Habari za mishughuliko,
najua hii ni blog ya jamii,nina swali langu napenda niliweke kwenywe blog hii pendqa.
Tangu niolewe huu ni mwaka wa 13 kwa kweli kwa sasa haya mambo ya unyumba siyapendi hata kidogo,na mambo mengine kuyauliza naona tabu,lakini nimeamua niyaulizie kwako.
jee jambo kama hili linawakumba wanawake wengine wowote au ni mimi ndie nina matatizo. Kwani kwa kweli huyo mume kwa sasa namuona kama ni rafiki wa kawaida tu. na hayo mambo ya unyumba miaka nenda miaka rudi natamani yawe na mwisho wake.
Jee kwa walio oa jambo kama hilo linawatokea kwa wake zenu?. Na kwa upande wa mwanamume, mwisho wake ni umri wa miaka mingapi mpaka hiyo hamu imuondoke?.Umri wangu ni miaka 35,na tumejaaliwa kupata watoto 3.
Najua kuna watu watanikandia lakini kwa kweli nipo serious na hili swali. Na natamani tungekuwa kama mwanzo wa ndoa yetu,kwani mwanzo nilikua napenda,na kwa upande mwengine namuonea huruma kwani yeye anataka lakini mie sitaki hata kusikia jambo hilo.
{tafadhali nakuomba usitoe email yangu.}
nasubiri mchango wenu.
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 72 mpaka sasa

  1. After you filter out all the media brainwashing, religious ideologies and various other types of social B.S. it boils down to basic human instincts. Women are programmed to find one good provider and have lots of babies with him. Men are programmed to have sex with lots of healthy young women of child bearing age.

    Kwa hiyo dada muda wako umekwisha. Mwambie Mister ruksa kukamata bi mdogo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2009

    Aiseee hii yako nafikiri ni saikolojiko tatizo lakini linatibika kama upo tayari kuirudia hali yako ya mwanzo......i knw the way you feel about it.Mbije,A-kafanabo

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2009

    ...Kupoteza hamu ya tendo la ndoa na mumeo kwa umri wa 35 yrs in maana unatembea nje ya ndo na kijana mdogo zaidi ya mmeo, nakushauri uache mara moja hiyo tabia then penzi lako na mumeo litarudi kama kawaida.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2009

    Je endapo kama wewe hujisikii, hutaki kabisa kusikia hiyo ishu kutoka kwa mumeo, upo tayari aende kuchapa nje?

    Upo tayari achape nje, kwa siri bila kuathiri mahusiano yenu ya ndoa? Bila kuwepo dalili zozote za kukudhalilisha?

    Upo tayari kutoanza kufuatilia nyendo zake za nje? mfano simu, etc?

    Kama majibu ya maswali haya yote ni ndiyo, basi tatizo utakuwa umelitatua.

    Kama una jibu mojawapo ambalo ni hapana, basi itabidi ujitahidi kumridhisha mumeo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2009

    Pole sana, lkn kwa informal research findings, most marriages ends-up or start problems at the age of ten to thirteen yrs. Chanzo kimojawapo ni ukomo kwa tendo takatifu na mambo yahusianayo na mahaba. Wewe sio wa kwanza jipe moyo zungumza na mwenzio mjue sababu kuliko kuishi kama 'juma na roza'

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2009

    pole sana dada kwa kupatwa na tatizo hilo na ukakaa kimya kwa muda huo wote. napenda tu nikuondoe wasiwasi kwamba umri wako wa miaka 35 sio sababu kubwa ya kukufanya usijisikie kuwa karibu na kumhitaji mwenzio,japo kuna wanawake wanao wahi kupata menopause mapema lakini hii ni mapema sana,na hata hivyo pia sio wote wanaopata menopause wanakuwa na tatizo kama lako.
    wapo wale ambao mabadiliko ya vichocheo[hormones]yanafanyika kwao kwa mtikisiko mkubwa,na wengine huwa yanakuwa ya kawaida tu.
    KUKOSA KUJISIKIA KUMHITAJI MWENZIO kunaweza kusababishwa na sababu nyingi ambazo naweza kuzigawa ktk makundi kadhaa:-
    1]kisaikolojia:-
    -stress[msongo wa mawazo unao weza kuletwa na sababu tofauti kama za kiuchumi,mahusiano ya kijamii,mazingira ya kazi,na majukumu kuzidi kiwango]
    -uchovu wa mwili[kutegemeana na aina ya shughli unazofanya]
    2]mabadiliko ktk tezi zinazo zalisha vichocheo yanayoweza kusabishwa na sababu tofauti tofauti kamavile:
    -lishe[upungufu wa baadhi ya virutubsho muhimu],-infection,n.k
    3]magonjwa mengine tu yasiyo ya kuambukiza,yanayo dhoofisha utendaji kazi wa mwili.au side effects za baadhi ya dawa zinazo tumika kuyatibu magonjwa hayo.
    UNACHOPASWA KUFANYA:
    -nenda hospitali umtafute dactari akufanyie uchunguzi wa awali,kisha ikiwezekana akuelekeze kwa gynaecologist au endocrinologist watakuchunguza na kukusaidia vizuri.
    -kama mahali ulipo kuna dactari sexualogist pia unaweza kuanzia kwake moja kwa moja iliyeye ndie akuelekeze unahitajika kufanya.

    pole sana,ila sijui mko wapi maana kama mpo tanzania basi sitaweza kuonana na nyie kwa msaada wa kitaalam. ila fuata utaratibu niliokupa tatizo lako litashughulikiwa linaweza kuwa siokubwa sana.

    Dr.mdau

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2009

    nakupa pole kwanza,pili naungana na huyu aliyesema ni(saikolojia)angalia ni vitu gani vinakuumiza kichwa maana kwa uri wako ni bado mno,tatu kuna tatizo la kina mama wakipata watoto hamu ina potea hasa kama unatumia dawa za majira,tendo la ndoa ni muhimu hata mabibi na babu wanafanya dadaangu we bado sana,jichunguze,napia siku hizi kuna mapepo wanaokupotezea hamu ya kufanya mapenzi,hata biblia inatuambia kuwa mwili wako ni wake na wake ni wako Mungu alikuwa na maana yake kuwa mdinyo hadi mmoja afe au nguvu ziishe.pata amani

    ReplyDelete
  8. saikologistMay 11, 2009

    naungana na wadau walio pita.mruhusu mwenzako aoe mwanamke mwingine.wewe utabaki kama first lady na utaishi kwa amani.wanaume huwa wanatoa hio huduma mpaka wanakufa na hivyo usitegemee kama mwenzako ata stop.
    Solution ya pili ni kujilazimisha kupenda ngono kwa kupitia mume wako kwa matendo kama outings, dinner, na safari za hapa na pale.hii itakusaidia kupata nyege.
    Ahsante.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2009

    Pole Shosisto wangu!
    Sababu yaweza kuwa;
    1. Wewe ni mzito sana, yaani umenenepa- watu wanene wanakosa hamu ya kujamiina mara nyingi hasa kama unene umeupata ukubwani.

    2. Njia ya uzazi wa mpango unayotumia yaweza kuwa sababu.

    3. Unamsongo wa mawazo

    4. Mume hajui kukutayarisha.

    5. Matatizo haya umeyafanya siri yako, hujamshirikisha mumeo.

    USHAURI
    Peleka watoto kwa bibi yao; ili wewe na mumeo mpate muda muafaka kiakili, kimwili nk. ikiwezekana safarini, na simu zima kabisaaaaaaa
    Pata muda wa kuwa peke yako na mumeo, jadili mada hii, halafu tafuta vichokoo ndani ya mwili wako ambavyo vitakupa akshi, sio kule ulikozoea kila siku ... nadhani umenipata

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 11, 2009

    Kuna baadhi ya wanawake umri unavyoanza kusogea hali kama hiyo yako inawatokea wengi duniani,ikiwa ni pamoja na mwili kupata joto kali sana kwa dakika kadhaa wakati fulani.
    Pia wanakuwa wakavu sana katika sehemu kadhaa muhimu,kwao tendo la ndoa linakuwa si muhimu sana.Kwa ufupi ndio uzee wenyewe unasogea.
    Hapa Norway kuna virutubisho unaweza kupewa japo sio rasimi.

    Wanaume tuna bahati, unadunda maisha yote,ndio maana kule kijijini unaona babu anaoa kasichana kadogo kama kajukuu kake. Japo hataweza kupanga mataruma kama akiwa na mika 20 mpaka 45,lakini anaweza kuendelea na shughuli zake za kila siku kwa kuwa anayo hifadhi ya mshale mmoja au miwili yakumlinda kila siku kama anapata chakula bora cha huko nyumbani.

    USHAURI-Anza kuwa karibu na mumeo ikiwa ni pamoja na kwenda jogging,sinema,kutembelea fukwe na kusikiliza musiki laini huku ukitumia matendo zaidi ya kumliwaza mumeo.

    Sishauri mumeo aoe mke mwingine,kwa kuwa imani nyingi hazikubaliani na hilo na pia kuna magonjwa mengi.
    Mungu akutie nguvu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 11, 2009

    Hi dada. Pole sana
    1. Unaweza ukawa na tatizo la kisaikolojia, please see a shrink ili urudie hali yako ya zamani
    2. Unaweza ukawa ulitembea nje na mwanaume mwingine ambaye alikuridhisha sana, sasa mumeo unakuwa huna hamu nae ingawa hata huyo mwanaume wa nje haupo nae tena, so, mtoe mawazoni mwako ili uweze kumfurahia mumeo upya
    3. unaweza ukawa unafanya kazi sana so unachoka, na ukirudi home umechoka mume hataki kukuelewa, so hii itasababisha ulichukie tendo. kama ni hivi, punguza kufanya kazi masaa mengi ili hali yako ya kawaida irudi, au chagua siku unazojua hauchoki sana coz hufanyi kazi masaa mengi, ongea na mumeo, hizi siku ndio ziwe mnazitumia kufanya mapenzi BUT, na zile zingine mzitumie mara moja moja ili isiwe kama ratiba

    Kama hayo ya juu yote are not applicable, nenda nje ya nchi au mkoa unaoisho kwa kama miezi mitatu, usifanye tendo la ndoa na mtu yeyote, utakaporudi, nadhani utakuwa na hamu ya mumeo kama zamani

    ReplyDelete
  12. pole dada[mama],ukweli hayo usemayo yapo na yanaumiza sana kwa m.mme ambaye anampenda mke wake;(only feeling with his wife), lakini inakuwa ni mateso sana kwa mume,mimi nimeoa na mtoto mmoja ndani ya ndoa miaka 2,mke wangu hana feeling na mimi kabisa naumia sana,na sio kama yeye ni muhuni kama mchangiaji mmoja alivyosema,ila kabla ya ndoa tulikuwa tunapendana sana na alikkuwa na feeling kweli .pia mimi kama m.mume sijui cha kufanya, ila ningeshauri tulichukulie positive hili tatizo na tuweze kupata msaada sisi waume tunaoteseka na tunawapenda wake zetu,michuzi pia na wewe ufanye utafiti kwenye hili

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 11, 2009

    pole dada kwa mume inaumiza zaidi haswa kama unampenda mke wako na yupo peke yake

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 11, 2009

    Pole tena pole sana
    Matatizo kama yako yanawasibu wanawake wengi lakini hawapendi kuzungumza shida hiyo
    Wahuni wasema betri ya gari imekufa
    Mie nakuomba usikate tamaa. kwanza mtafute daktari mwanamke mwenzio na
    umueleze shida zako kwa urefu.Kule marikani shida hii huitwa FSAD yaani Female Sexual Arousal Disorder, na madaktari wengine wayaita matatizo hayo Loss of LIBIDO
    Kuna mbinu mbili za matatizo hayo, kuna walio na maradhi,Mungu apishe mbali sisemi wewe una maradhi lakini betri yako ya gari huweza kuwa imekufa kwa maradhi ya kisukari. kisha kuna matatizo ya mawazo tu, yaani saikologia.
    Dada usitafute machimba mizizi au wachanja chale au mashehe wanaotaka kukupunga mashetani .Mtafute mjuzi wa matatizo hayo
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 11, 2009

    tatizo hili ni la kisaikolojia sana, kama mchangiaji mmoja alivyosema. lakini hasa huwapata wale watu ambao katika ujana wao walizoea kuwa na mabwana au mabibi wengi kwa wakati mmoja, au ambao walikuwa wakibadilisha mara kwa mara wapenzi, na wale ambao wakiachana na mpenzi huyu, hawakai wakatafakari nini chanzo cha kukosana, kisha wanadakia kwa mpenzi mwingine. kwa hiyo unajikuta upo much used to have different tastes, you cannot stay with one partner. hili tatizo limewakumba wengi, ingawa wengi hawasemi hadharani. ni vizuri ukatafuta mwanasaikolojia akakusaidia. labda uende hospitali ya Muhimbili au Mission Mikocheni, au Mirembe, pana madaktari bingwa wa Psychiatry ambao pia ni wataalam wa masuala ya akili, mambo ya ndoa yakiwemo. pole sana dada

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 11, 2009

    Fanya mambo yote uliyokuea unafanya hapo awali kabla hujamkinai mumeo.
    Punguza shughuli ambazo sio za lazima ili mwili wako upate kupumzika.
    Fikiria kama angekuambia anataka kuoa mke mwingine, je ungeridhia, kama jibu ni ndio basi mpatie ruhusa na wewe ubake unashangaa.
    Nimeshasikia mdada mwingine anadai hapendi na kila siku alfajiri yuko Kariakoo anafanya biashara hadi mchana. akirudi analala tu hoi. Mimi niliwaza kuwa ile alfajiri sio kila siku anaenda sokoni bali keshapata jamaa anahangaika nae. Mwenye mali yake alinikatalia basi nikimwambia mvizie huyu ataleta maradhi anakataa, hadi siku moja alipomleteaa kaugonjwa kazinaa. Na wala hakujali sana alimwambia dr. tu amuulize na akasema eti jamaa alipromise kusaidia jambo. ndio akapewa. Hebu fikiria nyumbani unaminya kariakoo unatoa ukirudi uko hoi, bwana jaribuni kuwa wakweli kwenye ndoa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 11, 2009

    dada tatizo lako dogo sana na linatibika hospitalini.hata hapa uholanzi wanawake wengi sana wenye umri mdogo wamekua wanakumbwa na tatizo kama lako na wamepona. ispokua tu jaribu kua muwazi kwa mumeo na kwa madaktari jinsi unavyojisikia.
    nenda muhimbili kitengo cha akina mama wanatibu pale ,waeleze madaktari kila kitu jinsi unavyojisikia.matibabu yake si ya mda mrefu.
    kila la kheri.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 11, 2009

    Pole,
    Mimi namjua mtu ambae alikuwa na matatizo kama yako.Kwanza mimi nilifikiri kuwa yeye ni wale wanawake ambao wanapenda wanawake wenzao.Lakini sikuweza kupata ukweli wa hilo.
    Mwanamke huyu alifika mpaka stage ya kumtaka mumewe aoe ili aweze kujiridhisha.Mwanamme kwanza alikataa. Lakini baadae enough was enough. Hawa jamaa sasa wameachana kwa wema hivi sasa.
    Kwahiyo mpe ruhusa aoe mke mwengine au muachane kwa wema.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 11, 2009

    tatizo ulilonalo kwakweli ni tatizo ambalo wanawake wengi kwa sasa linawakumba, na hii ni mojawapo ya chanzo cha kuongezeka kwa nyumba dogo na ukimwi.

    Chanzo chake bado hakijawa wazi lakini yaelekea ni upungufu wa hormons kutokana na matumizi ya sindano na vidonge vya kuzuia ujauzito.

    La msingi na kama unaipenda ndoa yako, basi tafuta jinsi ya kutatua tatizo hilo.Nakama umegundua ni lazima upendo umepungua kutoka kwa mumeo, kwa sababu mara nyingi mwanamume hapendi upinzani akikuhitaji kimwili na kama unachukulia rahisi basi ana poozeo nje.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 11, 2009

    shosti usimpe tabu wa ubani wako kama game imekushinda usipate dhambi bure kumsumbua mwenzio mruhusu akaoe ili aendelee kuishi mwenzio utakuja kumuadhiri bure, ukifanya hivyo atakupenda zaid na wewe wala hutasumbuka, huwezi hivyo jaribu kuongea nae mtafute wanaojua kutibu ili urudishe hali na kama hivyo huwezi mruhusu atafute nyumba ndogo lakni aoe sio azini nje hii hata kwa mungu haikubaliki na jukumu utabeba wewe kama huamini waulize wanaojua. good luck

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 11, 2009

    Maskini. Yani dada I know how u feel... Yani pole sana.
    Sasa...hebu try to think of the past...mlivyokutana for the 1st time,the way ulivyokuwa ukim-feel... Ila nafikiri uko na Psychological Problem. Tafuta tu Dr mzuri akufanyie cancelling itakuwa sawa tu.. If u still love your hubby na hutaki atoke nje au awe na mtu mwingine.. Please... Tena fanya fasta! Manake mwenzangu kama unavyojua tena wanawake wapo wengi zaidi ya wanaume...akitoka nje mwenzio anawindwa kama nyati nakwambia... utatumbukiza shilingi yako chooni hivi hivi unaona ndugu yangu! Atagombaniwa kama mpira wa kona huko nje... Na ubaya wa hicho kitu sasa..AKIJARIBU KUCHOVYA NJE HAACHI NG'O nakwambia!!

    Ni hayo tu mama....

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 11, 2009

    Honestly i wish i could help but i understand your concern.........i want that help too

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 11, 2009

    kuhusu mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa na mwanaume huyu ni tatizo la kisaikolojia tu, kwa nini nasema hivi 1. ni kwamba kuna mahali walikorofisha na kutokana na hali hiyo basi tatizo likajengeka na nakusababisha kutokuwa na hamu naye.
    au 2.inawezekana unamuona mme hana mvuto wa sura uliolewa kwa taama yakimwili tu samahani kwa kusema hv nitatoa mfano: ila mh nikitoa naona michuzi ataweka kapuni ngoja niachie kwa hapo ila wakubwa watanielewa.
    ngoja nitoe tu mfano: mfano wewe umetafuta mtu wa kuoa au kuoelwa na mkaoana na baadaya kuoana mko kwenye ndoa na mkiwa kwenye ndoa mnasikia mme/mke wa fulani katoka kwenye ndoa lile tatizo litasababisha tarati kusema mh wanaume waongo au mh wanawake waongo basi taratibu, either litavunja ndoa au kusababisha upande wa mke/mme kutoka nje ya ndoa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 11, 2009

    Too much is Hamful sasa wewe ni miongopi mwa wale waliokimbia huu mchezo wa kunaninii ,singine ulianza kabla ya kuvunja ungo ,kifupi hayo ni matokeo yake.

    Sisi wezako wenye umri kama wako yaani ndiyo tunatamani na kufanya kila siku maana katika umri huu tuna maufundi yote ya huu mchezo yaani tumefuzu.

    USHARI
    kula vyakula vyenye kuleta hamu ya tendo,tazama movies au picha za porn.kama haijasaidia kajaribu kwa mtu mwingine kisha utaniambia.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 11, 2009

    TAFUTA MFANYAKAZI WA NDANI WA KIKE MZURI HASWA ANAETOKA MIKOA YA PWANI RUVUMA DODOMA NA KULE UKWENI ULANGINI HAPO NDIPO UTAKAPO PATA JIBU SAHIHI LA SWALI AU MJADALA WAKO.NDIPO UTAKAPO KWA NINI KANGA ANA MADOADOA SHENZI WEWE

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 11, 2009

    We dada unaupeo wa mbali sana maana mimi binafsi nina umri kidogo ufikie wa kwako nanina watoto wa 3,na mimi nina ndoa kama miaka 8 sasa lakini baada tu ya kuzaa mtoto wapili hamu ya mapenzi imenitoka napata hamu lakini si kama zamani,na ninajitahidi tu nimridhisha mwenzangu hata kama si jisikii, hivyo ni mejaribu kufikiri nimegundua tatizo linakuja kuwa(1)ni stress unazozipata kutokana na maisha unayo ishi aidha kazi nyingi au watoto inakufanya usitamani tendo la mapenzi.(2)Unawafikilia sana watoto,matokeo yake unachoka.
    (3)maumbile ya mwanamke yana change baada ya kuzaa, ukijifilia sana jinsi umbile lako lilivyo badilika hamu ya mapenzi lazima inaisha, yote hiyo dada ni stress,ndiomaana homone zako zinakuwa hafifu, ni kama mama unapo nyonyesha ukiwa na stress maziwa ni lahisi kukauka , ushauri wangu kwako nikujitahidi sana upunguze stress ili ndoa yako hidumu.na hamu itarudi kama zamani.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 11, 2009

    Tafadhali fuatilia hizo link - en.wikipedia.org/wiki/Hypoactive_Sexual_Desire_Disorder, pia fuatana na hii- www.livestrong.com/article/10382-treat-frigidity, pls copy and paste these links to the internet explorer and you will get most of information you need.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 11, 2009

    TATIZO LAKO NI LA KIROHO ZAIDI DADA YANGU. UNAOLEWA NA VIUMBE VINGINE PASIPO WEWE KUJIJUA. TAFUTA MSAADA WA WATU WA MUNGU, WAELEZE BAYANA WATAKUSAIDIA. MUNGU HAKUUMBA IWE HIVYO

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 11, 2009

    Yaani yeye anataka wewe hautaki,Kwanza hueleweki kama wewe pia huwa unataka ila si kwake au laa.
    Kuna mambo yafuatayowanaume wengi huwa hawajui ni wapi pakumgusa mwanamke na wanawake huwa hawasemi waguswe wapi.Kama ndio hivyo mwambie akuguse wapi sio kila siku anabonyeza kifo cha mende hafiki mahali.
    Jambo la pili nakuhisi kuwa utakuwa unamwibia mwenzako.Na ile ya wizi unaiona ni tamu kuliko ya ndani coz ni ya wizi kama kawaida huwa ni tamu.Kwani huwa m2 anataka umaarufu lakini ukifika ndani jamaa analeta ustaarabu naona ndio amcho hakikufurahishi.Acha wizi tulia na mumeo.[Mdau KRAI]

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 11, 2009

    Dada pole kwa kazi. Matatizo yako ni ya kawaida kwa akina mama wakizaa. Tatizo ni kuwa Bongo hakuna dawa yake. Rafiki yangu alimpeleka mkewe kutibiwa India kwa kuwa alikuwa na chemical inbalance mwilini ambayo haimruhuru apate hamu kulala na mumewe. Baada ya matibabu, mambo yakaendelea kama kawaida.

    Wewe labda una chemical inbalance au labla unatakiwa uwe na hali nzuri ya kimaisha nyumbani kama vile kupendana kwa kushikana mikono, busu kwa wingi ili mapenzi yajengeke tena kama zamani, sio tu anakuja kitandani usiku na kutaka mavituz. Usiogope kwenda kwa daktari upate jibu kamili.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 11, 2009

    Mwanamke mwerevu huijenga nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe na Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. sasa wewe endelea kuibomoa nyumba yako kwa kujidai hujisikii badala ya kutafuta solution. miaka 35 ndio kwanza mdada mbichi wengine umri huo ndio wanaolewa iweje wewe uone kuwa ni kawaida!!! hapo lazima ujue kuna tatizo na ni bora uliweke wazi watu wakusaidie la sivo ndoa hiyoooooooo inakuponyoka

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 11, 2009

    Je hujisikii kwa mumeo peke yake au kwa mwanamume mwingine yoyote yule? Hii ni muhimu kuiangalia kwa jinsi hiyo kwanza ndipo uombe ushauri.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 11, 2009

    Unachohitaji wewe ni talaka. Maana mume hawezi kuwa kaka, kama mume kawa kama kaka yako maana yake ni kuwa haumpendi tena na hautojali iwapo atakuwa na mwanamke mwingine (Labda uwe dictator kama Hitler, au yawe mambo ya simtaki na hawezi kuwa na mtu mwingine)vinginevyo wewe utakuwa ni mshenzi tu wa tabia.

    Kama unamuona mumeo kama kaka yako maana yake ni mapenzi yamekwisha kabisa kwake. Hivyo kama wewe ni mstaarabu ni lazima umuambie na umpe ruhusa akuache uanze mbele na yeye atafute mtu atakayempenda na atakakokuwa akionekana kama mume na si kaka.

    Kumuona mwenzi wako kama kaka au dada ni hatua ya mwisho kabisa kwenye uhusiano wa ndoa na inamaanisha kuwa hapo ndoa hakuna na ni sawa tu na kuwa hujaolewa.

    Ushauri wangu ni kuwa ongea na mwenzako mpe hali halisi na umruhusu aoe mwanamke mwingine atakayekuwa akimuona yeye kama mume na yeye amuone huyo binti kama mke na si kaka na dada.

    Lakini utakapomwambia usimweleze kuwa unamuona kama kaka yako maana hilo ni tusi kubwa sana kwa mwanamume lijali na ambaye ni mumeo ulozaa naye watoto.

    Swali kwako: Hao watoto umezaa na nani? Au wewe ndo wale wanawake wasiopenda kusikia habari za kwenda kupima DNA?

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 11, 2009

    Jamani mwenzenu anauliza swali ili asaidiwe nyie mnadhania kila kitu ni utani tu. Hayo matatizo ni yapo pengine unaanza kupata menopause yako (yaani kutokukosa siku zako za mwezi) Hivyo ninakushauri uwende kwa dr wa wanawake ili akuanzishie HRT (hormens replacement treatment) Usiwe na wasiwasi wanawake wote upitia huko, isipokuwa wengine huanza mapema na wengine huanza wakiwa watuwazima kabisa.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 11, 2009

    ushauri wangu nenda ukamwone Docta wa mambo hayo.Maana wapo madocta wa maswala kama hayo, kama utakuwa hujisiii kabisa hata kwa mwanamme mwingine, basi huo ni ujonjwa, sisemei kwamba utende tendo na mwanamme mwingine ila ujipime uone kama ni tatizo ni mme wako, au kwa wanaume kwaujumla, bali labda umemchoka mme wako, kama ni swala kumchoka basi ujue kwisha kazi, ndoa haipo tena hapo. Ila kama hutaki wanaume kwa ujumla basi, kamwone docta haraka sana. Ni mambo ya kawaida kabisa duniani, hutokea, ndo maana kuna madocta speshio wa ngono.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 11, 2009

    dada yangu pole sana kwa hilo tatizo lako, hilo tatizo linawatokea wanawake wengi sana sio wewe peke yako, mimi ninaumri unaokaribiana na wa kwako, umenizidi kidogo tu, lakini umri huo sio kwamba ndio uchoke tendo la ndoa, la hasha. tatizo hilo wakati mwingine linatokana na majukumu, wakati mwingine umechoka na majukumu ya siku nzima, pengine umeshinda kazini siku nzima, unarudi nyumbani, nyumba inakungoja, watoto, kupika, kila kitu wewe mwanamke ufanye ndani ya nyumba unajua tena wanaume wetu kwa kiswahili, hata ile kukusaidia hawawezi, halafu wanataka usiku uwape chejo, wakati huo umeshachoka hata ile hamu huna kabisa. lakini dada yangu, yote hayo inabidi uyavumilie wakati mwingine, inabidi lazima ujilazimishe kufanya hivyo kunusuru ndoa yako kama mumeo unampenda. wanaume ni watu wadhaifu sana, atachoka huyo ataenda nje, itakuwa ndio balaa juu ya balaa. ushauri wangu kwako dada yangu, jitahidi ufanye hivyo, hata kama hutaki, lakini jilazimishe, otherwise ndoa yako itakuwa mashakani dada yangu. mdogo wako. London

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 11, 2009

    Dada fahamu kwamba 'tendo la ndoa' lina-form sehemu kubwa sana ya ndoa hasa from a man's point of view. Kutomtimizia mumeo haja hiyo ni kukaribisha mgogoro wa ndoa ambao utapelekea kuivunja kabisa. Umefanya vizuri kuomba ushauri, hiyo ni hatua ya mwanzo, lakini wakati unapata ushauri na kujaribu kuufanyia kazi, hakikisha unamtimizia mumeo haja hiyo hata kwa KUJILAZIMISHA. Najua inauma lakini waulize wanawake wenzio huwa ikibidi wanafanya hivyo, kwani kitchen party hukufundishwa? Kama mumeo hana mbinu za kuku-stimulate mwambie ukweli ili nae ajifunze, asifanye tu kama jogoo na temba, lazima akuandae na akuingilie ukiwa umeiva kabisa. Hakikisha hili halivunji ndoa yako na kumpeleka mumeo nje ya ndoa!

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 11, 2009

    Mimi ndio niliouliza hilo swali,na wewe unaesema natembea na mtoto mdogo,hilo sio kweli kabisa. Na kama ningekuwa nafanya hivyo basi nisingeuliza kabisa ningejinyamazia kimya tu. Kwa hiyo naomba usiropoke tu.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 11, 2009

    Someni dini zenu na vitabu vyenu vinawaeleza hapa hakuna ushauri,

    jamani hizi ndio dalili za mwisho.

    muombeni allah na mfatisheni allah nini anataka mfate na mfanye ndomana mnaambiwa ndoa muhimu na uzinzi ni zambi,

    ukishaona hamu inapunguwa dini imesema jaribuni kutengana mmoja akae rumu nyengine mwengine rumu nyengine, sio zambi sababu anajuwa mkiwa mbali kimuda mtaanza kumisiana tena.

    Hamu itarudi tu wacheni fikra za uzinzi vuteni subra msifate tabia za kiengereza na watu wa west shaurizenu.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 11, 2009

    Dada naona uke wenza au nyumba ndogo inakunukia. Kila la kheri.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 11, 2009

    Pole sana dada kweli hiyo hali inatisha kwani bado uko umri mdogo sana kuwa Husikii hamu ya kufaidi tunda na mumeo wa ndoa.Shida yako yaweza kuwa ni vitu viwili jaribu kutafakari
    1)Je huyo mume alipokuchumbia mpaka kukuoa ulikuwa unampenda hasa kutoka rohoni au ulikuwa na vitu vilivyokupelekea wewe kumkubali na kufunga naye ndoa???? yawezekana hiyo ikawa ni sababu ya wewe kutokumtamani tena kitendo kwani kama ni hivyo lazima penzi lako litachuja
    2)Pia yawezekana ukawa umekumbwa na pepo ambaye huwa unafanya naye mapenzi ukiwa usingizini na kuenjoy naye hivyo ukitaka kushiriki na mumeo huoni kama anakupa raha yoyote(kwa jina pepo huyo anaitwa MAHABA).....hivyo basi kama ni hivyo inabidi utafute tiba kwani huwezi kuponakwa rahisi.....vitu hivyo vipo na vinawapata watu sana hapa duniani
    POLE SANA DADA

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 11, 2009

    Ni kweli kihali-halisi umri unavyokwenda ndivyo shauku kwa mke inavyopungua ukilinganisha na ya mume, lakini miili yetu inaboreshwa na mazoezi, vyakula na aina ya kazi tunazofanya.
    Wanawake wengi hasa wa vijijini wanakuwa `busy' na kazi kiasi kwamba hawana muda na mazoezi, ya miili yao. Mazoezi ni mazoezi ya kawaida sio `ufusuka'
    Lakini tukumbuke `shauku' ya mwili hujengeka na hisia yenyewe. Mfano kama utaliona jambo lenyewe halina maana, basi na shauku nayo hupotea. Lakini unaweza ukairejesha kwa `kutafuta' vichochezi' na zaidi ni kusaidiana na mumeo nk.
    Tungeeleza zaidi lakini nahisi hapa sio mahali pake, kwanini usilipeleke kwenye blog zinazoendana ma maswala haya kama ile ya Dinahicious?

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 11, 2009

    sikiliza ili jambo hauko peke yako, wanawake wengine huwa linawatokea wakizaa tu. lakini nilishaona kwenye kipindi cha oprah wakilizungumzia na walisema linatibika. Na kama kumbukumbu yangu ni nzuri walisema wanawake wawe wanatumia sinema za ngono ili kuamsha hisia kabla ya kuanza tendo la ndoa. vile vile mazoezi ya kukimbia na yaina nyingine pia yanasaidia katika kuleta hamu.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 11, 2009

    Mwenyezi Mungu alipoumba wanyama (kibaiolojia binadamu tupo katika kundi a wanyama), madume yameumbwa na hamu ya asili ya kupanda majike mengi kwa kadri itakavyowezekana.

    Binadamu kutokana na imani mbalimbali, tamaduni, mazingira n.k. imekuwa ikilazimika kwamba mwanamume mmoja awe na mwanamke mmoja. Lakini hii inakuwa ni kinyume na hamu ya asili/utashi wa mwanamume.

    Mtakubaliana nami kwamba, karibu kila mmoja wetu anayesoma au kuchangia hapa, babu au mababu zake, kihalali, zamani hizo, walikuwa "wanamiliki" wake zaidi ya mmoja.

    Na pia kwa wanaume (rijali) mtakubaliana nami kwamba, kila unapomwona mwanamke (ambaye si mama yako, au dada yako, au ndugu yako wa karibu) ile tamaa ya asili huwa inaamka, inawaka, haya ni maumbile na imewekwa hivyo na mwenyezi Mungu.

    Sasa dada yangu, unapoona mumeo kila siku yupo moto chini, anataka kama inawezekana mara tatu kwa juma, ujue kwamba hayo ni maumbile asilia.

    Kwa wanawake kwa kweli inakuwa ni tofauti, haya nayo ni maumbile yao. Mara nyingi mwanamke atajisikia hamu ya mwanamume siku chache katika mwezi pale yai linapopevuka, lakini wakati mwingine wote, hamu kwake inakuwa si sana mpaka iamshwe.

    Sasa hapa ndipo ugumu unapojitokeza, "...mimi nataka, wewe hutaki, lakini kumalizia hamu yangu kwa mwanamke mwingine huniruhusu.......??!!!!"

    ReplyDelete
  45. Mama umefanya vyema kusema tatizo lako ukitegemea ushauri. Tatizo umekuwa na aibu ya kuficha contacts zako ambapo ushauri unahitaji kuuliza maswali na kushauriana kwa kila hatua.

    Hii ni profession yangu na nijambo ninalolipenda kufanya kwa maana ya ushauri wa mambo ya ndoa na mapenzi.

    Usisite. watu wanauliza maswali na kujibiwa iwezekanavyo.

    Niandikie mariamkude2@yahoo.com
    Please usisite
    Amini ni msiri na muelewa na tutasaidiana vyakutosha

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 11, 2009

    Dada kama walivyosema wengine, JARIBU KUFANYA MABO MAPYA KWENYE MASUALA,VAA VIZURI,JIREMBE UPENDEZE,TAARISHA CHUMBA CHAKO VIZURI,MANUKATO, KWAKO NA MUMEO,TAFUTENI MUDA TOFAUTI NA MAHALI TOFAUTI SIO USIKU TU KILA SIKU,TOKA NA MUMEO OUT MKAPATE KINYWAJI.MWANAMKE ANAPOKUWA NDIO ANAPATA HAMU NA KUPENDA ZAIDI MASUALA, MIAKA 35, NDIO KWANZA UNAANZA KUSIKIA UTAMU WA MAMBO.
    MIMI NA MMWENZANGU TULIBADILISHA UTARATIBU TUKALETA MAMBO MAPYA SASA AKA TUNAFURAHA TELE.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 11, 2009

    KINACHONISHANGAZA UMRI WAKE MDOGO SANA,MIMI NINA MIAKA AROBAINI NA TISA,UMRI UNAPOZIDI KWENDA NAONA KWA NINI SIONGEZEWI WAKATI MWENZETU HANA TAMAA KWA KWELI MAISHA NA MAUMBILE NDIVYO YALIVYO WENGINE TWA TAMANI WENGINE HAWANA HAJA YOTE MAISHA

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 11, 2009

    Mika 35, bado kabisa. usiwasikilize hao,Mapenzi wakati mwingine yanachuja hata ukiwa 18.Soma maoni yote kuna pointi nyingi za Muhimu,hao wanaoongea ujinga achana nao.kila la kheri na Pole Mama mdogo.

    Mdau-Kandoi Nzumbe.UK.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 11, 2009

    Mama pole sana kwa hali iliyokukumba, imekuwa ni vyema kwamba umeweka wazi swala hili kwani matokeo yake ni mabaya sana. Wewe unamatatizo ya kisaikolojia na yanatibika. Umri wako ni mdogo sana kupoteza hamu ya kufanya mapenzi na mumeo. Tatizo ni kwamba mumeo sasa hivi lazima atakuwa na kimada nje kama sio mmoja itakuwa ni zaidi. Hatari ni kwamba kwa hali ilivyo sasa hivi ya magonjwa ukifanya mchezo mtapoteza maisha yenu mkiwa bado na umri mdogo. Mkumbuke mna watoto wanaohitaji kulelewa na ninyi wazazi wawili na kusomeshwa shule. Sasa inabidi uwahi kabla mambo hujayaharibu wewe mwenyewe kwa mikono yako. Usije ukamlaumu mumeo kwamba amekuletea gonjwa ndani ya nyumba tatizo litakuwa ni wewe mwenyewe umelisababisha kwa kutompa unyumba. Na wanaume sio wavumilivu wanahitaji unyumba hata mara tatu kwa siku. Cha kufanya tafuta daktari wa mambo ya wanawake akupe ushauri na wala tatizo lako halihitaji dawa linahitaji therapy ningekuwa karibu ningekusaidia.
    Kuna mambo unayotakiwa kuyafanya na mumeo pia anatakiwa kufanya ili kurudihsa ile hamu ya kujamiiana kama ilivyokuwa mwanzo wenu wa mapenzi.
    Inabidi umshirikishe mumeo mapema ili muanze kulifanyia kazi kabla mambo hayajaharibika kwani itafanya ndoa yako isiwe na amani tena.
    Kuna mambo mengi ya kufanya kwanza tafuta picha za watu wanaofanya ngono kisha angalia wewe na mumeo aina mbalimbali za stail zinazotumika, inaelekea kwa miaka yote ya ndoa yeni mnafanya style moja ya kifo cha mende, na vile vile ni mnarukiana tu bila hata kushikana na kuleta ile hali ya kufanya tendo la ndoa. Uelewe kitu kimoja tendo la ndoa ni hatua ya mwisho katika kufanya mapenzi, unahitaji kubadilisha mazingira ya kufanya mapenzi wakati mwingine sio kitanda kile kile na mtindo ule ule miaka nenda rudi.
    Kuna mambo mengi ya kufanya ila inaelekea mnahitaji somo la mambo ya ngono. Kwa ushauri zaidi wasiliana na mimi nikupatieni vitabu na DVD zitakazowasaidia katika kurudisha hali ya kupenda kufanya tendo la ndoa.

    ReplyDelete
  50. Dada, umeleta tatizo lako pabaya.

    Kwanza demographics ya Michuzi hamna wazee humu ambao wanaweza kukueleza kama hamu yao katika kipindi fulani huwa inaisha. Maana umeuliza kama hii hamu ya wanaume huwa inaisha, na kama inaisha, inaisha lini?

    Badala yake vijana wa humu, wake kwa waume, ambao wamelelewa katika mfumo dume, wanataka kukupa ushauri kuhusu jinsi ya kupata hamu na kuendelea kumfurahisha mumeo. Wakati wewe umeshasema hutaki tendo hilo period.

    Wengine wanakwambia uruhusu mke wa pili humo ndani, wana assume kwamba huyo Bwana wako ni Mengi au Manji anaweza kusapoti wanawake kibao. Wewe umeuliza jinsi ya kuendelea na ndoa hiyo hiyo wakati hutaki kufanya mwenzio anataka.

    Wengine humu wanakwambia ongea na mumeo, wana assume hujaongea. Hatujui. Na kama bado, inaweza kuwa ni false move kumfahamisha mumeo kwamba mnapofanya, wewe huwa umelala kama gogo. Hata akiendelea ndio hapo mwanzo wa utungu, na vimada na ukimwi.

    Ushauri wangu, nenda kwa professional. Kuna maswali inabidi uyajibu huko, hapa hakuna dialogue kati yako na unaowataka misaada, isitoshe si wazoefu wa ndoa hawa kutokana na demographics yao na background yako. Angalia hata wanavyo andika. Haiwaingii akilini wakisia mwanamke anasema hataki tendo hilo, hawakulelewa hivyo hawa product wa mfumo dume. Professional atakuelewa, sio hapa kwa Michuzi.

    (Michuzi usiogope ku publish hii posti, blogu yako ita grow ikionekana inakaribisha wigo mpana wa michango. Huwa hau publish baadhi ya maoni kosoa. Blog inapaswa kuwa na moderation, lakini wewe hujui nini cha ku posti na nini cha kuminya. Usiminye critics wa MICHUZI, minya matusi.)

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 11, 2009

    POLE DADA HAUKO PEKE YAKO NA POLE KWA MUMEO. HIYO NI HALI INAYOWAKUTA WANAWAKE WENGI SANA SIKU HIZI WENGINE WADOGO TU. CHANZO NI MIAKA YA KUTUMIA MADAWA YA KUZUIA MIMBA AMBAYO HAPO BAADAE YANABADILISHA HORMANE BALANCE ZA MWANAMKE NDIO MAANA SIKU HIZI KUNA MADAWA MENGI YA KUBALANCE HIZO HORMNES ILA NA ZENYEWE ZINA MATATIZO KAMA BREAST CANCER AND OTHER CANCER. POLE SANA DADA HAUKO PEKE YAKO TUKO WENGI. MIMI HATA KUSIKIA NENO LA KUFANYA TENDO LINANITIA KICHEFUCHEFU!!!!

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 11, 2009

    Pole dada mimi nakukaribisha kwenye blog ya harusi yangu, huko utakuta wanawake kibao wenye issue nyingi sana, pliz karibu sana huko tutakusaidia sana huko kuliko hapa, hapa naona point of view ya wanaume inaanza kuniboa kishenzi, huko pia kuna wanaume lakini watakupokea na kukushauri vizuri kuliko wajinga wanaokuambia eti una kijana anakupa raha upuuzi mtupu, pliz google harusi yangu uandike topic yako tutakushauri vizuri naona kama hapa si mahala pake, mwanamke mwenzio
    Judith.

    ReplyDelete
  53. Vere simpo, anza kufanya mazoezi na muda si mrefu hali itabadilika. Na pia kama unakipato kizuri unaweza kwenda safari za hapa na pale wakati wa wikiendi naamini itasaidia sana. Mazingira ni muhimu sana kwenye habari ya ngono. Badilisha mazingira, fanya mazoezi na mabadiliko utayao. Unadhani kwa nini mimama ya kizungu inakimbilia Gym kila siku na kuishia kulala na matraina?

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 11, 2009

    Ushauri
    a) Angalia kwanza kabisa kama una maradhi sugu yatokanayo na intecourse mfano:- Fungis sehemu ya siri, gonorea, syphilis,(hii inakaa hata miaka 20) etc ulishawahi kuumwa nenda fanya medical check up
    b) Sycholigia kama walivyosema wengine
    c) Una "kinembe" kama ulikatwa kinembe then hamu inapungua sana kwa kina mama lakini maandalizi ya muda mrefu, sychology itakusiadia
    d)Ama kuhusu Umri wako "BADO KABISA" mimi nina mke ana miaka 38 ni moto ile mbaya, tunakula raha miaka 15 ndani ya ndoa dont loose hope Dakatari wa kinamama UK

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 11, 2009

    U need to spice it up, like more foreplay, try Oral sex and see How it works out, ur too young not to enjoy sex, try outside ur home or different room, may be the guy is boring u both need to read more about sex life or rent movies u never know

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 11, 2009

    Huyo mumeo hajawahi kukuterera yaani kukupa katerero western staili? Angekuonjesha hiyo kitu usingekuwa unalalamika hapa!

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 11, 2009

    mimi naomba nikupe ushauri offline:
    tuma email rahaleo.leo@gmail.com
    nitakupa jawabu la tatizo lako!

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 11, 2009

    Pole sana dada, ushauri wangu ni kuwa usiwe selfish sana na mumeo kaa nae muongelee kitu hicho pamoja na mtafute solution before third part, hilo tatizo sio peke yako ni watu wengi yanawasibu lakini cha msingi ondoa hofu na rudi katika hali ya kawaida huku mkipeana mawaidha na mwenzio. Mkiona hali ndio kwanza inazidi hapo itabidi muwaone wataalamu wa maswala ya saikolojia. Karibu sana.

    ReplyDelete
  59. NungununguMay 11, 2009

    Duh!! Nimeamini waswahili interest yetu ni NGONO, NGONO na NGONO 24/7..angalia jinsi jamaa wanavyochangia hii mada! Si vibaya..ila swali: Mbona mada zingine za uchumi au jinsi ya kuendelekeza nchi yetu, moto kama huu hatuuoni??...Anyway natumaini dada yetu amepata ushauri utakaomsaidia kudumisha ndoa yake.
    Waasalaam,

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 11, 2009

    1) mumeo ni mchagga nini? Wale wakusema mama nanii jiandae nakuja home. Labda romance imeisha ndani ya nyumba. kama romance ipo basi

    2) tumia vitamins unadeficiency fulani imepungua kwenye mwili wako

    3)Find (ME TIME) - wanawake bongo tunafanyakazi 24/7/365 na wala hatuchukui muda wakujitunza na kucharge back the energy. Find muda uwe unarelax, massage, hata utafute rafiki zako mfanye girls night mara moja kwa mwezi.

    4. Mwambie mume huyo you need a date night too. Wanaume wakibongo wakishaoa basi dating nayo inaisha. Nenda alone na mume wako out hata mara moja kwa mwezi.

    Wanaume wa kibongo wanahitaji lesson sana kuhusu haya majambo. Sio bongo tu hata huku nje ya nchi. Mume wangu yeye alikua kila siku kuhang out na rafiki zake jioni mimi nipo home na watoto peke yangu. Akija home ndio hivyo yeye yuko so ready lakini miye there was nothing stimulated me zaidi ya watoto vilizi the whole day alone. Mind you I had my career na sasa nipo home natunza watoto, no adult conversation siku nzima. Ndoa yetu ilikuapata kashi kashi. Nilimwona DR na nilikua sina tatizo lolote. couceling na pastor juu ndio mwanamume akaamka na kufungua macho. Right now things are not 100% lakini we are getting there.

    Wish you all the best

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 11, 2009

    dah! waswahili kwa ngono, ona coment zilivotiririka, anyway swali lilikua zuri na maoni mazuri, cjaoa bado lkn naomba mungu ncpate mke km ww

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 11, 2009

    35 unapaswa kuwa bado moto. Ungekuwa 45 tungefikiria menopause. Niliwahi kuona kipindi cha Oprah akizungumza na watu wenye tatizo kama lako, na njia za kuepukana nalo. Kwa ujumla ni saikolojia tu baada ya kuzoeana na mumeo na hatimaye mnaishi kama dada na kaka. Mnaacha mambo muhimu ya mapenzi kama kissing, outing, touching, jocking etc. Jaribu kutafuta DVD hiyo ya Oprah, ni very interesting na kuna feedback wahusika wanatoa baada ya ku-rekendle their love baada ya ushauri wa kivitendo wa wanasaikolojia. Ukiacha hali hiyo iendelee ndoa lazima itakumbwa na msukosuko usiotarajia...nyumba ndogo, bi mdogo, malaya nk wataingia katika nyumba yako!

    ReplyDelete
  63. JAMANI WATANZANIA HEBU TUACHE NEGATIVE MTU KAOMBA USHAURI BADALA YA KUMUELEZA NINI AFANYE,MNAANZA KUMSHUTUMU HATA MIMI NI MWANAMKE NA NIMETUMIA SANA SINDANO ZA KUZUIA MIMBA ,MATATIZO HAYO NAYAPATA NA NIKITU KINANISUMBUA SANA SINA TATIZO NA MUME WANGU HATA YEYE ANALIELEWA FIKA,KWAHIYO MTU ANAPOOMBA USHAURI TUMSAIDIE KUMUELEZA KUWA AMUACHIE MUME ATOKE NJE UKIMWI UTAISHA KWELI ULIZA WANAWAKE WANGAPI WA UK WANATATIZO HILO (DEPO-PROVERA)INAFANYA KAZI ANGALIA HISTORIA YA DAWA ZA UZAZI WANAWAKE WENGI HAWANA SIKU MAALUM ZA KUTUMIKA MAMBO YAMEHARIBIKA,NA MA1DAKTARI WANASHAURI UTUMIE CHOCHOTE ILI KULAINISHA KIMA ACCORDING TO DR WILLIAM READING,ROYAL BERKSHIRE HOSPITAL,UK......TUWE NA USHAURI WA MAENDELEO

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 12, 2009

    Tatizo mumeo tu! Angekupiga maufundi ungetamani kuwa nanihii! Mpe jamaa e-mail yangu nimpe skuli. Hii kazi rahisi sana. Nenda kwenye google, halafu andika neno "sex", kisha click kwenye kiboksi cha "I'm Feeling Lucky," utaona kivumbi yake. Ukimaliza hii, nitafute.

    Kisha acheni kufanyia chumbani, hamieni jikoni, ukumbini, nendeni baharini kama mna gari, safirini mikoani, vaa shanga, jamaa naye mwambie apige deki - asione haya, siyo anajitupa tu. Halafu mwambie atumie manukato ya kutia hamu.

    ReplyDelete
  65. AnonymousMay 12, 2009

    JAMANI JAMANI MSIMSEME SANA HUYO DADA HMJAFIKWA NYIE, NMAPA POLE NAJIPA POLE PIA KWANI HALI HIYO NILIZANI MIMI TU KUMBE KUNA BAADHI YANAWAKUTA, MIMI BINASFI HALI HIYO NINAYO TENA NINA UMRI WA MIAKA 32 NA WATOTO WAWILI ILA NAKUBALIANA NA WADAU WALIOSEMA KWAMBA HALI HIYO INATOKANA NA TATIZO LA SAIKOLOJI : PIA UCHOVU, MAUDHI, MSONGO WA MAWAZO ULEZI WA WATOTO SASA MIMI NALEA WANGU NA WASO WANGU HAPO NDIO BALAA YAANI MPAKA MZEE AKIJA NASHINDWA KUMFURAHI INGAWA SIONYESHI WAZI IKIFIKA ANATAKA MAVITUUUUUUZZZZZZZZI NDIO KABISA CHUKI INAZIDI LKN NAMEZEA TU... AGH! BASI NDIO HALI HIYO WAKATI MWINGINE NAAMUA TUTOKE ANGALAU NI REFRESH MIND THEN TUKIRUDI KIDOOOGO KUNAKUWA NAKAUNAFUU FLANI KWENYE MAJAMBOZI. SO BI DADA KAMA MDAU ALIVYOSEMA PELEKA WATOTO KWA BIBI, MJOMBA AU SHANGAZI MWISHO WA WIKI MOJA HIVI HALAFU WE MZEE MKUMBUSHIE ENZI ZILEEEEE KAMA MKO HIGH SCHOOL VILE...

    ReplyDelete
  66. AnonymousMay 12, 2009

    Pliz anon wa-May11, 1009 6.31pm Umenifurahisha kwa ushauri wako mzuri, mimi nina umri wa miaka 32, sijapata tatizo kama la dada huyu lkn ilishanitokea nikawa simpendi mpenzi wangu wa mda mrefu na sitaki kusikia tendo la ndoa nae, ukweli tuliachana sikujua tatizo ni nini japo hakuwa akinifurahisha hata kidogo ktk suala la mapenzi na uhusiano, nilipopata niliyenae sasa naenjoy na sitaki kumpoteza hata kidogo, na ninaogopa lisijenikuta tatizo kama la dada hasa ukizingatia wazoefu wengi wanasema linatokea na lipo. Ombi langu kwako natamani kupata hivyo vitabu na dvd ulizosema unazo kama unauza pliz nazihitaji. My contact ni Email. jbabycandy@yahoo.com

    ReplyDelete
  67. AnonymousMay 12, 2009

    Tatizo kubwa liko kwa wanaume. Wadau wamechangia sana lakini ukiangalia ushauri ni kwa dada yetu hapa kumridhisha mumewe tu kwa njia yoyote ile au kwenda kwa "shrink", au kanisani n.k. Hebu jichunguzeni wanaume muone ni mara ngapi mnawasaidia wake zenu kazi za nyumbani ili nao waweze kufurahia tendo la ndoa wakiwa fresh? Halafu kuna mida iliyo ya ajabu ambayo ndio wanaume wengine wanataka tendo la ndoa bila kujali hata amemuamsha mkewe kutoka kwenye usingizi alioupata kwa shida baada ya kuhudumia familia nzima. Halafu suala jingine wanaume wa Kibongo siku hizi wameanza mtindo wa kuwategemea wake zao kwa kila kitu. Mwanamme atazurura mchana kutwa haleti kipato chochote nyumbani anategemea mkewe ambaye amepata anayechacharika. Mke akiuliza matumizi hasira wanaume wengine wanahama chumba kabisa na saa nyingine kulala kwenye gari. Huyo utapoteza muda wa nini kumbembeleza? Wengine wanaume nao wameathirika anakuwa ngoma haichezi dakika moja kusimama inakaa. Huyo anaamua kuweka ukuta kwa mkewe asimchokoze na mke anasema alhamdulilahi wacha nipumue. Haya mambo ni very complex.

    ReplyDelete
  68. AnonymousMay 12, 2009

    we kama umemchoka mumeo mwambie acha kuficha,

    ReplyDelete
  69. Katika komenti zote mi nimemkubali anon wa May 11, 2009 11:14 AM (huyo wa kwanza kabisa juu).

    Jamaa katema pointi ya nguvu sana ... lakini kwa sababu ya mazoea watu wengi wanaweza kupinga. Ila ukicheki wanaume wenye ndoa zao jinsi wanavyopenda dogo dogo ndio utaamini kuwa mwanaume ni mtu wa kuchapa chapa. Halafu wengine ni wasiri kweli, unaweza kusema mwanaume wangu katulia wala hana tabia hiyo lakini siku huna hili wala lile unashangaa mtoto wa nje huyo kazaliwa.

    ReplyDelete
  70. Katika komenti zote mi nimemkubali anon wa May 11, 2009 11:14 AM (huyo wa kwanza kabisa juu).

    Jamaa katema pointi ya nguvu sana ... lakini kwa sababu ya mazoea watu wengi wanaweza kupinga. Ila ukicheki wanaume wenye ndoa zao jinsi wanavyopenda dogo dogo ndio utaamini kuwa mwanaume ni mtu wa kuchapa chapa. Halafu wengine ni wasiri kweli, unaweza kusema mwanaume wangu katulia wala hana tabia hiyo lakini siku huna hili wala lile unashangaa mtoto wa nje huyo kazaliwa.

    ReplyDelete
  71. AnonymousMay 14, 2009

    Dah natamani kama kaka Michuzi ungelirudisha hili swali juu sababu naona linaishia lipo mwisho wa page....

    Huyu dada namuunga mkono kwani mimi ni mwanamke pia na nimekaa muda mrefu na mume wangu japo sijamsaliti....Hili tatizo lipo ila yatubidi kuweka heshima kwa waume zetu tujenge fikra...hisia za kulitamani kwani mlishaahidiana kuridhishana, kusaidiana...kuwa wote hadi kifo.....Hili tatizo lipo hivi:- Mwanamke anapokuwa na mwanaume mwanzo wa mapenzi huwa matamu sana na ndio maana hata unaona mfano wapenzi mkikutana huwa mara vizawadi, mara outing nyingi lkn kila mnapozidi kukaa inaanza kupunguza...Na pale mnapooana inakuwa kwamba umeweka akili kuwa yule ni wako tuu hata uende wapi ukirudi yupo tuuu mtaonana...Then labda mwanaume awe na style tofauti tofauti lkn mwanaume akiwa na style moja kila mara hii inaleta mazoea unajua aah tukikutana ni vile vile utamu wake unaujua style unaijua wakati mwingine unakuwa kama unakinai...Ni sawa na kula chakula cha aina moja mapishi yale yale kila siku..hata kama chakula ni cha aina ile ile japo mapishi yabadilike...siku nyingine mchemsho...siku nyingine kaanga ndivyo mapenzi yanavyokuwa...Watu wengi wamekuwa sio wagunduzi hasa watu wakishajua wameoana....

    Pia kinachochangia kingine ni kuwa ndani ya nyumba chumba kile kile style ya kitanda Room settings ile ile...Wkt mwingine haileti ladha ya mapenzi...Inahitaji kila baada ya miezi kadhaa unabadilisha mpangilio wa chumba mara kitanda kikae hivi mara vile ndivyo inavyotakiwa na mipangilio yote ya chumba ibadilike... au mkiamua mnaamua kutoka kabisa nyumbani mnaenda labda hoteli nzuri mbadilishe mazingira..hapo hamu ya mapenzi inakuwepo.......

    Pia kwa wale wenzangu waislamu tunafundishwa...Mwanume anatakiwa sio kila siku perfume akuzoee ile ile..Mara wakti mwingine unajipulizia perfume, wkt mwingine akija anakuta chumba kinanukia udi na wewe mwenyewe udi...Wkt mwingine...HII SIO TUU KWA MWANMKE NASEMA IWE NA HATA KWA MWANAUME UONEKANE TOFAUTI sio style moja tuu..kwani wewe mwanaume unahitajika kuwa mjanja kama unampenda mkeo ujibadilishe badilishe...Toka mpeleke mkeo hoteli...Safirini wkt wa livu hata mkoa mwingine...Mfanyie mkeo suprise za vitu...Siku nyingine ukirudi kazini kama ulishazoea kuja tuu na kukaa siku nyingine anzia mabusu mlangoni...cheza nae kama mtoto....mtanie tanie kwani nyie pia ni watani akinuna unambembeleza...Usiwe mkali wkt wote....Pia ngono/mapenzi sio kila siku kama dozi pumzishaneni siku mkikutana mnakuwa na hamu wote....Siku nyingine unakuja na maua fresh unamletea mkeo angalau mahaba yanaongezeka...Siku nyingine ukija home unaanza kufanya kazia au weekend unamwambia mkeo kaa wewe unapika unafanya kila kazi...Hapo naamini mapenzi hayata chuja wala mwanamke hata kinai mapenzi kwakwe wewe mwanaume...Pia style za kudoo sex ibadilike sio mwanaume kila leo style moja tuuu no no no...Kuwa mtundu...jifunze....HAYO NDIYO MAONI YANGU MIMI MAMA YENU....Nina mengi ila kwa leo yametosha haya..

    ReplyDelete
  72. AnonymousMay 14, 2009

    Nimerudi tena mama yenu...Nimesahau....Wkti mwingine ni kazi ngumu zinachangia wewe mwanamke kutokuwa na hamu ya mapenzi...Mawazo mengi...Ugumu wa maisha...Wkt mwingine labda na mwanaume anabadilika ndio maana unakuwa huna hamu na mapenzi yake.....Nakusihi mwanangu jitahidi kujicontrol urudishe hali iwe kama zamani shetani asiingilie ndoa yenu...Jibadilishe..Mbadilishe mumeo naye muambie...Najua wanaume wengine wanajifanyaga vidume hawapendi kuambiwa ila si vyema wafanyavyo..Jitahidi kumuelewesha...Pia wkt mwingine safiri kidogo kama wiki ukirudi utakuwa na hamu ya mumeo....Kama pia zamani mlikuwa mnatoka pamoja sasa hivi hamtoki pamoja mapenzi hayata kuwepo tokeni pamoja msikubali uzee... Mabaa mengi kaleni nyama, vinywaji...nendeni disco tokeni mbadilishe mazingira sio kila leo tuu mnakuwa home mnakula hapo hapo kwani mwanamke sio km mfanyakazi....Mabusu yawe mengi mtokapo....Vaa vizuri, Mumeo avae vyema mtegane..Sio kila leo mumeo yeye kuvaa shati tuu suruali ya kitambaa...Ajiangalie kama anafaa kuvaa jeans avae akumbuke ujana...Tshirt......

    Nawatakia mema wanangu....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...