katibu mkuu wa shirikisho la soka (tff) frederick mwakalebela akitoa mada wakati wa semina elekezi ya waandishi wa habari ya kombe la taifa cup ambalo limeanza wikiendi hii.

leo bingwa mtetezi, mkoa wa kimpira wa ilala, itamenyana na timu ya mkoa wa iringa (ruaha stars) uwanja wa sokoine, mbeya. kwenye gemu la ufunguzi juzi ilala waliwatungua mapinduzi stars ya mbeya bao 1-0 huko huko mbeya.
iringa, ambao walianza michuano kwa ushindi wa bao 2-1 dhiri ya mkoa wa rukwa (pinda boyz), leo itacheza na mbeya.
kundi la kwanza lina mkoa wa mtwara ambao walishinda mabao 1-0 dhidi ya lindi kwenye uwanja wa ilulu, mjini lindi. mtwara leo inakwaana na ruvuma ambayo ilianza kwa sare ya 1-1 na timu ya mkoa wa temeke. Lindi watakipiga na temeke kwenye mchezo wao wa pili leo.
mji kasoro bnahari a.k.a morogoro, ambao walianza vyema kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya singida 'kindai shooting stars', leo itacheza na tabora ambayo katika fungua dimba waliifunga dodoma mabao 2-1.
mwanza heroes ilianza kwa ushindi wa bao 2-2 dhidi ya kagera, na leo inakipiga na shinyanga wana igembesabo. gemu lingine huko mwanza ni kati ya manyara na kilimanjaro.
kundi la sita lilianza kwa wenyeji tanga kuinyuka pwani bao 3-0 na leo itakutana na kinondoni ambao wanacheza mchezo wao wa kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2009

    Balozi Mithupu heshima kwako.
    Globu hii ya jamii nadhani inaweza kufikisha ujumbe huu kwa wausika.
    Balozi! hii inahusu TBC. Kuna bwana mmoja anaitwa Pendaeli Omari nadhani ni mhariri wa michezo TBC, sijajua utaratibu wa kuandaa habari kama mtangazi ndio anaandaa au kuna jopo la wahariri. Habari za michezo zinaposomwa na Pendaheli yani zile highlights mpaka unafurahi lkn wengine wanasoma habari hawaonyeshi picha mpaka wanaboa. Nimekuandikia kwanza umpe shavu mdau Pendaheli Omari pili ujumbe ufike kwa Mh Tido nadhani kwa wale wanaotizima habari TBC hasa za michezo wataniunga mkono kama si mguu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2009

    Yaani Tanzania watu wanakula mishikaki mpaka wanatanuka hivyo!na ufupi huo si ndio noma.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2009

    DAAA WE MWAKALEBELA NINI HICHO KWAMBA TFF MAMBO SAFI AU NI URAFIIII UNAKUWA KAMA DADA ZAKO WA TUKUYA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...