JK akiwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Barak Obama wa Marekani White House.
JK akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyere jijini Dar es salaam kumpokea wakati aliporejea nchini akitoka Marekani leo.Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein na kushoto ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

JK amerejea nyumbani mchana wa leo- Jumatatu, Mei 25, 2009- baada ya ziara yenye mafanikio ya kikazi ya siku nane katika Marekani.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam, Rais Kikwete amelakiwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine wa Serikali.
JK na ujumbe wake alianzia ziara yake mjini San Francisco ambako alikutana na kuzungumza na Rais wa Chuo Kikuu maarufu cha Stanford, na kutembelea Silicon Valley, eneo maarufu zaidi duniani kwa shughuli za teknolojia ya kompyuta duniani.
Miongoni mwa makampuni makubwa ambayo Rais alitembelea katika eneo hilo ni CISCO, Google na IMB ambako alisisitiza shabaha ya Serikali yake ya kuifanya teknolojia ya kompyuta moja ya ngome kuu za maendeleo ya Tanzania.
Baadaye Rais alikwenda mjini Los Angeles ambako miongoni mwa mambo mengine alitunukiwa tuzo maalum la maendeleo ya afya na taasisi ya madaktari ya US Doctors for Africa.Rais Kikwete alikuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kupewa tuzo hilo kwa sababu ya mchango wake katika maendeleo ya huduma za afya katika Tanzania na Afrika.
Kilele cha ziara hiyo kilikuwa mjini Washington D.C. ambako alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Marekani, Barack Obama na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mama Hillary Clinton.
Mazungumzo kati ya JK na Rais Obama yalichukua muda wa saa moja katika Ofisi ya Rais wa Marekani ya Oval Office, na Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kualikwa ili kumtembelea na kufanya mazungumzo na Obama, tokea kiongozi huyo achukue uongozi wa Marekani Januari, mwaka huu.
Mjini Washington, JK pia alikutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Dominique Strauss Kahn, na viongozi wa taasisi nyingine muhimu kwa maendeleo ya Tanzania ikiwemo MCC na USAID.
JK pia alitembelea hospitali maarufu ya kijeshi ya utafiti ya Marekani ya Walter Reed pamoja na makumbusho ya Taifa ya kijeshi hapo hapo Washington. Katika hospitali hiyo aliweza kujiuonea shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kitengo cha huduma kwa majeruhi wa kivita, na kitengo cha utafiti wa magonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2009

    Kwanza napongeza kama kwweli unasafiri kwa ajili ya kufuatilia mambo muhimu yanchi.Ila ni kama ni kutalii tu ndugu rais,kwa style hiyo tumechoka.Watanzania sio wajinga sasa.Kuna mambo mazito sana ndani ya nchi hayajatekelezwa.Tuangalie umuhimu wa safari za rais sasa.Rais anatumia pesa zetu za kodi kutembea kwa hiyo tunahitaji kuuliza.na watanzania wenzangu tuamke na tushutumu kuhusu hizo safari za rais.Viongozi wajue leo leo umeshika madaraka lakini ujue tutakushitaki kesho kuhusu matumizi mabaya ya pesa za serikali.tokea mwaka jana na hadi mwaka huu huyu rais wetu amekwenda huko zaidi ya mara tatu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2009

    NI SAFARI YA MAFANIKIO MAKUBWA MKUU WETU JK TUNATAKA TUWE NA TEKNOLOJIA KAMA INDIA.

    UMEKULA ZALI KUBWA KUWA RAIS WA KWANZA MWAFRIKA KUKUTANA NA OBAMA,HILI LINAUMA SANA WATU WA KUJA.

    KWANI WALIKUWA WANASEMA KUWA JK HATAWEZA SIASA ZA KIMATAIFA.

    SASA ANAUNGANISHA KILA KONA WAO ROHO ZINAUMA KINA MWANAKIJIJI AU BENEDICT MWAKYANJALA WANAKESHA KWENYE JAMII FORUMS KUMLANI OOH JK ANASAFIRI SANA MLITAKA AKAE NYUMBANI?NA PINDA ANAFANYA KAZI GANI?

    MKUTANO KAMA HUU NI RAIS RAIS AENDE KUWEKA MAMBO SAWA.

    MWENYEZI MUNGU ATAKULINDA JK KUNA GENGE LA WATU WANAKUCHUKIA KWA VILE WEWE NI MUISLAM NA MTU WA PWANI WALITAKA RAIS ATOKE KANISANI KILA SIKU.

    DUA ZETU ZIKO KWAKO HAWA WATU WANAMCHUKIA HATA MICHUZI?
    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2009

    Swali.
    Hivi kuna umuhimu gani wa viongozi kuacha kazi zao na kwenda kumpokea rais airport? Kama wanataka kumuona si waende ikulu baada ya kazi? Nchi za wenzetu waliondelea mbona hawafanyi mchezo huu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2009

    mtalii karibu nyumbani. enhe tuambie baada ya marekani wapi tena???

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2009

    HILI SWALA LAHAWA VIONGOZI KURUNDIKANA AIRPORT TUTAONGEA MPAKA JK ATANGAZE KULISAWAZISHA.TUMECHOKA BAADA YA HAPO TUNASIMAMISHWA BARABARANI MASAA KADHAA ILI WAPITE.HUU NI UPUMBAVU TUTAELIMIKA LINI?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2009

    Nilishawahi kulisema hili na nitalisema tena. Kwa nini Rais akirejea kutoka kwenye ziara za ughaibuni mpaka apokelewe na utitiri wa viongozi wa ngazi za juu serikalini? Kwani hajui njia ya kufika Ikulu? Hili ni jambo ambalo ingekuwa vema tuige mfano wa tunaowaita wenzetu. Tunapoteza sio tu muda wa viongozi wakuu wa serikali bali pia wa wananchi wa kawaida wanaoumizwa na foleni za barabarani zinazosababishwa na utitiri wa misafara.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2009

    NI WIVU TU HAMNA KINGINE HIVI SASA TANZANIA INAJULIKANA DUNIANI.

    ASANTE JK KAZA BUTI USIWASIKILIZE HAWA WAPINZANI.WALITAKA WAO NDIO WAWE WA KWANZA KWENDA WHITE HOUSE.JIPANGE MWANANGU WAMEKUKALIA VIBAYA.
    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2009

    natoa wito kwa vyombo vya habari kuacha kuchapisha habari na picha za viongozi wanaopanga foleni uwanja wa ndege eti 'kumlaki' rais akitoka nje ya nchi. hii itasaidia kuondokana na utaratibu huu usio na mafanikio. kwani baada ya hapo hamfanyi vikao vya kuhabarishana ikulu bila kamera? inakera sana, mibaba mizima kujinafikisha.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2009

    nimesoma kwa makini mizunguko aliyofanya rais wetu. ni mategemeo yetu kwamba safari zijazo zitafanywa na wajumbe wa baraza la mawaziri.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2009

    Hili la viongozi kulundikana airport limeambukizwa hata mikoani na mawilayani. Rais/Waziri Mkuu/Waziri akienda huko basi msafara wa magari unatisha na shughuli zingine zote zinasimama. Sijui ni kujikomba au ndo utaratibu?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 26, 2009

    KWANINI UYU JK ASIWEKE UWANJA WA NDEGE NYUMA YA NYUMBA YAKE KAMA OBAMA,BADALA YA KUTUGANDISHA TU BARABARANI.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2009

    kuna jamaa hapo anaitwa Dr.Lawrence Summers. huyu hapo amebeba faili jekundu. ni mmoja kati ya wachumi waliobobea na alikuwa waziri wa fedha wakati wa Clinton.

    kwa kweli Kikwete alichemsha sana kwenda na yale makaratasi yake mbele ya mijitu yenye bongo kama Obama na Dr.Summers.

    Michuzi unadai mkutano ulifanyika Oval Office, mbona picha hazionyeshi hivyo?

    kama Raisi anataka Tanzania iongoze katika Teknolojia anachopaswa ni kufungua vyuo vikuu vya Teknolojia(Institute of Technology) kwa kufuata mfano wa India.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 26, 2009

    KWANZA, VIONGOZI WANA HAKI YA KUPOKEA KIONGOZI MKUU ,NA PIA NDIO NJIA MOJA WAPO YA KUKUTANA NA KUELEZANA AGENDA ZINAZOHUSU NCHI KWA JUMLA.
    PILI,HONGERA RAIS KIKWETE ENDELEA KUSAFIRI KWA MANUFAA YA KULETA MAENDELEO,KWASABABU WANANCHI HAWAFANYI KAZI NA SIO WABUNIFU ,KWAHIYO RAIS HAWEZI KUKAA IKULU KUTOKANA MNAWEZA KUFA KWA NJAA,NDIO MAANA ANATOKA KWENDA KUATAFUTIA CHAKULA.TATU,CHUKI,MALALAMIKO,UCHOYO,UKABILA,UDINI,NDIO MACHUNGU YA MTU MJINGA NDIO MAANA HAMKUPEWA NYINYI KAPEWA RAIS KIKWETE KWASABABU NI MTU MWENYE ROHO NZURI, HURUMA,ANAJA,MCHAPA KAZI.

    ReplyDelete
  14. Michuzi, kwenye hiyo picha ya mapokezi ya Rais, hao Shein na Pinda tunawajua. Weka caption ya huyo anaesalimiana na Rais, na hao wadau wengine.

    Michuzi wewe mpiga picha wa wapi wewe hujui kwamba caption haiendani na mwenye cheo kwenye picha?

    ReplyDelete
  15. kaka karibu jumbani na kwa hakika ukoa bize sana lakini majumuhisho kama hayo tusingeyapata kama balozi asingukuwa kenye msafara wa jk sas wewe kule jf ulitaka faida zaidi hii kutoka kwa balozi wa Tegeta wa nyumba kumi tuwe wakweli tuache kukurupuka,Nanyi mnao sema jk anasafiri sana kuna vitu vingine lazima aende na ukizingatia uchagua huo waja lazima ajizatiti mafisadi nao wanamipango yao ni hayo tu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 26, 2009

    SHABAHA YA SERIKALI YAKE NI KUIFANYA TEKINOLOJIA YA KOMPYUTA MOJA YA NGOME KUU ZA MAENDELEO TANZANIA; HUU NI USANII NA KUIJENGEA HOJA ZIARA YA WIKI NZIMA MAREKANI! KOMPYUTA HAZIJAINGIA LEO TANZANIA, MITAANI WATU WANAZITUMIA SANA LAKINI CHA AJABU SERIKALINI KOMPYUTA ZINAONEKANA BALAA, PALIPOANZISHWA MITANDAO LEO HII IMETELEKEZWA NA KUBAKI YATIMA, MKAPA YEYE ALILETA UTANDAWAZI, SERIKALINI ULITELEKEZWA. MIMI NADHANI CHA MUHIMU BAADA YA KUREJEA ILIKUWA ATUELEZE ZIARA ITAKAYOFUATIA NI YA KWENDA JAPANI AU BURMA.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 26, 2009

    Watanzania fahamuni kwamba the way Obama anavyomuona JK sio kama vile tunavyoona sisi.

    Someni habari hapa ya AFP ambayo ni mtazamo wa kimarekani kuhusu kikao cha Obama na Kikwete.

    http://news.yahoo.com/s/afp/20090521/pl_afp/ustanzaniapoliticsobama

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 26, 2009

    ASSALAM ALLEYKUM WADAU..
    WEWE MDAU MSWAHILI 12:47, HAUKO SAWASAWA KICHWANI (UNA TATIZO KUBWA SANA, NA UNAHITAJI MSAADA). TOKA NIMEANZA KUBLOG SIJAONA MTU HOVYO KAMA WEWE. HIVI HII HABARI YA JK KUCHUKIWA KWANZA UMEITOA WAPI? HALAFU KAMA NI KWELI ANACHUKIWA, NANI KAKWAMBIA KUWA INAKUWA HIVYO KWA SABABU NI MWISLAM?? AU KWA SABABU KATOKA PWANI!!!!! NANI KAKWAMBIA KUWA WATANZANIA WAMESEMA WANATAKA RAISI TOKA KANISANI (CONNECTION IKO WAPI!!!URAISI NA KANISA/MSIKITI!!!)...ACHA UPUMBAVU CHANGIA KWA HOJA ZA MAANA NA TUONDOLEE UDINI NA UKABILA WAKO HAPA.. KATIKA NCHI HII KUNA UHURU WA KUJIELEZA. KAMA MTU ATAONA KUWA RAIS ANAKOSEA MAHALA FULANI ANA HAKI YA KUKEMEA KWA UWEZO WAKE (KUMBUKA SERIKALI INAENDESHWA KWA KODI ZA WANANCHI), NA KUNA MAMBO KIBAO AMBAYO HUHITAJI KUWA NA SHAHADA ZA CHUO KIKUU KUONA KUWA YANADORORA..SIKU NYINGINE TAFAKARI UNAYOTAKA KUYASEMA KABLA HUJAANZA KUBWATABWATA HAPA..

    Mdau Gordon, Deslam

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 26, 2009

    Maoni yaliyotolewa na huyo ndugu aliyehusisha issue ya trip za jk na udini yanachefua sana tena sana. watu wanamna hii huwa hawakosi chenye jamii hivyo naomba hayo maoni tuyachukulie kuwa ni ya mtu mgonjwa yaani mlemavu wa akili. watu wanamna hii kazi yao ni kuamsha tu hisia za udini kwakusudi la kupotosha hoja na kuficha ukweli wa mambo. Kumbuka mateso ya umasikini hayana dini wala kabila. tulimchagua jk tukiamini kuwa anajua kwa dhati shida na umasikini wa watanzania na kwamba ana nia, dhamila, utashi na uwezo wa kupambambana nao. sasa hii longo longo ya kuzunguka huku na huku na kupewe sifa za kitoto "eti raisi wa kwanza mweusi kukutana na obama" inasikitisha sana. Ukiwa mtu mzima ni shart uwaze kama mtu mzima. kumbuka miaka 10 sio mwisho wa dunia. itakwisha na atapata fedheha kama ya mkapa aliyoipata ya kuuza nchi kwa bei poa. mkapa hana nguvu ya kusimama hadharani kwa nguvu ya dhamiri yake kwasababu matendo yake yanamsuta. na huyu bwana mkubwa akitoka madarakani atakuwa mtu wa kudhalauliwa sana pengine kuliko mkapa.

    ni hatari kudanganywa na watu na wewe ukaukubali udanganyifu huo. lakini ni jambo la hatari zaidi mtu unapokuwa unajidanganya mwenyewe na kujifariji kuwa yuko sana. self deception haina msaada isipokuwa wa Mwenyezi Mungu. huyu ndugu yetu jk anajidanganya!!!!!!!!

    Rais ni sharti awaze kama Rais, afikiri kama rais, atafakari mambo kama rais na atoe maamuzi na kutenda kama rais. Rais anapotafuta ubishoo na sifa reja reja za "KITOT0" anakuwa ameudharirisha na kuishushia hadhi hiyo nafasi. Je,unajua kuwa hivi hata mwanafunzi wa sekondari naye ana waza kugombea urais? Kwanini anawaza hivyo? kwasababu the job is no longer demands responsibility and accountability!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 26, 2009

    mie kamwe siko tayari kupinga safari za rais nje ya Nchi huenda zina tija kwa taifa mie kinachoniuma ni ukubwa kwa msafara wa raisi tena hadi kwa watu ambao hakuna haja kabisa kuandamana nao!
    Imefika mahali tuambiwe hadi grarama zilizotumika na ni akina nani wametumia na tumepata nini katika safari hizo.
    kuna safari za ndani ambazo zingekuwa na tija sana kwa wananchi kuliko hizo ambazo kila kukicha zinalalamikiwa


    Mangi wa K'koo

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 26, 2009

    'CISCO, Google na IMB '
    Katika hizi kampuni, hii ya tatu hapa naona muanikaji amechapia.. i think inatakiwa iwe IBM !!!
    just a comment i thot of sharing.
    peace

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 26, 2009

    Anonymous wa 12:47 umekosea sana kusema JK watu wanamchukia kwa sababu yeye ni Muislamu.Huo ni u-dini unataka kuanzisha sasa!Kumbuka kuwa itikadi ya nchi hii haijajengwa na Uislamu au Ukristo bali Utanzania.Tafadhali sana nyie ndio mnaoleta matatizo kwa ku-comment vitu vitakavyoweza kuchafua amani ya nchi.Huu ndio ukweli,mbegu mnaipanda wenyewe halafu pale amani itakavyochafuka mnaanza kutafuta mchawi.Let us be realistic and reasonable tunapotoa comments.Mwalimu alifanikiwa sana kufuta haya mambo ya ukabila na udini - TUSIRUDI NYUMA NA KUANZA KUPANDA HIYO MBEGU TENA.

    Mdau - London

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 26, 2009

    Jamani hivi kweli kuna watanzania wana mawazo mgando kiasi hiki.Sikutegemea kwenye karne hii kuna mtu atakurupuka aseme eti Rais anaandamwa kwa kuwa ni muislam.Hivi katika nchi hii unaweza kuwa Rais kwa kuchaguliwa na Waislam peke yao? Katu siamini. Rais Kikwete ni Rais wa watanzania. Walio na dini na wasio na dini. Acheni ushamba wenu ninyi mujahidina kwani hakuna aliyewatuma mlete hizo. Kwa akili zenu fupi mnadhani watanzania ni mazuzu ambao watawachagua watu kwa kuangalia kabila lao, dini yao n.k Ingekuwa mawazo hayo wanayo watu wa bara kama mliyonayo wa Pwani Mh. John Momose Cheyo angekuwa Rais wa nchi hii kwa kuwa wanyamwezi na wasukuma wote wakimtaka Rais awe Cheyo uchaguzi ujao atakua. MUNGU ATUEPUSHE NA WATU WA AINA HII KWANI HERI MFE MTUACHIE TANZANIA YETU SALAMA. KIKWETE TUNAMPENDA KWA UWEZO WAKE WA KUONGOZA NA SI KWA DINI YAKE, KABILA LAKE, AU ANATOKA PWANI.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 26, 2009

    Anony wa tarehe 26 may, 12.47 sina imani na wewe kama kweli una elimu dunia... ingekuwa pakistani au somalia nisingepoteza muda kutafakari uelewa wako. nina wasiwasi na wewe endapo ukikaa kiti cha mbele siku kiongozi mkuu akiongea....


    Nondo

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 26, 2009

    TUNAKUSHUKURU KWA KURUDI SALAMA.HII TABIA YA KILA MTU KUJA AIRPORT KUPOKEA NDUGU ANAPOKUJA KUTOKA NJE AU KUSINDIKIZA NDUGU NAONA IMEFIKA MPAKA SERIKALINI.
    WEWE UNA WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA RAISI WOTE WAKO AIRPORT KUMPOKEA RAISI NANI ANAWATUMIKIA WANANCHI KWA WAKATI HUO? AU MATATIZO YA NCHI SIO MENGI KIASI CHA KWAMBA WOTE WAKUBWA WANAPATA MDA WA KWENDA KUMPOKEA RAISI? HII TABIA TUIACHE KWANI MDA HUO MCHACHE WAZIRI MKUU ANGEWEZA KWENDA KUKAGUA KAZI YOYOTE YA MAENDELEO YA TAIFA. NA PIA MSAFARA WOTE HUO NI KERO TU BARABARANI KWA RAIA WENYE KWENDA KUANGAIKIA FAMILIA ZAO.
    MDAU mzawa

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 26, 2009

    udini upo na ukabila upo mkubwa tizama TRA HUPATI KAZI HADI UWE MUSHI,TESHA,KIMARO,MUSHI,MBOWE,TARIMO.
    WACHUNGAJI WA KIKRISTU WALIKUWA WAKIANDIKA BARUA ZA KICHUNGAJI KUMFEDHEHESHA MZEE MWINYI WAKATI AKIWA RAIS.

    SOMENI KITABU CHA KANISA KATOLIKI NA SIASA TANZANIA KIMEANDIKWA NA PADRI SIVALON.

    NANI ANATAKA KUSEMA HAKUNA UDINI NA UKABILA?

    SHIRIKA LA BIMA LILIWAHI KUUNDIWA TUME KUTIZAMA UKABILA BAADA YA KUWA WATU WA MBEYA NDIO WANAOPATA AJIRA.

    JK ANAANDAMWA KWA CHUKI ZA KIDINI.

    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 26, 2009

    ANONY WA 12:47!!! We mtu wewe!!! he! am kweli!!. Hivi wewe ni mtu kabisaaa na kichwa unacho!! ubongo wako je vipi uko sawa?? mbona unaongea kama umekatwa kichwa?!!!
    siwezi kuongea mengi sababu wewe unahitaji muda mrefu sana kueleweshwa mambo!!! ha'fu unaonekana m-baguzi flani, wewe umeshamuona nani kaleta udini humu we vipi wewe??
    kwanza unahitaji maombi ya nguvu halafu ukishawekwa sawa kimaombi sasa utatakiwa kurudishwa darasani kwa miaka kama 13 hivi ili angalau basi uweze kuendana kimawazo na kiakili na kiuchambuzi na binadamu wenzako!!!
    Ndugu zanguni hebu msomeni vizuri maoni yake mtagundua ni kwa nini i'm like this!!
    eti Kazi ya rais ni kusafiri!!! eti ni lazima rais asafiri nje kwenda kutafuta chakula, eti rais ni kama baba hawezi kukaa nyumbani tu ni lazima atoke kusaka chakula ili watoto/wananchi wasilale njaa!!! eti rais akikaa tu nchini je na Pinda ana kazi gani!!! enhe!! mh kwa hiyo rais baba anatoka kusaka chakula na Pinda ni mama abaki kulea wana!! nikijaribu kuwa mjinga ka wewe basi hiyo ndio tafsiri nyepesi!!!
    HARAFU NDUGU YANGU PAMOJA NA KWAMBA UNAONESHA WAZI SHULE ULIIKIMBIA, MBONA UNA INFERIORITY COMPLEX KIASI HICHO??? ACHA HIYO INFERIORITY COMPLEX ITAKUFANYA UISHI MAISHA YA KUNUNG'UNIKA SIKU ZOTE!!! JARIBU KUJIAMINI!!! USHAURI WANGU TU KWAKO NI KWAMBA JARIBU KURUDI DARASANI KIDOGO ILI UPEO WAKO WA KUFIKIRI UBADILIKE!!!
    Mbona unaleta udini humu??? ni nani kamchambua kikwete kwa kuangalia dini yake??? unaweza kutukopia hata comment moja ya namna hiyo???? we vipi lakini ndugu mbona unataka kutusikitisha kiasi hicho??? je wewe umeoa?? una watoto??? sasa kama umeoa na una watoto siku mkeo akiona comment yako hiyo si ni aibu?. atajisikia vibaya kuona mumewe anaandika pumba mbele ya wasomi??? siku wanao wakiona hii comment si aibu???
    kwa taarifa yako kikwete si mtu mjinga. humu tunamchallenge hatumchallenge yeye pekee bali ni serikali yake yote sababu hata yeye ana washauri!! serikali yake ni ya dini zote kwa hiyo wenzako kwenye udini hatuko!! siku kikwete akiona hizi comment ataona kuwa zile zinazomchallenge ndio zenye maana na hiyo yako isiyo na pointi yoyote zaidi ya kujaa udini ataidharau sana sababu yeye mwenzako darasa kalipiga!!!!
    nakushauri usiwe unarukiarukia discussions tu humu utaumbuka. Kwa upeo wako nadhani kabla ya kutoa maoni yako humu ni vema ukaprinti maoni yooote uende nayo nyumbani kwako uyasome kwa umakini, kisha tumia kama wiki tatu hivi na wewe kuandika komenti yako, ukimaliza kuiandika jaribu kuwapa watu wengine hasa wanaokuzi upeo waambie hiyo ndo komenti yako unataka kuipeleka michuzi blog. waache waipitie, wao watatumia kama dakika moja tu kuisoma kuielewa na kuisahihisha kisha watakushauri kama uilete au la!!! tatizo moja utakalo kumbana nalo baada ya hizo wiki tatu za kuandaa michuzi blog comment yako ni kwamba ukija kutaka kuipost sasa utakuta hiyo ajenda ilishasahauliwa zamani sana na hata haipo kwa hiyo itabidi ukae nayo mwenyewe au ukaipublish magazetini hiyo komenti.
    maoni yangu ni kwamba unahitaji kuombewa kisha kurudishwa darasani la sivyo mkeo na wanao kazi wanayo!!!!
    Ahsante
    MACMUGA

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 26, 2009

    Mdau wa 8:02AM nakushukuru kwa kutuwezesha kupata mtazamo wa upande wa waandishi wa marekani.kwani watanzania tumezoea kusifia kila kitu hata tusichokijuwa.mimi binafsi sioni ushawishi wa kikwete kwa jumuiya au nchi za kiislamu hat kama yeye ni muislam.kwa hiyo hiyo hoja ya muandishi haina uzito.pia sioni manufaa ya hizi safari toka enzi za clinton,bush wote tumeona vyandarua tu, lakini watoto msingi wanafanya mitihani chini tena jijini dar es salaam!hivi hizo pesa au misaada ya mcc ni kununulia mashangigi tu? bora akae ahimize kilimo tuwatumie waatalam wetu sua kwa ufanisi kuliko huo uomaomba usio na tija kwa maskini wa kawaida.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 26, 2009

    BIG UP KWA JK jinsi unavyopata international recognition so is our country na watu wake,jamani mtake msitake JK yuko juu,

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 26, 2009

    nyerere alijaza watu wa musoma jeshini na wakuu wa jeshi.

    ukabila upo na udini.someni kitabu cha untold history of the muslims of Tanzania struglled against british colony au life and times of Abdulwahid sykes.

    au someni uamuzi wa busara 1958 kinapatikana madukani mjue udini na ukabila.

    CRDB hupati kazi kama sio mchagga.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 26, 2009

    Tanzania, many complain, is a “slow” or even “terrible” place to do business—and “ungrateful” for foreign aid or investment. Even its boosters admit it is wrapped in red tape and lacks skilled workers. Almost everyone says Mr Kikwete is spending too much time burnishing Tanzania’s image abroad and not enough fixing problems at home. Last year he chaired the African Union.
    For full article go to:
    http://www.economist.com/search/search.cfm?rv=2&qr=kikwete&area=1

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 27, 2009

    UKWELI UNAUMA.
    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...