Meneja wa promosheni na matukio wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (katikati)akiongea na wanahabari juu ya upimaji wa afya katika maandalizi ya kushiriki mbio za Vodacom zitakazofanyika tarehe 20 mwezi ujao. wanamichezo watapimwa Afya zao na tarehe 21 Mei ambapo wote wanaopenda kushiriki mbio hizo watapimwa Afya zao.(kushoto)katibu wa Afya Club Dr Deogratus Pissa,(kulia)Mwenyekiti wa chama cha riadha Dares Salaam Christin Malundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2009

    sasa michu na hawa voda wako? tarehe 21 mei si imepita jamani? au ni mwaka ujao? Na huyo wa kushoto mbona hatumuoni?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2009

    TAFADHALI
    RUKIA MTINGWA SI MWANAMUME!!!!!!!

    "KATIKATI"

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2009

    Please katikati hauna macho wewe kaka lol! Rukia yupo kushoto !

    ReplyDelete
  4. Baba UbayaMay 29, 2009

    hiyo May 21st watapima afya zao au walishapimwa?na huyo Rukia si huyo mrembo wa kushoto?hapo katikati me namwona mwanaume.ama sijui labda macho yangu tu haya ya uzee.acheni kutuchanganyia habari.next time jaribu kusoma tena unachoandika kabla hujaposti.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2009

    Ningependa kutoa ushauri wangu kuhusu habari za michezo katika blog hii.Mara nyingi hua naona ni soccer ndio inapewa kipaumbele,sana sana ligi za ulaya!! sioni habari za michezo ya tanzania kwa ujumla.Michezo iko mingi na sio kila mtu anapenda soccer.ningeomba uwe una report michezo ya aina yote ili tulio nje tuweze kujua tanzania kuna michezo gani ambayo inachezwa na pia hii itasaidia kuitangaza michezo hiyo na wanamichezo wake.nachoshwa na habari za soccer la ulaya.Je, tanzania hakuna wanariadha,wacheza tennis za aina zote,waogeleaji, rugby,cricket,au michezo yoyote tu ambayo inachezwa tofauti na socccer.kwasababu soccer yenyewe inayoongelewa hapa ni ya ulaya tu.Inachosha kwasababu habari za soccer za ulaya zinapatikana kila mahali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...