Habari bro Michuzi,
Naomba uniulizie Swali hili kwenye Blog. Kila siku unakuta matawi ya CCM yanafunguliwa nje ya Nchi na watu wanachukua kadi za chama. Why? Nini kizuri ndani ya CCM kwa sasa?. "People , this is not time to support Crime , its time to push the gorvenment and its party into doing good for their people", Huku Polisi wa CCM wanakula Rushwa na kunyanyasa Raia, Jee munajiunga na CCM kusapoti hayo?.Ni unafiki mtupu. Au ndio watoto wa Mafisadi wa Tanzania waliopata kwenda nje kwa Ufisadi?
Wako Mdau,
Mbarouk Said

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 58 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2009

    unajua walishaona ccm kuna ulaji si lingine

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 08, 2009

    Mbaruku acha uvivu wa kufikiri, mafisadi ni watu na sio chama, Tanzania inaitwa nchi ya mafisadi ila si kweli kila mtanzania ni fisadi. Ukitaka kubadilisha mambo ndani ya system ni rahisi kama utaingia kwenye hiyo system, ingawa pia unaweza kubadilishwa wewe uliyeingia. Hata katika timu ya Yesu yenye watu 12 tu ilikuwa na mamluki. Hata hivyo mimi ni mpinzani mkubwa wa CCM

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2009

    Mdau hili ni swali au unaeleza maoni yako. Tanzania ni nchi huru na watanzania wana haki ya kujiunga na chama chochote wapendacho bila hutajika kutoa maelezo kwa mtu yoyote, ili mradi wamependa sera za chama. Tunachotakiwa ni kuvisaidia vyama vyetu tuvipendavyo kuwa na sera zinazovutia wanachama

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2009

    Ukitaka kujua uzuri wa CCM ingia ndani uone. Wewe uliye nje utabaki kulalamika weeeeeeee na hali ya uchumi itakuwa ngumu sana kwako milele.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2009

    hili liujumbe limekaa mwake!

    inatia kichefu chefu kama cha swine flu kuona matawi ya chama kimoja!

    hao ccm wanataka kuendesha nchi kama timu ya mpira...
    kwani ccm A-ni kama timu A -wapo Tanzania (wana mtandao)

    ccm B- ni kama timu B - wapo tanzania-ila wametoswa(mtandao matumaini.

    ccm c-kama timu C - wapo tanzania arosti mbwa kachoka -hawana vyeo vya zamani,wapo wakuu wa mikoa,n.k

    ccm d.........utajaza mwenyewe!
    ccm e------''-------
    inaendelea hadi........
    ccm Z----ndio hao waliopo nzi za nje. wao wanakumbuka ndugu zao zamani sana walikuwa ccm na wakawarusha kwenda kusoma au kupiga boksi.

    wana ndoto za ali nacha siku moja watarudi ulingo!

    mimi simo!

    ReplyDelete
  6. Ndugu Mbarouk Said, mimi ni mmoja wa wale ambao wamewahi kuelezea hadharani mtazamo wao kuhusu suala hili. Maoni niliyowahi kutoa ni haya
    hapa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2009

    mimi nafikiri tungeyachambua kwa kina yale ambayo tunataka jamii itujibu kabla ya kuyaweka hadharani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 08, 2009

    JAMANI MTAWACHUKIA WATOTO WA MAFISADI MPAKA LINI JAMANI . WAZAZI WAO WALIHANGAIKA NA WAKAENDA SHULE ENZI HIZO ,ELIMU YA BURE WEWE UNAHANGAIKA NA WATOTO WAMAFISADI, INAELEKEA UNAWIVU SANA NA WAZAZI WAO WAKIPATA MATATIZO AU WAKIFA UNAFURAHIA HUO NI USHETANI WA HALI YA JUU.yesu na bible imeendika waliokuwa nacho wataendelea kuwa nacho na wasiokuwa nacho hata kile walichokuwa nacho kitachukuliwa.KAMA WEWE NI MTOTO WA MLALA HOI HATA UENDE MAREKANI MAISHA NI YALEYALE shida ni ileile . UTAJIRI NA MAISHA MAZURI NI BARAKA YA MWENYEZI MUNGU WAMEBARIKIWA HATA HAPA MAREKANI UTAONA . KENNEDY WANAENDELEA KUWA KENNEDY ,OBAMA WATOTO WAKE ANAWAPELEKA SHULE 48,000 KWA MWAKA WATOTO WAWILI 98,000 WAKIFANIKIWA BABA YAO FISADI , CLINTON NI CLINTON HATA UFANYE NINI. MFANO KAKA MICHUZI ANAKUMBATIA WATU WAAINA ZOTE ATAFANIKIWA ,. HANA HASIRA NA MTU. WATOTO WAMAFISADI WATAENDELEA KUWEPO KWA SABABU WANAOPPORTUNITY NA WAMESOMESHWA. MUWE NAUPENDO KWA WALOIOFANIKIWA SIO WIVU NAKUHARIBIA MAJINA WATU. MAJINA HAYO YAMEANDIKWA MBINGUNI YAMEBARIKIWA USIACHE KUINGIA UFALME WA MBINGUNI KWA AJILI YA WATU WALIOBARIKIWA NA WEWE ULISAHAULIWA TAYARI . AHSANTE KAKA MICHUZI KWA BLOGU HII UTAFANIKIWA

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2009

    swala siyo swali au maoni......wote mafisadi tuuuuuuuu ...hizo hela wanazoandaa nazo hizo shughuli bora wangetuma vijijini kwao visaidie sg=hughuli za maendeleo

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2009

    Hivi ni kwanini mtu akitaka kutoa mada yake lazima aichafue kidogo dini yetu tukufu ya kiislamu? Eti Mbarouk Said!!! Jina umetunga hilo..

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2009

    wivu wivu roho zinawauma watoto wa mafisadi wanaishi maisha hayana stress nyiyi kutwa nzima kushindana nao . mnaumia bure follow the croud you wont reach any were

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 08, 2009

    Labda hizo nchi wanakataza kufungua matawi ya vyama vingine...kama wanaruhusu mnasubiri nini? au mnaendelea kuhesabu matawi ya CCM !!! bado sijaelewa kinachoendelea hapo jamani...kitu gani kinawafanya msifungue matawi ya vyama vingine??

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2009

    Hili kweli ni swali la kizushi, kwanza hakuna Polisi wa CCM, pili Polisi siku hizi hawachukui rushwa ukilinganisha na miaka iliyopita na minyanyaso ya polisi kwa raia imepungua sana. Mzushi mkubwa we... na hizo ndizo sababu za watu kujiunga na CCM.
    Tuangalie miaka 10 iliyopita, ni viongozi wangapi wa upinzania walikuwa wanapigwa na kufungwa bila makosa? Leo hii hebu nipe mfano angalau mmoja..sijaona wala kusikia.. mzushi we usilaumu polisi kabisa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 08, 2009

    ni kweli kabisa nashindwa kuelewa matawi ya ccm nje ya nchi ni nini si ni ujinga tu
    ni watu wale wale wanaofadika na kodi za watanzania walio nyumbani wanateseka huku hao wakisomeshwa na kufaidika na pesa wa walalahoi watanzania zinazofisadiwa na wazazi wao
    shenzi type

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 08, 2009

    Hivi kipi ni bora, kujiunga na CCM au na chama cha MREMA au chama cha Wapemba (CUF) au chama cha wachaga (chadema). Binafsi naona ni bora kujiunga na CCM na natarajia kujiunga nacho nitakaporejea bongo mwezi julai ili nishiriki katika kuchagua kiongozi bora. Tatizo la vyama vya upinzani ni kufadhiliwa na mafisadi huku wao wakijifanya ndiyo wapiganaji wa ufisadi na pia kuwa vyama vya kifamilia zaidi kuliko kitaifa. Mfano mzuri ni huu wa sasa ambao kila kiongozi wa upinzani pamoja na wanaCCM wachache kumtetea R.ABRAHAM MENGI wakati naye pia ni fisadi ila anatumia vyombo vyake kutugawa. Kimsingi si MENGI wala ROSTAM anayepaswa kutetewa mbele ya umma kwani wote ni wezi wa mali zetu na tunapaswa kuwajadili kwa uovu wao na siyo rangi zao. MENGI katoa tuhuma bila vielelezo wakati ROSTAM katoa vielelezo na hivyo ni kazi ya R. A.M kkwenda kujisafisha mahakamani au naye apeleke vielelezo vyake TAKUKURU. Kumbukeni ule msemo, Kikulacho kinguoni mwako. Magazeti yetu (isipokuwa habari leo)sasa hivi yanaboa kwani kila 1 lina makala nyingi tu za kumtetea mengi na kumponda Rostam. Hivi MENGI hawezi kuwa fisadi kwa kuwa yeye ni mzawa? Hivi ni pesa ngapi za walalaho zinaibwa na wafanyakazi wazawa? Kama tunataka kusafisha nyumba ni bora kutoa kila aina ya uchafu bila ya kujali huu umeletwa na wageni au wenyeji

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 08, 2009

    umeuliza swali hili kama mtu mwenye frustration. anyway pole. mie sio mpenzi wa siasa. nachukia siasa kuliko kitu chochote hapa duniani.

    kwa kifupi unatakiwa kuangalia trend na unatakiwa kujua unatafuta nini. unatakiwa kutafsiri nyakati kisha kuangalia wapi pa kutua.

    mdau wa arusha

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 08, 2009

    Mdau,

    We jiulize, umeshaona watu wenye kazi za kueleweka ulaya wakijivalisha hayo magwanda ya CCM? Hao unaowaona mitandaoni wakipiga miluzi ya kwamba wao ni CCM damu wote walelosti uko Ulaya na wanatafuta alternative "job" to do nyumbani siku watakaporudi. Wamechoka kuosha vyombo ulaya so wanategemea CCM itawapokea. Walishindwa kwenda shule uko ulaya so hawana vyeti vya kueleweka. Kama wanavyo basi vitakua ni vya kutoka kwenye degree mills like Washington International University ambako waheshimiwa wetu wengi wanadai wamesomea.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 08, 2009

    Ahhh Mbarouk, mbona wewe unasoma akili za watu. Yaani ni jana nilikuwa nataka nimtumie Michu ili swali.
    Kusema ukweli, sio kwamba wale walioko Tanzania wamechanganyikiwa ila naona wengi tulio nje tuna mtindio wa Ubongo.

    Kwamba CCM ndo kuna ulaji, kumbe nia ni fwedha sio nini kizazi kijacho kitanufaika vipi.

    Mimi ninapoona hizo uniform zao natamani hata kutapika. Tena watu wamesoma (ila hawakuelewa) bado wanapanga mistari kuchukua kadi za CCM, kama sio mtindio wa Ubongo ni nini?
    Mtanisamehe kwa kutumia lugha mbovu ila ukweli ni kwamba most of us are not ready to use our brain and analyze the real situation of our country. We would rather stay abroad and than home, but doesn't want ask ourselves why we are running away from Tanzania.

    We got to think critically people.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 08, 2009

    fikra mbovu za hawa walio nje kuanzisha matawi,kwanini wasirudi nyumbani kujiunga na vyama?wizi mtupu

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2009

    Mbaruku sijui wewe ndugu yangu unatokea Kenya! kwani unapouliza swali hasa kwa watu wengi duniani hebu siku nyingine muulize rafiki yako wa karibu kabla ya kuomba majibu kwa watu mbalimbali. Swali lako ni la msingi ila majibu yake ni wazi kabisa.
    Itachukua miaka mingine si chini ya 20 kuing'oa CCM madarakani.
    Ukitaka ulaji ndugu yangu inabidi ujipendekeze na CCM.
    Ukihitaji ulinzi na kuweza kufanya shughuli zako vizuri jiunge na CCM.
    Unapoona watu wanafungua matawi sehemu mbalimbali wenzako wanajitengenezea njia ya ulaji, siku hizi ulaji ndani ya CCM ni nje nje kuna ubunge wa kuteuliwa( Special seat) Rais akikuona unajuhudi na CCM hata kama umemaliza darasa la saba unapata ubunge wa kuteuliwa na rais. Kama upo nje ya nchi na unataka kurudi tanzania itabidi ujiunge na CCM ukifika kule utaonyesha picha mbalimbali kwamba ulikuwa unatetea CCM ukiwa ulaya au marekani kisha utapachikwa ulaji wa nguvu.
    Ninakupa kazi moja ya utafiti, Je wabunge na mawaziri wanalipwa mshahara pamoja na marupurupu kiasi gani kwa mwezi. Ukipata jibu utashangaa mwenyewe na itabidi utafute hiyo nafasi ya ubunge na wewe.
    Kuna wabunge wengine tangu wameingia bungeni miaka 3 iliyopita hawajawahi kuuliza swali wala kuchangia hoja yoyote kazi yao ni kwenda kukusanya kichele na kuendelea na shughuli zao binafsi.
    Sasa hao wanamuakilisha nani.
    It's all about ulaji hakuna sera mpya hapo.
    Ufisadi upo kila corner sio CCM tu hao ni wachache waliojulikana lakini wapo mafisadi wasio na chama maalum.
    Na ufisadi upo dunia nzima ni vigumu kuupiga vita, kama sasa hivi tembo wanapigana manyasi ndo yanaumia kwa kukanyagwa.
    Jifunze siasa ya ndani ya tanzania kuna sirikali hiyo ndo maana ya serikali.
    Nafikiri umenielewa bwana Mbaruku!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 08, 2009

    Ndugu yangu uliyemkosoa Mbaruku nadhani wewe ndo mvivu wa kufikiri. Kwa ujumla umechanganya mambo ambayo mi binafsi naona yamepungua uchambuzi yakinifu.Ni kweli mafisadi ni watu na si chama lakini si ni hao watu ndo wanajenga mihimili ya chama na ilani ya chama. Hivyo wako ndani yake na chenyewe ndani yao??. Mi CCM na lawama hatutazikwepa bila kuambiana ukweli na kutosana. Si akina Batholomeo basi wamwambie Yuda Isikarioti kwamba u mamluki na usituharibie!!!! Hata hivyo nashukuru umekubali kuwa kuna uwezekano wakiingia wakawa mafisadi. Huenda nao ni zao la mafisadi. Ni mawazo yangu tu. Mungu Ibariki TANZANIA

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 08, 2009

    UKIANZISHA TAWI LA CHADEMA, UBALOZI UTAKUFUKUZA NCHINI.

    KULA NA KIPOFU.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 08, 2009

    KUSEMA UKWELI WATU WANAOJIFANYA KUFUNGUWA MATAWI NJE YA NCHI SI WASTAARABU NA ELIMU ZAO NDOGO,,
    NAWANATIA AIBU KWA KUTEMBEA BILA KUSTAARABIKA AU NI WAFA MAJI

    UJUWE MFA MAJI HUWA HAACHI KUTAPATAPA
    HUENDA WAMEKOSA WALIYOKUWA WAKIYAKIMBILIA SASA WANARUDI NA GIA YA CHAMA HAO NI WEHU TU TUSIWAJALI SANA

    ReplyDelete
  24. Waacheni wafungue matawi, Ulaya, Marekani, Asia et al. haya ni matawi ya birthday parties na kutafuta watu wa kudate na kuibiana wake/waume. Si unajua ulaya mambo ya kujichanganya yanakuwa magumu kila mtu kivyakevyake tu na kupata mtu wa kumdanganya akukubalie inatakiwa na effort kubwa zaidi ukilinganisha na mwanachama mwenzio na mmbongo mwenzio mbeba box mwenzako mnaejuana.

    Sasa basi mkitaka kujua kuwa matawi haya ni useless ngojeni warudi bongo wajifanye wanataka kugombea uongoz, wakikutana na zengwe na kuendeana kwa sangoma na kupata kura tatu au moja wanapanda ndege na kurudi abroad huo unakuwa mwisho wa tawi.

    Hivi bongo ni nani akuchague wewe unayeishi ulaya hata kwenye misiba huwa hakuoni jirani akifiwa?.

    Wabongo tuache huu utamaduni kama birthday parties anzisheni vyama vya kitaifa au kikanda si kuleta U-CCM, hakuna anayewajua mkirudi bongo. Tena hata viongozi wa chama wanawaona kama ni maadui zao wakubwa mnaotaka kuchukua nafasi zao za ulaji kwa kisingizio mlikuwa ulaya. Watawapenda mkiwa huku mkirudi bongo wanawaona maadui zao.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 08, 2009

    Michuzi comment kama hizi tafadhali uwe unaziweka kapuni. Au na wewe ni katika wavivu wa kufikiri? CCM ina wanachama milioni tano nchi nzima, wengi wao wakiwa ndani ya Bongo. Hawa majuha wanaoona ajabu watu kuingia CCM mbona hawaoni ajabu watu kuingia strip clubs, kunywa gongo, na kuingia chama cha Mrema ambaye sasa kishakuwa mwehu. Huyu mdau aliweka hii post sio mwanademokrasia kabisa. Acha watu wachague kujiunga na Chama wanachotaka. Katiba ipo kulinda ujuha wa kila aina ili mradi usivuke mpaka. Wewe pilipili usiyokula inakuwashia nini.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 08, 2009

    Ni kutokana na watu kukosa uzalendo na uchungu wa nchi yao. Wana macho lakini wanajifanya hawaoni, wana masikio wanajifanya hawasikii yanayojiri katika nchi yao. WIZI MTUPU! Wanadhani kwa kujipendekeza kwa CCM nao watapatiwa mgao wa keki ya taifa bila jasho. Waache waendelee kufungua hayo matawi lakini kuna siku CCM itaondoka madarakani na watabaki na aibu! Nani alitarajia vyama kama UNIP, KANU na vinginevyo vilivyojisahau, kama vingesahauliwa? Dawa yao iko kwenye chupa ya watainywa wapende wasipende. NI SUALA LA MUDA TU.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 08, 2009

    MUULIZE TAMBWE HIZA. YEYE ALITOKA UPINZANI AKAINGIA CCM

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 08, 2009

    ccm london ni mtihani nadhani ni buzwagi fulani-mradi wa wajanja.
    kwani wao wameomba dola elfu themanini kuimraisha chama toka makao makuu.wamngekuwa na huruma wao ndio walitakiwa kuwasaidia watu waliopo nyumbani.

    kibaya zaidi hakuna la maana wanalofanya. vyema CCM ingefanya utafiti wa kutosha kuwajua kuwa kuna matapeli wanaotumia kivuli cha ccm kufanya malengo yao.

    hata utaratibu wa chaguzi hawaujui. wanakutana watu sita wanaenda kwenye mgahawa wanapiga picha wanazituma kwa michuzi kuwa tunazindua tawi la ccm.

    hivi sasa kuna credit crunch ndio kila mtu yuko kwenye chama huko nyuma wakati hakuna credit crunch hatukusikia kuwa watu wako UK wanataka kufungua matawi walikuwa busy na kutafuta pounds hivi sasa hakuna pounds ndio wameamua kuja na ushuzi huu.

    kwa vile nia zao sio za dhati mambo haya yakupita tu ikifika 2010 baada ya uchaguzi na wao hutawasikia.

    pia ni kikundi cha watu kama wanne tu hakuna kitu zaidi ya watu hao ambao wanabadili kanzu tu, yaani utasikia tumefungua tawi birmingham la ccm kumbe ni wale wale watu toka reading.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 08, 2009

    Mbona Vyama vengine jamani havionekani nje ya nchi.Au ndo watanzania sasa wanaijuwa Democracy wanajifanya wakati uchaguzi wa visiwani zenji watu wanakula risasi na mabomu ya machozi kila uchaguzi.
    Sasa hawa CCM wanashangaza sana kuonekana kila nchi wana matawi kama mti.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 08, 2009

    NILISHASEMA KUHUSU HILI NA NINASEMA TENA, MATAWI YA VYAMA VYA SIASA NJE YA NCHI YANATUTENGA KIITIKADI, HAPA UGHAIBUNI TUNAHITAJI MSHIKAMANO KAMA WATANZANIA, SIO KUTAMBUANA KWA MI CCM AU MIMI CUF NK. TUTAANZA KUCHAPANA BAKORA UGENINI HUKU !!

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 08, 2009

    Ukitaka mambo yako yakunyookee wewe ingia CCM-Sumaye speech!!

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 08, 2009

    Asante sana Maoni haya mazuri.Watanzania wanafikiria ulaji tu.Sasa hivi jamani tufikirie mbele.Na msingi unatakiwa kuwekwa sasa na sio kesho.Tuwaonyeshe watoto wetu kuwa sisi hali hii ya watu kushabikia au kuhamia chama kwa maslahi binafsi imepitwa na wakati.Sasa tunataka tuweke msingi wa kubadilisha tabia zetu za kushabikia kitu ,hata kama kina aharibu future ya watoto wetu sote.Tujue rais wa 13 wa nchi hii yupo kwenye jamii hii
    watoto Sasa tunawafundisha nini?kujipendekeza kwa ajili ya pesa au kuitumikia nchi yako.Tunatakiwa tuwaandae akina nyerere wengi zaidi sasa.MUNGU IBARIKI TANZANIA.TUTAFIKA TU.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 08, 2009

    Habari za kazi Kaka Michuzi, nimesoma maoni ya watu wote hapo juu lakini nashangaa watu wote au baadhi yao wanatoa shutuma,kama kweli wote waliotoa maoni ni watanzania sioni sababu ya wao kubishana kama siasa kila mtu anaingia kwa faida yake wanasiasa wa kweli wote wamashakufa au kuzeeka,nani asiyejua kwamba siasa ni mradi mtu uwezi kujitolea pasipo faida kama unavyowaona matajiri Tanzania wanatoa michango ya mamilioni kwa CCM unategemea nini,kabla ya bomu la epa kulipuliwa ulikuwa inaona watu wanatoa mamilioni ya fedha kwa chama kumbe ilikuwa janja toto sasa kuna kesi mahakamani michango imepungua ila umetokea mtindo mpya watu wamejitokeza kutaka kuchukua katika chama ndio maana unawaona wanfungua matawi.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 08, 2009

    jibu hili apa.
    hawa ccm wameshtukia dili, wanajua watu wengi wakitoka nje ya nchi wanazinduka na kujua kama ccm haina maana, so ili kuwawahi wakirudi wasilete zogo wanataka wawaanze ukouko walipo, keep it up ccm, lkn iko cku watu watashtuka na mafisadi wote watajulikana

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 08, 2009

    kwa kifupi hao ni watu walioko nje kwa hela za walipa kodi wa tanzania. baba zao waniba na kuwapeleka nje. sasa wanaona hali tanznia si shwari , wananchi wameanza kuamka. sasa na wao huko nje ndo wanakusanya nguvu kutetea kitumbua kisiingie mchanga. mana ccm ikipigwa chini wataishije hao na wamezoea kuisha kwa hela za wizi??

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 08, 2009

    jamani mliopo nje ya nchi anzisheni association zenye akili!

    mfano ni hii ya Wa tanzania - Hyderabad - India!

    http://tsah.org/
    http://tsah.org/Gallery.html

    tukiendeleza hizi za ccm, chadema, cuf nk sio vizuri kwani kama kuna tatizo mtaanza kuulizana hivi huyu jamaa ni wa chama gani??
    afu..mkikuta sivyo ndivyo mnampa kisogo!!

    tutafikia hata kuanzisha jumuiya za kidini ughaibuni.......
    au za wazenj na wa Bar!!

    haipendezi!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 08, 2009

    Nafikiri watu wa Tanzania mtalalamika sana bila kupata ufumbuzi wa matatizo yetu.sasa tufanye hivi kwa mafisadi au watu wote waliojitajirisha kwa migongo na lasilimali zetu.Tujiunge tuform vikundi vya kijeshi tuwateke wao[mafisadi au watoto wao],then tudai lumpsum kama wasomali walivyoanza kwa meli za uvuvi kutoka ulaya na asia . Get the picture of you having rost tamu kama refugee! For sure kutakuwa na adabu hapo Tz

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 08, 2009

    si mchezo,kwa maandishi tu watu wanamalizana je wakikutana uso kwa uso itakuwaje. ni wangapi kati yenu ambao wakiwekwa kwenye mfereji wa hela hawatachota? inajulikana kuwa inauma sana kama huishi karibu na mfereji


    Mbega

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 09, 2009

    HAPO NI MRADI TU HUO NA KUTAFUTA PESA. CCM LONDON IMESHAPEWA $80,000 ETI KUBOLESHA CHAMA KITU GANI WALICHOFANYA ANAJUA MUNGU. PESA ZA WALALA HOI HIZO. IPO SIKU IPO SIKU CCM MTAKUJA KULIPA KUANZIA NYIE WA LONDON HATA AIBU HAMNA BADALA KUFANYA KILICHAWAPELEKA NENDENI SHULE NA KUFANYA MAMBO YA MAANA HAYO YA CCM WAACHIE WALIOKO BONGO. YAANI OF ALL THINGS YOU COULD DO MMEKUJA NA KUANZISHA TAWI. HIVI LEO WATU WAKIANZISHA VYAMA TOFAUTI VYA KISIASA NA KIDINI SI ITAKUWA MWANZO WA KULETA VURUGU NCHI ZA WATU NA HATA NDANI YA NCHI.TUKO NJE JAMANI TUPENDANE KAMA KUNA HAJA YA KUANZISHA UMOJA BASI UWE UMOJA WA WATANZANIA NA TUTAFUTE NJIA YA KUWASAIDIA WENZETU WA NJE NA NDANI YA TANZANIA NA SIO KUWATENGA KWA SIASA.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 09, 2009

    Kwa taarifa yenu.. watoto wa vigogo walio nje baba zao hawana hela wala dili yeyote. Kama m-sure ana hela huende nje kufanya nini bwana? Kubeba box. Fanyeni utafiti mtajua siyo lazima niwatajie majina.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 09, 2009

    CCM UK HAKUNA MTOTO WA KIGOGO UKIONDOA SUSAN LYIMO-MZEE AMBAYE NI NDUGU WA BASIL MRAMBA,WENGINE NI WALALAHOI WANATAKA KUTUMIA MWANYA HUU,TENA WOTE HAO WANA CCM HAKUNA MWENYE ELIMU AU DIGRII ZA MAANA WAMESOMA KOZI AMBAZO UKIRUDI TZ HUPATI KAZI.

    WENGI WAO WANALEA WAZEE KWENYE HOMES KAZI MAARUFU YA CARE, HIVYO KAZI WANAYOFANYA HAIWAONGEZEI UZOEFU WA KAZI -WORKING EXPIRIENCE AU ELIMU WANAYOTUMIA KWENYE KAZI HIYO HAIKO RELEVANCE NA KAZI ZA TANZANIA.

    HAKUNA MTU MWENYE SIFA KAMA ACCOUNTANCY CHARTERED CERTIFIED ASSOCIATION-ACCA.AU LLM AU MSC COMPUTER N.K WENGI WAO HAWANA DIGRI WANA DIPLOMA ZA VYUO VYA MTAANI,HAKUNA MTU ALIYE NA ELIMU TOKA PURE UNIVERSITY KAMA YORK,LEICESTER,MANCHESTER,UNIVERSITY OF LONDON,WARWICK ETC.HIVYO KUWEPO KWAO ULAYA AU KAZI WANAZOFANYA HAZIWAPI CHANGAMOTO YA KWENDA TZ NA KUCHUKUA KAZI ZA MAANA KWENYE MASHIRIKA MAKUBWA AU TAASISI.HIVYO NJIA YA KUPITIA NI CCM.

    HAWANA VISION WALA HURUMA NA NCHI WAMESHINDWA KIPINDI KAMA HIKI KUTOA MSAADA KWA WAHANGA WA MBAGALA.

    KITENDO CHAO CHA KUOMBA PESA ZOTE HIZO KUTOKA MAKAO MAKUU NI CHA KULAANI.JEE KILA NCHI IKIFUNGUA MATAWI IOMBE PESA MAKAO MAKUU?

    RUSSIA NAO WAOMBE DOLA ELFU THEMANINI,MAREKANI KWA VILE KUBWA NI MARA 52 KUILINGANISHA NA UINGEREZA YAANI UK INAINGIA MARA 52 KUPATA MAREKANI MOJA, HIVYO WANACCM WA MAREKANI WAOMBE DOLA ELFU THEMANINI MARA 52? BADO MATAWI YA INDIA, MALAYSIA ETC.

    CCM MAKAO MAKUU TIZAMENI ATHARI ZA HUU UTARATIBU WA MATAWI YA CCM NJE.

    JIULIZENI HAWA WOTE WAMEONDOKA TANZANIA WATU WAZIMA WAKIWA NA UMRI ZAIDI YA MIAKA 18 KWANINI WASICHUKUE KADI ZA CCM WAKIWA NYUMBANI? WALISAHAU NINI?

    PIA KAMA WAMEKIPENDA CHAMA WAKIWA UGHAIBUNI KWANINI WANAPOKWENDA LIKIZO WASICHUKUE KWENYE MATAWI WANAOWAJUA VIZURI?

    KWANI KUCHUKULIA HUKU UGHAIBUNI KAMA MIENENDO YAO HAIJULIKANI NANI ATAFANYA VETTING?WANA UHARAKA UPI HADI WASISUBIRI WAKIRUDI NYUMBANI WACHUKUE KADI ZAO?

    WANAAMINI KUWA WAKIRUDI NYUMBANI WATAPEWA UONGOZI WA KITAIFA,HUWEZI KUMPA MTU UONGOZI WA JUU KAMA HANA REKODI KWENYE LOCAL BRANCHES ZA CCM TANZANIA.

    HIVI KARIBUNIPROFESSOR SAFARI WA CUF ALIOMBA UENYEKITI TAIFA WA CUF, AKAULIZWA SWALI JUU YA USHIRIKI WAKE WA SIASA KWENYE TAWI LAKE NA PIA NANI KATIBU WA TAWI LAKE LA CUF AKASHINDWA KUJUA.

    KHADIJA KOPA ANAKESHA KUINADI CCM ASIWE BORA,WEWE AU MIMI KWA VILE UMETOKA UK UPEWE UONGOZI,SIDHANI CHAMA MAKINI KAMA CCM KITARUHUSU UJINGA HUO.TUSITUMIE KUWA ULAYA KUWABANA WENZETU AMBAO HAWAKUPATA FURSA YA KUJA HUKU.

    UTENDAJI WA WANA CCM ULAYA UTOKE KWENYE MATAWI YAO TANZANIA.KINYUME NA HAPO NI UTAPELI AU WIZI MTUPU!

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 09, 2009

    we fara kwani umeshikiwa panga kuingia ccm?si achana nao

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 09, 2009

    HATA MIE CCM NIMEWACHOKA NIMEWACHOOOOOKAAAAA VIBAYA MNO..TUMESHAONA HAWAWEZI KAZI..MIAKA 47 SASA NA BADO KIJIJINI MWANACHI ANABEBA MGONJWA MGONGONI KUMPELEKA HOSPITALI. INGEKUWA WANA UONGOZI WENYE UADILIFU NA UTENDAJI KAZI BORA TANZANIA SASA HIVI TUNGEKUWA MBAAAALI SANAAAAAAAA KUTOKANA NA UTAJIRI TULIONAO... LAKINI SASA HIVI NI KAMA TUNAPIGA MARKTIME....WALALAHOI WANAZIDI KULALA..HAMNA MATUMAINI..NA HUKU SERIKALI INAZIDISHA USANIIIII

    ITS TIME FOR CHANGE JAMANI....SERIOUS WE NEED CHANGE..CCM TUMEWACHOKAAAAAAA..ENOUGH IS ENOUGH

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 09, 2009

    Kelele za chura hazimzuwii tembo kunywa maji.
    CCM kiboko!

    ReplyDelete
  45. Advocate JashaMay 09, 2009

    KUANZISHWA KWA MATAWI YA CCM UGHAHIBUNI HAKUNA MAANA YOYOTE MBALI NA KUJIPENDEKEZA KWA MANUFAHA YA KUJIPATIA POSTI ZA KAZI HUKO NYUMBANI.KWANI BILA KUA MWANACCM KUPATA POSTI NI KAZI .KUNAWATAALAM KIBAO AMBAO WANAWEZA KULISAIDIA TAIFA LETU KWA KAISI KIKUBWA LAKINI KWA VILE SIO WANA CCM KAMWE HAWATAPATA POSTI NAKUTOA MCHANGO WAO KATIKA TAIFA.WASOMI NA WATANZANIA UGHAHIBUNI BADALA YA KUUNGANA NA KUJARIBU KUJADILI NA KUFIKILIA JINSI YA KULISAIDIA TAIFA LETU KWENDA MBELE TUNAANZA KUJADILI MAMBO YA KUFUNGUA MATAWI.HAYA MATAWI NAWEZA KUYAITA MATAWI YA SHEREHE WATU WANAKUSANYANA WAKATI WA SHEREHE YA MUUNGANO IKIISHA IMETOKA M PAKA SHEREHE IJAYO.CHAKUSIKITISHA NI YA KUA HAYA MATAWI MENGI YAMEAANZISHWA KWA KUFUATA MKUMBO AU KUNAFISADI KATIKA CCM KABUNI KAMRADI KAKUJIPATIA PESA KUPITIA MATAWI HAYA YA UGHAHIBUNI KWANI NAAMINI SI HIVIHIVI KUNA PESA KUYASAIDIA MATAWI YAO.HAO WANACHAMA UGHAHIBUNI WANANUNULIWA COCA-COLA NA VODKA MAFISADI WANAJENGA MAJUMBA.KIONGOZI YEYOTE WA HAYO MATAWI ANAWEZA KUNIAMBIA HAYO MATAWI NINI CHA MAANA YAMEKIFANYA KUWAUNGANISHA WATANZANIA.KATIKA MIAKA 10 KUADHIMISHA KIFA CHA BABA WA TAIFA NI MATAWI MANGAPI UGHAHIBUNI YALIANDA MAKONGAMANO KUMUENZI BABA WA TAIFA?NIMATAWI MANGAPI HUKU UGHAHIBUNI YAMEJARIBU KUANZISHA UHUSIANO WA KICHAMA NA VYAMA VINGINE UGHAHIBUNI?NI IMANI YANGU HAKUNA MAJIBU.HIVYO KWA MAWAZO YANGU YA KUA HAYA MATAWI MBALINA KUNUFAIKA WATU WACHACHE WENYE AJENDA ZAO ZA SIRI HAYANA MANUFAA YOYOTE KWA WATANZANIA UGHAHIBUNI.MUNGU IBARIKI TANZANIA!

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 09, 2009

    Hata siku moja watanzania waishio UK waliosoma vyuo mashuhuri kama Oxford, Cambridge, Edinbrugh, Bristol, etc. huwasikii kujinga na vyama vya siasa zaidi ya kuunda jumuiya za ndogondogo kusaidia miji na vijiji walivyotoka. Kuna dada mmoja msomi wa kibongo anaishi UK kaungana na wazungu wa kanisa lake wanatoa misaada huko Masasi na maeneo mengine ya kusini. Na wazungu walionaye wanajitolea kwenda Tanzania-Masasi kufanya kazi za kujitolea za maendeleo (kujenga madarasa, kufundisha, kutoa baiskeli za walimu, mashine za unga, vyerehani za wajane waathirika, etc.). Na bado hao wazungu kila familia wana mtoto huko Mtwara wanamlipia ada ya shule secondary. Kuna watoto zaidi ya 30 wanalipiwa ada toka kwenye mradi huo.
    Hivyo ndio vyama/vikundi na miradi tunayotaka vianzishwe UK na kote ulaya ajili ya maendeleo ya wale tuliowaacha Tanzania, sio matawi ya vyama vinavyoomba pesa za walalahoi toka Tanzania kuja UK. Hata hawa wazungu wakitusikia naona watatuona sio majuha kweli.

    Mdau UK
    P. Malela

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 09, 2009

    MBAROUK, MAMBO YA KUFUNGUA MATAWI YA CCM YAKO UINGEREZA,INDIA NA ITALY UPUMBAVU KAMA HUO HUTASIKIA MAREKANI NA CANADA UNAJUA NI KWANINI?UINGEREZA NA ITALY MAISHA MAGUMU WANAJIPENDEKEZA KWENYE CHAMA TAWALA WAKAPATE ULAJI MUDA WA KUISHI UINGEREZA UMEISHA WANATAFUTWA NA ASKARI WA UHAMIAJI KWA HIYO WANAJIWEKEA AKIBA YA BAADAYE SIKU WAKISHUKA BONGO.HILI SWALA LINANITIA KICHEFUCHEFU BADALA YA KUCHANGISHA PESA WASAIDIE WATOTO YATIMA,MAHOSPITALI NA MASHULE WANAFUNGUA MATAWI YA CHAMA NCHI ZA WATU HILI LINASHANGAZA WENGI SANA HAPA MAREKANI.

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 10, 2009

    SUALA SIO CCM KIBOKO ILA UKWELI WA HAWA WANAOFUNGUA MATAWI HAUELEWEKI.
    INAONEKANA NI MRADI WA WAJANJA KAMA AMBAVYO WATU WANATUMIA JINA LA KUFUNGUA NGO KUFANYA UJANJA WAO.

    SUZAN LYIMO MZEE KAMA NI NDUGU WA MRAMBA BASI NI HATARI AU YEYE ATAKUWA TOFAUTI NA BASIL MRAMBA?
    WANA CCM UKEREWE TUMIENI NAFASI YA KUWA ULAYA KUCHUKUA ELIMU YA MAANA AU KUSAIDIA NYUMBANI SIO NYINYI KUOMBA PESA TOKA NYUMBANI.

    ILITAKIWA NYINYI MUWE DARAJA LA WATANZANIA NA NCHI ZA ULAYA KWA KUPELEKA MAENDELEO TANZANIA SIO KULETA MIGAWANYIKO KAMA INAYOANZA KUJITOKEZA.

    PIA KWA SHERIA ZA UK NI KOSA KUWA NA MATAWI YA CHAMA CHA SIASA HILO MNALIJUA?

    NIMESHANGAZWA KUSIKIA KUWA HAWA HAWANA ELIMU YA MAANA SASA MTAONGOZA VIPI CHAMA KAMA HAMNA ELIMU TOKA VYUO VIKUU VYA UK? WANA CCM WA TANZANIA WANATEGEMEA NYINYI MNA ELIMU YA MAANA,SASA KAMA ELIMU YENYEWE NI YA CARE KUTAKUWA HAKUNA TOFAUTI YA NYINYI KUWA ULAYA.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 10, 2009

    HIVI HAWA WATAPIGA KURA VIPI HUKU ULAYA WAKATI WA ELECTION, TANZANIA INA TEKENOLOGIA YA KISASA KAMA ZA USA KWA AJILI YA WANANCHI KUPIGA KURA KWA WANACHAMA WA VYAMA VIKUU.

    KITU KIMOJA NAWEZA KUSEMA NYIE MNAPOTEZA MUDA KUFUNGUA MATAWI HUKU, KUNA VIJANA WANAHITAJI MSAADA WENU.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 10, 2009

    ccm london mmeona kazi ya mama salma kikwete shule ya NYAMISATI?msaidie kupeleka vitabu sio blah blah tu.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 11, 2009

    NDUGU YANGU ULIYEULIZA SWALI LA KIZUSHI,SIYO LA KIZUSHI KWA KUWA HUJAZUSHA.
    tENDO LINALOFANYWA NA WANA C C M NI TENDO CHAFU KAMA TENDO LA NGONO HADHARANI,C C M CHAMA CHAKAVU NA KICHAFU, WATU WAKE WACHAFU,SERA CHAFU PIA, KUANZISHA MATAWI HUKO UJUE HUKU c c m HAITAKIWI NDO MAANA WANASAKA MI MBU MBU MBU HUKO NJE.hEBU FIKIRIA mkoa WA MARA ANAOTOKA BABA WA tAIFA IKIWEMO tARIME NA MUSOMA MJINI HAWATAKI KABISA KUISKIA C C M WALA MAKAMBA YAKE.IWEJE HUKO NJE IKUBALIKE ?,C C M INAPATA MBUMBUMBU WAPYA SIO WANA cHAMA TENA fULL MAAMUMA.JITAHIDINI SANA KUCHAMBUA MADA NA KAMA HUNA CHA KUTETEA BORA UTETEE VIBAKA SIO C C M

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 11, 2009

    hahahahahhaaaaaaa
    kwi kwi kwi
    tih tih tih
    uwiiiiiiiii.....

    nimemaliza and i call it a day

    kwa tashwishwi nilikuanayo before kuhusu ivo vyama UK

    asanteni sana

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 11, 2009

    WEWE LAZIMA MWANACHAMA WA CUF AU CHADEMA. HIYO NDO HALI HALISI NA NYIE MNAPAMBANIA HAKI ZA WANANCHI WAAMBIENI WAFUNGUE MATAWI ABROAD.

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 11, 2009

    aiseee duh!!

    ivi hizi jumbez zinawafikia walengwa UK au mashushu wa ccm au usalama wa taifa Tz???

    misupu zifikishe kabisa,laah naomba mjadala huu uwekwe magazetini watu wadondoke essays izi uko,,,asa magazeti ya UDAKU ambayo uswazi ndo tunayasoma saaNAA

    so michu form today on usiweke post za ao wanaCHAMA umu blogun watu weeengi hawazifagilii!!inaboa

    watu wana hasira!!jicho limentoka apa

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 11, 2009

    KELELE ZA CHURA HAZIMZUII TEMBO KUNYWA MAJI
    1. CCM OOYEEEE!!!!! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
    MTOA MASWALI NI YA KIZUSHI NA PIA MAJIBU YALIYOTOLEWA SO FAR NI YA KIZUSHI, HAMNA DATA ZOZOTE SAHIHI MLIZOKUWANAZO, YOTE NI UZUSHI MTUPU!!!NA MNAIPOTOSHA JAMII ILI IWAAMINI NYINYI MAHAYUWANI WENYI UFINYU WA FIKRA, BINAADAMU ANA HAKI YAKE KUAMINI KITU CHOCHOTE AIDHA KATIKA DINI,ITIKADI,JINSIA N.K ILIMRADI TU ASIVUNJE SHERIA, KWA TAARIFA ZENU HAKUNA SHERIA YOYOTE ILIYOVUNJWA HUKU (UK) KATIKA KUFUNGUA HAYA MATAWI YA CCM, NA NDIO MAANA WANACCM BADO WANAPETA,KITU USICHOKIJUA NI MIPANGO GANI YAKINIFU ILIYOWEKWA NA WANACCM UGHAIBUNI KATIKA KUMKOMBOA MTANZANIA KATIKA HALI YA UMASIKINI,MARADHI,ELIMU, N.K, SUBRA HUVUTA KHERI, WAKATI UTAFIKA NA MTAYAONA MATUNDA YAKE.

    2.ETI MNAWAPONDA VIONGOZI NA WANACCM UGHAIBUNI YA KWAMBA HAWAJASOMA, ACHENI UONGO NA UZUSHI PATENI PERSONAL PROFILES ZAO ZA MASOMO NA KAZI WANAZOFANYA NA MTAPIGWA NA BUMBUWAZI, WENGI WAO NI WASOMI WALIOSOMA KWENYE VYUO VYA MAANA NA ELIMU YA JUU, NA SIO KUSOMA TU PIA WAMEELIMIKA NA BADO WANAENDELEA KUSOMA, UKITAKA UKWELI ZAIDI HEBU TUITISHE MKUTANO WA TANZANIA WASOMI UINGEREZA HALAFU UONE MAJORITY YA HAO WASOMI NI HAOHAO WANACCM NA VIONGOZI WAO. WATU TUMEWAVUMILIA VYA KUTOSHA KWA MAONI YENU YA KIZUSHI NA CHUKI BINAFSI KWA WANACCM, SASA KARIBUNI KWENYE UWANJA WA MAPAMBANO WA HUU MDAHALO WA UANZSHWAJI WA MATAWI YA CCM NJE YA NCHI - PLEASE BE MY GUEST, BUT I WARNED YOU THAT, DON'T THROW TOYS OUT OF THE PRAM.

    3.UNAPOTOSHA JAMII KUWA WANACCM (UK) WAMEPEWA DOLA ELFU THEMANINI($80,000)KUTOKA WAPI? JE UNA USHAHIDI WA KUTUMWA HIZO FEDHA? JAMANI ANGALIENI SANA, SISI WANACHAMA WA CCM LONDON UK HATUNA TAARIFA RASMI, HIVYO AS FAR AS WE KNOW THERE IS NOT SUCH A THING,ANGALIENI SANA MTAKUJA KUFUNGWA JELA KWA KUWAZUSHIA MAJAMBO YA UONGO WANA JAMII. TOA USHAHIDI WA HIZO FEDHA ZILITUMWA LINI NA NANI?

    4.PIA NAPENDA KUWAPONGEZA WATANZANIA WOTE HUKU UGHAIBUNI KWA KAZI KUBWA WANAYOIFANYA KATIKA KUINUA UCHUMI WA TAIFA LETU, WANATUMA FEDHA ZA KIGENI TANZANIA KWA AJILI NA MIRADI MIDOGOMIDOGO NA MIKUBWA NA PIA KUSAIDIA FAMILIA ZAO, HATA KAMA WANABEBA BOX AMA WANAFANYA KAZI ZA CARE LAKINI WAMEJENGA KWAO TANZANIA KWA JASHO LAO (ULIZA HAO WABEBA BOX AMA MACARER WANALIPWA £££££ NGAPI KWA MWEZI/MWAKA - HALAFU UIBADILISHE KWA HELA YA MADAFU TSHS), NA SIO NYINYI MNAOPATA FEDHA ZA HARAKA HARAKA ZA KIFISADI NA UTAPELI, WIZI MTUPUU!!!TUNAKUJA HUKO TANZANIA HALAFU TUONE KAMA MTAENDELEA NA WIZI WENU HUO

    5. KAZI SASA NI MOJA TU, TUTARUDI TANZANIA KWA NGUVU KUBWA NA KUWANG'OA NYINYI AMBAO MNAFANYA MAMBO YA KIFISADI NA KUIPOTOSHA JAMII KUHUSU SISI WANACCM UGHAIBUNI, TUNAJUA NA KUELEWA SASA ROHO ZENU ZINA WASIWASI KWA KUWA HAMJUI NI NINI KINAFANYIKA NA KITAFANYIKA, TIME WILL TELL!!!!

    6.ETI UNASEMA WEKENI HOJA HII KWENYE MAGAZETI YA UDAKU!!!! HII INAONYESHA MLIVYO KUWA MAPUNGUWANI WA AKILI KATIKA KUIPOTOSHA JAMII, NA ITAKUWA ZE NINI!! TENA SITAKI KUSEMA HILO NENO.

    7. WANADIASPORA TUTAJIANDIKISHA NA KUJA KWENYE MKUTANO HUO WA MWEZI WA DECEMBER, TANGAZO TUMELIPATA VIZURI.
    MDAU - CCM UK

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 11, 2009

    Hakuna chama kilichokatazwa kufungua matawi nje ya nchi, sema wanachama wa vyama hivyo hawana mapenzi na vyama vyao ni wanachama wa midomoni tu. Hata hapo Tanzania yenyewe hivyo vyama vingine havina matawi ya kutosha, mbona hamsemi hilo?

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 12, 2009

    Ni kweli kabisa mimi naunga mkono anon hapo juu kuhusu waosha vinywa wanaokashifu CCM na Viongozi wa CCM huku ughaibuni. Hivi mna data kamili za mnaowakashifu au mnalalama tu?? Kuweni waangalifu mnapotoa maoni yasiyo na ukweli ndani yake. Watanzania wote tunataka maendeleo ya nchi including wana CCM. Hakuna mwana CCM huku ughaibuni anaesherehekea matatizo ndani ya CCM Tanzania. Tena infact hao ndo wa kwanza kutafuta solutions ili kuboresha CCM na Uchumi wa Tanzania kwa ujumla.

    Kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wakilalamika kwamba vijana hawahusishwi kisiasa, sasa uwanja ndo huu, bado mnatukana. Sasa sijui wasiyokuwa na elimu ni wakina nani. Kama CCM huku UK ingekuwa haina maana wasingeendelea kufungua mashina kila kukicha, inaonesha jinsi maneno yenu yasivyoweza kuvunja mfupa, maana hayana ukweli ndani yake.

    Na pia naomba ufafanuzi wa huyu Dada mnaemuita Susan Lyimo-Mzee. Mnamuongelea katibu wa CCM Uingereza ama mtu mwingine. Inabidi muwe waangalifu na mfanye utafiti wa kutosha kabla ya kuongea mambo yaliyo vague with no truth in it whatsoever. hebu huyo aliyezusha hapa alete hizo data zake tuone..

    Nachotaka kusema tu ni kwamba hakuna mtu anaekuzuia kujiunga na Chama au kutokujiunga na Chama chochote hata cha walevi. Ushauri wa bure, kama mnataka hizo changes mnazoziongelea, kwa nini hamuanzishi mfano?? Then others will follow.
    Kwa sababu kila siku naona ooh hamjasoma, mara kazi nzuri hamna, wewe kazi yako ni nini?? Lete profile yako hapa, na sitashangaa ni majobless, maana unaonekana una muda mrefu sana wa kuingia kwenye mablog na kutukana watu bila sababu.

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 12, 2009

    Mimi kwa ushauri wangu mnapokuwa nje jengeni udugu wa kitaifa, sio sera za kubaguana baguana. Chama kiwe mioyoni mwenu, lakini sera zenu ziwe za kusaidia taifa.
    Taifa letu linahitaji misaada yenu,sio kupitia kwa vyama, tunataka misaada ya kitaifa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...