
mdau huyu wa kitasha alikuwa anakatiza kichochoro cha makao makuu ya jeshi kutokea palm beach jijini dar, na kukuta daladala limezima na abiria wameamriwa kutelemka ili kulisukuma liwake. akawa anajiuliza kama ni noma ama la kula taswirazzz. mdau mmatumbi aliye karibu naye anajiuliza amwelezeje kwamba bongo haina noma kwa mtasha kula taswirazzz. 'yes, you ken beat ze picha' akawa anasema kimoyomoyo, ila kutamka ilikuwa shughuli...

ah, kama noma na iwe noma...mtasha akaamua na kujipinda huku mwenyeji wake akimsubiri pembeni...

click...click...click akaendelea kama hana akili nzuri, na hakuna aliyemsemesha ama kumgusa

roho kwatu; anamaliza na kuondoka taratiiiiiibu kama si yeye vile. globu ya jamii, ambayo imeshuhudia hii kitu laivu, inajiuliza ni wapi taswirazzz hizo zitaibukia....?
Kazisubirie CNN au BBC International.
ReplyDeleteBy the way, katika pitapita yangu kwenye mitandao nikakutana na jamaa wengine wanasema wameanza kuiangalia Afrika kwa jicho tofauti (positively), lakini ukiwasikiliza...mm!! wamegeuza namna ya kutuponda. Wanatuponda kwa data zetu wenyewe. Hebu angalia na wewe kwenye hii website:
http://seeafricadifferently.com/watch-all-films
Unauliza ni wapi taswira zitaibuka?
ReplyDeleteKwenye globu yake ya jamii.
Hii imenikumbusha mbali sana wakati wa gazeti la sani katika sehemu ya yule babu mpekuzi aliyekuwa akitoa maneno ya kiswahili kupitia methali na misemo.
ReplyDeleteKatika picha hizo hapo juu yule babu angesema 'muosha huoshwa' Mtasha anafikiri kuwa anapata yeye tu, kumbe kuna wengi wanampata yeye.
Hii movie imetulia sana
hao wanatakiwa wapewe kipigo cha mwizi huyo akifika huku anajidai kutengeneza documentary,mfano kuna moja huwa naiona hapa uk inaitwa unreported world huwa wanaonyesha mambo mabaya kutoka central na west Africa na kufanya ukiwa mwafrica ujisikie vibaya sana,kana kwamba wao hawana mambo yao mabaya ya kustaajabisha mimi sio siri kwa hapa nakaa sehemu kama uswazi kwa huku uk,yaani wazungu hawana adabu kuna magay wapo free mpaka wana tv chanel unaona live, siku izi kuna hii mitindo wanaita group sex,ndio zao mzungu kufanya mapenzi na mtu yoyote ni kawaida,ndoa hakuna huku ,wanawake wanalala na mambwa,loo Africa licha ya umaskini tuna utu sana,wabakaji wa watoto wauwaji tu wa wanawake na wageni wako kibao,mimi mwenyewe nataka niandae documentary yangu kuonyesha mambo mabaya ya wazungu lakini sijui ntaionyesha wapi.
ReplyDeleteWazungu wakija Africa siku zote huwa wakirudi kwao basi wanaandika experience yao. So hii taswira itaibuka somewhere tu!
ReplyDeleteIngekuwa Ulaya abiria wangerudishiwa pesa zao!
Hahaahaah Sweet Potato Kanyamazishwa duh wanasifu nakuponda. ila wana Point sema nimechunguza sie tunategemewa kwa kuwekwa kati, ila Tunawategemea ndio sana hatujui kutumia mali zetu na kuringia. Ndomana CHINA NA WEST wanagombana kwa njia ya kila mtu kumponda mwengine,
ReplyDeleteAmerica wanawaponda CHINA kwamba wanataka kuitawala Africa, ndomana viongozi wetu wanaambiwa wasikubali vitu vya CHINA kwamba ni vibovu ni SIASA tu kwamba kila mtu anajuwa wanunuwaji wengi wapo Africa na wakitupa msaada si kwasababu wana huruma wakutaka kutupa msaada,
wanajuwa watachokitaka kutoka Nchi za Africa watapata sababu wametusaidia na kutuwekea Madeni ambayo hatuwezi kulipa, Malipo yake Ardhi yetu Nusu inakuwa Yao.
Africa Elimu yetu lazima tufundishane kwenye Ma TV na wengine wajue na tufundishane kwa Lugha zetu ndio wataelewa wengi.
South America na Africa ndio zinazotegemewa Ukiwacha Asia ni Mafuta tu. Nje Europe na America wametuzidi Elimu lazima tusome. Pazi.
Sasa na wewe uliyechukua hizi picha mbona ulishindwa kumuuliza atazipeleka wapi? Au nawe ulibaki kujiuliza kimoyo moyo kama yule jamaa ambaye kingereza hakikupanda?
ReplyDeleteBasi WOTE SAWA SAWA na jibu hatutalipa mpaka tuzikute kwenye BBC, CNN au kwenye globu.
hahahah! sasa hapo cha ajabu ni nini? kwavile kafanya mzungu? taswira zitaibuka mahali alipopakusudia yeye,,,kama ni nyumbani kwake au kwa vyombo vya habari vya kwao? au kwa blog ya jamii maana tayari umetuletea,,,
ReplyDeleteMdau Singida
Sawa sawa kabisa why not Bongo ni free country as long ujavunja sheria siyo mbaya kabisa kupiga picture kwa nia nzuri na pia hitasaidia kuelimisha jamii.Now days the World too small.
ReplyDeleteNaona si mda mrefu tutakua experts wa kulinda manyonge yetu! Ni kweli hatutaki mtu atudharirisha sababu ya umaskini wetu, ila nadhani tunapaswa kujua wapi tuwekeze nguvu zetu kwa wingi. Kuficha mazagazaga yetu au kuyashughulikia ipasavyo! Sisi pia tuna uhuru wa kumwaga zagazaga zao kwa namna yoyote tupendayo ndani ya media zetu! Kwangu naona busara kupambana vita hii ya media kwa kuipresent vema nchi yetu ktk mambo yaliyo na mvuto kwa dunia na kwa uzalishaji wa bidhaa zetu wenyewe! Uzalendo mbeleeeeeeeeeee!
ReplyDeleteHii issue ya hawa wazungu kupiga picha wabongo hiyo sio mara ya kwanza hiyo, sasa naona ndio wanazichukua hasaa kwa kasi sijui wanazipeleka wapi picha hizi...Siku hiyo tulikuwa mapumziko tukipalilia afya zetu pale DIDIZ PUB- Oysterbay wakaja wakapiga picha watu kama tatu wakiwa na wafuasi wao wakibongo katika gari..Tulifikiri kuwa labda watakaa nao wale au wanywe lakini walishuka tuu kwenye gari na wengine kubakia ktka gari kuchukua picha haraka haraka wakatimua...Nilishindwa kuuliza sababu kaumbo kangu kadogo sana lingeamka soo ningeshindwa..nilijitahidi kunung'unika kwa sauti kwanini picha zinachukuliwa then tunakaa kimya lakini sikupata support kwa wengine ili wawaulize....Tujiulize lkn wabongo ni kwanini wanachukua picha hizi? Wanazipeleka wapi? Usijekuta ndio wale wanachukua picha za ovyoovyo then wanaenda kutafutia misaada nje wanakula kupitia mgongo wetu sisi hazitufikii(Watakuwa Mafisadi nyangumi hawa)...Sababu nimenote wanachukua zile picha za ovyo ovyo tuu (Zenye kuonyesha maisha ya shida shida)...Sina hakika kama ni wema hawa wazungu na hawa wafuasi wao wakibongo....Watanzania tusikubali kupigwa picha ovyoovyo tupende kuuliza, wanatakiwa wakamatwe waulizwe wanafanyia nini picha hizi......
ReplyDeleteuwiiii
ReplyDeletehahahaaaaa
sasa nimefurai sana,,aisee ningekuwepo mie apo,walhahi ningemchimba mkwara angepotea,tena kwa kumwambia ukileta za kuleta tunabeba camera yako tunaipasuapasua apa,,mambo gani aya jaman??yan apa anawapeleka documentary tu.
bongo mteremko
hahaaaaa
Brother Michu, umesema Pembeni ya Ukuta wa Jeshi????? haoiwezekani... nina hakika jinsi vikosi vyetu vilivyo macho hizi sinapu hazikufika popote, Angalieni isijekuwa aliendelea chukua nyingine Michu ulipokula kona...
ReplyDeleteBongo enzi ya Mwalimu....
Itategemea anatokea wapi. Kama ametokea nchi za ulaya za kimasikini basi hii ni issue ya kawaida. Lakini kama ametokea nchi zilizoendelea basi hii inaweza kuwa ni so maanake wao basi likiharibika wataletewa lingine. Hamna anayesukuma hivyo itaonekana ni kitu cha ajaabu abiria kusukuma basi tena kwa free na bado watatozwa nauli.
ReplyDeleteJamani huyu mtasha si kapiga picha tu?au ndio yeye aliyeharibu hilo basi?
ReplyDeleteMbona hapa huwa tunaona picha nyingi zilizopigwa na wabongo wakiwa nchi za wengine?mbona sijasikia mtu akilalamika eti wasipige picha?
Je mpiga picha angekua mweusi kama sisi mgesemaje??As long as hakuna kibao cha kukataza kupiga picha na humpigi picha mtu usoni direct bila idhini yake huyo jamaa ana haki kama Mmatumbi yoyote.Kama ata weza kuziuza kwenye CNN,BBC huo ni usharp wake.
ReplyDeletetatizo nini apa, m coni tatizo lolote, kwani hana haki ya kupiga picha, mbona waafrika wanaenda ulaya na kushangaa na kuchukua picha, hakuna kosa apo, wacheni upofu uo, anye kuku tu akinya bata kahara!
ReplyDeletenimeipenda sana hii picha
ReplyDeletesafi sana jamaa
ila michu una akili sana,yan uyu jamaa angejua na yeye ANALIWA tena mbele kabisa??asingekaa izo pozi za kiwizi-wizi kupiga picha ao jamaa wanaotoa msaada,,,hahahaaaaa
photo of the year