiro"Mukami,Hadji Helper,Elvis Doto Mnyamuru na Ebra Nyagaly wao watajiunga na kambi siku nne za mwisho kutokana na kutopata ruhusa kutoka kwa mwajili wao,Kambi iko shwari na inaendelea vizuri,tupo tayari kwa mpambano,ujumbe wetu kwa Houston " NYAMA IKISHAINGIA BUCHANI HARUDI KUA NG'OMBE"
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2009

    wabongo bwana...hapo ukiwauliza america wanafanya nini au wana mpango gani...hawana lolote kazi kuiga mablack kwenu hamtaki kyrudi
    sina anything against them but I don see why they are stuck kwenye nchi za watu...zamani watu walikua wanaenda kusoma wanarudi home sasa saa hivi watu wanafanya makazi kwa kazi za $10...shame
    mdau

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2009

    masikini mdau mwenye husuda na chuki, baba yako alizaliwa ludewa akenda dar kutafuta maisha akaamua kubaki huko na kutuma ziada kusaidia nduguze, wewe nini kinachokwasha watu wakiishi nje, hawaigi mablack thats how it is mamtoni, we kaa kwenye kanyumba kako kinyerezi, usiku jifunike chandarua using`atwe na mbu, acha mambo kushabikia mambo isio yajua

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2009

    Huyo mbwiga wa kwanza hapo juu hajapata tu mchongo wa kuibuka hapa duniani na akija harudi fala huyo atuche sisi na raha zetu huku..na nyie BoNgo uNitED mnachonga sana hukumu yenu subirini tunawaletea watoto wadogo wawakimbize na vitambi vyenu mkitoka sana 3-0.
    mdau
    H-taun

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 13, 2009

    I agree na mdau wa kwanza cause mini mi mtanzania niliyesoma abroad nikarudi nyumbani...Jamani wazalendo wenzangu asiwadanyanye mtu maisha mnayoyaona kwenye tv sio maisha wanayoishi wabongo huko marekani. wanaogoma kurudi tanzania wengi wanapiga mzigo(kazi za bei rahisi) na asilimia kubwa hawana makaratasi .wakitaka makaratasi wanafunga ndoa haramu ili wapate makaratasi. I think mdau wa kwanza katoa ushauri wa bure. Watanzania wenye kazi professional marekani ni wachache mno wengine hamna lolote kazi kupiga schedule halafu week end wanaenda kwenye club zao za kichovu za kwenye mahall. Hiyo ndio reality
    mimi ni mbongo aliyeishi Marekani miaka kadhaa na sasa niko bongo nazichanga kama kawa.Mkitaka hela ya nauli nitafuteni angalau mje kusalimia ndungu na jamaa(kwa wale wenye makaratasi) msio kuwa nayo sijui nitawasaidiaje nyie endeleeni kuosha wazee,kubeba maboksi and kutukanwa kwenye simu(telemarketers and collectors)
    mdau Bongo

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2009

    ivi hii ndio kazi yao au "wanapokua vekesheni"ndo wanacheza mpira?

    sijaelewa mnieleweshe,mana niliulizwa sana ili swali sina jibu

    kwa uzuri tu nauliza!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2009

    Wewe Mdau Bongo 7:51 Am. Ushindwe katika Jina la Yesu. Kama uliamua kurudi ni kivyako vyako. Na kama watu wafanya ndoa haramu ni za kwa. Pili pili usizokula zakuwahsa nini? Kazi ni kazi. Kwani kuna mtu ameisha kuomba msaada wako? Umeshindwa kuwasaidia wabongo walioko huko bongo, uje kusaidia mtu ambaye anafanya kazi yake. Hakuna mtu anahitaji msaada wako. Fisadi wa mafisadi wewe. Kama hauna cha kuongea toa pumba zako hapa. Ulisoma kwa msaada wa serikali sasa unakuja hapa kutoa kizaazaa chako. Uvae chupi ikubane kichwani matakoni ipwae" Mnyooo Embe dodo tamu kolea kama sukari.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2009

    Wewe unaejiita mdau Bongo huna lolote kama ulikaa marekani inawezekana kabisa uhamiaji walikusomba kinguvu na sasa unatamani uje kula kuku kwa mjirija lakini haiwezekani. watu hao kwenye picha wako safi kuanzia kielimu, familia, kifedha hadi kimakaratasi. Wewe endelea kung'atwa mmbu na kupigwa vumbi fala wewe, watu wamepanchi kimaisha hapa mujini na wana life expectancy ya kuishi kubwa kuliko yako yenye average ya miaka 50 yaani hapo ndo umeishi kinoma wakati hapo mtoni watu mpaka miaka 80 na gari ninaendesha vile vile. Unachekesha kweli ktk hiyo picha kuna watu wana lot zimejaa magari ya biashara zao na wamewaajiri wazungu na wao kazi yao kubwa kunapokea cheki na kwenda benki ku-deposit...wewe zichange tu kimpango wako lakini sisi ni matawi ya juu and u already know goddamn it.

    ReplyDelete
  8. Fikiria kila mtu angeishi ktk nchi yake aliyezaliwa dunia ingefika hapa ilipo?
    Nadhani hawa wanatukandia tuliohamia/kuzamia(au vyovyote vile mnavyotuita) majuu mna matatizo binafsi.Kuna wale mlioshindwa na maisha bongo mnakuja kutopunguza frustration zenu kwa kupiga madongo tulio ughaibuni,kuna wale mlioshindwa ku-adjust na hali halisi ya ughaibuni mkaamua kurudi bongo sasa mnataka wengine wajiunge na nyinyi.Hawa walioshindwa kuadjust ughaibuni ndo wenye chuki kali sana.Kifo cha wengi si harusi ndugu zangu.Hakuna anayetaka kufa nanyi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2009

    nyama ale mwingine we ujichokonoe vijiti!!!!!, wote tunaoishi mtoni tunajua waliorudi nyumbani mambo hapa yaliwashinda kwa papara zao, either wakapigwa bomba au wanerudi kutegemea kupigiwa pande na ndugu zao ili kuendeleza ufisadi, mnatamni kurudi kuoda msisi kwenye drive through lakini haiwezekani,ACHENI HASIRA WAZEE!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2009

    Mdau wa 7:51am acha wivu, wewe kama uliharibu ulipokuwa usa we kivyako na kafie mbali nyambafff kasoro mkia. Hapo ulipo unatamani ungekuwa wewe kwenye hiyo picha..yaaani machizi wametoka sikitoto na hapo jaamaa wako camp. Wewe endelea kula vumbi na batiki zako ka mzaire na tutumie adress yako tukuletee vyandarua aina ya ngao usije pata homa ya malaria.Hizo kauli zako ni za mtu aliye desperate..eti atutumie nauli?? kwa nini usianze na kumsaidia ant yako aliyeko bush hata nusu kilo ya dagaa ni shida kwake na ukaachana na watu ambao tunamishahara mizuri na tunakula balanced diet hata kama tunakula boxi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 14, 2009

    from what has been commented by the above wadau mi hoi.Watu waliocomment wanasound kama wana uswahili sana design kama wametoka kwenye shida bongo(if you know what am talking about) .maana hata comment zao mara dagaa,mara chandarua. I can see why hawataki kabisa kusikia bongo maana wakiwaza walikotoka hailipi..good luck wabongo endeleeni na drive thru zenu. sisi tunajichana fresh stuff

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2009

    Huyo Mbwea 7:51AM. Mimi nina uhakika wa 100% kuwa ulipata Deportation na katika Passport yako ukagongewa "NO ENTRY TO USA AFTER 10 YRS." Sasa huko TZ linakuchwea la STRESS/DEPRESSION kibao unaanza kuonea wivu watu ambao wapo wanakula maisha. Kama unajihamini basi nenda BLOG MICHUZI ukawaonyeshe Passport yako kama hujagongewa "NO ENTRY TO USA AFTER 10 YRS.
    Kama unajihamini kwa nini umeficha information. Mbwea wewe, Per Mkundu wako.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 14, 2009

    nyie Houston kumkimbiza mtamkimbiza nani kwa timu nzima ina miguu ya kushoto,mumeisha elekea kibra,bucha lenu lina wasubiri,msisahau kuja na kile kikombe

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 14, 2009

    This is such a great feud.Misupuu hebu itafutie mda uposti ili watu wachangie mada maana mimi ni mtanzania I work for UN na nabase home...I travel a lot especially huwa natembelea US...I'm not going to lie me huwa sitaki hata kukukaa hata more than 1 week maana it's not an American dream...mi sisemi Mengi ila nakubali bongo kuna shida na pie ni vizuri wabongo wanaoishi US wakubali kwamba majority hawaishi American dream ni shida tupu.but wanapata convinience ya vitu kama infrastructure,fast food,systems nyingi hazina corruption of course bila kusahau discrimination(unabaguliwa kama black then kama international) kuna mtu hapo juu kanichekesha eti anadai diet funny
    overall I am for kwenda America kutembea sio kukaa.

    ReplyDelete
  15. mdau ohioMay 14, 2009

    soka wandugu, jamaa walichofanya ni kitu cha kawaida katika kujiandaa na mechi, ilitegemewa houston nao waonyeshe maandalizi yao yalipofikia basi, ila kuna watu wanatumia kila nafasi wanayoipata kuondoa frustration zao za maisha,turudi kwenye houston tupeni mambo yenu

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 06, 2009

    Hakuna Ubishi hapa Wabongo Majuu ni
    Wachovu kinoma.Wengi wetu tumeingia
    Mkenge kwani tuliamini kuwa Majuu ndiko Peponi,kumbe ni Sinema tu za
    Hollywood,tukubali Ukweli ingawa daima unauma sana.Mimi natamani kurudi Bongo ila naoni sana aibu kwani sin kitu baada ya miaka 8 ya kusota hapa USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...