Habari kaka Michuzi.
Ninaomba uniwekee tangazo langu katika globu yetu ya jamii. Nauza Ultra sound machine kutoka Germany. Ni mpya. Nimekutumia na picha nilizozipiga baada ya kuiunganisha.
Bei ni $3600 ila kuna makubaliano.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kwa simu namba
0655123000
Mdau
Birungi
Sinza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2009

    si uitumie mwenyewe??? yani kwa kuangalia picha tu inaonyesha ni bomu!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 28, 2009

    Wadau mnaojua hii ngoma niknunua niiweke geto,nitapigiaje dili(Itanisaidia vipi)?Hii huyu jamaa anawalenga wadau wa mahosipitali?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 28, 2009

    Hiyo ngoma ni NEW lakini imetengenezwa EAST GERMAN, miaka mitano kabla ukuta wa Berlin haujavunjwa, pamoja na upya wake hata huku TZ vijijini hicho kifaa ni obsolete!

    ReplyDelete
  4. Kaka TrioMay 28, 2009

    Hizo ni medical equipments zikoo regulated na sio vitu vya kuuza mitaani kama pipi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 28, 2009

    Nzuri kwa kujichekia afya yako, hasa sehemu za ndani ya tumbo kama utakuwa umekula kupita kiasi au umevimbiwa itasaidia kuona ndani ya tumbo kunani?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 28, 2009

    Kaka Michuzi hebu naomba uongee na huyu Mdau na Wengineo wote wanataka kuthubutu kuuza vifaa vya hospitali wakati Nchi yetu yenyewe Maskini watu wanakufa mahospitali ya Taifa kwa kukosa vifaa kama hiyo Ultra Sound. Najua Bongo kuna Njaa lakini jamani saa zingine tuwe na moyo wa kutoa kwani kutoa ni moyo usanmbe si utajiri, wewe kam Ulikuwa unaitumia hii Ultra Sound yako kwenye ka-private hospil kako kumbuka Kwamba Hospitali zetu za Rufaa mbali na Urasimu uliokithiri zina umaskini sana wa vifaa na hivyo watu wa hali ya chini wanazitegemea wanakosa matibabu amabayo ni ya haki yao kama binadamu wengine. Kwa hiyo Mimi ushauri wangu ni kwamba ni kwamba muombe kaka Michuzi na Kamera yake Mfuatane Mpaka Mwananyamala ama Ilala ama Hospitali ya Temeke tuanie tuu hapo mjini Ukaitoe Hiyo Ultra Sound Bure Akupige kapicha ukikabidhi Maabara ya Hospitali , utolewe humu watu tukupe sifa na shukurani. Na la msingi ni kwamba Mungu atakujaalia zaidi ukitoa sadaka na utapata zaidi ya hiyo dola yako 3600. Na mwamnza nilijumuisha na wote wale watakaoiga hii tabia ya kuuza vifaa vya hospitali humu bloguni kwetu mana wabongo kwa geza geza nambari wani hivi kaanza mmoja basi ndio mtafanya trend kama kawa so kaka Michuzi please usiwape nafasi hebu mfikirie mara mbili ndugu zenu na jirani zenu wanakufa kwa kukosa vifaa hospitali jamani Wabongo lazima tuwe na moyo wa kujitolea na tuache ubinafsi ndio mana hatuendelei mana kila mtu ni kwa nafsi yake na ya mtu wake what about the rest of them ? NARUDIA NAOMBA MTU ASINUNUE HIYO MASHINE NA ATAKAE NUNUA AIPELEKE HOSPITALI ZA WILAYA AU MUHIMBILI MANA BORA IFIKE HUKO MUHIMBILI NA NESI NA DOCTA FULANI WAFANYE NA WAO NDIO DILI LAO HUPIMWI BILA YA KUTOA KIDOGO DOGO BUT ILI MRADI ITAKUWEPO ! wasalam nimesema sana kwa jazba mnisamehe wadau.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 28, 2009

    hiyo ni model za zamani inaonekana tu kwa jinsi ilivyo, je unaweza weka jina na model tui search tuone na details zaidi? kwanza wewe upo nayo ya nini na kwa nini unaiuza, sema basi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2009

    BIRUGI SIJUI BURUGA KAMA UNAVYOJIITA HICHO KIFAA NI MUHIMU SANA NYUMBANI KWAKO. DAKTARI HAKUDANGANYI TENA MKEO ANA MIMBA YA MTOTO GANI USIIUZE BADILI MAWAZO MTANI MALI HIYO NI DOMESTIC UZEFUL VERY MUCH NEEDED teeh teh teh

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 28, 2009

    umeichapa wapi ten wewe?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2009

    mashine nzuri sana nimependa zaidi hiyo fingerprint reader hapo haibi mtu, hujasema kama inaplay DVD, hard drive, ram kiasi gani?inatumia operating system gani? na hiyo keyboard inaonekana imechoka

    ReplyDelete
  11. BIBI UMEMEMay 28, 2009

    jamani watu wana vituko, mbona comments not helpful to mdau ? si umtanie pia umsaidie ? mdau please try to also advertise through to private hospitals, many lives would have been saved if only people n especially doctors go a step further and do an ultra scan; my colleague nearly died of a burst appendicitis just coz they never did an ultra scan, n when they did, couldnt make out what was within him because itd already bursted so it was a calculated guess, but for 8 months he was complaining of the same, he was pronounces dead on the operating table but managed somehow thru God's will to survive that
    ; so many private hospitals dont own one, i wouldnt mind being checked with this one hata kama ni ya before christ au after wwII cha msingi ni afya in absence of those industry best practice ambazo mnaona ni better than hii, hospitali nyingi za mikoani na baadhi za dar zinakupa referral kwenda 'hospitali kubwa' kufanyiwa ultra sound.
    ila naomba nimalizie na swali la kizushi, why on earth did you buy this?? unless you were into a frenzy of collecting medical equipment...somehow..

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 29, 2009

    Mmiliki ikiwa umeammua kuitangaza biashara humu kwenye blog ungeweka details kiasi fulani za umiliki wa hii mashine ili tangazo lijitosheleze kiasi, kabla ya atakaehitaji kufahamu zaidi hajakupigia simu i.e labda wewe ni doctor na vitu kama hivyo. Maana sinauhakika kama mashine kama hii huwa zinamilikiwa na mtu binafsi kama kifaa cha nyumbani au lazima awe ni mtu mwenye hospitali/dispensary (inatia shaka kuipata toka kwa mtu binafsi kama hakuna maelezo ya ziada,sijui huko kwa wenzetu). Hata hivyo ni muhimu kama itapata mteja hospitali sehemu yoyote itasaidia maisha ya wengi maana sehemu za kupata huduma hio muhimu ni chache.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 29, 2009

    Michuzi naomba hawa watu wanatangaza biashara bila kuweka details za muhimu waweke kapuni. Ni aina gani hii machine? Kuna vifaa vyote, guidelines za kutumia, kwanini anaiuza au ni mfanya biashara. Na kwa nini anauza kwa dola, acha kudharau shilingi yetu. Unaweza hata kubadilisha kuwa Tshs tukajua bei. Halafu kama iko chumbani vile.

    Itakusaidia sana kama ungeweka email yako hapa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 29, 2009

    hii ngoma siyo hile iliyokwapuliwa Ocean Road Hosptal?????

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 30, 2009

    Je kifaa hiki muhimu kwa afya ya mgonjwa kina warranty ya miaka mingapi kwa mnunuzi. Pia after sale service itakuwepo? Kuna ma-engineer/technician wa kufanya service? vipuri vyaweza kuchongwa na idara ya uhandisi wa mitambo ya hospitali Tanzania?

    Mdau
    Kiparamoto DSM

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 01, 2009

    kwa taarifa tu

    kifaa chochote cha hospitali kitokacho ujeremani hakina spare parts bongo

    pili,vifaa vyote vya hospitali + madawa yana ONLY one auothorized supplier mf.......ningesema apa sema ni siri

    so wee michuzi mambo ya kukurupuka na kubandika matangazo nyeti km aya blogun ni tatizo

    sawa???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...