kocha wa taifa stars marcio maximo  aongea na globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2009

    He got points. Wazushi semeni sasa zamu yenu....

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2009

    huyu mzee mbona anabwabwaja.. aende kwanza veta ingrish koz pale,then tutaongea

    ReplyDelete
  3. afande midakoMay 13, 2009

    hana nia njema na timu yaani mpaka leo hajui kuongea kiswahili ndo maana tunafungwa ujumbe unafika tofauti au haufiki sasa anawaelekeza vipi wachezaji? na kama ujuavyo wachezaji wetu staz sijui ni wangapi wamemaliza form 4 kama maofisini kwenyewe ndo hivyo ngeli zero, wadau nisaidieni

    next time TFF ktk kusaini contract mpya coach must be able to speak fluent swahili language within five months ni kwanini wazungu wanaokuja kufanya field tz jambo la kwanza huanza kujifunza kiswahili na wanaongea within 2months ndo ije yeye coach miaka mi3!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. SINA MAKOSAMay 13, 2009

    yah! He really knows what is doing! he's got a big plan to restore the lost glory!! No Bongo manager has ever come up with such strategic planning!!We need to offer him long term contract to profess his extraordinary expertise!
    I am very optimistic now than ever!!
    Thank you michuzi!keep up good work!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 13, 2009

    Mwaka jana Michu ulinibania stori niliyokutumia kuhusu suala la wachezaji wetu, mada yenyewe ilikuwa hii hiyo hapo chini na Maximo ameunga mkono:

    "Haya naleta issue nyingine, nilianza na waimbaji kuimba kiingereza ni njia pekee kutoka kimataifa. Sasa naleta football academy, nimewaangalia wachezaji wa timu ya Simba na Yanga, inasikitisha sana. Mimi naona sasa haya makampuni waanzishe a football academy kwa sababu wachezaji hawajapata lishe ya kutosha na mafunzo mazuri. Hebu waangalie wachezaji jinsi walivyo wadogo kweli tutafika, msimamishe Adebayor na mmoja wao, utaona jinsi gani tulivyo wadogo, namna hii hatutafanikiwa kufika katika African cup of nations. Hii yote na mengineyo mengi yanatupeleka ktk football academy run by these sponsors ambao wataweza kuwajenga wachezaji chipukizi kupitia mafunzo, lishe, na kadhalika. Kama sponsor mmoja ana uwezo wa kutoa millioni 600 kwa show ya Miss Tanzania basi itakuwa rahisi kuwalisha, kuwavalisha, kuelimisha wachezaji chipukizi kwa mwaka mzima wakiungana pamoja. Haya wadau hoja zenu muhimu hapa!"

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 13, 2009

    Waungwana kujua kiingereza sana sio tija...wezi wote wa EPA wanajua sana kiingereza lakini wamelifikisha wapi taifa letu..muhimu ni nia njema

    wasomi wote wanaopitisha mikataba mibovu wanajua sana kiingereza kinachoandikwa ndani ya hiyo mikataba, mbona kiingereza kimeshindwa kuwasaidia wakaweza kuliokoa taifa lao lisiangamie?..tuache kasumba zilizopitwa na wakati.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 13, 2009

    how cn u say anabwabwaja? Kuna mdau mmoja hapo juu anasema alikuwa anabwabwaja??? Tanzania, Now is time to get serious, people should start to get serious now, in order to critique positive way mtu unaongelea negative...

    English is all about accent, Maximo has Brazillian accent, but we understood what his plans.

    Kuna mdau mwengine anasema hajui kiswahili, hatutakii mema...mm naona its stupidity to say that, wadau tuanze kuwa serious.

    A topic here was soccer in Tanzania, about Taifa stars and youth teams. But instead of discussing what he said people just jump to somethng else. When there is a topic somebody needs to stay on topic, tusianzishe vengine.

    Kuna kitu wazungu wanaita Parliamentary Procedure...so when you listen to anything or orginise any meetings or even watch a movie au kuangalia article yeyote then, should follow those procedures it will help in staying on topic other than judging ujinga...inaonesha jinsi elimu inavyokuwa ndogo bongo...
    Watanzania wenzangu inafaa tubadilike, Nchi yetu ipo sehemu mbaya sana. Lets struggle kwa pamoja kuleta maendeleo kwa taifa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 13, 2009

    hey guyz i just found an interesting blog which we can all find usefuly stuffs
    www.youthtale.blogspot.com

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 13, 2009

    Watanzania lazimatujifunze kua na maono ya mbali. Huyu jamaa meongea mambo ya maana kiasi kwamba kama wewe ni muelewa utaelewa na kujua jinsi alivyo na mipango mizuri kwa nchi yetu hasa siku zijazo.
    Huyo aliyesema kuwa anabwabwaja nadhani hajui lugha AU kuelewa kwake ni kidogo.
    Nilikuwa nasikia maneno mengi juu ya huyu kocha lakini sasa nimemsikia mwenyewe. Tumuache akamilishe mipango yake, tupunguze kidogo lawama. Asante sana michuzi.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.
    Mdau Birmingham

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 13, 2009

    Michuzi kwanza asante kwa clip, pili out of curiosity kocha wetu hutumia lugha gani kuwasiliana na wachezaji wetu? it's amazing... najaribu kuconclude kwamba binadamu tunaweza kuwasiliana na kuperfom hata kama lugha ni tofauti au mtu hajui kuizungumza.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 13, 2009

    mdau kisiju.
    najiandaa nitakuja na nondo za kumjibu looser maximo. amemkataa godfrey bonny kuwa ana miaka 28 wakati fergusson kamchukua babertov akiwa na miaka 28 mwaka jana september.
    pia van der sar alisajiliwa 2005 akiwa na miaka 35 .
    maximo hajui kitu.aondoke.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 14, 2009

    Mdau Kamongo naingia.

    Kwanza naanza kwa kukushukuru kaka mchuzi kwa jitihada zako na mungu akujaalie.

    Nina mambo kadhaa ambayo ningependa kuzungumzia. Kwa uchache kuna wadau kazi kutupiana maneno wenyewe kwa wenyewe badala kuheshimiana na kuelewa kua hakuna hoja butu.

    Kwa wale wanaojifanya kua wasomi wangetakiwa kuelewa kua hata kusomea UDAKTARI unit ya Communication skills Lazima iweko. Kuna uwezekano mkubwa kuna gap ya mawasiliano kati ya kocha na wachezaji kwa sababu ya lugha. Hilo tusilipuuzie.

    Swala la gym alitakiwa alisisitize tangia siku ya mwanzo ya kazi yake lakini si leo baada ya miaka mitatu. Kwani swala la fitness kwa mchezaji ni muhimu sana hata ka uwezo wake ni mkubwa. Na kama hilo la fitness ni muhimu mchezaji kama godfrey bonny lazima angekueko kwenye timu. Kwani ki ukweli hakuna hata mchezaji mmoja wa kingo anae mfikia kiuezo, stamina na heshima nje na ndani ya kiwanja.

    Kama tunafuatilia sana mpira wa nje kwa walimu waliobobea majuzi Harry Regknap wa SPURS alisema kua mwakani atachukua wachezaji ambao wako kweye prime age ya nao nikuanzia 25+.
    Timu changa ya Arsenal ina strugle bila wazoefu, Man u walihangaika pia miaka ya nyuma mpaka chelsea wakachukua vikombe mara mbila mfululizo sasa huyu bwana mkubwa analonga nini??

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 14, 2009

    MDAU KISIJU.

    HANA KIPYA KILA SIKU ANAKUJA NA GEA MPYA.
    AMESEMA KINA BOBAN WANAVUTA BANGI NDIO MAANA HAWEZI KUWA NAO JEE WABRAZIL WENZAKE WAMEMKIMBIA JEE NAO WANAVUTA BANGI?

    MFANO TINNOCCO NA MWINGINE KAENDA KUTUMWA KWA BAKHRESSA KULIKO KUFANYA KAZI NA MAXIMO.

    MAXIMO SIO KOCHA KWANI KINA GAZZA,GEORGE BEST,STEVEN GERRARD,RONALDO ,ROONEY WAMEKUWA NA MAKOSA NJE YA UWANJA KAMA ULEVI AU KUPIGANA LAKINI HAWAJAFUKUZWA KWENYE TIMU ZAO.

    RIO FERDINAND PAMOJA NA UKOROFI WAKE KAPEWA U CAPTAIN WA MAN UNITED HAO NDIO MAKOCHA WENYE KUJUA KUTUMIA VIPAJI VYA WACHEZAJI.

    MARADONA ALIKUWA ANAKULA MADAWA YA KULEVYA NA SASA NI KOCHA WA TIMU YA TAIFA.

    MAXIMO ACHA KUKUZA HABARI KUWA BOBAN NI MTOVU WA NIDHAMU.

    MBONA PHIRI AU KONDIC WA YANGA HAWJASEMA KUWA CHUJI NA KASEJA HAWANA ADABU?
    MAXIMO ANA MATATIZO MAKUBWA YA AKILI HAFAI KUWA MWALIMU.

    AMELETA MAZEZETA WENGINE TOKA BRAZIL AMBAO HATUJUI VYETI VYAO WALA REKODI YAO.

    INAWEZEKANA NI WACHEZA SAMBA WA BRAZIL MACHONI TU HAWAONEKANI KUWA WALIMU WA MPIRA.
    KAZI YA MAXIMO NI MWALIMU?WAKALA WA MAKOCHA, MKUU WA UFUNDI WA TFF?

    MANAGER WA TIMU,AU MWANAUME MWENYE TABIA ZA UMBEYA KUWA OOH MAFTAH NILIMUONA NA CHUJI NAYE NAMFUKUZA TIMU YA TAIFA.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 14, 2009

    Huwezi kumlinganisha Godfrey Bonny na Babertov au Van der sar...Hao wachezaji wapo level nyingine...

    Kama umemsikia vizuri Maximo, anasema wachezaji wetu hawana afya, kipaji wanacho but afya hamna(Physical fitness).

    Kwahiyo wewe unaona bora kumchukua mchezaji wa miaka 28 ajengwe afya au bora kumchukua mchezaji mdogo ajengwe afya? ipi akili hapo?

    Sitashangaa kusikia Drodga kasajiliwa na mapesa mengi na ana miaka 30...kwasababu kakamilika, afya ipo.

    But Tanzania tunapeana sifa za uongo...sasa inabidi kushindana na international standards, tuache kugeana sifa za uongo...
    Watu kuwika humu humu ndani(i mean Tanzania) ndio wanaona wamefika...

    Wabongo tufunguke, sasa ni muda wa mabadiliko...kwahy tubadilike.

    Tumuache Maximo afanye kazi yake...
    But vizuri kuja na wazo lako, linaweza likawa sawa...bt the above is what i think...

    ReplyDelete
  15. Maximo anaongea lugha gani na wachezaji?

    Nimeishi Uingereza miaka kumi na tano, Kiingereza nasikia vizuri, lakini kwa Maximo nimempata kama 70% hivi. Uunasikia tu sasa hivi anaongelea nutrition, sasa hivi discipline, sasa hivi kunyanyua vyuma, lakini details hasa hupati.

    Kwa mfano, pointi ya stamina. Tunajua stamina ni muhimu, lakini sijamwelewa pointi yake ni nini haswa, hawapewi hela za kutosha kula, au wana utapiamlo? Tatizo lake ni nini? Kapewa timu miaka mitatu hadi sasa. Ukiingia gymn kama huna kazi nyingine maishani bali mpira na kunyanyua vyuma unakuwa fiti vibaya vibaya ndani ya wiki sita. Sasa huyu tatizo lake nini anasema? Haeleweki.

    Mchezaji mswahili wa kawaida wa Kibongo sidhani kama ataambulia zaidi ya 50% ya kinachotoka mdomoni mwa huyu kocha, tena hilo ni kadirio la juu haswa. Ni kwamba nusu ya instructions za huyu kocha wachezaji hawaelewi.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 14, 2009

    Si Ngasa ni mfano mzuri...Bongo wenyewe tunaona kakamilika, bt kufika westham kazi akawa anayo...afya ndogo. Hlf hiyo ni westham, hajaenda Liverpool wala Manchester...

    Mpira ni si mchezooo...Mm nimecheza sana mpira, i was big star bongo. nacheza 90mins na bado sichoki. But nimekuja huku kwa wenzetu mpira wao si mchezo. Strikers wanakupelekesha si mchezo. mara zangu za kwanza ilikuwa nikifika dakika za 40 hoi...

    Bt after attending physical fittness course and follow the balanced diet...sasa naweza kusema nimebadilika.

    Huku wanatu-train kuweza kuwa kiwanjani for 120 minutes...hlf kumbuka hii ni college tu, bt still are serious ktk hayo mambo.

    Nini kilichomponza Anelka wkt alipokuwa Arsenal na Real Madrid?Ni utovu wa nidhamu akaondolewa.

    nini kilichomponza Diouf Liverpool?? ni utovu wa nidhamu.

    Nini kilichomponza Pennant Arsenal? ni utovu wa nidhamu.

    Samaki mmoja akioza, wote wataoza. kama coach hatoweza kukemea utovu wa nidhamu wa mchezaji mmoja, ujue wengine watafata.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 14, 2009

    WAUNGWANA WAPENDA SOKA, KINACHODUMAZA MPIRA WA BONGO NI UENDEKEZAJI WA HULKA ZA KISWAHILI NDANI YA VILABU VYETU,MASHABIKI WA SOKA LA BONGO BADO HAWAJAELEWA KABISA DHANA NZIMA YA UKOCHA NA MAJUKUMU YAKE..WANAIANGALIA TAALUMA NZIMA YA UKOCHA KATIKA MTAZAMO FINYU SANA NDIO MAANA HAKUNA KOCHA YOYOTE WA MAANA ALIYEWAHI KUJA HAPA BONGO NA AKAHESHIMIWA

    MAXIMO ALIPOFIKA TU TANZANIA NA KUZIONA TIMU ZETU ALIZISHAURI TIMU ZETU ZIANZISHE TABIA YA KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI NA TIMU NGUMU KULIKO HIZI TIMU ZA KWETU..LAKINI MPAKA LEO YANGA INAJIANDAA KUCHEZA MECHI YA KIMATAIFA KWA KUCHEZA NA MIEMBENI AU JKT RUVU..HAPO UTAPATA KITU GANI KIPYA?..AL AHLY YA MISRI MWAKA HUU HUU WA 2009 INA MPANGO WA KUCHEZA MECHI KADHAA ZA KIRAFIKI NA TIMU BORA ZA ULAYA..KWA HIYO SIKU WATAKAPOKUJA KUCHEZA NA YANGA KWENYE KLABU BINGWA YA AFRIKA, WATAKUWA KAMA WANAFANYA MAZOEZI, HUO NDIO UMUHIMU WA KUENDESHA TIMU KISAYANSI..SASA UNAPOKUWA NA KIONGOZI KAMA DALALI, KIONGOZI AMBAYE HAWEZI HANA HATA ULE MUONEKANO WA KIONGOZI..UNATEGEMEA WAZO LIPI LA KISASA LITATOKA KWAKE...AKILI ZA AKINA DALALI NA MADEGA ZINAISHIA KWENYE MECHI ZA SIMBA NA YANGA TU.

    TUNAWEZA TUKATAFUTA KOCHA BORA KULIKO MAXIMO NA ANAYELIPWA PESA NYINGI KULIKO MAXIMO LAKINI KAMA UOZO ULIOPO SIMBA NA YANGA UKIACHWA UENDELEE BASI HATA HUYO KOCHA MPYA ATAONEKANA HAJUI LOLOTE, KUMBE USWAHILI WETU NDIO SABABU ITAKAYOMFANYA ADHARAULIKE MBELE YA JAMII

    MAPINDUZI YA SOKA YANAANZA KWENYE VILABU, VILABU VINAANZISHA PROGRAMU ZA MAZOEZI PAMOJA NA CHAKULA BORA NA HAPO NDIPO TUTAKAPOWEZA KUANDAA WACHEZAJI WENYE UWEZO WA KUCHEZA HATA DAKIKA 120 WAKIWA FITI, HAWA AKINA NGASSA, NDITI, SUED,BOBAN,CHUJI NA WENGINEO NI KIELELEZO CHA UBABAISHAJI TULIOKUWA NAO KWA MIAKA MINGI.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 14, 2009

    TUMESHAWAHI KUWA NA MAKOCHA BORA DUNIANI NA TULIWAPA HESHIMA ZOTE.MFANO VICTOR,TAMBWE LEYA,JEFF GUTENDOF ETC.
    MAXIMO HAWAFIKI HATA KIDOGO HAWA MAKOCHA.
    MDAU KISIJU.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 15, 2009

    Exactly....Mdau hapo juu ameongea la maana.

    Team nzuri ya taifa inaanzia ktk vilabu(Mfano Simba na Yanga), Kama vilabu vibovu na team ya taifa itakuwa butu.

    Angalia England sasa inavyopata tabu, Haina wachezaji wazuri wengi ktk vilabu ndio mana Capello anapata tabu na team yake.

    Cheki Spain inavyojidai au Holland au Argentina... Coz wachezaji wao wengi wanacheza club za maana hlf kali.

    Kwahiyo, akina Simba na Yanga inafaa ianzishe mbinu za kisasa. Waanze kutafuta match za kimataifa kama friendly match.

    Ni ujinga kushindana Simba na Yanga wkt wote wabovu, waanze mashindano na team za nje. Najua sometimes pesa inaweza kuwa kikwazo, but in some way or another we need to pull our sox up.

    Mafanikio hayaji kirahisi jamani...inabidi kuumia sana tufike tunapotaka kufika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...