Ndiyo mkuu wa wilaya ya nanihii,
natumai unaendeleza libeneke kama kawaida.Mimi ni mmoja ya mwafuatiaji wa taarifa mbalimbali kwenye hii blog ya watu nikiwa nimetulia zangu vekesheni.
Nimekuwa pia nikifuatilia maada kuhusu mvutano kwa watani zetu (Kenya) kuhusu kisiwa cha Migingo. Kwa kifupi sijui kama Kenya ndiyo mmiliki halali wa hiki kisiwa au la kulingana na mpaka unaotambulika kimataifa.
Lakini kitu ambacho kinaninya raha nikuona kuwa, mpaka kati ya Tanzania na Malawi haupo au hautambuliki kimataifa, na cha kuhuzunisha zaidi mpaka usio rasmi unaonyesha kuwa mpaka ni ziwa nyasa kwa upande wa tanzania, ina maana ukikanya tu maji ya ziwa nyasa , utakuwa umeingia Malawi kinyume cha sheria.
Katika kumbukumbu zangu, maada hii ilishafikishwa Bungeni na Mh Zitto Kabwe kama sikosei, lakini sikumbuki kama ilitolewa majibu ya kuridhisha. kwahiyo basi, nakuomba mkuu wa nanihii uweke maada kuhusu hili suala ili wadau mbalimbali waweze kuchangia hii mawazo.
Zaidi ya yote nakutakia tu kazi njema ya kuendeleza libeneke na vekesheni
mdau Richard

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2009

    WANDUGU ZANGU BONGO TAMBARARE HII INAJADILIWA HAPA. HEBU BONYEZA UONE MWENYWE KUHUSU HILI SWALA LA MPAKA. WATAALAMU WAMEJADILI SANA HAPA JAMII FORUM. CHUKUA HII LINKI
    http://jamiiforum.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2009

    wewe hapo juu sio mashindano,eti nani wakwanza kujadili.ndio yale ya JK Rais wa kwanza Africa kukutana na Obama SO WHAT?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2009

    ANGALIA RAMANI,MPAKA WA TANZANIA SIYO ZIWA NO NO ANGALIA RAMANI VIZURI INGAWA NI KWELI HATA BANDA MWAKA KAMA SIKOSEI 1969 AU 1970 ALIWAHI KUSEMA MBEYA MPAKA NJOMBE ILIKUWA SEHEMU YA MALAWI

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 29, 2009

    HUYU MHEIMIWA ANAYELALAMIKIA MPAKA INAELEKEA NI MMOJA WA WALE WASIOSIKILIZA HABARI AMA KUSOMA MAGAZETI, YEYE NI BONGO FLAVA KILA KUKICHA, VINGINEVYO ANGEJUA NINI KINACHOENDELEA KATI YA SERIKALI ZA TANZANIA NA MALAWI. HATA HIVYO WAKAZI WENGI WA KYELA WANAFAIDIKA ZAIDI KWA BIASHARA NA ELIMU WANAYOPATA BURE UPANDE WA MALAWI.

    ReplyDelete
  5. Mdau, umanganiMay 29, 2009

    Mkuu wa nanihii, long time hujatuletea bei za madafu kwa hela za kigeni, maana wiki ijayo Inshaallah ntakuwa bongo hivo nataka nijue hizi nilizonazo ntapata ngapi za madafu

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 29, 2009

    WEWE MDAU ULIYECHELEWA, TANZANI INAZO MELI KWENYE ZIWA NYASA, MELI HIZO ZIPO KWA MIAKA MINGI SANA TANGU ENZI ZA MWALIMU, SASA SIJUI WEWE HAYA YA KUKANYAGA MAJI UMEYATOA WAPI?

    ReplyDelete
  7. MliakuvanaMay 29, 2009

    Hilo swala lipo tangu enzi za mwalimu na si ajabu tangu kabla ya Uhuru.

    Kwanza, nadhani sheria sa kimataifa kwenye mipaka ya majini ni kwamba mpaka utakua katikati au kilometer 14 tokea nchi kavu. (Inawezekana nimekosea kidogo au/na kuchanganya mambo - unajua tena maritime law sio kitengo changu).

    Pili, wananchi wa Malawi husema jina halisi la ziwa sio Nyasa bali ni Malawi - I think its still open for debate and interpretation.

    Inasemekana Mwalimu Nyerere alishawaambia hao waMalawi kwamba kama mpaka upo ufukoni wa Tanzania basi wao wayazuie maji yao yasiguse nchi yetu, jambo ambalo ni impossible. Depending on wat map or atlas you are using mpaka utaonekana tofauti. Atlas zilizo TZ-centric zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa na atlas iliyo Malawi-centric unaonyesha mpaka unaambaa kwenye beach za Mbamba Bay, Liuli, Manda, Matema beach, etc.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 29, 2009

    Why should there be a mpaka anyway
    All these international boundaries in Africa are *artificial* and makombo ya ukoloni.We will never get rid of our colonial scars if we dont radically change our thinking hatuna haya kukaa na kuzungumza mipaka baina yetu na ndugu na majirani iliyowekwa na our colonial masters to divide weaken and rule us
    We want Africa babu mpya
    We want Africa a huge global power
    Wakey. wakey
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  9. Mliakuvana..Aidha ramani za sasa zinaonyesha kuwa mpaka unaambaa katika fukwe za Tanzania, na jina la ziwa hilo sio Nyasa tena bali ni Lake Malawi

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 29, 2009

    "kama migingo ni ya kenya basi maji yanayokizunguka ni ya uganda" teheteheteheteheteheteheteheeee

    ReplyDelete
  11. hhaha mmhh haya hata mie nilikuwa sijui haya ,gonja tusikilize wenye blog wazungumzie.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2009

    Mliakuvana naona homework yako umeifanya. Lakini matatizo yetu na Malawi kimpaka ni makubwa zaidi kuliko yaliyoko Ziwa Nyasa.Kuna sehemu mpaka wetu na Malawi ni mto Songwe. Na mto huu hubadilisha njia mara kwa mara wakati wa masika na masika hii inaweza kumega ardhi na kuingia Malawi na masika ijayo ikageuza na kumega ardhi na kuingia Tanzania. Ramani inaonyesha tu kwamba mpaka ni mto!Mto unageukageuka tu kutoka msimu mmoja hadi mwingine. Mpaka uko wapi sasa? Na wananchi wa hayo maeneo anaweza akajikuta yuko Malawi na msimu ujao yuko Tanzania. Patamu hapo!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2009

    HANA LA KUSEMA, MIMI NINA MIAKA ZAIDI YA 50 NA NI MNYASA WA MBAMBABAY, MTANZANIA MPAKA UPO KATI YA ZIWA SIYO BEACH UPANDE WA TANZANIA KAMA ANAVYOLOPOKA HUYU BWANA, ACHAENI UZUSHI HAPA.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 30, 2009

    Ninyi mnaombishia huyu jamaa kuhusu tatizo la mpaka ni kwamba hamfahamu ukweli. Huyu jamaa siyo mzushi. Kimataifa hilo suala la tatizo la mpaka linafahamika. Na asili yake yake ilianzia tangu enzi za ukoloni. Reference za uhakika kwa sasa hivi sina. Lakini tatizo hili limetajwa utalikuta kwenye website ya CIA the-world-fact book. Link yake ni hii; https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html

    Hapo wametaja kwa kifupi tatizo hilo, hivyo lipo katika kumbukumbu za kimataifa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2009

    Hili swala ni kubwa ingawaje kuna wanaosema ni makombo ya mkoloni sawa lakini hata wewe ukiwa na nyumba yako utataka ujue mpaka wako na jirani yako. Wasipoliongelea kama wanavyofanya Kenya/Uganda ndio mwanzo wa nchi moja kuwa na silaha za mass destruction.

    ReplyDelete
  16. MliakuvanaMay 30, 2009

    Kinda odd that the border of Mozambique and Malawi is in the middle of the lake and further north it appears to be on the beaches of Tanzania. https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 30, 2009

    Sasa hawa jamaa ndio wamekonfyuz kabisaa! http://www.worldatlas.com/webimage/countrys/africa/tz.htm
    I guess wametaka koakomodeti waTzanzania na waMalawi - angalia majina ya hilo ziwa. Lake Nyasa kwetu, Lake Malawi kwao - go figure.

    And check this out - http://www.infoplease.com/atlas/country/tanzania.html Indeed wewe anony wa Mbamba Bay mlikuwa mnavua ziwani illegally!

    ReplyDelete
  18. hivi Kafulila David umetumwanani wewehayo ndiyo matatizo ya watu wajimbo lako?acha kuchemka mapema au umepata ubunge bila kujipangana kukutana na wanajimbo kujua niwananchi wangapi ambao wana mahitaji ya umeme halafu bwana mdogo acha kukurupuka ebo.matatizo kibao weweuna zungumzia starehe tu acaha ulimbukeni .Kwakweli uemetia aibu kwa wananchi walio kuchagua kumbe walifanya makosa hawatorudia kosa ,kaa na watu uopate mawazo yao nakushauri kama mdogo wangu na mbunge wangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...