Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Wiliam Lukuvi (kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni Ishirini kutoka kwa Meneja wa Vodacom Foundations Yessaya Mwakifulefule ambazo zitatumika kusaidia wahanga wa milipuko ya mabomu iliyotekea katika ghala la kambi ya jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Mbagala hivi karibuni. Msaada huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka (kulia) ni Afisa Maafa wa Chama cha Msalaba mwekundu Vivioliva Shoo na Mratibu wa Uhusiano wa Vodacom Mwanamvua Mlangwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Wiliam Lukuvi (kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni Ishirini kutoka kwa Meneja wa Vodacom Foundations Yessaya Mwakifulefule ambazo zitatumika kusaidia wahanga wa milipuko ya mabomu iliyotekea katika ghala la kambi ya jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Mbagala hivi karibuni. Msaada huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana.  Wa pili kutoka (kulia) ni Afisa Maafa wa Chama cha Msalaba mwekundu Vivioliva Shoo na Mratibu wa Uhusiano wa Vodacom Mwanamvua Mlangwa.

VODACOM TANZANIA YATOA MILIONI 20 KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MABOMU MBAGALA

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kijamii wa Vodacom Foundation, umetoa msaada wa Milioni 20 ili kuboresha mahitimu ya wananchi waliopatwa na madhara ya kulipukiwa na mabomu Mbagala jijini. 

Akikabidhi msaada huo leo mjini hapa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam William Lukuvi, Meneja wa Mfuko huo Yessaya Mwakifulefule alisema kwamba msaada huo umetolewa kwasababu Vodacom wamegushwa na kusikitishwa sana kama Kampuni wakaona ni bora wachangie kidogo ili watu wasije kupata matatizo mengine zaidi ya haya yaliyotokea, Kama vile njaa au kipindupindu.

Alisema msaada huo una lenga kusaidia jamii nzima iliyopatwa na mkasa huo na kuisaidia serikali kama sekta binafsi siyo kuiachia serikali pekee kwenye janga kama hili lazima tuwe pamoja.  

    

Naye Mkuu wa Mkoa, akipokea msaada huo aliishukuru kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake huo. 

Alisema hivi sasa sera ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutoa misaada mbalimbali ya kuiokoa jamii kama Vodacom ni mfano wa kuigwa na mashirika mbalimbali ili waweze kuisaidia serikali na wananchi waliopatwa na janga hili kubwa.

“Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji ili kuhakikisha kwamba uwekezaji una kua na wawekezaji pia wanapata fursa ya kuchangia maendeleo ya sekta ya kijamii nchini’ 

Alisema makabidhiano hayo ni mfano hai kwamba sera ya kusaidia jamii serikali imefanikiwa kwani sekta binafsi hivi sasa imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Watanzania wengi wanapata haki sawa hata pale wanapopatwa na janga zito kama hili. 

    



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2009

    Aaaaaah aaaah shemeeejiiiiii. wapi nguri.

    naona misaada mingi tu, natumai itawafikia walengwa mazali imetua mikononi salama.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2009

    *Quality Group 30,000,000
    Mengi 25,000,000
    *Vodacom 20,000,000
    Mwanakijiji 0
    Mimi nina swali kwa mwanakijiji. Je, na hii misaada tususie au tususie makampuni yao huku hela tunachukua?
    Swali langu la pili ni kwa wadau wote. Kuna mbunge mmoja alisema hela wanazopewa ni nyingi kiasi wanakosa matuizi nazo, sasa mbona huyo mbunge hajachangia kitu mpaka sasa hivi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2009

    Nashukuru sana kuona na kusikia michango ikitolewa,,,swala linakuje je kweli itawafika walengwa kweli? au ndio usanii utatunia? hapo mimi simo! hofu yangu hizi tesa zitaundiwa kamati na siasa itachukua mkondo na badala yake zitawafikia wahusika muda na mahala ambapo hawaziitaji tena,,nawashauri wahusika fanyeni fasta kwani wahanga wanazihitaji hizo pesa kwa sasa jamani
    Mdau Singida

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2009

    bro misupu naomba nimjibu jamaa hapo juu,ni kwamba dr slaa anaropoka sana,na hajui anachofanya,anazidi kuingiza chadema shimoni,na ukichukulia alishinda karatu kwa pacent ndogo sana mpaka ukatokea utata hadi kwenda mahakamani,nadhani 2010 atakuwa kwenye wakati mgumu sana,ccm wataichukua karatu bila wasiwasi.namshauri arejee upadre tu,michu usibane ni maoni tuu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2009

    Slaa nini 2010 ? kuna watu hamko Tanzania lazima mpo Kiribasi au jirani yake

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2009

    Slaa nini 2010 ? kuna watu hamko Tanzania lazima mpo Kiribasi au jirani yake

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2009

    Mheshimiwa Lukuvi sijui una nguo nzuri au nguo zinakukaa vizuri,anaway!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2009

    mHESHIMIWA LUKUVI madamme wake ana boutique pale BEN MKAPA TOWERS kiasi avae vya kutosha halafu ana mnyororo shingoni! our leaders !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...