Mimi ni Mtanzani, sitaki kusema nimeukana utanzania kwa kuwa ninatumia pasi ya kusafiria ya Taifa lingine; hii ni kwa matatizo tu.
sasa swali langu ni kwamba iwapo itatokea bahati mbaya nikafa je jamaa zangu hapa ughaibuni wataruhusiwa kuigiza maiti yangu Tanzania kwa kutumia pasi ya Taifa lingine? kwa sababu pasi ya Tanzania ninayo je wanaweza wakaitumia hiyo kuonyesha uhamiaji hapo Dar Airport?
swali hili ni muhimu sana sababu kuna watu wengi sana wamechukua uraia wa mataifa mengine kwa sababu binafsi na wanakuja kuona wazazi wao kwa kupata viza huku hali ni watanzania na ndugu zao wote wapo hapo Tanzania.
Asante mdau.
ughaibuni
jina kapuni
Ndio unaweza ingizwa Bongo kwa Pasi ya Nchi nyingine. Hakuna shida. Watu wengi wamekufa wa mataifa mengine (ulaya, amerika n.k) na wamekujazikwa Bongo. Toa hofu hilo ni swala dogo sana
ReplyDeleteDuh! we mnafiki kweli...yaani utanzania umeukana kwa sababu ya maslahi binafsi,yaani huo utanzania umeutupa uchochoroni ili ujunufaishe na hivyo vijisenti vya nje...na kweli nyie wabeba maboksi utumwa mpaka kiama!!!
ReplyDeleteMwili wako (yetu)Itakuwa kilutubisho cha udongo,Kwaiyo inakua faida kwa nchi.
ReplyDeletemaiti inachukuliwa kama cargo kwenye ndege.cargo haina uraia. hakuna tabu kufa tutakuzika.
ReplyDeletemdau kisiju
Mambo ya KUZIKANA yamepitwa na wakati. KUCHOMWA MOTO ndiyo njia sahihi na ya gharama nafuu kwa walio nje ya nchi(Developed Countries only)
ReplyDeletePesa zinazopotea KUSAFIRISHA miili ya marehemu ingetumika kusaidia JAMAA ZA MAREHEMU kujikimu na maisha magumu.
Pia ni SULUHISHO la Hodi Hodi za kila kukicha kuombana ombana MICHANGO ya MAZISHI.
Kwani KIFO ni jambo la kawaida tu, na mbaya zaidi sisi Waafrika tunakufa sana kwa wingi mara moja, hivyo hii CHANGIA CHANGIA ya kila siku ni kupoteza tu HAZINA zetu ndogo tulizonazo.
Najua ni VIGUMU kwa wengi KUELEWA mantiki iliyopo, but MKITAFAKARI vema mtagundua UMUHIMU wa hili swala.
Hawa Wakenya wameishiwa ardhi ya kuzika wafu wao sasa wanataka kuja kujaza ardhi adimu ya makaburi ya Tanzania kwa utapeli wa kwamba walikua raia wa TZ kabla hawajafa.
ReplyDeleteHatutaki unyang'au.
Kama Tanzania haikuwa nzuri wakati wa uhai wako kiasi cha kuikana kwa kiapo hadharani badala ya kuijenga kama Waghaibuni walivyojenga ya kwao basi fia, chomwa moto, zikwa, sahaulika huko huko ulikochagua kuishi. Msikimbie mkiwa na uhai baadae mtuletee maiti. Wafu hawajengi nchi.
Yap, kama unafikiria kufa na kuzwikwa TZ ni wewe mwenyewe tu unapotaka uzikwe pale utakapofia. Kama unataka zikwa TZ, na umefia ugaibuni basi utasafirishwa na kuzwikwa TZ , hakuna mjadala.
ReplyDeleteMaana utazikwa kutokana na familia yako kuwa WATZ , yaani baba au Mama, au Watoto. Pia utazikwa kama raia wa awali wa TZ, kama sehemu uliyozaliwa bila kujali uraia wako wa sasa na hata kama TZ itakuwa haina Dual Citizenship kwa wakati huo.
Pili kama ulifariki kwa mfano UK na wewe ni MTZ na ukataka uzikwe UK na UK sio nchi yako kwa Pasi, uraia au kwa kuzaliwa, na unataka kuzwika UK utazikwa tu UK.
Chaguo lako baba, ila huwezi fia TZ halafu ukataka uzikwe UK wakati wewe hauko UK, au huko UK sio raia na wala hukufariki huko UK , basi huwezi pelekwa UK kuzikwa.
Kuhusu issue yako Usiwe na wasiwasi utazikwa unapotaka tu, kama:
A) Ndipo ulipofarikia e,g UK
B) TZ , kam aunataka kuzwika hata kama kwa wakati huo sio raia, lakini familia yako iko hapa TZ
Nimeambiwa ubalozini kwetu kwamba hata ukiwa na pasi ya Tanzania ya zamani na iliokwisha muda wake, unaweza kuingia nayo Tanzania. Jamaa zako waonyeshe tu pasi yako ya zamani wakisafirisha maiti ....kama hujaichana.
ReplyDeletewewe wasiwasi wako nini, si utakuwa umeshakufa?. acha watakaobaki watajua nini cha kufanya. Dongo halikatai mtu bwana
ReplyDeleteSio Mara zote unaweza ingia Bongo. Ni vizuri wasomaji wajue kuwa Tanzania haina utaratibu wa zaidi ya uraia mmoja. Kuna watu wanafabadili uraia wakijua kuwa watarudi TZ sometimes kwa hushikilia pasi zao. Ila nchi nyingi huijulisha Tanzania mara tu watu hao wanapoukana uraia wao na hivyo kuondolewa katika rekodi za Raia wa Tanzania. Kama Serikali ikiwa imeshapata taarifa za namna hiyo basi mhusika si raia wa nchi hii na ni vigumu mwili wake kuingizwa. Ni vizuri watanzania waishio ughaibuni wakawa makini na taratibu hizi na waombe ushauri mara katika mamlaka husika za nchi zao au walizozikana. Inaonekana ni easy ila hakuna free lunch.
ReplyDeleteWahusika wa Idara ya Uhamiaji na Wizara ya Mambo ya Nje wanaweza tusaidia kwa hili. Tafadhali Michuzi tupatie ufafanuzi.
ReplyDeleteWEWE UNAJALI NINI KAMA UMEKUFA HAYO MENGINE HAYAKUHUSU.UZIKWE BONGO AU HUKO ULIKO YOTE SAWA.UNATAKA KUTULETEA MAMBO YA KUABUDU MAKABULI SASA.
ReplyDeleteNdugu sijui unawasiwasi gani. Biblia katika Mhubiri inasema.."Kwamaana walio hai wanajua kuwa watakufa, lakini wafu, hawajui neno lolote." Sasa kama utakuwa hujui neno lolote unapozikwa panakuwangisha kichwa kwanini? Nafikiri ni afadhali uhofu kuwa hutaruhusiwa kuingia na passpoti ya nchi nyingine ukiwa hai..lakini ukiwa maiti...who cares...!! Mdau-USA
ReplyDeletekwa kuwa bongo hatuna sheria ya kuruhusu mtu kuwa na pasi zaidi ya moja, basi hii ina maana kuwa tayari we sio mbongo, hivo pasi yako ya bongo ni batili. kama unaletwa au unakuja, inakubidi ulipie visa pale airport, nadhani ni dola 100 kwa miezi 3.
ReplyDeletenina wasiwasi kwamba jibu hilo hapo juu ni sahihi.Kwani hadi ukapewa pasi ya nchi nyingine lazima uliukana Utanzania wako maana Tanzania hatujawa na sheria inayoruhusu Dual citizenship.Hivyo wewe si mtanzania japo uwa ni mzaliwa wa Tanzania,kama sheria ikishika mkondo wake unaweza usiruhusiwe na hasa inatakiwa usiruhusiwe kuingia Tanzania bila visa.Sijui nchi unayo ishi lakini najua kwa walio Marekani kabla maiti haijasafilishwa kipo kibali toka ubalozini ambacho watu wa funeral home watakidai,na hata baadhi ya mashirika ya ndege yanaweza kukataa kusafirisha mwili wako kwa kuhofia uhamiaji/customs kutoruhusu mwili uingie nchi.Hivyo endelea kufanyia kazi swala hili anoy hapo juu amejibu harakaharaka kwani wakati mwingine bongo mambo yanafanyika kienyeji.
ReplyDeleteVery good question:- Ila mimi naona watu mkichukua uraia wa nchi nyingine msikane uraia wa nchi zenu jamani-chukueni kinachoitwa "dual au multiple" citizen yaani ina maana unakuwa na uraia wa nchi yako na bado unauraia wa nchi nyingine mfano, amerika, canada, italy au uturuki nk... nchi nyingi sikuhizi zina ruhusu hilo sema kuipata hiyo inabidi ulipie hela zaidi kidogo nadhani-kila nchi ina vipengele vyake vya sheria inabidii muulizie sio tu unakuwa bendera fuata upepo...asanteni, ni wazo tu nimetoa wadau..thanks a lot.. :-0
ReplyDeletekama wamezikwa bongo wakiwa wanatumia passport nyingine,wanafaa walipe ushuru aisei! kwani iweje raia wa nchi nyingie azikwe bongo? jiulize kwanza,ni kitu gani kinachokufanya uwe na uhuru kwenye nchi yako? yaani kitambulisho cha kusema wewe ni mtanganyika? sasa iweje uwe na uraia wa korea uje uzikwe bongo? ni ufisadi fulani hapo unafanywa,kuna harufu ya wizi !! kwa hakika napinga, tuombe mungu hii kitu ya uraia mbili iruhusiwe ndio tutakuelewa.la sivyo hukawii kusikia maiti imekosewa baada ya kupelekwa thailand ikaletwa bongo.mara usikie Taiga wudi amezikwa bongo kosa alienda kutafuta huko pakistani.nahisi unapata ujumbe!kwa hakika ,WEWE HAPO SI MTANGANYIKA kwa kuhodhi passport ya taifa jingine,ingawa ni katika kutafuta mkuu.
ReplyDeleteAkihito
mtwara
Unaweza tumia pasi yoyote ila muhimu mwili wako unafikishwa nchini kwa lengo la mazishi na ndugu na jamaa zako wataufata airport. Huu ni uzuri wa nchi yetu Tanzania hatuna ubaguzi na kwenye kifo hatubagui. Kama lengo lako kuziwa Tanzania basi wajuulishe ndugu zako mapema. Usiwe na shaka kabisa.
ReplyDeleteMtu wetu umepatikana na ngoma nini mbona umeanza kuulizia eti kama maiti yake inawezwa kurudishwa kwa kutumia pasi ya nje .
ReplyDeletemdau USA 1
Bongo si umeshapakataa. unataka kuja kuzikwa bongo tena kwa nini? acha unafiki.
ReplyDeleteKAMA ITAFUATWA MWILI WAKO HAUTARUHUSIWA KUKANYAGA ARDHI YA TZ, LAKINI KWA UKARIMU NA MOYOWA UPENDO ULIYOCHANGANYIKA NA UVUNJAJI WA SHERIA NA HASA BAADA YA KUPNEKANA BAADHI YA NDUGU ZAKO MACHO YAMEWAIVA YAANI YAMEKUWA MEKUNDU KWA KILIO BILA KUSAHAU MAAFISA WETU WA UHAMIAJI WANAVYOPENDA RUSHWA, UTAZIKWA BONGO BILA TATIZO LOLOTE, MUNGU TUSAIDIE TUPOWENGI SANA HUKU. MDAU-MAJUTO
ReplyDeleteUSIJALI UTAZIKWA POPOTE NDUGU ZAKO WATAKAPOONA PANAFAA. MBONA AMIR JAMAL ALIYEKUWA BALOZI WA TZ HUKO USWISS ALIPOKUFA ALIZIKWA CANADA (NB: ALIKUWA NA URAIA WA NCHI MBILI ILA ALIMFICHA NYERERE)
ReplyDeleteDu wadau
ReplyDeletehaya ndiyo mambo ya msingi ambayo Dr. Shayo alikuwa na kigugumizi cha kuyaeleza pale alipopata nafasi ya kuongea na wanajamii hapo majuzi.
Kama nilimwelewa vizuri alitoa mfano wa mtu kushitakiwa, lakini akaeleza kuwa kuna haja ya kuangalia mambo ya msingi alipoulizwa suala la uraia wa nchi mbili.
Sijui ni lini tutakubali mawazo ya hawa vijana wetu , lakini mnaweza kuona ni busara gani hawa vinaja walizonazo.
Sasa endapo umeamua kuchukua "uraia wa nchi nyingine" kwa shida zako binafsi inamaana kuwa utanzania umeukana. Sasa iweje ukipata tatizo taifa likusaidie?
Jamani, tuwe makini na hatua za kimaisha tunazochukua kwa sababu zetu wenyewe. Kaa , fikiri kabla ya kuamua.
Naombeni e mail ya dr shayo, kama mnayo ili nimuombe atufafanulie hayo mambo ya msingi ambayo tutaweza kuyajua na kuwa na manufaa kwa wana jamii hasa sis tuliko ugaibuni.
KWANI HIYO PASI YAKO YA NJE IMEANDIKWA UMEZALIWA WAPI?naadhani hili jibu lako limejibiwa
ReplyDeleteMtu anauliza swala, mijitu inauliza kwa nini ana uraia wa nchi mbili. Haihusiki na swala lake.
ReplyDeleteKwanza wanaosema kuwa mwili unasafirishwa kama mzigo bila ya kuonyesha kitu si kweli. Lazima uwe na dokumenti iliyotoka polisi na iliyothibitishwa na hospitali kuwa marehemu hajauawa na sababu ya kifo (death certificate). Alipofariki mzazi, agenti wa kusafisha maiti na kuitayarisha sandukuni ndio anayefanya hio kazi kwa malipo. Malipo haya ni pamoja na usafiri.Ajenti ana ofisi na contact yake hospitalini. Nikaletewa dokumenti zote hotelini na mihuri kamili ya polisi na hospitali. Nilivyofika kiwanja cha ngede, mwili ulishapelekwa zamani na ajenti na kuweka katika friji ya ndege. Nikapelekwa kuhakikisha kuwa ndio mwili wa marehemu ikiwa bado frijini mpaka nyumbani.
Mimi pia nina pasi mbili. Japokuwa sio halali Tanzania, hakuna aliyenisimamisha nilipoomba viza ubalozi wetu wala nilipoingia Tanzania japokuwa inaonyesha nimezaliwa Tanzania. Marehemu pia lazima awe na pasi na kama anaingia na pasi ya nchi nyingine, lazima ndugu zake waonyeshe serikali kuwa wao ni Watanzania na ni ngugu wa karibu kama watoto au mke wa marehemu au ngugu wa tumbo moja. La sivyo, itakuwa kasheshe kuitoa mwili huo. Kama marehemu ana pasi ya Tanzania na hajaichana hata kama imekwisha muda, pasi inatumika kuingia nchini. Kama hana pasi, basi ngugu lazima wajitokeze na kuonyesha kuwa marehemu ni ndugu yao kwa damu na kuwa na vithibitisho kama pasi zao au vitambulisho vinavyojulikana.
Binafsi, nimeamuru kuchomwa na kuzikwa nje kwa kuwa mke na watoto wangu wanataka nizikwe kwao. Sioni faida ya kupeleka mwili nyumbani.
Maswala ya pasi mbili yanazungumziwa bungeni. Sidhani itapingwa kwa kuwa Uganda wamesharuhusu na si muda Tanzania wataruhusu. EAC huwa ina sheria moja au wanategemea kuwa na sheria moja katika hii jumuia. Sioni kuna faida yoyote ya kupinga. Watu wanaongelea usalama wa nchi uko hatarini kama vile Tanzania ni nchi tajiri na yenye mali sana duniani. Kuna nchi tajiri mara mia kuliko Tanzania duniani na wamewaruhusu hata maraisi wao kuchukua madaraka japokuwa wana pasi mbili. Pia, Wazawa wengi kama mimi tuna pasi mbili tunaishi nje na tunaishi Tanzania, hii sheria kamwe haituingilii wala kutuhangaisha katika maisha yetu. Nadhani tu wale wanaopinga pasi mbili ni wenye roho za korosho na wasio na macho ya kuona mbele.
Anony wa hapo juu acha ushashi usio na maana. Kama una uhakika hao jamaa wala rushwa kwanini usiwapeleke mahakamani au toa taarifa sehem husika.Uliwahi kutoa rushwa kwao au kuna mtu unamjua katoa rushwa?
ReplyDeleteAnaetoa na anaepokea rushwa wote wana makosa. Kama tutazingatia vyema ukweli huu rushwa haitakuwepo.
Swali la mdau anaeweza kulitolea majibu ni mamlaka zinazohusika kama wadau walivyochangia. Nenda ubalozini au Uhamiaji au Mambo ya nje watakupa maelezo ya kina. Vinginevyo mithupu afuatilie amwage ze dataz hapa. Wachangiaji wengine wavivu kufuatilia ukweli wanaharibu mada kwa kuleta visingizio vya rushwa.
naona wadau mnachanganya mambo. unapochukua uraia wa nchi nyingine-sio kweli unaukana utanzania bali unaapa kuwa utakuwa raia wa hiyo nchi. Hakuna kiapo kinachosema kuwa "kuanzia leo mie sio mbongo".
ReplyDeleteMambo ya kufa sidhani kama ni issue, labda ungeulizia maswala ya viwanja na faida nyingine za raia akiwa hai sio aliyekufa.
Ni vipi je kama amejilipua (amejifanya mkimbizi) na anaishi kwa pasi ya nchi iliyompa ukimbizi (mfano; amesema yeye ni m-Rwanda na amepewa uraia wa Holland) bado ataweza zikwa TZ? hapa naona patakuwa kazi kweli kweli, maana wapo wengi waishio kwa mtindo huu.
ReplyDeleteMdau
Tunabishana Jinsi ya Kupeleka maiti tanzania, kwanini tusibishane jinsi ya kupeleka computer na mitambo ya Umeme Tanzania. Kweli Wabongo tambarare.
ReplyDeleteUtamaduni wa kubishana tumejaliwa!!!
Unachofanya huko uliko sisi hakitusaidii chochote, upelekwe bongo usipelekwe taifa halina cha kupoteza ila, ukifika huko Uliko ukashindwa kuangalia uliko toka tumekupoteza.
Fikiria jinsi gani familia yako wataishi ukifa mambo kama life insurance lakini utakako zikwa sio shida yako, na wala haina haja ya kuuliza. Urudi bongo usirudi sisi itatusaidia nini, lakini ukiacha watoto hawana maisha sisi umetuachia mzigo mzito na tunalia si kwasabu ya Uchungu bali kwasababu ya ukali wa maisha uliotuachia
Hebu nyanyueni vichwa wabongo acheni kuangalia miguuni tuangalie mbele
Mdau
Duu!Comments zote nimezisoma,mimi binafsi nina passport ya nje, kama nikifa heri nizikwe hapa hapa nilipo ULAYA ninapoishi manake naamini 'MTU AKIFA BAADAE LAZIMA ATAFUFUKA'na sasa kama nikifa leo hii kisha nikazikwe BONGO ukifika wakati wa kufufuka si ajabu nitakuwa sina kitu nimechacha,haya 'ULAYA'nitarudi vp miye?wee acha tuu,nakushauri kama utapenda bora uzikwe hapo hapo ulipo ili upunguze gharama kwa ndugu na jamaa zako manake maisha ni magumu na yana zidi kuwa magumu.ukiangalia familia yako yote wanakutegemea wewe!Its not a jocke jamani.
ReplyDeleteTATIZO TANZANIA BADO HAINA DUAL CITIZENSHIP yaani uraia wa nchi mbili au zaidi. hembu nyie wadau niambieni, ukipewa uraia wa nchi lets say Marekani utaukataa eti kisa unataka ku-keep uraia wa bongo? it is true mtu utajivunia uraia wa nchi yako, pamoja ma mafisadi wake. lakini when maslahi is concerned, itabidi tu nibane majuu. after all Visa ya Bongo kuipata ni rahisi kuliko ya majuu...
ReplyDeletesasa wewe mdau ukidedi, unaweza kuzikwa anywhere. lakini kama mdau hapo juu alivyosema kumbuka kuna kufufuka hapo baadaye kama sisimizi au ndege au kobe etc. imagine unafufuka kama kobe halafu unajikuta bongo kwenye matope na vinyesi, si afazali ufufuke mahali ambako watakuweka kwa zoo na matunzo mazuri na nini na nini. wabongo mlioko majuu inabidi muanze kununua life insurance inasaidia kupunguza michango, halafu hata jeneza la kukusafirisha litakuwa bab kubwa.
BWANA MDOGO RUDI BONGO KABLA HUJAFA, ARDHI YA KUZIKIA TELE, NA KUNA MAPAPA NA MANYANGUMI HAPA
ReplyDeleteNdugu mtarajia kufa, wewe kufa tu, hakuna dili yeyote kuzikwa bongo au ughaibuni. People will take care of you. Bali, uwaachie posho kidogo kabla hujatema kete
ReplyDeleteKwani unampango wa kufa lini? Eeeh kweli wadau wa humu wa issue.
ReplyDelete