Katibu Mkuu wa chama cha Riadha nchini RT Suleiman Nyambui akizungumza na wanahabari juu ya Mbio za Vodacom Dar Half Marathon zitakazofanyika juni 21 2009. Kati ni Rukia Mtingwa wa Vodacom na kulia ni mratibu wa mbio hizo, John Manyama
mbio hizo zitaanzia kwenye uwanja wa Taifa na kuishia hapo, amesema wanariadha maarufu mbalimbali wamejiandikisha kushiriki baadhi ya wanariadha hao ni Dickson Marwa (Tanzania)Victory Gatundu (Kenya) Osward Revelini (Tanzania) Samson Ramadhan(Tanzania)Christopher Isegwe (Tanzania) David Kiplagat (Kenya) na wengine wengi.
Kaka huyo Rukia Mtingwa nitapataje kontak zake huyo?
ReplyDeleteMe huwa ananiuwa sana huyo!
Bi Rukia hujambo? Pole sana kwa kazi.
ReplyDeleteKwa hakika ina tia moyo sana kuona kuwa hata katika miji yetu nyumbani, watu wanapata muda wa kufanya michezo. Huwa inaniuma sana kuona wenzetu wanafanya sana michezo katika miji yao, huku nje ya nchi, lakini home hakuna unalosikia zaidi ya matatizo na shida za kila siku tu. Hongereni sana kwa kuliona hili. Mimi niko pamoja nanyi, muda si mrefu insh nitajiunga nanyi, tutashauriana na kuboresha zaidi, michezo kama hiyo isifanyike Dsm tu, bali hata mikoani, Mwanza, Tanga, Songea, Pemba nk, najua watu wanapenda ni swala la mikakati tu na kuwapa nguvu. Hii itasaidia sana kuwapunguzia watu muda wa kuwaza mambo magumu muda wote. Hongereni sana wote mnaohusika na kamati za maandalizi hayo, Hongera sana mzee Nyambui.
ReplyDeleteMdau
rukia hali yako dada. mzima wa afya. salamu tu dada katika kujuliana hali.
ReplyDelete