Home
Unlabelled
gazeti la kwanza jamii mitaani leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
kamanda naona sasa umechoka unatuletea gazti linaloanza na MAJUNGU?il kumbuka kamati ya DR slaaa wajumbe wote ni wabunge wa C C M
ReplyDeleteHili gazeti katika kila toleo lake ukurasa wa mbele na habari kuu ni kuhusu Bunge na Wabunge.
ReplyDeleteHalafu hakuna kitu kama Kamati ya Dk Slaa kuna Kamati Ya Bunge.
Pathetic, gazeti limejaa waandishi waliobobea na maprofesa kibao lakini linaandika MICHAPO na MIPASHO.
Ah kumbe hili rigazeti naro ni ra CCM na majungu?
ReplyDeleteVipi tena Mjengwa? Si tulijua unaleta kitu cha uhakika.
Jamani huu ugonjwa wa tamaa si ugonjwa wa chama wala wa Tanzania. Kuna kashfa inauguruma ya wabunge wa Uingereza hivi sasa- ambayo imewakumba wabunge wote- si mawaziri, si wabunge wa chama tawala si wa upinzani ambao wote wamedhihirika kuwa na madai ya kilafi na ya kifisadi ya allowances. Ni binadamu wachache sana ambao wnaoweza kuwa na nidhamu ya kutosheka na kutojilimbikizia mali isisvyohalali wanapopata madaraka.Hivyo tunachohitaji ni sheriamna taratibu zinazobana na kuminimise ulafi.Hata Slaa ni binaadamu kama sisi tu; na hatua ya kwanza ya kuwa na tartibu zinazofaa ni kuachana na tabia ya woga na tabia ya kutukuza binadam mwenzako!
ReplyDeleteKweli vita ya ufisadi sasa imekuwa capitalised. Yaani jamaa kaacha kuandikia gazeti wa watu makini la raiamwema na kuanzisha gazeti la majungu. Aaaaah! ama kweli 2010 imekaribia wenyewe wanasema wakati wa mavuna ila ukiwa umepanda mapema kama vile kuanzisha gazeti n.k.
ReplyDeleteMjengwa,gazeti hilo ni la mafisadi tu.Wewe mwaka mmoja tu uliopita ulichangisha pesa za kununua kamera-mtaji wa kuanzisha gazeti umetoka wapi?
ReplyDeleteMheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya
ReplyDeleteNikiwa ni mmoja wa hao maprofesa wanaoandika kwenye gazeti hili, la "Kwanza Jamii," nimevunjika mbavu kusikia nimo katika orodha ya mafisadi. Kweli Bongo tambarare :-)
Ninapenda kuandika katika gazeti hili na nitaendelea. Baada ya kuandika makala ya kwanza, nilipata taarifa kutoka kijijini kwangu kuwa wanakijiji wameichangamkia makala ile na wanataka niendelee kuandika. Nitafanya hivyo.
Nafurahi kupata fursa ya kuwasiliana na wananchi vijijini, maana gazeti hili linajitahidi kufika huko. Kwangu mimi kama profesa wa kiIngereza hapa Marekani, kuandika katika gazeti hili ni changamoto ya kujipima uwezo wangu wa kuandika kiSwahili. Ni muhimu kufanya hivyo, kwani wasomi wengi tunajisahau kwa hilo, na hata viongozi wetu wengi hawaonyeshi mfano wa kutumia kiSwahili ipasavyo. Kwa upande wangu, kuandika katika gazeti hili ni namna ya kujifunza na kuwajibika.
Wanaotaka maandishi yangu katika taaluma ninazoshughulika nazo katika utafiti na ufundishaji, wanaweza kutafuta makala zangu na vitabu, ambavyo taarifa zake ni rahisi kupatikana huko mtandaoni.
Mkuu wa Wilaya ya Tegeta.
ReplyDeleteNaomba usibane hii comment.
Kuna kundi fulani la watu limejivika ukamanda wa kupambana na ufisadi na lina mtanado mzuri ila nalo ni la kifisadi.
Wanachofanya ni kuhakikisha wale wote ambao wana fikra tofauti au ukweli tofauti kwenye vita hii wana wasupress kwa majina mbali mbali mabaya.
Na ubaya zaidi ni kwamba hao Mabosi wao wakifanya ufisadi watatafuta njia ya kuwasafisha na hawataki waguswe au kusemwa.
Kwanza jamii msikatishwe tamaa na hao watu, sisi wananchi wa kawaida tunahitaji habari nyingi iwezekanavyo na za kila aina ili tuweze kujua chuya na mhele ni upi
Aisee sasa ndiyo nimejua mengi kweli hii blog ya jamii. Kumbe huyu Mbele ni profesa wa kiingereza marekani?, Mi nilijua yupo pale UDSM kwenye vichwa vya kinoko maana pale ili upate u prof ni lazima uwe unakaribia kustaafu.
ReplyDeleteMarekani wao mtu ukiwa unafundisha hata ka chuo ka ufundi tu unaitwa profesa yaani ni kama Bongo tunavyowaita walimu wa shule za msingi.
HUYU SLAA NI MNAFIKI SANA ANAGEUKA GEUKA RANGI KAMA KINYONGA MAANA YEYE AKIKATIWA KITU KIDOGO NA MAFISADI ANAANZA KUONGEA PUMBA ZAKE
ReplyDelete