familia zote zingekuwa hivi ingekuwa mswano.
wadau mnasemaje? tujadili mada hii ya ijumaa.
asante mdau kwa kushea nasi taswira hii maridhawa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 64 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    Oh yeah. Ila tatizo la siye waswahili bwana,sababu hatuna upendo na familia zetu basi hapo wangetokea wamenuna hao. Na watoto wangemkumbatia mama pekee. Na mama angekaa kama hatua moja mbali na baba.
    Viongozi wetu nao watoe picha na familia zao

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2009

    Umejuaje kama ni maridhawa? Kwa vile wanacheka hadharani ama?

    Well, labda kweli ni maridhawa, ila kuta za nyumba ndio pekee zinazojua ukweli wa hali na mahusiano ya dhati za familia.

    Ni wengi hutabasamu na kuonyesha upendo na furaha wakiwa nje, ila wakiwa pekeyao hali ni tofauti.

    Na hapa simaanishi familia ya obama, naongelea kwa ujumla tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2009

    Safi sana na yapendeza kupita kiasi, lakini kumbuka pia sote tuna mapenzi ya familia lakini umasikini siku nyingine watutia pingu.Baba kenda kubeba maboksi na mama kaamka alfajiri yuko kwenye shamba la mihogo michungu
    Mungu awabarik,awazidishie kila la kheri
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  4. Mkubwaa,asante sana kwa kutupa nafasi ya kusema chcochote kuhusu familia ya huyu muheshimiwa...la kwanza nalo weza kusema hii ni picha tu,mana watu wahuku ugaibuni wana kamtindo kakusema smile wakati unapiga picha kwahiyo isitutishe sana,naamini bibi yangu na babu yangu kule kijijini kwetu MSOWELO-MOROGORO wanafuraha zaidi kuliko hii familia,kingine tunacho hitaji kujua haya ni mambo ya protokali tu kama ya mzee wetu aliye toka madaraka na mke wake MKAPA,h ahha..unaweza ukakuta ndani kwenye maisha yakawaida ni ngumi mtindo mmoja..haya mkuu ni hayo tu kutoka hapa HELSINKI mji mtukufu...

    Mdau wa UFINI...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2009

    hiyo yote ni sababu ya shule na kumtambua mungu ndio maana familia imekuwa hivyo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2009

    WANA GENDER MPOOOO...Mdau MBIJE,A-Kafanabo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2009

    Familia nzuri,yenye furaha na inafaa kuigwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2009

    Ama kweli wamependeza, nami naenda kupiga nzuri kama hiyo au zaidi, Michuzi usinibanie kuiweka kwenye globu hii ili kuwathibitishia waungwana kuwa familia maridhawa si hiyo tu, kwani avumaye baharini ni papa lakini wengine pia wapo!

    ReplyDelete
  9. Lakini aliyesema "familia zote zingelikuwa hivi..." hakuweka wigo. Je anamaanisha, idadi ya wanafamilia, au wote kuwa Wakuu wa nchi, au kuwa na watoto wa kike, au kutabasamu, au kukumbatiana, au kujipanga kwa picha, au mavazi au nini? Tunaweza kusema chochote kuhusu hayo na mengine. Kuweka wigo kungeliichonga kwa mwelekeo michango yetu.
    Mimi naongelea sura. Wote wana sura nzuri na zinazoeleweka mbele ya umma.
    Mdau New Jersey

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2009

    mdau wa #2 umenena vyema ni kwa ujumla wake tu

    tabasamu nini bwana???mambo yako in ze hausi

    anyway,binti mkubwa kafanana na dad,binti mdogo kamlanda mamy

    aya

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2009

    nendeni zenu kuna familia kibao tu zinapendana,sio kila kitu wakina obama tu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2009

    Familia zote zingekuwa na watoto wa kike tu basi dunia ingekuwa inakaribia kufika mwisho, maana sijui wangezaana vipi tena!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2009

    watoto mbona warefu ivo??
    wamefika miaka 10 kweli??

    kula lifa kwa raha zenu ngozi nyeusi

    dhehebu gani nyie?mana sijawai sikia mwasali wapi au no dini kabisa

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2009

    MICHUZI HAWA WAMESHAPIGA BREAKFAST YA NGUVU, LUNGU KUNA MBOGA SABA KUJISEVIA ,WANADONOA KAMA KEYBOARD WAANZE NA MBOGA GANI , HAPO HIVYO VITOTO VIMETOKA KUPUP CHOO LAINIIIIII UNAFIKIRI HAKUNA KUCHEKA?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2009

    yan uyu michelle amekaa vibaya-vibaya,analipa kichiziiiiiiii
    dah katulia shepu la kibantu aswaaa

    jamaa kweli mu East Afrika shepu za kibantu tunazihusudu

    hello Mr presidenti,karibu Tanzania,majirani wajinyonge kwa udenda

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 05, 2009

    Kaka Michu kiukweli watu tusipende nyoosheana vidole,Maana Watanzania mtu nakana mimba yake unategemea nini?Hapo si laana tunajilaani wenyewe kwa mtu kukataa damu yake wengine wanazaaa na waume za watu ,What du u expect?Huwez kuwa happy na mwanao sawa na hao wanaume wanaokana damu zao hiyo laana haaishi nakumbuka Mwakasege alisema Watu tubadilike jamnai Mvunje hizo Nira Mbovu looh Obam Family their really happy watoto hapo lazima wawe na akili wanpata upendo pande zote na wanaadabu pia huku Tz watu wanapretend wacha mungu kumbe wao ndio nyumba zao zimevunjika kbs wanahitaji maombi jamani

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 05, 2009

    Kuna mdau nilimsikia akisema kwamba, mara nyingi ukikaa mida ya asubuhi pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi road, maeneo ya daraja la salender bridge utaona wadau wengi wakiwa kwenye magari yao wakielekea makazini. Ila akasema kwamba, ukiona kwenye gari kuna mwanaume na mwanamke wakipiga story na kucheka ujue "kapewa lifti", ila ukiona hawaongei na wamenuna (majority) ujue ni Mume na na mai waifu wake.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 05, 2009

    wewe mtoa maoni wa kwanza nakushangaa sana. wewe kama familia yako haina upendo,usisemi familia zote za kibongo hazina upendo.Jiongelee mwenyewe,wewe na familia yako,sio uongee kwa niaba ya watu wote.Pia acha kujidharau,la sivyo utaishia hapo hapo ulipo.Na wengine mnasema utajuaje ni maridhawa,sijui nini. Kikubwa ni kua wapo happy,highly educated,worked hard for where they are and they deserve that happiness and smile. na yoyote yule anaweza fikia hapo, wao ni mfano mkubwa sana,kuwa kila mtu anaweza kuachieve dream yake akifanya kazi kwa bidaa.

    Nice family photo,i love it. the kids are beautiful and happy.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 05, 2009

    Kitu kimoja mnabidi muelewe, siku zote watu kama hawa wakiwa ktk public places wanakuwa wana onesha furaha ila hauwezi kujua kama wanagombana, hawapendani au chochote, mfano clinton ktk scandal yake ya mapenzi, kila siku akiwa ktk picha uwa ana smile na wife wake lakini wakiwa ndani definitely wanagombana.

    Kuwa maarufu sio kuwa na amani na upendo, na msidanganywe na picha.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 05, 2009

    hii familia wala si kihivyo mnavyoona hapo. watoto mademu wote au mr. president hajui watoto wa kiume wanapatikana sehemu gani kwenye nanihii ya mke wake.mgogoro ndani ya nyumba lazima upo, ila siri yao.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 05, 2009

    Obama atafute kadume sasa kakurithi mikoba kwikwikwi

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 05, 2009

    Jambo lingine kwetu waafrika kwa ujumla ni tujaribu kuridhika na watoto wetu: wawe wakike au wakiume. Tuna tabia ya kupendelea zaidi watoto wakiume au lazima wa kiume atafutwe na kuishia kuzaa watoto 9 na hivyo wasiwe na maisha mazuri!
    Mtoto ni mtoto na baadaye watatulea vyema tu......Its so hard to ignore that though as its a cultural thing.
    Tukembuke tuko karne ya 21.

    J.
    Toronto, Canada.

    ReplyDelete
  23. Al MusomaJune 05, 2009

    Mchangiaji wa mwanzo unakosea ama kwa sababu una kumbukumbu za makabila ya Kikurya au Kinyakyusa ya miaka ya 50 na 60 au kwa sababu hujui watu wanaishi vipi katika maisha ya kileo. Kusini, kaskazini magharibi na mashariki ni kawaida kuona familia kama hizi - si ya Obama pekee. Kauli kwamba "familia zote zingekuwa hivi" haina maana kwa sababu haiwezekani - wapo mama au baba wasojali watoto na wapo ambao hawakujaaliwa kulelewa na wazazi wawili kwa namna hii. Mtoto mdogo wa kike kuweka mapenzi kwa baba ni kitu cha kawaida sana na ndo asili ya msemo wa kiswahili "mtoto wa baba".

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 05, 2009

    watu bwana eti familia infuraha,unafikili watu wote hawana furaha,kwakuwa hujaona pix za familia yangu ni bomba zaidi ya huyo rais,watoto wangu hunikumbatia na mama pia,na huwa wanacheza na mimi,msiwe fikla fupi,wa 22,uk hapa

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 05, 2009

    hayo yote sawa lakini msijizalilishe ati kusema watu huwa wananuna,au kwa kuwa familia ya rais,mie huwa pia na furaha na familia yangu,watoto na hata mama pia hunikumbatia,jisifie wewe kwanza ndo umsifie mtu baki,wa 22 hapa uk.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 05, 2009

    HEBU ACHENI UZAMANI, WATOTO WA KIUME, WHAT, WEE UNAESEMA FAMILIA SI KIHIVYO SABABU YA WATOTO WOTE WA KIKE, UNA AKILI FINYU,WATOTO NI WATOTO, AU WEWE BABA AKO NA MMA AKO WOTE WANAUME? KAMA MAMA AKO ASINGEZALIWA UNGEKUWEPO WEE NYAU,ELIMISHA FAMILIA YAKO NA ILEE KATIKA MALEZI BORA ITAKUWA FAMILIA INAYOHESHIMIKA, NA ACHA KUDHARAU WANAWAKE WOTE WENYE MAWAZO KAMA HAYO.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 05, 2009

    Hiyo tabasamu ya Obama ni kimarekani. kwa utamaduni wetu wa kiafrika, imezidi mipaka!! wanaume wa kiafrika huwa hatutarajiwi kutabasamu au kububujikwa machozi. hiyo haina maana kuwa hatuna furaha au uchungu. ilikuwa na maana yake. lakini katika muktadha wa kitandawazi, siku hizi tumeanza kuziona hizo tabasamu ili 'tuwe kama wamarekani!!!"

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 05, 2009

    eti obama atafuta kadume...how silly...yaani we have a long way to go

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 05, 2009

    NI AIBU KUSIKIA HADI LEO KUWA KUNA WATU WANA UBAGUZI WA WATOTO. KWANI WA KIKE NA WA KIUME WANA TOFAUTI GANI? KAMA SHULE WOTE WANAENDA NA WANAUWEZO WA KUFAULU VILE VILE. KAMA KAZI HALI KADHALIKA, IWE PILOT, ENGINEER, DAKTARI NK. NI MARA NGAPI TUMESHUHUDIA MADARASANI, WATOTO WA KIKE WAKIFANYA VYEMA KIMASOMO KULIKO WA KIUME? UNAWEZA KUPATA MTOTO WA KIUME AKAWA MSUMBUFU AU MVUTA BANGI, MWISHOWE HUYO WA KIKE UNAEMUONA SIO BORA NDIO AKAKUFAA KATIKA UZEE WAKO. MAMBO MENGINE BORA UKAE KIMYA, USIONGEE MBELE ZA WATU KATIKA MIAKA KAMA HII, UTACHEKWA. SHUKURU HATA KWA HUYO WA KIKE, KUNA WATU WANATAFUTA HATA HUYO WA KIKE HAWAJAMPATA....

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 05, 2009

    Mbali na yote ni ngumu sana ku "pretend" kuwa unafuraha. Ipo sehemu utashindwa tu. Naimani familia nyingi zinaishi kwa upendo. Maoni mengine kama ya mtoa maoni namba MOJA huenda anawasilisha hali yake binafsi.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 05, 2009

    Wewe anon wa 5:05 pm

    Uko dunia gani?

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 05, 2009

    wewe anon. hapo juu, watoto wa kike ni wazuri lakini wanakaribisha matusi nyumbani kirahisi.bora tu obama aendelea kuchimba shimo lake mpaka apate kadume.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 05, 2009

    wanaume wa kibongo wanaona noma kuwa karibu na wake zao, sababu naomba mnisaidie

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 06, 2009

    Kweli watu wengine wanashangaza sana na kumkufuru Mungu aliewapa zawadi ya watoto hivi wakati huu kweli ni wakuchagua watoto? Mtu alie na mawazo ya ubaguzi kwa watoto sidhani kama anawahudumia watoto wa kike alio nao kwa haki. Inasikitisha sana kuwa na fikra kama hizo.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 06, 2009

    Sio smile tu hapo ni real deep love and affection. Mliioona interview ya Mrs Obama kwenye NBC mngeelewa. Mrs obama anasema sio rahisi kuwa hivi. Is a hard working and still working on it everyday. Pia kila unyumba kuna ups and downs. Ila alisema heshima, trust na upendo ndio inawakeep together like this. Na alisema good communication is a must.

    Na pia obama alisema Michelle ndio anarun family. So if mom isn't happy nobody is happy. Hivyo wabongo mfungue ubongo...mpe mke madaraka kidogo...sio nyumba za kibongo nyumba inakua kama boot camp...baba ndio mwenye final saying.....corporal punishment...Unademand respect etc etc na kweli mwishowe mkipiga picha watoto wanaishia kumkumbatia tu mama yao kwa vile hawajui wakikushika itakuaje?

    Heshima sio kuogopwa jamani

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 06, 2009

    Sasa ni kwa kuwa Obama's Family? Hapa Marekani familia kibao zipo namna hiyo. Nadhani hata wewe mwenyekiti wa nanii familia hiko hivyo hivyo, kuna familia kama Dionis Malinzi...nilikuwa likizo mwaka jana nikawakuta pale Ghmakana wanacheza Gofu, nadhani siyo Obama's familia peke yake, ni wengi sana including wewe mwenyekit

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 06, 2009

    Ati obama atafute kadume kakuridhi. Acheni mawazo pumbafu ya kikoloni. Kwani mwanamke hawezi kurithi na kuendeleza jina la kwao. Baba yangu alituachia urithi watoto wake wote regardless of the gender. Mimi nimeolewa na mapaka leo natumia jina la baba yangu hyphenated my hubby's name. Na watoto wangu wetu mmoja jila la baba.

    Huoni Caroline Kennedy anavyopeperusha jina la kwa baba. Queen Elizabeth hakukua na dume sasa yeye anazidi kuendeleza kingship yao. So wenye mawazo ya kikoloni ya kuzalisha mwanamke mpaka apatikane mtoto wa kiume mtaishia kuwa masikini.

    Clinton - one girl
    Bush - two girls
    Obama - two girls

    Go figure na walakula kuku kwa mrija. mtoto ni mtoto

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 06, 2009

    And that is only J crew, Marshall, TJ max or gap. kweli sio lazima uvae designer clothes uonekana umependeza

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 06, 2009

    Ok,wote tuna mawazo mazuri. Lakini mada ni kwamba, familia hii inaweza kuigwa? yaani kimafanikio, upendo kwa baba, watoto na mama. Hawa watu wanapendana. Tuliwaona kwenye kampeni na nadhani hadi ndani ya nyumba.
    Twaweza kuwaiga? naamini twaweza ila tu dada zetu wakiacha tamaa (Waishio Houston) mnanielewa). Dada zetu wana tamaa sana kiasi kwamba kama wewe ni Obama, huna baba na mama hayupo, basi wewe hufai. Inabidi wajifunze kwanza kwamba upendo ni kuvumiliana. Kuna milima na mafanikio. Ikionekana milima, haimaanishi hamna mafanikio.
    Pia upendo ni uvumilivu. Ni dada wachache sana wa Houston ambao wangeweza kumvumilia Obama kwa shida zote alizopitia. Yaani atakusumbua sana. Atakuwa na namba ya simu ya kila mtu na kutishia kukuacha. matokeo yake ndo maana tunakuwa na nyuso za uzuni pichani na kupenda mama zaidi au baba zaidi.
    Ila naamini kila mtu anaweza kuwa chochote ikiwa ni pamoja na maisha ya furaha. Kina dada Houston, pesa tu haiwezi kukupa raha! pengine raha ni priceless. Hivyo basi kila mmoja ana nafasi ya ku-smile ila lazima tujue kanuni za mapenzi kwamba pesa tu sio furaha.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 06, 2009

    duh.."And that is only J crew, Marshall, TJ max or gap. kweli sio lazima uvae designer clothes uonekana umependeza"... unachanganya mchele na mchanga Marshall, TJ max ni maduka tu hayana nguo... hayo maduka umejua kwenye mtandao? Sijawahi kuona mtu anavyaa Marshalls au TJ Max. Kweli mabox yanachanganya watu ubongo.

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 06, 2009

    Wabongo acheni wivu na akili finyu. Hiyo ni familia bora,imetulia,furaha tele.wapeni sifa wale wanazozistahili.maoni mengi hapa inaonekana wazi kabisa kua ni mazungumzo ya vijiweni.

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 06, 2009

    Wanapendeza,wametoka mbali,wamefika mbali, wanakwenda mbali,tusiseme sana.True love never die,true love never decay.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 06, 2009

    Kina dada wa Houston ndio kina nani? Acha kugeneralize mambo, Houston jiji kubwa acha ubaguzi kuna wanawake kila aina na tabia tofauti sana fungua macho yako kwani lazima uwafuate madada wa Houston wenye tabia ulizosema hupendi? Umitoka nao mtaa mmmoja kule uzunguni koko? Mikocheni/Oysterbay/Sinza/Ilala/Kinondoni/Temeke?
    Hama mji kama wanakukera na tabia zao au nenda mji mwingine katafute walioelimika wenye tabia tofauti. Mi naona matatizo unayo wewe sio hao madada unaowalalamikia tabia zao. Do your thing and move on man why give a shyt? Au huwezi kutongoza kwa English/Spanish/French/Arabic/Chinese?
    Nenda kaombe kazi kwenye restaurant ya Yao Ming utapata mtoto wa Kichina!! pole sana kaka, ni aibu lakini usiharibu.Act like a gangsta and don't give a shyt what they do.Aibu kulalamika namna namna hiyo,siku hizi kuna facebook,n.k. huwezi kumzuia mtu asiwe na namba za watu saa ingine anaweza kuwa mapepe au sio mapepe. Just chill out you ain't seen shyt yet, keep looking and you'll regret for wasting time.You crack me up!! That story is crazyshit Nigga.Goodluck.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 06, 2009

    MIMI MDAU WA DSM MBAGALA MABOMU AREA NASEMA HIVI

    TATIZO KUBWA LINALOTUPONZA SISI WA BONGO KUTO KUWA VERY CLOSE KIFAMILIA NI HILI

    WAZAZI WETU HAWAJIANDAI VEMA KTK WAKATI WAKIWA NA NGUVU AU UJANANI

    WAKISHA STAAFU WANAKUWA WEUPE MATOKEO YAKE WANAKODOLEA MIMACHO KWA WATOTO WAO WAKISAHAU KUWA WATOTO WAO NAO WANAMAISHA YAO

    SASA MUME AKIELEZWA UKWELI KUHUSU
    MINDUGU KUJAZANA HOME ANAANZA KUMWONA MKE HAPENDI NDUGU ZANGU

    HAPO GAP LINAANZA

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 06, 2009

    wakati nyie hapa mnatoa negative zenu na wivu uliojaa kupita kiasi,familia hii inazidi kuwa na furaha na Mungu anaendelea kuwabariki ili wasaidie watu na kutimiza ndoto zao za kimaisha.
    Mungu saidia Tanzania ili waache wivu na kujiweka chini siku zote.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 06, 2009

    Kitanda usicholala utajuaje kunguni wake?

    Mtoto ni mtoto hata kilema.

    Wabongo mwanmke ajifungua mtoto mwenye kasoro anakimbia. Sasa hapa unafikiri utakuwa na amani. Azaliwe wa kiume ama Kike kama anakasoro mwanamke atakimbia tu.

    Sasa eti ajitahidi atafute kakiume? Yaani wanaume wa kibongo huwa nawashangaa sana. Kila mtu ataumbwa kwa mfano wake.


    Mdau

    UKONGA-UWANJA WA NDEGE.

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 06, 2009

    FAMILIA ZOTE ZIKO HIVYO NDOMAANA WATU WANAONA NA KUZAA WATOTO,UPENDO SIMAANA YAKE KUKUMBATIA ZA ZOTE, HAO TUNAWAONA WAZI KWA VILE NI PUBLIC FIGURES IN THE COUNTRY WITH MULTI-PRESS,SASA UNATEGEME KUONA UPENDO WA BABA WA MPITIMBI NA FAMILIA YAKE KWENYE GAZETI LA WAPI,HAO TUNAWAONA KWA VILE WANAPIGWA PICHA,WATU WOTE TUKO HIVI HATUNA FUSA TU YA KUPINGWA PICHA,THAT IS IT,PLEASE BE ANALITICAL BEFORE UJAROPOKA

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 06, 2009

    huyo mdogo anampenda sana baba yake nimeona picha nyingi tu yupo close na obama. safi sana ninawapenda

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 06, 2009

    picha nzuri,familia maridhawa.

    Kama na wewe familia yako ni nzuri kuliko, hongera. kama bibi na babu yako wanafuraha kuliko hawa,hongera pia.

    kwanini mnajaribu kulinganisha na kutoa walakin?

    Umaridhawa wa familia hii, haumanishi wengine hawana familia nzuri. Actually dunia itakuwa bora kama familia zoote zitakuwa maridhawa.

    ReplyDelete
  50. Watanzania tutaedelea line wakati tunazaa watoto wengi utafikiri mashindao, Familia itakuwaje na furaha wakati una watoto mia na huwezi kuwatunza? Igeni mfano wa wenzetu sio kuzaa wengi na huwezi kuwatunza

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 06, 2009

    Hee, Jamani, Mama Obama anatarajia ama ni Macho yangu tu?

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 07, 2009

    Sasa kama familia nyingi za kimarekani zina upendo hivi mbona wanaachana kuliko mataifa yote duniani. Kinachovunja mapenzi ya waafrica wengi ni wanawake kibao. love is for two people,not otherwise. Mke mmoja ingekuwa sheria ya nchi zetu. Obama ni baba wa dunia lazima aonyeshe ulimwengu yale mazuri.

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 07, 2009

    SIJAELEWA KUHUSU MJADALA...
    YAANI FAMILIA ZINGEKUWA HIVI MAANA WAZAZI NA WATOTO WAWILI AU WAZAZI NA WATOTO WA KIKE?
    AU KUCHEKA KWENYE PICHA?

    ReplyDelete
  54. AnonymousJune 07, 2009

    KILA MTU MBONA ANASMILE KWENYE PICHA UNLESS NI PICHA YA MSIBA.

    ReplyDelete
  55. AnonymousJune 07, 2009

    AND YES MAMA OBAMA ANATARAJIA MTOTO WA KIUME MWEISHO WA MWAKA...KAENI MKAO WA BABY SHOWER YA NGUVU INAKUJA

    ReplyDelete
  56. AnonymousJune 07, 2009

    wewe mdau wa june 07 saa 2.02

    una akili sana ni kweli tuwaige kwa kipi,kwa kuwa na watoto wawili,wakike watupu,au walivyokumbatianana kutabasami?


    hata mimi na mume wangu aitwae mtraveller na watoto wetu wawili wa kiume waitwao moses na abrahamu tunapendana sijui ninyi

    ReplyDelete
  57. AnonymousJune 07, 2009

    KIDUME MUHIMU....jaman....!! ila kama mungu kakunyima basi ushukuru!!ukoo unakuzwa na kidume,mbona wewe wanao huwapi majina ya ukoo wa mkeo? au kabila la mkeo? tungemjua wapi OBAMA ni MKENYA bila kidume babu yake aliye mleta baba yake obama? mbona hakutaja UKOO WA MAMA YAKE nani asiyejua mama yake Obama ni MZUNGU!! LAKINI YEYE KASEMA NI MKENYA, sababu ya kidume BABA...!!
    Mungu ailaze roho yake peponi huko aliko.
    tuache dada zetu waeneze ukoo kwa wengine.

    ReplyDelete
  58. AnonymousJune 07, 2009

    Jamani vidume ni muhimu mno kwa kulinda heshma na jina la ukoo lisipotee.Bila ya kidume ukoo unakuwa si endelevu.Ambao hawana vidume poleni na si kwa mapenzi yenu.Bila dume familia inakosa hata harusi, nyinyi mnakuwa watu wa send off tu na kitchen part kila wakati, haipendezi.OBAMA TAFUTA KIDUME MTU WANGU!

    ReplyDelete
  59. AnonymousJune 08, 2009

    YAANI MIE NA MUME WANGU WA KIBONGO NILIYEMPIGA KIBUTI TULIKUWA HATUPENDANI. TUKIENDA KWENYE PARTY, AKIINGIA TU ANAENDA KUSHOTO NA MIE KULIA HADI SAA YA KUONDOKA NDO TUNATAFUTANA TURUDI HOME. PICHA ZOTE ZA KWENYE PARTY YUKO NA WASHIKAJI NA MALAYA KADHAA, NA MIE NAKUWA NA MIDUME AMBAYO HATA SIIJUI, YAANI ILIKUWA ADVENTURE BAB KUBWA. TUKIWA SEHEMU MUME WANGU ANANI-IGNORE KAMA HANIJUI. ILA MIE HAIKUNIPA SHIDA, MAANA NILIJIKUTA NAPATA SERVICE MURUA KUTOKA KWA NJEMBA FLANI LA KUTOKA AFRIKA YA MAGHARIBI, SERVICE AMBAYO MUME WANGU ALIKUWA HANITIMIZII. NA HIZO NDO TABIA ZA WANAUME WENGI WA KIBONGO. YAANI THEY ARE NOT ROMANTIC, BASI ALIMRADI TU. JAMANI PIGA UA, GALAGAZA, WANAUME WA KIPOPO WANALIPA. YAANI UNAJASIKIA KAMA QUEEN, LIFE IS TOO SHORT! WHO CARES KAMA WEZI! NI AFAZALI KUWA NA MWIZI ANAKU-TREAT VIZURI KULIKO KUWA NA MBONGO MWENZIO ANAKU-TREAT LIKE LEFTOVERS. Mrs. Ogunsiakan Oludamilare

    ReplyDelete
  60. AnonymousJune 08, 2009

    kaka michu, mie nafikiri kuna tofauti kati ya fake smile na real one, kwa kweli hata waliosoma psychology watakubaliana na mimi kuwa hiyo familia hapo wanafuraha ya ukweli hiko kicheko si cha kinafiki, lakini matatizo ya ndoa hayakosekani, lakini tujue kuwa mapenzi yanajengwa kwa kusameheana, unapoweza kusamehe ndio unaimarisha pendo, nawasilisha

    ReplyDelete
  61. AnonymousJune 08, 2009

    NYIE OSHENI VINYWA VYENU LKN UKWELI NI KWAMBA IYO FAMILIA NI BORA KULIKO NYINGINE NYINGI SANA HAPA DUNIANI. BABA NA MAMA WANAWEZA KU-FAKE LKN SIO WATOTO. MKIONACHO KWENYE PICHA NDIVYO ILIVYO HATA WANAPOKUWA PEKE YAO TENA ZAIDI YA HIVYO. TATIZO LENU WIVU NDO UMEWAJAA WENGI WENU KWAVILE WEWE HUNA FURAHA NA FAMILIA YAKO BASI ILI UJIRIZISHE NAFSI YAKO UNACHOFIKIRIA NI KUTOA KASOLO TUU. MTAKUFA NA VIJIBA VYA MOYO.

    OBAMA JUU ZAIDI, MUNGU AKUZIDISHIE BABA WENYE WIVU MJINYONGE TUU.

    ReplyDelete
  62. AnonymousJune 08, 2009

    annons:
    1.Dr Kai AM
    2.Bold letters
    3.DSM mbagala mabomu area

    hahahahahahaaaaa kwi kwi kwi tih tih uwoooo hahahahahahhaaaaaa

    asante

    ReplyDelete
  63. AnonymousJune 08, 2009

    ooh God!
    from the heart i love this family,hata mnaoponda ukweli mnaujua basi tu kawivu!i pray mungu anipe this kind family with love and careness after few months!
    God bless u!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...