

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ya Akhee
ReplyDeleteNimeziona picha hizi kwenye globu ya bwana mdogo. Hakika zilinitia hasira na huzuni in equal measures
This poor woman could have been my sister au shangazi
Ile kitu kinachoitwa heshma kiko wapi hapo
Wakatabahu
Nakubaliana na mdau wa hapo juu mwanzo. Mama huyu anaweza kuwa ni mzazi, dada au mke ambaye anajaribu kutetea anachoamini kuwa ni maslahi yake. Kwa hakika baada ya kuchukuliwa nyanya zake atarudi nyumbani akiwa mikono mitupu - pengine ana deni la jirani au mwanaye anahitaji sketi ya shule. Michuzi, tafadhali shauri jinsi gani naweza kumsaidia mama huyu japo kidogo nilicho nacho - inawezekana sitofautiani naye sana kimapato, lakini kutoa ni moyo usambe ni utajiri. Naelewa wapo wataosema kuwa ninatetea "uhalifu" kwa sababu jiji lina kanuni zake lakini tunaelewa sote kuwa uhalifu wake ni mdogo sana kulinganisha na uhalifu mkubwa unaotendeka bila hatua kuchukuliwa. Tafadhali shauri jinsi ya kumsaidia.
ReplyDeletethatz extensive use of forces and itz normal to our country. am always afraid when i face tanzanian soldiers or policemen. they think this country belongs to them and they are always above the law.this is not women discrimination alone even men are humiliated too, ive never heard any govt authority rant or ask for forginess to her people on such colonial practices.
ReplyDeleteJamani jamani jamani...
ReplyDeleteHivi hii nchi inaenda wapi?
Wa2 jamani hawamwogopi MUNGU.
That unacceptable...
Mtanzania mnyonge huyo jamani.. wala si mwizi anajitafutia riziki yake yaan wameamua kumdhalilisha kiasi hicho??? Uhuru wa 1961 ni kweli au story..
Ningekua mahakama ningewahukumu hao mgambo na huyo aliyewatuma sawa na wabakaji... Thats not right bwana... It pains alot..
Jamani vyombo husika...
tunajitafutia laana wenyeweeeeee..]
inauma sana kwa kweli...
kama hao wagambo wana hasira ningefurahi sana kama wangewashughulikia vibaka..
maana sasa ha2waelewi..
polisi wao, mahakama wao, wanajeshi wao...
Thats nonsense.
Jamani mama wa watu amekuja kujitafutia riziki ili watoto wapate ada na chakula halafu wanatoke watu wasio na huruma wanamnyanyasa kiasi hiki kwa kweli serikali isipochukuwa hatu za haraka ili tatizo litaendelea kwa sababu sasa hivi limeota mizizi kila kukicha mgambo wa jiji wananyanya wafanyabiashara wadogo hivi nchi hii inataka kuendeshwa na wafanyabishara wakubwa tu??????? je wafanya biashara wadogo wakimbilie wapi eee mungu shuka uje utusaidie watanzania tunanyanyasika sana jamani inaniuma sana!!!!!!.
ReplyDeleteMhh jamani, Watanzania tuone aibu, maana kila siku tunasema tuna utawala wa sheria, sasa hii ni nini? Hao mgambo kuwadhalilisha Watanzania wenzenu ndio kufanya kazi, oneni aibu, mbona mengi yamewashinda, tunahitaji kuondosha udhalimu huu,tuamke Watanzania
ReplyDeletedawa ya hawa mgambo ni kuwapiga vipigo kama wezi.. kipigo cha mwizi anachopigwa.
ReplyDeletekuwatia moto tu firauni hawa.
wanajidai wanajua sana wakati hakuna lolote.. wehu tu hawa.
wanantia hasira kweli kweli hawa.
ningelikuwa na miguvu .. ningelipambana nao.
Mgambo wenye tabia hizi shenzi zenu na hamna adabu.
hamkufundwa kwenu wehu nyie.
Mie nashangaa kweli kweli huyo jamaa huyo ni kama wife wake au shangazi yake?
ingekuwa wife wake anafanyiwa namna hii angejisikia vipi? au hata dada yake...
pumvu zao..
na huyo mgambo wa kike hana akili kama yule yule mwehu wa bongostar search anayekebehi wadada kama yeye.
shenzi wote.
kaka Michuzi, nyinyi kama waandishi kaalamu yenu ni Muhimu, Hili suala la Asjkari kumshika mwanamke hivyo.. tena askari wa mgabo ni fedheha sana. Hapa UK kumsjhika mtu bila kuwa na kibali au ruhusa yake ni kosa la jinai (assaults) hebu waelimisheni jama zetu kuhusu masuala yote hasa ya sheria mikononi.
ReplyDeleteHAWA WAGAMBO NI VIBARAKA MBWA WENYE NJAA!!BADALA YA KUKAMATA WAHALIFU WANAKAMATA MASKINI MASKINI WENZAO WANAOTAFUTA RISKI KIHALALI
ReplyDeletemichuzi hawa askari wa jiji ni wapumbavu sana.. kwani wamemkuta anafanya biashara ya kujiuza?? c alikuwa anatafuta ridhiki yake kwa kuuza nyanya!! sasa iweje wamsumbue na kumzalilisha hivi? 4 sure its sad!! fanya mpango ili tumsaidie hata kipato kidogo tulichonacho..
ReplyDeleteunyanyasaji wote huu tunaouna hapa si kitu kingine bali mi mizizi ya rushwa iliyoshamiri kwenye nchi hii. Ni nani ambaye anawapa majukumu haya hawa mgambo? na huyo anayewapa majukumu haya hafaidiki na kile wanachorudisha mgambo hawa? Je nini majukumu ya city council au municipal? usafi wa jiji ni kama tunauona, hali ya barabara ndo usiseme, mitaro ya maji machafu, hospital za jiji huduma ni duni kuliko kitu chotechote... msongamano barabara za jiji ni hatari.. publicl beach kama coco uchafu mmh.. sasa wajameni hebu niulize kazi za hawa munipal ni hizi tu za kukamata wakina mama na kuwadharirisha?
ReplyDeleteJe tunaweza kuwapeleka mahakamani ili mahakama iwashutushe kutimiza majukumu yao? hivi mayor wa jiji anafanya nini akiwa ofisini???????
Je na wakugenzi wa manispaaa wanafanya nini... wadau tujadili na mwisho tutoe maaazimio yetu
Jamani jambo hili juzijuzi 2 Mhe. Lukuvi alisema kuhusu hawa mgambo, badala ya kufanya vitu vya maana wao wanakamata wajasiliamali tena wanawake imeniuma sana kuona mwanamke mwenzangu anatafuta pesa kwaajili ya watoto wake mgambo wanamnyanyasa tena kwa kumwacha uchi Mhe. Lukuvi hawa mgambo lazima wapewe adhabu tena ya kumlipa huyu mama wa watu na heshima yake! Mimi ninachojiuliza hivi vitu wanavyovichukua huwa wanapeleka wapi kama si makwao kweli mgambo awe na familia kisha akamate hoho, karoti, nyanya mh si wanagawana hawa na kupeleka makwao MHE LUKUVI ingilia kati hili baba
ReplyDeleteInasikitisha pale unapoona kuwa yule anaefanya shughuli ya halali kujipatia rizki yake anafatiliwa na kunyanyaswa laisa-l-kiasi! wale wanaofanya shughuli haramu wanaachiwa huria. Wanawake siku zote ni walinda familia na watafutaji, ukikuta mama anajishughulisha kama hivi kutafuta rizki inabidi umpe pongezi badala ya kumnyanyasa. Mama huyu ameacha wanawe nyumbani kutafuta kula yao na ada yao ya shule, unaweza kuta mume hajishuhulishi sasa ukishamzibia mama familia hii itaishi vipi??? Ni kweli ukipita huko ukiwakuta wamejazana njiani mtu pa kuweka mguu huna unakereka lakini tusisahau maisha halisi ya mtu huyu. Mimi nnavyoonelea ni angalau wakapewa kipaumbele akina mama katika biashara zao hizi ndogo ndogo za angalau kuhakikisha wana wanapata dagaa la kutolea ugali wao na wanalipia wana wao angalau ada ya shule.
ReplyDeleteLaana tullahi kweli hawa mgambo...Wananikera sana...Si vyema watu wanatafura rizki zao kwa wema then wanakuja kuwanyanganya...Hao vibaka na mateja hawawakamati coz wanajua hawatapata kitu...Wanapenda rushwa sana hawa mgambo. Si vyema kabisa naomba serikali iangalie kwa jicho la pili kuhusu hawa Mgambo.
ReplyDeleteKusema kweli moja kati ya KERO kubwa ktk mji wa DSM
ReplyDeleteni hawa mgambo wa jiji na ndio maana RC MPYA MH.LUKUVI vitu ambavyo ameviongelea mwanzo kabisa ni hii kero ya hawa mgambo vimeo wa jiji,ukiondoa kero hii ya kukimbiza wafanya biashara wadogo ovyo kuna kero kubwa jioni wanasumbua sana wafanyabiashara wanao shusha bidhaa toka bandarini ktk makontena ata ukiwa na kibari chao bado ni wasumbufu chakufanya ni kumpatia mkandarasi jiji aliendeshe kwa mkataba na kuwatimua awa wapuuzi wote wenye kuleta kero kuliko ufanisi hiyo ndio njia pekee.
Huu ni udhalilishaji wa kijinsia. Mgambo wa jiji wamekuwa na tabia ya kuwadhalilisha sana walalahoi. Wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali.
ReplyDeleteFranz Fanon kwenye kitabu chake cha Viumbe Waliolaaniwa (The Wretched of the Earth) alisema "Walala hoi wanaposhindwa kumkabili mkandamizaji hugeukian na kuanza kukandamizana wao kwa wao".
ReplyDeleteJana nilipoitazama hii picha kule kwa Bwana Mdogo wazo la kwanza lililonijia lilikuwa baya. Niliwaza kwamba siku moja Wamachinga warushe bomu la mkono kwenye lori la mgambo wa city. Wazo jingine likanijia akitokea "a good samaritan psychopath" akawapatia wamachinga AK 47 halafu wazifiche chini ya meza zao za biashara. Mgambo wa city wakija kuleta za kuleta Wamachinga wawanyunyuzie risasi.
Niliona picha nyingine kwa Mpoki mgambo wa city wakimnyang'anya magazeti muuza magazeti.
Inasikitisha na kukasirisha sana.
kaka huyu mama namjua sana maskini sio mwizi wala anaekiuka sheria za nchi kaka michuzi imeniuma kupita kiasi jee serkali haioni hii ati anajiita askari wa jiji jee sheria inaruhusu askari wa kiume kumkamata mwanamke? mpumbavu huyo askari na ni waonevu wakubwa tena sana jee ingekua amedhalilishwa mamaake ama bibiake siezi kumtaja dadake cuz dadake ni malaya wa kutupwa kwa ivo siwezi kumtaja kaka michuzi vyombo vya kuwalinda wanawake wajasiria mali vikowapi? mbona mjeshi alivompiga trafik kibao watu walisema? kova yuko wapi hayajui yanayo tendeka? kaka michuzi mimi imeniuma sana huyu mama ni kama mlezi wangu cuz mimi nakaa hapo hapo k/koo ni mama mchapa kazi leo anawekwa uchi mbele ya kadamnasi ya watu hivi nchii hii haiendeshwi kwa sheria? huyo mpumbavu akamatwe na aadhibiwe na mungu atamlaani nae mamaake ataachwa uchi na watu wamshuhudie amin
ReplyDeletekuna siku nilikuwa naangalia taarifa ya habari kwenye TV moja ya hapa nchini nikaona jamaa amevuliwa nguo zote na hao hao migambo wa K'koo nilihuzunishwa saaaaana. leo hii tena... hii hali inatuzihirishia jinsi serikali ilivyo lala usingizi wa pono na hii inaonyesha dhahiri serikali haikuwachukulia hatua wale migambo ndio maana wanaendelea kunyanyasa masikini. labda waje wamvue nguo Lukuvi hapo itakua pooowaaaa
ReplyDeleteNondo
Inanisikitisha!Inasikitisha!Inasikitisha!Hao mgambo na vyombo vya dolo serikali ambavyo vimeshindwa kupambana na mafisadi zinaeelekeza ngovu zao kwa walalahoi ambao kutokana na ugumu wa maisha amabayo mengi yamesasababishwa na ufisadi wanajaribu kujitafutia riziki ulikuishi kuwasomesha watoto wao n.k.Mafisadi hata hao tunaowahita mbuzi au kondoo wa kafara wanapelekwa mahakamani kwenye mashangingi.INASIKITISHA! MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteHii habari ni ya kusikitisha na kunaonesha hali ya juu ya unyanyasaji wanayoifanya hawa mgambo. Wangeweza kuwa na njia mbadala ya kuwaita mgambo wa kike wamshughulikie huyu mama kama ingekuwa inaulazima.
Swala hili inabidi liangaliwe, na hawa mgambo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Ni kweli hawa wanawake wanajitahidi angalau kuwatafutia watoto wao mkate wa kila siku, na kama kuna jinsi ya kuwaambia kiutaratibu, basi hizo njia zitumike!
Mdau wa Ughaibuni!
Mgambo wachukuliwe hatua za kisheria. Nakuachishwa kazi haraka iwezekanavyo. Mbona mafisadi hawafanyiwi hivi. Watanzania inabidi muandamane mpka Ikulu ndi Kikwete atajua kuwa watu wanachungu wa maisha. Hawa watu wapewi mafundisho ya kutosha ndo maana wanafanya kazi yako utafikiri wanatawanya wanyama mbugani. Wananchi kimea sana vitendo vya udharirishaji kama hivi na vinginevyo. Hii sio kazi kwa mgambo ni upovu mafundisho.
ReplyDeleteutu umepotea kabisa hv kwanini hatujifunzi kila siku??nakumbuka mkuu wa mkoa mheshimiwa lukuvi katoka kuongea juzi tu na madiwani kwamba mgambo wajiji wasiwe wanatumia nguvu katika kuwaondoa raia maeneo yasiyo ruhusiwa kufanya biashara na hata wiki haijaisha leo linatokea hili tanzania tunakwenda wapi!mimi nampa 5 mheshimiwa lukuvi kwa kuwa alichokizungumza hata wiki haijaisha kimetokea leo hii tatizo kubwa ni kwamba hawa mgambo hawana limu na ndio maana na utu umepotea kabisa pia wengine wana asili ya ukatili tu na yawezekana bidhaa hizo zinapelekwa kwa fisadi fulani tunaomba mgambo hao wote wanaoonekana kwenye picha watafutwe na wachukuliwe hatua ikibainika wanamakosa wapewe adhabu inayostahili ili iwe fundisho kwa wengine hv watanzania tutabadilika lini jamani??embu hao mgambo wafikirie ingekuwa mke wao ndiye anayevuliwa nguo hivyo wangefanyeje???nikiwa kama mmoja wapo wa watanzania picha hii imeniuma sana na nashukuru kwa mpigaji kwa kutuonyesha hali hali halisi inayofanywa na mgambo wetu maana ingekuwa habari tu bila picha zingeanza siasa hapo!viongozi mpo wapi???tunaomba shughulikieni hiyo kitu pamoja na watu wa haki za binadamu tena unaweza kukuta huyu dada ni mtu wa mbagala kuu kulikolipuliwa na mabomu sasa anajaribu kujiweka sawa jamaa wanakuja wanamrudisha tena na ana watoto wapo shule awalishe awasomeshe leo hii watu wanauchezea mwili wake tena kariakoo sehemu yenye mkusanyiko wa watu!!haipendezi namna hii!plz wahusika lioneni hilo na mlitafutie ufumbuzi!
ReplyDeletenamingwea
Sera za chama tawala, kwani wao wana mtandao maeneo yote iwe vichochoroni, vijijini, mijini,taasisi za serikali, serikali za mitaa mpaka serikali kuu.
ReplyDeleteIla mtendaji wa maeneo hayo ana kijitabu cha kijani kinachoelezea jinsi ya utekelezaji wa ahadi(manifesto) zilizotolewa wakati wa uchaguzi.
Mojawapo ni kupambana na umasikini.
Mdau
mtaa wa Kongo, Kariakoo
THIS IN NOT FEAR KWA KWELI.INATAKIWA WAHUSIKA WA HAYA MASUALA YA KUSHUGHULIKIA YA HAKI ZA BINAADAMU MUFANYE KAZI.JAMANI LASIVYO WAGAMBO WANATESA SIO KIDOGO SIO MARA MOJA AU MBILI KUONA HABARI KAMA HIZI........
ReplyDeleteMSIPOCHUKUWA HATUA YOYOTE JAMANI TUTAWAUMIZA KUSEMA ILE HAKI TUACHE KUNYANYASANA WATANZANIA KWA WATANZANIA....
Mr lukuvi alisema mapato ya jiji lakini cha kushangaza hatujaona hata Siku moja vikipingwa mnada hivo vitu na kukuza Halmashauri na kununua vifaa madhubuti kulitunza jiji wao wanawakamata and then wanagawana hapo hamna haki?Mimi naona la msingi kukamata vitu wauze mapato wasafishe jiji wawe Creative sio Ucreative wakuchukua mali na kujaza majumbani kwao,Kumvua mtu nguo ndo wako kazi Eboooh.Huyo mama anione nitamsaidia kisheria
ReplyDeleteAslaam Alekhun Kaka Issa hii ilitoka Pwani raha Jumatatu 25/05/09 ingia kwa picha zaidi kulikuwa na mwanae hivi cjui tunakoenda badala kutafuta njia mbadala wao kuvamia watu kibabe tuuuu ,Michu ingia www.pwaniraha.com ukajioneeeeee
ReplyDeleteKuna kitu kinaitwa
ReplyDeleteTAMWA na TAWLA ambazo zilikuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya akina mama mnataka ushahidi gani zaidi ya huu? Simamieni haki za wenzenu, Tamwa mna bahati wenzenu kibao wameukwaa ukuu wa wilaya na wengine wabunge (Mh.Lucy Mayenga)watumieni hao nyie.
Viongozi wetu wajifunze kuwajibika kwa upuuzi kama huu unapotokea jamani khaaa kinyaa hiki!! Eboooo
Jamani mie nimeguswa na habari na picha za kundhalilisha mama wa watu kwakweli siyo ubinadamu haileti maana kabisa hawa jamaa kaka michuzi wanashindwa kwenda kusaka vibaka wanategeshea wanaofanya biashara ndogo ndogo hii yote ni kutaka kitu kidogo
ReplyDeleteUkweli hawa Wanamgambo wa Jiji ni mbumbumbu kabisa Elimu hamna kwasababu reasoning haipo. Sasa ukiona mabosi wao wanajua vitendo hivi bila kukemea wao ni mbumbumbu mara nyingi zaidi ya hawa mgambo. Utakuta hawa mgambo mama zao, dada, wake zao wanafanya kazi hizi kupata chochote. Nadhani Uongozi uhojiwe wana nia gani. Vitendo hivi vipigwe marufuku.
ReplyDeleteNi kweli kabisa kuwa jambo hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote. Nimepata taarifa mchana huu kuwa kumetokea vurugu za hao Mgambo na wafanyabiashara Kisutu sokoni pia na uharabifu mkubwa umetokea kwa baadhi ya magari yanayo simama neneo hilo zikiwepo teksi. Hawa mgambo wa manispaa ni kero. Mh. Lukuvi inabidi atuondolee hii!!
ReplyDeleteHongera sana Askari Mgambo wa Jiji na uongozi mzima wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kusafisha jiji letu la Dar-Es-Salaaam, hawa wachuuzi ndio wachafuzi wakubwa wa mazingira ya jiji. CCM Oyeeeee CCM Oyeeee, Kazi nzuri sana na Zidumu Fikra Za Mwenyekiti. Maisha Bora na Amani Iliyoje imeletwa na inaendelea kuletwa na CCM.
ReplyDeleteThis is not fair at all. Im sure there r some other way they could have used other than this. This is total humiliation and violation of women rights. They were not even suppose to teach her never the less pulling her like that till wanamvua nguo. Mi ndio maana bongo sirudi kwa kweli.
ReplyDeleteYaani nimekasirika mno! Hasa kuona mwanamke anayefanya kazi kujitafutia senti ili asaidie familia yake. Angetaka angeweza kuwa CD lakini yeye ana heshima zake na anauza nyanya halafu anadhalilishwa hivyo! Ni kweli kwa nini hao mgambo hawakamati vibaka! Badala yake ni WAVIVU na wanatafuta eay targets kama hao akina mama wa sokoni!
ReplyDeleteTukiendelea kuongozwa na sisim wote tunaweza kupata nafasi kwenye ufisadi kwa hiyo tutapunguza kabisa umasikini.
ReplyDeleteKatika mambo yananifanya nijute kuzaliwa Tanzania ni mambo ya udhalilishaji tunayofanyiana sisi wazawa.Huwaga najiuliza huwa tuna matatizo gani sisi Watanzania.Emagine ingekuwa Mzungu au Mhindi amekutwa anauza nyanya pale wala asingefanywa kitu lakini sisi wamatumbi hata Mama yako waweza mvua nguo hadharani kisa unatekeleza majukumu ya Serekali.Jamani tuweni na huruma na hawa kina mama wajasiria mali.Hapa sasa Sophia Simba ndio unatakiwa kupiga zile kelele zako na sio kupiga kelele mahali hapastahiki.
ReplyDeleteSuala la watu kufanya biashara kiholela halikubaliki katika jamii zilizostaarabika. Hilo halipaswi kuachwa liendelee. Cha kuwalaumu mgambo, ni utaratibu wanaoutumia katika kufanikisha kazi zao. Uporaji wa bidhaa, unyanyasaji nk, ni suala lisilokubalika pia. Hivyo, wakati sheria za nchi zikilindwa, watu na mali zao wanapaswa kulindwa pia.
ReplyDeleteHIVI KWELI OFISI ZOTE ZIMESHINDWA KUBUNI MBINU YA KUTAFUTA STRATEGIC AREA YA KUWEKA WAUZA BIDHAA KAMA HAO.MAANAKE TUNAYO OFISI YA MKUU WA MKOA, MKUU WA WILAYA, OFISI YA TUME YA JIJI NA PIA WIZARA HUSIKA . KWELI MIMI NAM SUPPORT KIKWETE LAKINI KUNA WATU KWA UKWELI WANAMDONDOSHA KATIKA UTENDAJI.AT THE END LAWAMA ZOTE ATABEBESHWA YEYE.
ReplyDeleteHII PICHA INAONYESHA KITENDO CHA KINYAMA KINACHOFANYA HUU MGAMBO,NI UKIUKAJI WA HAKI ZA BINADAMU,VILE VILE NI KITENDO CHA KUDHALILISHA MWANAMKE.KWASABABU SERIKALI INAYOZIKATEA SHERIA ,HAIWEZI KUFANYA KITENDO HICHO KWA KUTIMIA ASKARI WAKE.
PIA, SASA HUU MWANA MAMA AU DADA AKISHANYANYWA BIDHAA ZAKE AFANYE NINI,KWASABABU KAZI INAYO IMPA KULA.HALAFU TUNAPIGA MAKELELE UKMWI,ITAPELEKEA MWANA MAMA KUJIUSISHA NA VITENDO VYA BIASHARA YA KIMILI.
MICHUZI SIKU WE KAWATEMBELEE HAO KINA KIMBISA, LUKUVI NA OFFICIALS WENGINE,ANGALU UWASHAURI NI WAFANYE ILI WAOKE MAISHA YA MTANZANIA MASIKINI ANAFANYA BIASHARA KWA KUTUMIA MFUKO WAKE BINAFSI.
NCHI ZENYE DEMOKRASIA LAZIMA BAADHI YA VIONGOZI,WANGESHAWAJIBIKA KWA KUJIUZULU, KWASABABU HIYO NI ADMINISTRATION ERROR AMBAYO IKO KILA SIKU, MGAMBO WANANYANYASA WATU WENYE BIASHARA NDOGO NDOGO.
HALAFU VYOMBO VYA HABARI AZINE KAMPENI ZA KUSAIDIA HAO WATU JAMANI,KWASABABU UKIUKAJI WA SHERIA NI NJIA MOJA WAPO YA UFISADI.
PICHA INASIKITISHA SANA!
hivi meya wa jiji ni mungu nani? kwa sababu sasa huu upumbavu ufike kikomo. kwani hakuna sheria na adhabu ya wafanyabiashara wanaokikuka sheria? hili jambo sio la kuliendekeza tena wala kilijadili ni kuchukwa maamuzi. Viongozi wa jiji wawajibishwe, watu wangapi wanatenda makosa tena ya kusababisha hata wengine wakafa bila sababu lakini hawashambuliwi hivi! kwani mafunzo ya mgambo ndio alkaida ya jiji. kwa kweli viongozi wasipochukuwa hatua na kuwajibika juu ya hili tutafikishana pabaya. Kumvua mwanamke mwenzio nguo maana yake nini, wengine wamesomeshwa na hizo nyanya na ni watu maarufu kwenye taifa, tafadhali mama zetu wanahangaikia maisha ili wana wao wawe na maisha bora. kwani nani anataka au anafurahia kubebana na karai siku nzima kwenye jua akitafuta pesa?hili jambo likomeshwe mara moja. Mnaweza kujitetea kwamba ni wabishi lakini mbona basi msiwapige na kuwadhalilisha wanaojenga hovyo, wanoiba mali za uma na kadhalika?
ReplyDeleteHii tabia ni mbaya sana tena ikemewe kwani kufanya biashara sio tatizo.Halimashauri ya Jiji wamekuwa vibaraka wakubwa sana wa wenye maduka hapo kariakoona wapumbavu wakubwa mnoo.Sasa huyo Aunt anafukuzwa na kuhadhirishwa walimwambia kwa kwenda zaidi ya pale alipo kuwa??mbili je aliko ambiwa aende kunauwezekano wa kufanya mauzo??Leo imamtokea huyo dada si ndugu yangu Bali ni mtanzania mwenzangu na naona haki za wengi sana zinachukuliwa kwa mtindo huu.watanzania tutaendelea kunyayaswa mpaka lini nyumbani kwetu.Nchi nyingine kitendo cha kumfanyia mwanamke mambo kama haya ni kosa lajinai na kufungiwa licence ya kufanya mambo hayo kwani niudhalilishaji.{MDAU}
ReplyDeleteWatu tunapenda sana kulalamika, kwanini huyo mama amekwenda kufanya biashara sehemu zisizoruhusiwa kisheria ? Hayo maeneo yalishapigwa marufukua kufanyia biashara.Hivyo inabidi aondolewe kwa nguvu.
ReplyDeleteKwa kweli inasikitisha sana lakini mimi nipo na mawazo tofauti,pamoja na jiji wanatumia nguvu sana lakini ni lazima ujue kuwa katika nchi zisizofuata sheria na mambo ya kisasa mmojawapo ni Tanzania kwa kweli ni uchafu mtupu na hii ni jadi yetu. kila mtu kama atakuwa anajifanyia anavyotaka kweli tutafika??? nchi gani watu wanapanga biashara popote hata njiani kwa wapita njia je kweli huu ni ustaarabu na kweli tunataka maendeleo na mabadiliko ya kweli?????? jiji lazima lisikubaliane ni biashara hizi kwa nini watu wasielimishe kuwa hairuhusiwi na lazima wafuate sheria hatuwezi kuendelea kwa namna hii kilamtu kama ataruhusiwa kufanya popote pale hii haifai kabisa
ReplyDeleteTanzania mnyonge ndie anaeonewa. polisi, jeshi na mgambo wanatakiwa kutulinda wanyonge na kututetea haki zetu lakini wapi? huyu mama alichofanya ni kosa kubwa? huyu mama anajitafutia riziki kwa njia za halali na anaonewa kwa kuwa tu ni masikini. kuna vibaka tele mitaani na kuna wezi wa kweli wanaoiba mamilioni ya nchi na hawaguswi ng'o. inaudhi na inauma kuona mnyonge anadhalilishwa namna hii. nani wa kumtetea hapa? wanajiji wanajifanya majabari kwa kuonea wanaotafuta riziki kwa uhalali.
ReplyDeleteKina nanshii kesi zao zinafutwa mara wengine zinaimbiwa nyimbo mpya kwa hasara kubwa waliyosababishia nchi wala hawakudhalilishwa, Maskini mama wa watu anatetea maslahi ya familia yake wanamsaulia nguo mwee! tutafika kweli na maisha bora kwa mtanzania?
ReplyDeleteKitendo kama hiki hakikubaliki. THIS IS BABARIC. Tanzania ustaarabu uko wapi? Mimi (Dume) nimeshusha machozi. My heart is broken.
ReplyDeleteTAMWA/KITVO CHA SHERIA CHUO KIKUU (Research Project)
Huyu mama atafutwe,
apatiwe msaada wa kisheria kuhusu udhalilishaji huu,
Jiji limlipe fidia,
Gharama za kesi (kama ni project ya research students au wanasheria) zilipwe na Jiji
Askari wa jiji wachukuliwe hatua,
Jiji lihakikishe kwamba kitendo kama hiki hakirudiwi tena.
Mkuuu wa Mkoa na Meya wa Jiji watoe ushirikiano kuhakikisha kwamba haki inachukua mkondo wake.
Utekelezaji wa hili unawezekana kwa kuwa Jiji lina fedha za makusanyo ya kodi.
Wahusika shughulikieni, na tutafurahi kupata maendeleo ya suala hili humu blogini.
Huyo Mama alikuwa anakiuka sheria za jiji na nchi kwa kufanya biashara sehemu isiyoruhusiwa, hongera sana Mgambo wetu wa Jiji kwa kazi nzuri za kulinda Sheria za nchi, sasa Sheria zisipofuatwa si ndio kutakuwa na chaos nchini? Watu kama huyo Mama pichani inabidi wadhibitiwe kwa sheria kali zaidi na tena ilibidi akamatwe na kushitakiwa kwa kukataa kukamatwa kwa hiari. Hongera kwa uongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa kusimamia sheria za nchi kwa ufanisi mkubwa.
ReplyDeleteCCM Juu Juuu Zaidii.
Ni mimi Kada Mkereketwa Wa CCM.
WE MGAMBO MWENYEWE HATA KUSOMA AJUI NDIO ATAWEZA KUREASON? YAANI DA ALL SYSTEM OF TANZANIA ILISHAKOSEWA KWA HIVYO KUREKEBISHA INABIDI TUANZE SASA HIVI KWA KUPANDIKIZA MAADILI MEMA NA USTAHARABU KWA WATOTO WADOGO SABABU HAYO MAMGAMBO YASHAKUWA MABWEGE MAJITU MAZIMA UWEZI KUYABADILI TENA NGOJENI YAFE TU YAPISHE NJIA VIJANA WADOGO.MFANO,ANGALIA JINSI WATOTO WADOGO WALIOPO MAREKANI WALIVYO NA AKILI ZA KIKUBWA YAANI HADI MTU UNASHANGAA,HATA MTANZANIA UKIZAA MTOTO HUKU ANAKUWA NA AKILI ZA AJABU SOMETIMES KULIKO BABA YAKE AU MAMA YAKE,AM SURE WATU WENGI HUWA MNALIONA HILI,HAPO NDIO UTAJUA WENZETU WANAJUA KUMTENGENEZA MTOTO TANGU MDOGO,THEN WAKIKUA AUTOMATICALLY WATU WENGI WANAKUWA WASAFI AWATUPI TAKA OVYO THEN MITAANI KUNAKUWA KUSAFI UKIJA BARABARANI HIVYO HIVYO WATU WANAENDESHA VIZURI SIYO KAMA DALADALA ZA BONGO,SIKATAI KUA PIA WAPO WEHU WACHACHE WALIOLELEWA VIBAYA MITAA HII,MTEGO HAPO NI MALEZI TU WAZEE!!
ReplyDeleteBE SMART GUYS
ReplyDeleteSIONI KOSA LA MGAMBO KAMA ALIKUWA ANATIMIZA WAJIBU WAKE
TUSIWE WANAFKI HATA KAMA HAIPENDEZI
SHERIA NI MSUMENO
WATOKE WASIFANAYE HAPO BIASHARA
This has generated extreme anger,let us channel that anger into helping this lady. ewe Michuzi au bwana mdogo, do you have paypal accounts?
ReplyDeleteI would also like to congratulate mdau 3.59pm what a pleasing incongruous epigram--a good samaritan psychopath--a gem of an oxymoron. I will try and remember it for future use
Wakatabahu
jamani hata mimi sijapenda hata ni kitendo cha uzalilishaji wa kijinsia
ReplyDeleteYani siielewi serekali yetu kabisa.Hawa wanaoitwa wamachinga wanajitahidi kuepukana na umasikini pia kutokuwa vibaka lakini ndio wanaopata shida kila kukicha.
ReplyDeleteWamejenga Machinga Complex lakini haifunguliwi na utakuta walengwa hawatapewa nafasi zao wanazostahili so wafanya je?
Jamani Mkuu tunaomba ulitazame kwa ukaribu jambo hili,mbinu wanazotumia mgambo sio sahihi
huu ni upumbavu wa hali ya juu,until now hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kwa hawa mgambo wanaochukua mali za watu kwa nguvu na ukipeleleza hivyo vitu wanavyovichukua huwa wanachukua wenyewe mbwa hawa.inawezekana kabisa mama huyu amechukua mkopo sehemu ili kufanya biashara yake na kuingiza pesa halali badala ya kwenda kujiuza,kuwamwizi ama jambazi.naona nchi yetu inakoelekea siko kabisa hata kama kusafisha jiji plz tafuteni njia nzuri ya kuwaondoa watu na si kuwachukulia vitu na kuwavua ngua like that nyie shwain.USE UR BRAINS DONT USE UR STREANGTH ASS HOLES...js imagine ingekuwa wewe mbwa unafanyiawa hivyo.its nt fair.kwa hali kama hii uhalifu hautoisha TZ,ndio utaongezeka.
ReplyDeleteinakera na inauma sana,mnajifanya kusafisha jiji,shwain nyie mnajua hata UK,US kuna watu wanapanga vitu barabarani??msijifanye mnaendelea sanahapa,hata nchi zilizotupita kila secta wanawatu kama hao,kuna mpaka omba omba,tanzania ni nchi masikini sana na tupo nyuma sana ,mapapa hamwagusi ila dagaa ndio eeh wanavuliwa hadi nguo shwain nyie.hatakama mnyonge mnyongeni ila hakiyake mpeni.GOD IS WATCHING US
ReplyDeletemgambo wanawake wanamzalilisha mwanamke mwenzao kiasi hiki!!! hebu angalieni mgambo mwanaume amesimama pembeni wanawake ndo wanamvua nguo mwenzao! wajinga kbsa hawa
ReplyDeleteyusta
Nchi inapofika hali kama hii yakumzuwilia mtu asipate riski yake na kumdhalilisha basi uelewe Bakora ya Mmungu haipo mbali kwani hata mwenyezimu anasema ni yeye peke yake ndie anae towa na kusimamia riziki ya mja wake na ndio maana hakuna malaika wa kutowa Riziki lakini wapo Malaika wa mambo mengine ,bakora ya mmwenyezi mungu haichaguwi Nchi hii kwa miaka mingi sasa tumekuwa na kiburi kama vile tumejiuma
ReplyDeleteHayo ni mambo ya maisha bora kwa kila Mtanzania. Huyo mama wa watu si ajabu kakopa mkopo kwenye SACCOS. Mgambo wameamua kummalizia frustrations zao zote.
ReplyDeleteNoma sana.
Pole mama wa kitanzania.
ReplyDeleteNajua ni vigumu sana kuona mateso yako.
Wanakukumbuka husani siku za uchaguzi baada ya hapo malipo yake ndio hayo.
Si ajabu kwa sasa hivi unaishi kwenye hema baada ya "MABOMU YA MADE IN CHINA KULIPUKA" mbagala.
Zama nchi ikiongozwa na wasomi wachache,watoto wako walipewa madaftari na vitabu bure shule.Leo wanasemaELIMU IMEKUWA BORA kila mzazi achangie elimu.Unajitahidi kupata pesa ya kumnunulia mwanao japo daftari unakumbana na NGUVU ZA DOLA.
Wezi wa mabilioni wanaenda kwenye kesi zao wakisindikizwa na wapambe ndani ya gari zenye viyoyozi.
Pole sana naamini yote haya ipo sikuyatakuwa na mwisho wake.Angekuwa mzungu anamfanyia mweusi tungesema wabaguzi..sasa wenyewe kwa wenyewe..
Pole sana mama uliokubwa na mkasa najua umewakilisha wafanya biashara mamia ambao kila kukicha wadharirishwa kwa KIBALI cah kusafisha jiji
Utawala wa sheria.
ReplyDeleteThis is bs ...yaani hawa mgambo waliomembarss mama wa watu wawe punished no exceptions ili next time wawe na adabu ala
ReplyDeleteJamani jamani mgambo kwenye sheria zao hawajaambiwa wawe wanavua nguo wahalifu sawa mama anaweza kuwa alikosea kuuza nyanya zake mahali pasipotakiwa lakini si kwa kudhalilishwa kuvuliwa nguo, Kuna polisi siku mbuki nchi gani walimvamia mtu kwa kumpiga pamoja na kuwa alikuwa amekosea polisi walishtakiwa, hao ni watu wanaotakiwa kutetea wananchi si kudhalilisha wananchi mimi kama ndio kamanda wao nawaweka ndani mara moja
ReplyDeleteWADAU, PAMOJA NA MATOKEO YA KURUPUSHADI KUTUFIKISHA KUONA DADA ALIYE NUSU UCHI, NAPENDA KUTOA CHANGAMOTO HIZI. KUWA SI VEMA ASKARI AKATUMIA NGUVU SANA HADI KUVUTA NGUO ZA MTU HASA MWANAMKE. JAPO HATUJUI HUYU DADA ALIZIVAA KWA USTADI GANI. LABDA ALIGESHA TU. SASA, YEYE KUDHALILIKA SI KIBALI PIA CHA KUMFANYA AUZIE SEHEMU ILIYOKATAZWA. KAMA NI SAWA YEYE KUUZIA HAPO, BASI WAITWE HATA WALIO NYUMBANI WENYE BIASHARA ZAO LAKINI WAMETII AGIZO LA JIJI LA KUTOUZIA HAPO.
ReplyDeleteWATU TUSILAUMU TU. HAWA MGAMBO HAWAJAENDA KWA HUYU DADA NYUMBANI KUMDHALILISHA. NA JE, LABDA HAYO YAMETOKEA WAKATI ANAKAIDI AMRI YA KUONDOKA HAPO, AU KUKAMATWA? MGAMBO WAMEAJIRIWA, WANALIPWA KWA KAZI HIYO. TUSITEGEMEE WAENDE HAPO NA KUMCHEKEA HUYO DADA.
CHANGAMOTO YANGU NI KWA SERIKALI YA JIJI, KUFIKIRIA NAMNA YA KUWASAIDIA WAFANYA BIASHARA NDOGONDOGO KAMA HUYU DADA, NA SI KUWAFANYA MGAMBO WAWE MBWA ASIYE NA MENO!
KAMA NINGEKUWA MIMI KIONGOZI WA SERIKALI. NAMWADHIBU KWANZA HUYU DADA, HALAFU PIA NACHUNGUZA KAMA KUDONDOKA NGUO KULISABABISHWA MAKUSUDI NA MGAMBO, AU NI TU KURUPUSHANI ZA KUMKAMATA ZILIZOSABABISHA. KOSA MOJA HALIWEZI KUHALALISHA VITENDO VINGINE. UMEUZIA SEHEMU ULIYOKATAZWA, SI HALALI KUKAIDI KUKAMATWA.
YANGU NI HAYA TU....
MDAU
Hawa wafanyabiashara ndio wanafanya makosa makubwa sana zaidi ya Mkapa na CCM.
ReplyDeleteNimesikitishwa sana na kitendo hiki cha udhalilishaji. Wanaacha kukamata mafisadi wanaanza kuangaika na akinamama wajasiriamali wauza nyanya. Wamama kama hawa inatakiwa serikali iwawezeshe, iwape mitaji wakuze biashara zao sio kuwanyanyasa na kuwakatisha tamaa. Serikali inapaswa iombe radhi kuhusiana na kitendo hiki. Yayo maisha bora kwa kila mtanzania yapo wapi?
ReplyDeleteSHAME ON U MGAMBO!!!
ReplyDeleteSHAME ON U (MKUU WA MKOWA, MK-WILAYA,WAZIRI WA MAMBO YA NDANI,MK-WAJIJI)!!
SHAME ON U TAMWA NA VYAMA VYOTE VINAVYO TETEA HAKI NA MAENDELEO YA KINA MAMA KAMA MTANYAMAZA BILA KUCHUKUA HATUA ZOZOTE!!
SHAME ON U WANASHERIA WOTE WAKE KWA WAUME KAMA MTASHINDA KUMSAIDIA HUYU MAMA MSAADA WA KISHERIA BILA GHARAMA YOYOTE, I SAY SHAME ON U!!!!
SHAME ON U MICHUZI NA WAANDISHI WAHABARI WOTE KAMA MTASHINDWA KULIONGOLEA HILI SWALA KWA UWAZI NA MAPANA ZAIDI MPAKA HAKI ITENDEKE!!!!
SHAME ON U WANAWAKE WOTE WA TZ WAISHIYO BONGO KAMA WATASHINDA KUANDAMANA KUAKIKISHA SERIKALI NA DUNIA NZIMA INASIKIA KILIO CHAO!!!
SHAME ON U FIRSTLADY MAMA KIKWETE KAMA UTAKAA KIMYA BILAKUKEMEA NA KUAKIKISHA SHERIA NA HAKI INATENDEKA!!!
SHAME ON U ALL MEN WAKIBONGO KAMA MATANYAMAZA KIMYA BILA KUFANYAKITU CHOCHOTE KUAKIKISHA UDHALALISHAJI WA NAMNAHII UNAKOMESHWA KABISA!!!
SHAME ON U RAISI KIKWETE KAMA UTAFANYALOLOTE!!!
SHAME ON U THE GOVT OF TZ !!!
MIMI NIMEAMUA KAMA TZ HAITAFANYA KITU KUHUSU HILISWALA, NITAAKIKISHA DUNIA NZIMA INAJUA, NITATUMA HII PICHA KOTE NI TAKAPOWEZA, CNN, OPRAH SHOW, ELEN SHOW, YOU TUBE NK, MPAKA HAKI ITENDEKE NDO NITANYAMAZA!!!!!!!!!!!!!!
NDO MAANA TUMEIKIMBIA HIYO NCHI HAIWEZI KUBADILIKA...
ReplyDeletePOLE SANA KWA HUYO MAMA
I need a lawyer who can represent this woman in a civil suit against City Council. Please dont ignore, provide me with ur email and I will hire you to represent this woman, all payments upfront.
ReplyDeleteEqual Justice
Michuzi, nitafutia namba ya huyu mama nintakuuliza kwenye email nina dola mia tano hapa za kwake
ReplyDeleteTAMWA ISAIDIE UVUNJAJI WA SHERIA? AU JIJI LIACHI WATU WAFANYE BIASHARA POPOTE PALE WANAPOPENDA. JE, ILI NCHI IWE NZURI SERIKALI IFUTE SHERIA ZOTE? WAJINGA TU NDIO WATAKAOKUBALIANA NA HAYA.
ReplyDeleteJAMNI TUSIWALAUMU SANA HAWA WANAMGAMBO! TUANGALIENI CHANZO CHA HAYA MATATTIZO TOTE.KUAJILI WAFANYAKAZI WASIO NA UJUZI NDIO SABABU KUBWA INAYOSABABISHA MAMBO KAMA TUNAYOYAONA KWENYE PICHA.RUSHWA, UFISADI, NA ROHO MBAYA ZA VIONGOZI WETU TOKA NGAZI YA MTAA MPAKA SERIKALI KUU NDIO WANATUSABABISHIA UPUUZI WOTE HUU.WADAU SOMETIMES TUNAPOLALAMIKA NI LAZIMA TUANGALIE KWA KINA NINI TUNACHOKILALAMIKIA.
ReplyDeleteJAMANI HAYA NDIO MATUNDA YA KUWA NA SERIKALI YA KIBABAISHAJI. YANI WAO BADALA YA KUSHUGHULIKIA MATATIZO SERIOUS KAMA YA UFISADI AMBAYO NDIO HASWA YANAYOTURUDISHA NYUMA, WAO KAZI KUHANGAIKA NA HAO AKINA MAMA WANAOJITAHIDI KU-SURVIVE. SHAME SHAME SHAME!!!
ReplyDeleteWatanzania wenzangu,lazima tuzingatie sheria za nchi,kuwa mwanamke sio sababu ya kufanya mtu avunje sheria,kimsingi huyo mama alikua akifanya biashara sehemu isiyoruhusiwa na alipokamatwa hakutaka kutoa ushirikiano kwa kisingizio kuwa yeye ni mwanamke ndipo nguvu ikabidi itumike. Kivazi alichotinga ndio kinafanya aonekane kama kadhalilishwa lakini ameshughulikiwa kama wahalifu wengine. City's askari kazeni uzi kulifanya jiji liwe na hadhi ya kuigwa.
ReplyDeleteKWELI JAMANI IMEFIKA WAKATI SASA WANANCHI KUAMKA NA KUPINGA KWA DHATI UZALILISHAJI HUU
ReplyDeleteMHESHIMIWA KOVA KILA SIKU ANARUKA NA VIBAKA. TULIJUA MTAMSAIDIA KUMBE MNAKOMAA NA KINA MAMA.
HII SWALA NAIMANI MHESHIMIWA LUKUVI ATAKUWA ANAPENYA PENYA KATIKA HII BLOGU YA NANIHIIIII AONE NA KULITAFUTIA UFUMBUZI
what are mgambo???street warden?? ama ndio kina nani???...kazi zao ni zipi?
ReplyDeletehao wafanya biashara ndogo ndogo..kila mahali wapo hata huku ughaibuni...
cha msingi,sio kuwapa tu sehemu ya kufanyia biashara...bali sehemu zenyewe ziwe..za kibiashara,i mean sehemu zile ambazo biashara zao zitatoka...
hamjiulizi kwa nini,mtu kama huyo dada..anakuja kuuuza bidhaa zake sehemu iliyokatazwa?..ni sababu anaamini hapo ndipo nyanya zake zitatoka...
huku birmingham..watu kama hao wametengewa sehemu yao,iko isolated kidogo...but iko ndani..ya city center...!!!naamini hao pia wakitengewa sehemu hapo hapo kati kati ya jiji ambapo bidhaa zao zinaweza UZIKA,then hawata tangatanga huku na kule,cha muhimu ni kuwaandikisha majina...na kuwakata kodi kutokana na mapato yao,ambapo hio kodi inaweza kuadvertise biashara zao na sehemu hio walipo..hivyo kuwapatia wateja zaidi..
kuhusu huyu mama kuachwa uchi,inabidi hao walioajiri hao mgambo washitakiwe!!kama ni ofisi ya mkuu wa wilaya,au mkuu wa mkoa...inabidi washitakiwe!!!huu ni udhalilishaji!!!..am sure wakishtakiwa na kutozwa faini...watajifunza somo!...then wata TRAIN mgambo wao...jinsi ya kuarest watu bila kuwaHARASS....in case wanapata COMPLAINTS kama hizi tena..then mgambo husika..anakuwa DISMISSED...IMEDIATELY!!!!.in this way...utakuwa na uhakika wa kupata migambo ambao pia wanafuata utawala wa sheria na sio MIUNGU WATU!!!
NEY-BHAM.
Dar-es-salaam ni ya 12 kwa uchafu duniani kwa sababu ya wavunja sheria kama hao akina mama.
ReplyDeleteUtawala wa sheria na sheria ziheshimike.
Angekuwa USA wangempiga ma-TEZA yani heri ya huyoo mgambo kamsukuma kanga ikadondoka
kwa kweli migambo wana maudhi, unawezaje kumdhalilisha mwanamke mwenzio kiasi hiki eti sababu ya kuuza nyanya. Sio kibaka bali yuko katika kupambana na maisha. kweli mnyonge hana haki nchi hii.
ReplyDeletekutwa wafanyi biashara wadogo ni kukimbia kama vichaa wakikutana na mgambo, maana kama alivyosema mdau mmoja ni kama miungu watu, yote hii wasinyang'anywe biashara zao. bishara zenyewe wanagawana wenyewe wala hazipelekekwi kunakohusika. mateso haya mpaka lini jamani? kwa nini wasifanye kazi ya kukamata vibaka walioenea kila mahali...
Please activists out there sometimes we have to take a bull by the horns, tuandamani na kijulikane hiyo ndo demokrasia ya kweli tuacha uoga, mpaka lini jamani!! hii ni nchi yetu, siyo yao pekee yao
ReplyDeletePIGA SANA PIGA PIGA PIGA
ReplyDeleteWAMEZOEA HAO
WANAVUNJA SHERIA KWA KISINGIZIO CHA ZIKI
NO EKSICHUZ HAPA
ORUGHA WAPE KIBANO
HAKUNA CHA TAMWA, WANAWAKE, MAANDAMAMO
PIGA PIGA WATOKE NA WAKOME
UCHAFU MJINI NA MBOGA ZENYEWE WANAWEKA KWENYE VUMBI
TUBADIRIKE
Kuna siku Da best President Mkapa alihojiwa na CNN juu ya askali walivyofanya mauaji Zanzibar
ReplyDeleteSwali "Je umewachukulia hatua gani polisi hao?"
Mkapa alijibu "Niwachukulie hatua gani wakati walikuwa kazini?"
Be straight niggers
Kosa dawa kisago
inasikitisha kuona ya kwamba askari wa tz wanapenda kuchukua sheria mkononi..nyny askari (polisi au mwanajeshi)kumbukeni kuwa sio majaji...hamna haki ya kumpiga mtu (awe mtuhumiwa au la)wala kumshika kwa kumthatlilisha.
ReplyDeleteviongozi hata siku moja hawajawahi kukomesha au kukemea 'police brutallity'...hii kitu haitoisha, mpaka maaskari waathabiwe kwa kuthalilisha watu!
serikali inahitaji kufungua macho hapa kwa saana..najua kwny secta ya haki sawa serikali imefeli kabisa..plz do somthn on 'police brutality' matters..its easy n simple...brutal police officers should b fired or suspended, period!
na alaaniwe amdhalilishaye mwanamke kwa namna yoyote ile
ReplyDeletehakika mtalipa nyie askari feki na wote juu yenu waliowapa "kanuni"izo za kusulubu mtu atafutaye rizki yake KIHALALI
ivi mnataka wanainchi sasa tushike MITUTU YA BUNDUKI
me ndo mana watu wavaao migwanda ya geshi-geshi siwataki,siwaelewi kabisaaa,km geshi kule mbagala
wal'ahi shenzy zenu
heeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeletenchi gani hii?
police au vibaka ao??
siamini......
ReplyDeleteyan apo sahaun iyo kesi wala haipo wala nini!!ndo imetoka ivo
EPA,BoT,vifaa vya jeshi,Radar nk tu havishughulikiwi
Police waadhibiwe sana tu,kwanini wasiwe kama wa huku majuu where police hakugusi mpaka utakapo mtishi amani ya maisha yake.Huku wako so friendly police wa bongo hata kuumuuliza swali unajifikiria mara kumi.
ReplyDeleteMr. President do something,wazazi wetu wanadhalilishwa hasa akina mama hii si haki kabisa,naomba msifungia macho jambo hili.
JAMANI WATU TUMUOGOPE MUNGU,MIMI NINAAMINI KABISA HAO MGAMBO WAMETUMWA KUFANYA KAZI LAKINI SIO KAZI YA KUZALILISHA WATU KAMA HIVYO. KAMA KWELI HAO MGAMBO WAZAZI WAO HAWAKUUZA GONGO, VITUNGUU, NYANYA N.K HAWAKUPITIA KATIKA HATUA YA KUWAFANYA HAO WAFIKE WALIPO SASA KWELI WANGEISHI? IMENIUMA SANA SANA KUONA BINADAMU MWENZETU AKIZALILISHWA KAMA IVYO. UKO WAPI UTU JAMANI! MBONA BINADAMU TUMEKOSA HURUMA YA MUNGU!KUNA MTU ANAPENDA KWENDA KUUZA NYANYA KAMA SIO KATIKA HALI YA KUJIINUA KIMAISHA? HIVI KWELI WAKUBWA WANAONA HAYA MAMBO? JAMANI SERIKALI IKEMEE VIKALI HIVYO VITENDO. JAMANI NIMEMUWEKA HUYU MAMA EMBU FIKIRI NI MZAZI WAKO AMEENDA KUWATAFUTIA RIZIKI ANAFANYIWA HIVYO INAUMA SANA SANA JAMANI. NIMEANGALIA HII PICHA MACHOZI YAMENITOKA.NILITAMANI MDA HUO WANAVYO MNYANYASA HUYO MAMA MUNGU ASHUSHE RADI AWAMALIZE WOTE AMNYAKUWE HUYO MAMA.NI KOSA GANI ALILOTENDA LA KUWASHINDA MAJAMBAZI SUGU, MAFISADI PAPA. KWELI SIRI YA MUNGU YA KUWEKA KITU PESA NI KALI. TUNGEKUWA TUNAISHI KAMA NDEGE NAFKIRI YAHA YASINGE KUWEPO. MUNGU MPE UVUMILIVU HUYO MAMA NA KUJIONA NI MIONGONI WA WAPENDWA WAKE. MUNGU HATO MUACHA PAMOJA NA MAJARIBU ANAYO YAPITA YA DUNIANI.
ReplyDelete