katibu mkuu wa zamani wa simba sc.  kassim dewji aongea na globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    sasa hapo ungemuhoji Madega ungesikia utumbo wake..!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    Ni digrii gani mtu anasoma ili awe Mbunge, Raisi? Hatuhitaji hao wawe na Diploma fulani isiyo "Diploma in Ubunge?"

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 12, 2009

    ka-telefoni nakubaliana na wewe kuhusu makundi uliyoyataja katika heka heka za kuongoza soka. ila natofautiana na wewe unaposema digirii hazitasaidia. soka ya sasa ni soka ya kisayansi zaidi, kwa maana hiyo huwezi kabisa kutenganisha soka na shule kwa kipindi hiki (iwe kwa wachezaji hata viongozi, TUSIDANGANYANE HAPA) labda enzi za Mwalimu..!! Ukipata kiongozi wa mpira ambaye kawahi kucheza mpira, amepata exposure (samahani wadau, sijui kiswahili sanifu kwa neno hili. nisaidieni) halafu na shule hakuikimbia ni faida ya ziada. Halafu mshkaji naona kama unajipigia debe flani hivi...kwani uchaguzi simba lini??
    Mdau, Gordon Chiggs. DESLAM

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 12, 2009

    Nimefatilia kwa kina mazungumzo katika ya nd. michuzi na Katibu mkuu wa zamani wa Simba. Mimi si mpenzi sana wa mpira wa miguu hasa hapo Tanzania, lakini kwa kiasi fulani hufuatilia baadhi ya matukio muhimu ya michezo kwa ujumla yanayotokea Tanzania. Ndugu Kassim ametaja makundi matatu ya uongozi yaliyojitokeza katika soka la Tanzania. Aidha, mtazamo wake haoni umuhimu kwa soka la Tanzania kuendeshwa na wasomi[Hapendi soka la tanzania liendeshwe kidigrii]. Kama nitakuwa sahihi alisitiza kuwa hajawahi kusikia chuo chochote kinachotoa uongozi wa mpira wa miguu.Kwanza napenda niseme kwa heshima zote kwamba nayathamini mawazo na michango mbali mbali ambayo ameyatoa kwa madhumuni ya kuendesha soka la Tanzania kisasa na kifaida. Ninajua ulimwengu huu wa karne ya 21 ni hoja kwa hoja na yoyote anayekataa hoja labda ni mchawi.

    Tukirudi nyumba kwenye umuhimu wa wasomi katika kuliendesha soka la Tanzania ambalo kwa kweli limedorora, mimi binafsi natafautiana na rafiki yangu Dewji. Ninaamini kuwa elimu ni jambo la msingi katika kuliongoza soka. Ingawa sina ushahidi wa chuo gani kinatoa shahada inayohusiana na mpira wa miguu peke yake, lakini ninauhakika kuna vyuo vingi nje ya Tanzania vinavyotoa shahada ya uongozi katika fani za michezo. Miongoni mwa vyuo hivyo ni kile kilichopo Uk kinachoitwa University of Central lacanshire. Ni ukweli usiofichika kwamba tunaweza kuendesha soka kwa kubahatisha na tunafanikiwa kama ilivyotokea katika miaka ya nyuma aliyoyataja. Lakini moja ya tatizo la kubahatisha ni kutokuwepo uendelevu wa kile kinachofanyika. katika soka kuna mambo mengi kama vile sera na mikakati ambayo haya yote yanahitajika kuwepo ili iunganishe raslimali michezo iliyopo nchini ambayo kwa kweli nasikitika ya kwamba bado imezagaa na haijatumiwa ipasavyo. Bila ya taaluma ni ngumu na tutabakia tunabahatisha na kulaumiana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2009

    hebu niambie hapo wapi nami nikajichane mahanjumati? jamani naomba mnisaidie

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 12, 2009

    the african brother is deep.respect

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 12, 2009

    ukitoka hapo kawahoji na wengine sio kupendelea ngozi nyeupe tuu ok.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2009

    Michuzi ulifuata juice baridi hapo? Hahaha... Ungempa mfano wa Sir. Tenga ambaye amesoma na pia amecheza mpira na ameweza kuongoza mpira kwa kiasi kikubwa. Simba bwana utawajua tu na pumba zao hapo anapiga kampeni amuondoe tenga.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2009

    Hivi Dewji kweli kama huamini wasomi wanaweza kuendesha mpira kwa mafanikio, bado unajiita kuwa na wewe ni sehemu ya wadau wa mpira?
    Dhamira yako haioneshi kuwa uko tayari kupokea mabadiliko katika uongozi wa mpira, kwa maana hiyo endapo utapa nafasi ya uongozi hutaweza kutoa ushirikiano wa kutosha.
    Naomba nikupe ushauri, ni vema uwe na diplomasi ya kuongea na public kwani sasa hivi inawezekana viongozi kama wewe ndiyo mlikuwa mnaleta vurugu katika mpira wa miguu. Na hii inawezekana kuwa kweli kwani tangu TFF iliposafishwa na vilabu kwa kiasi fulani havina vurugu kama ilivyokuwa huko nyuma.
    Sasa hivi tunahitaji viongozi wenye vision nzuri na waliokwenda shule ambao wataweza kuweka malengo na kupanga mikakati ya kuweza kufanikisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...