dk. liky abdallah, mchambuzi nguli wa mambo ya soka anaongea na globu ya jamii juu ya michuano ya confederation cup inayokaribia kufikia tamati huko sauzi. huu ni mwanzo tu wa chambuzi mbalimbali ambazo dk. likyamekubali kufanya katika kuendeleza libeneke

Angalizo: utabiri wa wengi kwamba spain wangeifunga marekani umeota mbawa.

Gemu limeisha sasa hivi na USA 2 na Spain 0!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2009

    hahahaha uwiiiiiiiii mzee anareta raha huyu anachonga hata maneno hayamuishi kusema kawekewe keyboard mdomoni. halohalo i miss bongo uswaziiii oyeeeeee

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2009

    bro michu huyu jamaa ni dr. wa nini?
    finali USA vs South Africa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2009

    Hata mimi nilitabiri kama Dr lakini kumbe sivyo. Haya kesho, Brazil na SA...Brazil anapita

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2009

    Michu,
    Hebu tutafutie Dr Licky tena maana mambo si mambo, Spain wamebwia 2 mtungi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2009

    Huyu jamaa kwa nini asingepewa kuwa mshauri mkuu wa FAT ili tufike World cup?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2009

    Naomba mtumie Dr Licky hili swali ili atoe ufafanuzi..
    kama nawe unaweza jibu jibu.

    Hivi ukiwa mtangazaji wa TV ,je una huru wa kutoa mawazo yako bila kuingiliwa?[freedom of speech]

    Nimeona huku kwa Madiba mtangazaji kasimamishwa kazi kwa kusema ukweli..lakini wenye chombo wamesema ndivyo sivyo ndivyo!
    http://www.sport24.co.za/Content/Soccer/266/fbb73b02eb614a8eb41984fb318246cd/24-06-2009%2008-06/SABC_sports_presenter_suspended

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2009

    Dr Licky amenifurahisha sana jinsi avayochambua soka na kuingiza hostoria. Anaonekana ni mtu makini na soka analijua vizuri sana.

    Michu inabdi uwe unamuhoji Dr. Ricky mara kwa mara.

    Tulio USA:
    Huu ni ushindi mkubwa sana! Kwa vile Tanzania haijaingia kwenye haya mashindano chama letu ni USA!

    Koleo
    Youth Soccer Coach
    Connecticut

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2009

    MICHUZI NAKUSHUKURU SANA. I ALWAYS MISSED DR. LICKY. NAKUMBUKA NIKIWA DSM UTAMU WA UCHAMBUZI WA SOKA LA KIMATAIFA, ILIKUWA UMSIKIE DR. LICK AKICHAMBUA WAKATI WA MAPUMZIKO YA MCHEZO. HUYU JAMAA NI BALAA. MAANA ANAJUA MCHEZO, ANAWAJUA WACHEZAJI, ANAJUA HISTORIA YA DUNIA. KWA UFUPI ANAJUA MAMBO MENGI SANA HUYU JAMAA. ALITAKIWA KUWA MSHAURI WA F.A.T.

    KWA UFUPI, ANAZIJUA TIMU ZA AFRIKA, WACHEZAJI WAKE, TIMU ZA DUNIA (MAARUFU) NA WACHEZAJI WAKE, NA HISTORIA ZAO MIAKA KAMA 100 KURUDI NYUMA. HUYU ANGEKUWA STATES, NI KAMA AKINA LARRY KING WA CNN.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2009

    Unajua zamani wakati nikiwa high school nilifikiri huyu jamaa anadanganya , ila nimemkubali . Jamaa anaijua historia ya dunia , na hiyo inamfanya awe na persepective kubwa kuhusu analysis yake ya mpira . Michuzi mtafute tena huyu jamaa umpe dakika kumi au hata ishirini, mtu uwezi kuchoka kumsikiliza .

    Vitu vingi alivyosema ni vya kweli tupu ...ila aliunderestimate the heart of the a champion. GO USA, and God bless the United States of America.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2009

    Dr.Licky long time sijakuona mchizi wangu naona unga unakuja kwa kasi, tangu kwenye luninga kipindi kile mkichambua soka na Michuzi naye akiwa anachomekea chomekea kwani utaalamu wake ni kwenye taswira tu.Napenda sana uchambuzi wako Michuzi mtafute huyu jamaa atuletee uchambuzi, tumechoka uchambuzi wa wazungu huku !!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2009

    Hana udk wowote ni wabongo kama kawaida yetu kupeana majina na hasa jina lake linafanana na mvumbuzi maalufu dk lick wa olduvai. ndipo wakaona na yeye ana chambua vizuri mambo ya michezo wakampa cheo cha dk.
    Hata hivyo anatufaa sana kwani ni mchambuzi mzuri wa mambo ya michezo na hasa mpira wa miguu.
    kama anaona inafaa basi siku moja achukue form agombee nafasi yoyote ya uongozi katika chama chetu cha mpira wa miguu hapa bongo.

    ReplyDelete
  12. Al MusomaJune 25, 2009

    A real football pundit in the middle of Bongoland. Research-minded, analytical and knowledgeable. What a talent. He went to school with my uncle at Uyui (who knows when) and how they now look generations apart!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 25, 2009

    SISIS WATANZANIA NI WALALAMISHI SANA, SASA NAOMBA WACHAMBUZI WA MASUALA YA MPIRA WANIELEZE KWANINI TANZANIA HAIKUCHANGAMKIA MGAO WAKE WA TIKETI ZA BURE TOKA FIFA HUKU WAKENYA WAKICHUKUA ZAO MAPEMA! JE, HII INATOKANA NA UFINYU WA KUFIKIRI AU UVIVU WA KUFIKIRI? TUSINGEKUWEMO KWENYE LISTI YA MGAO TUNGELALAMIKA SAAAAAANA MPAKA DUNIA YOTE INGESIKIA KUWA TUNACHUKIWA.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 25, 2009

    duhhh mzee unaongea sana lakini waswahili wanasema mpira unadunda yasikutishe majina baba halafu chengine mpira hauna history unaleta mambo ya simba na yanga

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 25, 2009

    huyu mzee anafaa kuwa kocha mkuu na julio akawa msaidizi wake

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 25, 2009

    Pamoja na kuwa ni mbeba maboski ughaibuni lakini sijapendezewa na ushindi wa jamaa dhidi ya Hispania. Wabongo tukiwafunga Burkina Faso ni mchakamchaka kila kona tukifurahia ushindi. Jamaa huku wameifunga timu namba moja duniani lakini wengi wao walikuwa hata hawajui kwamba timu yao ilikuwa inacheza. Noma kichizi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 25, 2009

    Licky Mtoto wa GOGO VIVU Kariakoo, nakujua sana na ninakumiss nikija bongo nitakutafuta, na sio siri katika wabongo wewe unapenda mpira na unajua histori ya mpira, achana na waosha vinywa.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 26, 2009

    dah mimi namkubali dk licky kwa uchambuzi lakini naona tu aliwahi kuchapia enzi zile alipotuambia robbie kean na roy kean ni brothers that was it lakini he is always right i do believe that na history za wachezaji wengi anazijua ila hiyo tu ilipita pembeni au labda ulimi ulitereza manake si unajuwa ulimi hauna mfupa? keep it up baba tunakukubali ila mmhh kaka dk licky umri sasa unakwenda manake naona kichwani utadhani ulibeba gunia la unga ukakumwagikia kidogo kichwani na kwenye ndevu hahaha just joke kaka

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 26, 2009

    Wadau hivi ni mimi pekeyangu ninayeumizwa kichwa na sauti za hayo ma-vuvuzela wakati ninapoangalia mpira?Ndugu zangu wa bondeni hawana namna nyingine ya kushangilia?Sina maana ya kudharau utamaduni wa ndugu zangu kwasababu naamini no culture is superior to onother(naomba msinishambulie)Hawa wandugu hawawezi kuyapuliza kwa utaratibu wa DO-LE-MI-FA-SO-LA-SI-DO ili yatoe muziki unaoeleweka?Ninajaribu kupunguza sauti ya TV lakini mpira haunogi bila kuuona na kusikia sauti ya mtangazaji.Wadau hii imekaaje?Je hivyo ndivyo hali itakavyokuwa mwakani wakati wa kombe la dunia?

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 26, 2009

    fujo fujo,,,hatufanani na wazungu na hatutaki tabia zao ni zao
    acha tucheze sindimba,mdundiko na kelele zooote!!

    afrika utamaduni bwana!!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 26, 2009

    Bro! Yaani kumsikiliza huyu jamaa ni burudani tosha. Mtafute tena tuburudike.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 26, 2009

    MAREKANI KWAO MPIRA WA MIGUU AWANA DEAL NAO KABISA,WE WAAMBIE WATUKANE NA KUVAA KATA K,NI KWELI TEAM YAO IMESHINDA LAKINI ATA AWAJUI NA WALA AWAKUANGALIA MPIRA NDIO MANA UWA NAWATIA MASINGI NIKIWA NAO!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 27, 2009

    Mzee misupu
    kwa kweli sisi walioko pembeni na afrika huwa tunakumbuka taalifa zamichezo mbali mbali natunahuzunika sana kutokuwa na kufuatilia uchambuzi wa michezo kwenye redio hasa zahuko kwetu,,,sasa tunaomba uwe unatafuta watu kama hao wanatukumbusha habali za michezo kidogo,,mdau wa South Kolea.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 29, 2009

    Dk Liky nakubari sana uchambuzi wake mara nyingi ila huu naona alichokosea nikuweka big team mbela kabla ya kucheck team zinavyo change game day by day kwenye confed cup!

    Mimi nilikuwa kwenye live kwenye uwanja siku ya match ya USA and Italy niona jinsi US ilivyo kuwa inacheza vizuri though walishindwa na walivyo funga egypt ilionyesha jinsi walivyo kosoa makosa katika team yao pia match za Italy zote in other side Bafana bafana unona ilivyo toka mbali nadhani Dk Liky umeliona kwenye match ya jana ambayo mimi pia nimeona kwenye tv pia. bado wana hitaji kulekebisha team yao ila at least sio vibaya kama kabla ya confed cup kuanza.

    Final nayo nimecheck live from ellis park it was wonderful game i think US must be proud of it nadhani hata watazamaji pia na brazil walikuwa hawaelewi kilichotokea wakati wa half time na though ni team kali kweli ila yote yana wezekana kwenye soka hata france 98 iliwafanyia ghafla wakakosa kombe...

    maoni angu kwa confed cup nikwamba kila team sasa inapaswa ikienda kuwakilisha kwenye mashindano wajiamini na kuweka bidii tu wasitishiwe na majina makubwa.

    I thank God sana kwa mara ya kwanza nimeweza kuhuzuria match hizo.

    Niliweza kucheck 5 matches.

    US vs Italy,Italy vs Egypt,Brazil vs Italy. semi-final ya South Africa vs brazil na Finals

    It was great experiance in life...

    Vuvuzela kama kawa tu.

    Nakumbuka wakati Mark Foe anakufa nilikuwa kwenye tv kwenye bar moja na sikuwa na idea that one day i can watch this biggest event in the world live.

    I hope that wadau you can keep dreaming and God one day can make dream to come true just believe in Him....

    Jozi,SA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...