katibu mkuu wa zamani wa simba sc. kassim dewji aongea na globu ya jamii
Home
Unlabelled
kassim dewji aongea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
sasa hapo ungemuhoji Madega ungesikia utumbo wake..!
ReplyDeleteNi digrii gani mtu anasoma ili awe Mbunge, Raisi? Hatuhitaji hao wawe na Diploma fulani isiyo "Diploma in Ubunge?"
ReplyDeleteka-telefoni nakubaliana na wewe kuhusu makundi uliyoyataja katika heka heka za kuongoza soka. ila natofautiana na wewe unaposema digirii hazitasaidia. soka ya sasa ni soka ya kisayansi zaidi, kwa maana hiyo huwezi kabisa kutenganisha soka na shule kwa kipindi hiki (iwe kwa wachezaji hata viongozi, TUSIDANGANYANE HAPA) labda enzi za Mwalimu..!! Ukipata kiongozi wa mpira ambaye kawahi kucheza mpira, amepata exposure (samahani wadau, sijui kiswahili sanifu kwa neno hili. nisaidieni) halafu na shule hakuikimbia ni faida ya ziada. Halafu mshkaji naona kama unajipigia debe flani hivi...kwani uchaguzi simba lini??
ReplyDeleteMdau, Gordon Chiggs. DESLAM
Nimefatilia kwa kina mazungumzo katika ya nd. michuzi na Katibu mkuu wa zamani wa Simba. Mimi si mpenzi sana wa mpira wa miguu hasa hapo Tanzania, lakini kwa kiasi fulani hufuatilia baadhi ya matukio muhimu ya michezo kwa ujumla yanayotokea Tanzania. Ndugu Kassim ametaja makundi matatu ya uongozi yaliyojitokeza katika soka la Tanzania. Aidha, mtazamo wake haoni umuhimu kwa soka la Tanzania kuendeshwa na wasomi[Hapendi soka la tanzania liendeshwe kidigrii]. Kama nitakuwa sahihi alisitiza kuwa hajawahi kusikia chuo chochote kinachotoa uongozi wa mpira wa miguu.Kwanza napenda niseme kwa heshima zote kwamba nayathamini mawazo na michango mbali mbali ambayo ameyatoa kwa madhumuni ya kuendesha soka la Tanzania kisasa na kifaida. Ninajua ulimwengu huu wa karne ya 21 ni hoja kwa hoja na yoyote anayekataa hoja labda ni mchawi.
ReplyDeleteTukirudi nyumba kwenye umuhimu wa wasomi katika kuliendesha soka la Tanzania ambalo kwa kweli limedorora, mimi binafsi natafautiana na rafiki yangu Dewji. Ninaamini kuwa elimu ni jambo la msingi katika kuliongoza soka. Ingawa sina ushahidi wa chuo gani kinatoa shahada inayohusiana na mpira wa miguu peke yake, lakini ninauhakika kuna vyuo vingi nje ya Tanzania vinavyotoa shahada ya uongozi katika fani za michezo. Miongoni mwa vyuo hivyo ni kile kilichopo Uk kinachoitwa University of Central lacanshire. Ni ukweli usiofichika kwamba tunaweza kuendesha soka kwa kubahatisha na tunafanikiwa kama ilivyotokea katika miaka ya nyuma aliyoyataja. Lakini moja ya tatizo la kubahatisha ni kutokuwepo uendelevu wa kile kinachofanyika. katika soka kuna mambo mengi kama vile sera na mikakati ambayo haya yote yanahitajika kuwepo ili iunganishe raslimali michezo iliyopo nchini ambayo kwa kweli nasikitika ya kwamba bado imezagaa na haijatumiwa ipasavyo. Bila ya taaluma ni ngumu na tutabakia tunabahatisha na kulaumiana.
hebu niambie hapo wapi nami nikajichane mahanjumati? jamani naomba mnisaidie
ReplyDeletethe african brother is deep.respect
ReplyDeleteukitoka hapo kawahoji na wengine sio kupendelea ngozi nyeupe tuu ok.
ReplyDeleteMichuzi ulifuata juice baridi hapo? Hahaha... Ungempa mfano wa Sir. Tenga ambaye amesoma na pia amecheza mpira na ameweza kuongoza mpira kwa kiasi kikubwa. Simba bwana utawajua tu na pumba zao hapo anapiga kampeni amuondoe tenga.
ReplyDeleteHivi Dewji kweli kama huamini wasomi wanaweza kuendesha mpira kwa mafanikio, bado unajiita kuwa na wewe ni sehemu ya wadau wa mpira?
ReplyDeleteDhamira yako haioneshi kuwa uko tayari kupokea mabadiliko katika uongozi wa mpira, kwa maana hiyo endapo utapa nafasi ya uongozi hutaweza kutoa ushirikiano wa kutosha.
Naomba nikupe ushauri, ni vema uwe na diplomasi ya kuongea na public kwani sasa hivi inawezekana viongozi kama wewe ndiyo mlikuwa mnaleta vurugu katika mpira wa miguu. Na hii inawezekana kuwa kweli kwani tangu TFF iliposafishwa na vilabu kwa kiasi fulani havina vurugu kama ilivyokuwa huko nyuma.
Sasa hivi tunahitaji viongozi wenye vision nzuri na waliokwenda shule ambao wataweza kuweka malengo na kupanga mikakati ya kuweza kufanikisha.