wakati wa mkutano na waandishi habari ukumbi wa maelezo, dar
MASHINDANO ya urembo ya kumsaka kisura wa Tanga (Miss Tanga 2009) yanakuja kupitia kampuni yetu ya Five Brothers Entertainment yenye maskani yake mjini Tanga.
Kampuni hii inachukua jukumu hili zito ikiwa ni baada ya vitongoji mbalimbali vya Tanga kumalizika, tumekusanya krimu ya warembo bomba waliokamilika kila idara kutoka Miss Lushoto, Miss Korogwe, Miss Centeral, Miss Usagara, Miss College na Miss Ngamiani pamoja katika kambi moja ya Miss Tanga 2009 iliyoanza tarehe 19 Mwezi huu tayari kwa mashindano.
Warembo hao wanaendelea kunolewa chini ya walimu wao, ambao ni balozi wa Redds 2007, Miss Tanga na Miss Kanda ya Kaskazini 2007 Victoria Martin na Oliva Mango, Miss Tanga namba 4, 2008.
Lengo letu hasa ni kuboresha mashindano haya kuwa katika kiwango cha kimataifa, kama kauli mbiu yetu mwaka huu inavyosema, FULL RESPECT na Pia kuhakikisha kuwa safari hii Tanga inatoa wawakilishi walioandaliwa vema na wataoweza kutoa changamoto katika mashindano ya dunia.
Ni kweli tumedhamiria kulichukua taji la Taifa na mrembo wetu kufanya maajabu ambayo hayajawahi kufanywa katika mashindano ya urembo, Miss World 2009.
Malengo haya ni mazito na hayawezi kukamilika bila ushirikiano mwema wa walimu, warembo wenyewe, wazazi wa warembo hawa kamati ya Miss Tanzania, ninyi vyombo vya habari, wadau wa mashindano haya ya urembo na wadhamini kushirikiana nasi katika zoezi hili la kuwapata wawakilishi bora ili kutimiza adhma hii.
Fainali za mashindano haya ya Miss Tanga 2009 zitafanyika Juni 6 katika uwanja wa mpira wa Mkwawani ambapo zaidi ya warembo 20 watachuana kuwania taji hilo.
Kupitia mashindano hayo pia tuna mataji mbalimbali kushindaniwa kama Miss Talent, Miss Ishi, Media choice award, Miss Photogenic na Miss Popularity.
Washindi wa mataji hayo yote watajulikana tarehe 6 Juni, kwenye uwanja wa mkwakwani siku ya Shindano la Miss Tanga, lakini ili kupata nusu fainali ya miss Talent tumeandaa shindano jingine tofauti kabla ya mashindano hayo.
Miss Talent tumepanga kulifanya tarehe 29 May 2009, katika ukumbi wa Club Lakasa Chika, na litapambwa na burudani ya muziki kutoka kwa DJ maarufu nchini pamoja na kundi la Wakali kwanza, linalotengenezwa na wasanii watatu, Makamua, Q-Jay na Joseline, wengine katika kusindikiza shindano hilo wapo wasanii kutoka Tanga, Roma na Dulla wa Michano. Majaji ni pamoja na msanii wa maigizo Dude na Mr Ebbo.
Kwenye upande wa burudani katika shindano la Miss Tanga lenyewe tumejipanga kuwa na burudani za uhakika, tayari kampuni yetu imekwisha fanya mazungumzo ya awali na wasanii kadhaa hapa nchini na hata 'nje ya nchi'.
Kama tulivyosema tunataka kuboresha katika hadhi ya kimataifa zaidi.
Ambao tayari tumeshafanya nao makubaliano mpaka sasa ni msanii mahiri wa bongo fleva, mshindi wa tuzo ya msanii bora wa hiphop kwa miaka mitatu mfululizo, msanii mkali kuliko wote, wanamwita Chi chi chi chidi BENZ.
Ambao tayari tumeshafanya nao makubaliano mpaka sasa ni msanii mahiri wa bongo fleva, mshindi wa tuzo ya msanii bora wa hiphop kwa miaka mitatu mfululizo, msanii mkali kuliko wote, wanamwita Chi chi chi chidi BENZ.
Mwingine ni Berry 9 anayetamba kwa sasa na wimbo wake wa 'Sumu ya penzi... ukishairamba hata kwa maziwa huwezi kupona.' Na mwingine ni mkali wa Tanga, mshindi wa tuzo mbili za kili mwaka huu, Seif Shabani, pengine mtamfahamu kirahisi zaidi kwa jina la Matonya. Kutoka nje ya nchi tutawatangazia hapo baadaye.
Kwenye upande wa zawadi ni mapema mno kuzitaja, lakini ukweli ni kwamba tumeboresha suala la zawadi kwa mwaka 2009, tutatoa zawadi ambazo tunaamini zinakuja kubadilisha maisha ya hawa warembo.
Mpaka hapa tunapenda kuwashukuru sana wadhamini ambao tayari wamekwisha jitokeza kudhamini mashindano haya ikiwa ni pamoja na Vodacom Tanzania, Redds Premium cold, ambao ndio wadhamini wetu wakuu, CRDB Bank-Tanga Branch, Maziwa Tanga Fresh, Hotel Kola Prieto, Sofia Productions, Vayle spring, SD supermarket, DARWORTH, DOLLYWOOD TZ na Gazeti la Mwanasoka.
Labda tuwapashe kidogo tu kuhusu Kampuni yetu ya Five Brothers Entertainment, kampuni hii inahusika na utayarishaji wa matamasha mbalimbali. Tunao uzoefu wa kutosha katika shughuli hizi hapa nchini na hii ni fursa adimu na muhimu kwa wadhamini kushiririkiana nasi kama watataka kujitangaza ama kufanya kazi nasi.
Inaweza pia kuwa fursa ya kubadilishana uzoefu, kufahamiana na pia kupata kazi za matunda ya kampuni yetu. Huu ni wito na mwanzo mwema wa kujenga ushirikiano wetu kwao wadhamini na kwao kwetu.
Tunaacha njia zetu za mawasiliano wazi kwa yeyote anayetaka kudhamini na kufaidika na mpango huu, ...anaweza kuwasiliana nasi kupitiasimu nambari: 0713 711413/0713 256 884
Kwa barua:-
Kwa Mkurugenzi,
5brothers Entertaiment,
P.O.Box 14036
DSM.
Mwisho kabisa tungependa kutoa shukuru za dhati kwenu ninyi waandishi wa habari, wadau mbalimbali walioshirikiana nasi kwa namna moja ama nyingine, wadhamini, Kamati ya Miss Tanga, Kamati ya Miss Tanzania, Waandaaji wa vitongoji mbalimbali vya Tanga, Walimu, bila kuwasahau mashabiki na yeyote ambaye ingestahiki kupata pongezi hizi, japo kimya kimya.
Tunakukaribisheni sana, kushiriki nasi katika kuipa Tanga ramani yake na heshima inayostahili, hapa Tanzania na duniani kote. Ahsante sana na karibu!
Mwisho kabisa tungependa kutoa shukuru za dhati kwenu ninyi waandishi wa habari, wadau mbalimbali walioshirikiana nasi kwa namna moja ama nyingine, wadhamini, Kamati ya Miss Tanga, Kamati ya Miss Tanzania, Waandaaji wa vitongoji mbalimbali vya Tanga, Walimu, bila kuwasahau mashabiki na yeyote ambaye ingestahiki kupata pongezi hizi, japo kimya kimya.
Tunakukaribisheni sana, kushiriki nasi katika kuipa Tanga ramani yake na heshima inayostahili, hapa Tanzania na duniani kote. Ahsante sana na karibu!
NAS ES COBER
MKURUGENZI
FIVE BROTHERS ENTERTAINMENT
Yvonne Ridley - Nilivyokuja Kuipenda Hijaab makao nimeikata ili ikubalike hapa acha mail nukutumie full text)
ReplyDeleteNilikuwa nikiwaona wanawake wanaojisitiri ni kama, viumbe waliodhulumiwa - mpaka nilivyokamatwa na Taliban.
Katika mwezi wa tisa mwaka wa 2001, masiku 15 baada ya mashambulizi ya kigaidi katika nchi ya Marekani, Nilikamatwa ndani ya Afghanistan, nikafunikwa kutoka kichwa hadi vidole vya miguu kwa burqa ya rangi ya samawati, nikiwa nimedhamiria kuandika gazeti kuhusu maisha chini ya uonevu wa mfumo wa utawala. Badala yake, niligunduliwa, na kukamatwa na kufungwa siku kumi. Niliwatemea mate na kuwatukana walionikamata; waliniita mwanamke “mbaya” lakini waliniachilia baada ya kutoa ahadi kuwa kuisoma Quran na kujifunza Uislamu. [kwa kweli, sina uhakika nani aliyekuwa mwenye furaha zaidi wakati nilipoachiliwa huru; wao ama mimi.]
Niliporejea nyumbani London, niliweka nadhiri yangu ya kujifunza Uislam na nilistaajabu kwa yale niliyoyavumbua. Nilikuwa natarajia kuona kutoka katika surah za Quran kuwa vipi kumpiga mke wako na kuwadhulumu watoto wako; badala yake, nilikuta dondoo za uimarishaji wa ukombozi wa wanawake.
Miaka miwili na nusu baada ya kukamatwa, niliingia Uislamu, kulisababisha mshangao, uvunjaji moyo na pia tashtiti miongoni mwa jamaa na marafiki.
Nilikuwa mwanamke wa kimagharibi kwa miaka mingi, lakini niligundua kuwa wanawake wa Kiislaamu ni wenye hadhi zaidi kuliko ulimwengu unavyofahamu. Tunachukizwa na maonyesho ya wanawake warembo, na hatukufurahia katika mwaka wa 2003 ambapo majaji wa mashindano ya Mrembo wa Dunia (Miss Earth) walipopongeza kuvalishwa bikini hadharani kwa mrembo wa Afghanistan, Vida Samadzai, wakidai kuwa ni mkombozi hodari wa uhuru wa wanawake. Na hata walimpa Samadzai zawadi mahsusi kwa “kutoa mfano wa ushindi wa uadilifu wa wanawake.”
Katika Uislaam, cheo cha juu hupatikana kwa kumcha Mwenyezi Mungu – sio uzuri, mali, mamlaka, cheo au jinsia.
Sikujua nipige kelele au nicheke wakati Wataliano walipojiunga kuchochea mjadala wiki iliyopita kwa kuarifu kuwa ni “kitu cha kawaida” kusivaliwe Niqaab, kwani kuvaa Niqaab kunasababisha mahusiano ya jamii kuwa “magumu sana.” Ni upuuzi! Ikiwa hii ndio hali, kwa nini simu za mkono, simu za ndani, barua pepe, ujumbe wa maandishi, na faksi ni katika matumizi ya kila siku? Na hakuna yeyote anayezima redio eti kwa sababu ya kutomuona mtangazaji!.
Wanaume wenye shari hawatoki kwenye dini mahsusi au aina fulani ya utamaduni; kulingana na utafiti wa pande zote za dunia, kila penye wanawake watatu mmoja miongoni mwao hupigwa, hulazimishwa kujamiiana au hutendewa vibaya katika maisha yake. Hili ni tatizo la ulimwengu mzima ambapo limekiuka taratibu za dini, utajiri, cheo, kabila na utamaduni.
Ni kweli kwamba katika nchi za Magharibi, wanaume bado wanaitikadi ya kwamba wao ni bora kuliko wanawake, ijapokuwa wanawake wanalalamika. Ingawa wanapata malipo bora kwa usawa wa kazi – ikiwa ndani ya chumba cha posta au chumba cha baraza la halmashauri – wanawake bado wanatendewa kama ni chombo cha starehe, ambapo nguvu zao na utendaji wao unaoporomoka wazi wazi kutokana na kuonekana kwao.
Na wale ambao bado wanajaribu kudai kwamba Uislam unawakandamiza wanawake; rejea kauli ya 1992 kutoka kwa mheshimiwa Pat Robertson, pale alipotoa maoni yake juu ya kuwapa mamlaka wanawake: “Mwanawake ni kujitegemea.” Yaani kutokuwa na familia ni kuendelea kisiasa, hii inawachochea wanawake kuacha waume zao, kuua watoto wao, kutenda uchawi, kuangamiza ubepari na wanawake kuwa wasagaji.
Sasa niambie nani ni mstaarabu na nani siye?
Yvonne Ridley ni mhariri wa siasa katika Televisheni ya Islam Channel iliyopo London na ni mtunzi mwandamizi wa kitabu "In the Hands of the Taliban: Her Extraordinary Story" (Robson Books)
Loo! Mratibu yuko bomba kweli, samahani ni miss wa mwaka gani?
ReplyDeletehakuna kitu kinaniudhi duniani kama mwanamke avae nguo halaf mikanda ya sidiria ionekane kwa bahati mbaya..aaaggghhhh
ReplyDeleteAsma makao mdogo wangu vipi tena. mimi nilikuwa nakuona pale radio uhuru unajistah mpaka naona raha, leo waenda kuvisha watoto wa tanga vijichupi? acha tafuta kazi nyingine utapa tu hiyo pesa.
ReplyDelete