Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Joel Bendera

SERIKALI imewataka Wafanyabiashara Rostam Aziz na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuacha mara moja malumbano kati yao na kutotumia vyombo vyao vya habari kwa maslahi yao binafsi.

Sambamba na hilo imewataka kuwasilisha vielelezo na madai yao kwa mamlaka husika ili hatua zinazofaa zichukuliwe na wananchi wapewe taarifa na vyombo hivyo.

Akitoa tamko la serikali leo mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera kwa niaba ya Waziri wake, George Mkuchika alisema serikali haitakubali kusikia malumbano hayo ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani nchini yakiendelea.

“Serikali imeyatafakari malumbano ya wafanyabiashara hawa na kubaini yanalipeleka taifa letu mahali pabaya kwani yana mwelekeo wa uvunjaji wa amani kama yataachwa kuendelea. 

"…pia haitavumilia kuona vyombo vya habari nchini vikichangia kuligawa taifa katika makundi na kudumaza maendeleo”,alisema.

Badala yake amevitaka vyombo hivyo vya habari kutotomiwa kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji; viongozwe na maadili ya taaluma na jamii husika na kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu na kuchochea uhasama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2009

    Too little too late!! This is about business rivarly that has gone nasty!! These guys would do anything to get whatever they want, even if it means breaking the peace in the most peaceful country in the world! Wanatakiwa wachukuliwe hatua vile vile!!But we know that is not going to happen! Ndio nchi yetu ilivyo...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2009

    jamani mbona hakuna serikali tena?
    eti waache malumbano!
    hamjasikia mheshimiwa pinda kasema anayeona kuwa amesingiziwa akafungue kesi mahakamani?
    huyo rostam alikuwa wapi wakati wananchi tunalalamika kuhusu kagoda na richmond au rada?
    yeye si bingwa wa kujua data aisaidie serikali kutupa data za kagoda,richmond na rada kama alivyotupa data za mengi!
    the system is cursed and tanzania will always be poor as long as the system exists!period!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2009

    Serekali hapo inachemka, yale yale mambo ya kisirisiri ambayo yamepitwa na wakati. Mpambano wa ufisadi uwe wazi kuwapa fursa wananchi kuelewa jasho lao linavyoliwa. Sera zenu za usiri tunakuja kushtuka mabilions na mabilions yameshaliwa. Angalau sasa tunajua Mengi aliupataje utajiri wake. Wa Mh Rostam umekuja tu kwa kimiujiza maanake hana hata kaduka.
    Hivyo mheshimiwa Bendera hii ndiyo nafasi ya wananchi kujua jinsi ya nchi ya inavyoliwa badala ya kuishia kwenye ofisi yako kimya kimya.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2009

    HIVI KARIBUNI,WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI NA UTUMISHI WA UMMA),USTAADHA HAWA GHASIA,ALITOA ONYO KALI DHIDI YA WATU WANAOJIHUSISHA NA KILE ALICHOKIITA "WIZI WA NYARAKA ZA SERIKALI".NISINGEPENDA KUREJEA REACTIONS MBALIMBALI ZILIZOTOKANA NA KAULI HIYO LAKINI MMOJA YA SAUTI ZILIZOPINGA VIKALI TAMK HILO LA GHASIA NI MBUNGE WA KARATU NA KATIBU MKUU WA CHADEMA,DR WILBROAD SLAA.MWANASIASA HUYO NGULI WA MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI ALIELEZA WAZIWAZI KWAMBA NYARAKA ZINAZOFICHA UFISADI HAZIPASWI KUWEKWA KWENYE KUNDI LA NYARAKA ZA SIRI ZA SERIKALI.DR SLAA ALIELEZA BAYANA KWAMBA PINDI AKILETEWA NYARAKA ZA AINA HIYO ATAZIMIA PASI UOGA KWA VILE NI KWA NJIA HIYO NDIO TUMEFANIKIWA KUBAINI SKANDALI KAMA ZA EPA,RICHMOND NA NYINGINEZO.


    NI DHAHIRI TAMKO LA WAZIRI GHASIA LILENGA KUWATISHA WATU KAMA DR SLAA.LAKINI PIA WAZIRI HUYO ALIFANYA HIVYO KWA VILE NI MIONGONI MWA VIONGOZI WA SERIKALI WENYE DHAMANA NA MASUALA YANAYOHUSU IDARA MBALIMBALI ZA SERIKALI.


    BILA KUUMAUMA MANENO,HEBU TUJIULIZE: HIVI ROSTAM AZIZ ALIPOITISHA PRESS CONFERENCE YAKE NA KUTOA "USHAHIDI" MBALIMBALI KUPIGILIA MSUMARI HOJA YAKE KUWA REGINALD MENGI (MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP) NI FISADI NYANGUMI,ALIZIPATAJE NYARAKA MBALIMBALI ZINAZOPASWA KUWA KATIKA HIFADHI YA TAASISI HUSIKA ZA SERIKALI?

    ROSTAM SI MTUMISHI WA MAMLAKA YA MAPATO AU MWAJIRIWA KATIKA WIZARA YA FEDHA KIASI CHA KUWA NA "DATA" ALIZOTOA KUHUSU MENGI.NA KWA VILE MAMLAKA HUSIKA ZIMEKUWA KIMYA KUHUSU WAPI MBUNGE HUYO WA IGUNGA ALIPATA NYARAKA HIZO NI WAZI KWAMBA ALIPATIWA KWA RIDHAA YA WAHUSIKA.

    WATETEZI WA ROSTAM,KUANZIA WAZIRI SOPHIA SIMBA NA KAPTENI GEORGE MKUCHIKA WAMEKUWA KIMYA KABISA KUKEMEA "HUKUMU" ALIYOTOA ROSTAM DHIDI YA MENGI TOFAUTI NA WALIVYOKURUPUKA MARA BAADA YA KIPENZI CHAO KUTAJWA KUWA NA MENGI KUWA NI FISADI PAPA.BY THE WAY,MENGI SI MTU WA KWANZA KUMTUHUMU ROSTAM KUWA NI FISADI.HIYO NI OPEN SECRET,NA KINACHOKWAZA WATU HAWA KUCHUKULIWA HATUA NI NJAA TU ZA HAO WENYE WAJIBU WA KUFANYA HIVYO ZINAZOKIDHIWA NA JEURI YA FEDHA ZA MAFISADI HAO.

    SASA,SIJUI WAZIRI GHASIA ANAWEZA KUTUELEZA NINI KUHUSU WIZI WA NYARAKA ZA SERIKALI ULIOFANYWA NA ROSTAM.NAUITA WIZI KWA VILE ROSTAM SIO TRA,DPP,MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AU TAASISI YOYOTE YA SERIKALI YENYE DHAMANA YA KUWA NA NYARAKA ZILIZOTUMIWA NA MFANYABIASHARA HUYO KWENYE "KUJENGA KESI" YAKE DHIDI YA MENGI.

    SASA NAELEWA KWANINI ROSTAM ANAWEZA KU-WISH ASINGEJIBU HOJA ZA MENGI KWANI WATAPOFIKA MAHAKAMANI ANAPASWA KUULIZWA YEYE ALIKUWA NA NYARAKA HIZO KAMA NANI?ALIZIPATAJE?NA JE KUWA NAZO SIO KOSA (KWA KUREJEA "MKWARA" WA WAZIRI GHASIA?

    NA HIYO NI NJE YA TAARIFA ZA KUAMINIKA KUWA NYINGI YA DATA ALIZOTUMIA ROSTAM NI "MAKANJANJA" (FAKE DATA) AMBAPO WAJANJA WA MJINI WALIPOSIKIA KUNA TENDA YA FEDHA NYINGI YA KUWEZESHA KUPATIKANA KWA INCRIMINATING EVIDENCE DHIDI YA MENGI WAKACHANGAMKIA TENDA HIYO LAKINI KATIKA HALI YA UFISADI.WHY NOT,KUMFISADI FISADI NI SAWA KABISA NA KULIPA KWA NOTI BANDIA MANUNUZI YA CHENI ILIYOTENGENEZWA KWA DHAHABU FEKI.


    MWISHO,NAPENDA KUSISITIZA KWAMBA SINA CHUKI NA ROSTAM AU MTANZANIA YEYOTE MWENYE ASILI YA NJE YA NCHI.ILA SIFICHI UKWELI KWAMBA NINA ZAIDI YA CHUKI,HASIRA,DUA BAYA (NA MENGINE NISIYOWEZA KUTAJA HAPA) DHIDI MAFISADI.UTETEZI WA KIPUUZI WA MAFISADI UMEKUWA KWENYE VITU KAMA RANGI,DINI,KABILA,NK.MTAKUMBUKA MKURUGENZI WA IPC,EMMANUEL OLE NAIKO ALIZONGWA KUHUSU KWANINI ALITOA KIBALI CHA UWEKEZAJI KWA KAMPUNI YA KITAPELI YA RCHMOND,KIMBILIO LAKE KUU LILIKUWA UKABILA.ETI "NAANDAMWA KWA VILE NATOKA ENEO MOJA NA LOWASSA"!

    LEO HII AKINA ROSTAM,MANJI,SOMAIYA,JEETU NA SUBASH WANATAKA KUTUAMINISHA KUWA TUHUMA DHIDI YAO ZINACHANGIWA NA "UTANZANIA" WAO WENYE ASILI YA NJE YA NCHI.HUU NI UTETEZI MUFILIS NA NI WA KIFISADI KAMA WANAVYOTUHUMIWA.HIVI WANATAKA KUTUAMBIA KUWA TULIPOPAMBANA NA MKOLONI,MJERUMANI NA MWINGEREZA TULIKUWA WABAGUZI WA RANGI?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2009

    huyu rostam ana something fishy hata ukienda katika website ya bunge section ya who is who jamaa ana missing data howcome wamelist kuwa yeye ni graduate lakini hawasemi kasoma wapi hiyo degree wala hawasemi kasoma wapi previously very fishy kaangalieni wenyewe then mcheki wabunge wengine link hiyo hapo

    http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcv.php?vpkey=64

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2009

    kaka michuzi huna hata haya unabana comment zinazokugusa? tutafika kweli kwa mwendo huu? acha hizo nchi yetu wote najua blog ni yako ila kama umeamua kuifanya blog ya jamii acha tabia za kukandamiza wanyonge maana kama mtu hatatukanwa sioni sababu ya kubana comment zake.

    ReplyDelete
  7. Wizi mtupu, siku zote walikuwa wapi kuwazuia. Sasa wamefungua kesi mahakamani hawezi tena kuendelea kurushiana maneno, ndiyo serikali inajitokeza, eti walikuwa wanatafakari.

    Unajua ukiandika kwa herufi kubwa inakuwa vigumu sana kusoma comments. Huyu jamaa amecharaza herufi kubwa kuweka msisitizo lakini ndiyo kwanza watu tunairuka hiyo comment.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 11, 2009

    Nyie wenyewe viongozi mkiongozwa na simba wenu sophia ndio hamna busara, zamani viongozi walikuwa wanapima kila herufi na neno litokalo kinywani siku hizi utadhani baadhi ni vitoto vinacheza mtoni. Muwe na busara na mjue majukumu na matarajio yategemewayo kwenu. Acheni ushabiki na ujumwuishaji wa mambo kabla hamjayapima. Hakuna ubaya kama kiongozi akakaa kimya hata wiki lakini akatamka neno lenye busara, badala ya mtu kutoa maneno ambayo yanaongeza chumvi au kutia fitna juu ya rabsha(Sophia) Mjue hii ni nchi yenye watu wanaowasikiliza na sio mjumuiko wa ngoma ya mdumango. Acheni kupendelea muwe kama Mama ndani ya nyumba ambaye kila mwana ni sawa kwake hata kama jingine ni jambazi au kuna livivu kamwe huwa habagui wala haonyeshi mmoja ni zidi au finyu wa mwengine. Yaani tangu nilipoisoma habari ya Sophia nimemshusha daraja kabisaaa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2009

    Hivi hawa jamaa wanaomtetea MENGI wanafikiri ni NABII? wote Mengi na Rostam wanabidi wachunguzwe equaly bila kujali dini, kabila nk, Wahindi wachaga wote wan historia ya Ufusadi lazima wachunguzwe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 12, 2009

    Wananchi wanapiga kelele kuhusu ufisadi, naona ni vizuri hao mabwana wawili wakilumbana kwani serikali yenyewe iko kimya katika sakata la ufisadi.
    Hasira za mkizi furaha ya mvuvi waache walumbane ili siri zifichuke kabla ya uchaguzi manaake CCM haina maelezo ya fedha za kampeni

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 12, 2009

    muhindi kawachachafya sio,ndio bongo hiyo.mchina nae anaweka mizizi ngoja ajue kimatumbi mtakoma.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 12, 2009

    Mdau unayesema wahindi na wachaga wana historia ya ufisadi hujajishtukia lakini umeshachomekea ukabila. Watanzania wa makabila mbalimbali na rangi mbalimbali wamefisadi. Hii ya makabila ni utani tu. Angalia dili la Rada, EPA, Richmond. Makabila kibao yamewakilishwa.
    Huu uzalendo wa kutoa vielelezo dhidi ya mtu aliyekutuhumu kwa ufisadi siuamini. Siku zote hizo Rost alikuwa wapi kuvitoa vielelezo hivyo mpaka atuhumiwe ufisadi? Huu ni utetezi wa ile hoja maarufu ya "hiki kitu sio kibaya, mbona na wengine wanakifanya?"

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 12, 2009

    Viongozi wa bongo bwana.. sasa akiulizwa ataje vyombo vya habari vya Rostam anaweza kutaja?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 12, 2009

    Hongera sana nyote mliochangia.Swali kubwa ni serikali ilikuwa wapi siku zote? Kwa miezi mingi tu Rostam na magazeti yake yamekuwa yakimiwaandama bila ushahidi na very unprofessionally viongozi wa nchi wasiomuogopa na kumuita fisadi serikali ilikuwa kimya.Sasa Rostam mapigo ya Rostam yanajibiwa eti anajitokeza Sofia Simba na Mkuchika eti wanasema Mengi Kachemsha. Mbona walikuwa kimya wakati Spika wa nchi anakashifiwa kihuni kabisa na Rostam na magazeti yake. Wanasema eti amani itavunjika- kwa vile Rostam anajibiwa.'Kwa vile gwiji limeguswa?' kama John Chiligati alivyoulizwa na Dr Mwakyembe.Serikali,Sofia Simba,Chiligati, Mkuchika wote wamechemsha.Too litle too late kama alivyosema mdau hapo juu. Inaelekea mawaziri waliozungumzia hili jambo mpaka sasa wako mfukoni mwa Rostam. Hivi ni kweli huu ndiyo msimamo wa serikali lakini kwa maana kiongozi wa nchi (Spika) kakashifiwa na magazeti ya Rostam serikali haikutoa neno.Rostam kalemewa ndiyo eti wanasema waache- hivi unprofessional behaviour ya gazeti la Mtanzania na magazeti mengine ya Rostam haikuonekan mpaka Rostam alivyojibiwa? Hivi unprofessional behaviour ya gazeti la Mtanzania haikuonekana gazeti hili lilipounga mkono ile pyramid scheme ya DECI, kuwapotosha wananchi waliyotapeliwa pesa zao na kumkashifu mzee wetu Iddi Simba eti ameinjinia kufungiwa kwa DECI??? Hapana huu ni wakati wa kuongeza mashambulizi dhidi ya ufisadi kwa kila njia. Serikali sasa imepoteza credibility kwa kuunyamazia upumbavu wa wazi wa magazeti ya kifisadi.Afadhali serikali ingeendelea kunyamaza na kuachia hili swala mahakama maana wahusika kadhaa wameshafikisha haya maswala mahakamani sasa.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 12, 2009

    Ujinga mtupu, Serikali haina cha kufanya nini.
    Utawaambiaje Raia waache kulumbana , nyinyi inawausu nini?

    Ujinga mtupu

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 12, 2009

    NI NANI ANAYETAKIWA KULALAMIKA KUWA MENGI ANAINGILIA KESI ILYO MAHAKAMANI, NI WAZIRI WA HABARI AU MAHAKAMA? MBONA CCM IKILA SIKU HUTUMIA REDIO UHURU NA MAGAZETI YAKE KUWASEMA NA KUWAKASHIFU WAPINZANI HILO WAZIRI HALIONI AU HILO HALIHUSIKI KATITA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI ILIYOTUNGWA WAKATI WA VYOMBO VYA SERILKALI TU VIKIWEPO! PIA MBONA TBC NA MAGAZETI YA SERIKALI HUWA YANATUMIWA NA SERIKALI NA CCM DHIDI YA UPINZANI HILO PIA HALIONEKANI! LAKINI PIA VYOMBO VYA HABARI VYA CCM NA SERIKALI HUWA VINAANDIKA MATAKWA YA WAMILIKI WAKE TU , MKUCHIKA HALIONI HILO KWA SABABU YUMO NDANI YA HIVYO VYOMBO. HATA HIVYO MKUCHIKA ANAJITAHIDI KUWALINDA WAFADHILI WA CCM KUTOKANA NA MAOVU YAO.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 12, 2009

    KATIAK HILI UHASAMA UTAKUWA NI KWA WANACCM KUONA KUWA KWANINI MFADHILI WAO ASUTWE HADHARANI, MENGI HANA KUNDI LOLOTE KWANI YEYE NI MTU TUU, SASA KUVUNJIKA KWA AMANI KUTATOKEA WAPI? WAZIRI AFAFANUE HILO KUNDI LA MENGI NI LIPI, NI LA IPP, LA ROSTAM TUNALIJUA KUWA NI LA CCM. NADHANI WAZIRI ANATUMIA VITISHO AMBAVYO HAVIPO KUNYAMAZISHA WATU, HIZO SIASA ZA KALE.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 12, 2009

    Nilitaka kutumia lugha ya Matusi dhidi ya serikali, ila nimejizuia kwa ajili ya maadili mema niliyopata toka kwa wazazi.Hivi hii serikali Gani ya upumbavu isyo na msemaji mmoja mwenye Msimamo?wenzetu Kenya msemaji wa serikali Ni ALFRED MUTUA hapa kila mbunge wa c c m ni msemaji wa serikali,tena kama kahongwa uwaziri ndo kabsaaaa.miaka ya juzijuzi alowasa kabla ya kukumbwa na Kashafa ya RICH alisema kuwa tatizo la watanzania huwa wanasema tu KIGOGO KAHUSIKA ila hataji majina na akasema"WATAJENI KWA MAJINA HATUTA JALI MADARAKA YAKE WALA UWEZO WAKE TUTACHUKUWA HATUA DHIDI YAKE MARA MOJA"
    leo mangi kawataja majina imekuwa shida kwake.,ila pia mengi(mangi)kweli kachemsha eti "kikwete ndi number one kupiga vita Ufisadi" hapo ndo alipochemsha hadi simba wa majungu Sophia aliposema kachemsha.
    nadhani sasa ni muda wa wananchi kutafakari kwa kina wajue hawa wanaotuhumiana ni wa Chama gani.halafu anagalia wa Vyama vingine kama wana tuhuma.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA usisahau kuumbua mafisadi na wanafiki

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 12, 2009

    Hoja za msingi za kuzingatia kutoka kwa Mwalimu:

    1.Mtu anayetaka uongozi wa nchi yetu nisharti ajue kuwa nchi hii na watu wake ni masikini na anakelwa na umasikini wa watanzania na ana dhamira ya dhati ya kupambambana nao.

    2. Mtu anayetaka kuwa kiongozi wetu, na anautaka uongozi wa nchi yetu kwa hali na mali, na katika kuutafuta anatumia pesa (rushwa) ni wa kuogopa kama UKOMA.

    3.Kama mtu anataka uongozi kwa kutumia pesa; kwanza kabisa kapata wapi hizo pe? na kama amekopa, atalipaje?

    4.Mtanzania katika hali halisi na uchumi wake ulivyo hawezi kununua kura bila yeye kununuliwa kwanza!

    Kwa jinsi hiyo tunavuta tulichopanda. Rostam Aziz ndiye defacto leader wa nchi hii. Kama jambo alikwisha litolea maelezo PM bungeni kulikuwa na haja gani hawa mabwana kwenda kuongea na vyombo vya habari. Halafu mbona tunawapa vichwa na significance wasioustahili watu? Hivi kweli ktk akili hii ya chekechea tutafika kokote? Mengi na Rostam wagombane, nchi iyumbe? hivi Tanzania ni nyumba ya balafu?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 12, 2009

    Mdau anonymous May 12, 2009 1:37 PM i wish i could shake your hand.Well said. Naomba niongezee tu hili tu: alitukanwa Sita Kiongozi wa kitaifa alitukanwa sana na magazeti ya Rostam hakuna cha Mkuchika, Bendera, Sofia Simba wala Sofia Mbuzi aliye sema kitu. Mwakyembe kazushiwa conflict of interest na Rostam nje ya bunge kwenye magazeti yake tu wote kimya. Wakati kama kuna conflict of interest basi Mwakyembe angekuwmevunja kanuni ya bunge na utaratibu ni kwamba angeshtakiwa bungeni na si gengeni kama alivyomshtaki Rostam. Huu si utawala bora aliyofanya Rostam kama anaamini kweli kavunja kanunui ya bunge basi amshtaki bungeni na taarifa basi ziibukie hulo kuingia kwenye vyombo vya habari.Simba hakusema kitu hapa. Mengi kasema maafisadi papa basi looh Mkuchika Simba Bendera wacha wahangaike- wakati waziri wao mkuu kesha sema ambao hawapendi aliyosema Mengi waende mahakamani.Hawakumsikia mkuu wao wa kazi, ambae ni makini na mwanasheria mzuri tu, wakaanza kusema kupitia vyombo vya habari eti ooh basi acheni, oh sijui Mengi kachemsha.Sasa hii serikali basi ya Rostam jamani. Mawaziri wanashtuka kuliko hata akisemwa Kikwete!!!Usiibanie hii Michuzi!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 13, 2009

    bana hii sasa....unaboa sana

    ivi eti nchi imekaliwa na uyo mmbunge au wale wafanyabiashara wakihindi???

    kama Mungu wetu aishivyo,mtakiona

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 13, 2009

    yani simpendi uyu jamaa rangi-rangi

    aokoke tu

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 13, 2009

    AMANI HAITAVUNJWA NA WANAOSEMA "UKWELI" ITAVUNJWA NA WANAOTEKELEZA "WIZI/UFISADI".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...