Ras Makunja akiwa na the Ngoma Afrika Band kwenye moja ya matamasha kibao waliyoalikwa mwaka huu ambapo FFU inaendeleza libeneke kwa kwenda mbele.
Bendi ya mziki wa dansi "The Ngoma Africa Band" yenye maskani yake mjini Oldenburg,Ujerumani wataupeleka mzimu wa dansi katika jukwaa kubwa la maonyesho la Masala Festival,mjini Hannover,Ujerumani siku ya jumapili ya Juni 14 -2009 .
Bendi hiyo yenye tabia ya kuwapeleka mashabiki mchaka mchaka kwa muziki wake murua huko ughaibuni, inatarajiwa kutumbuiza majira ya saa 10.00 alasiri,ambapo washabiki wa nyimbo za kiswahili na muziki wa dansi wanaisubiri kwa hamu bendi hiyo, iliyofanikiwa kujizolea umaarufu kwa kutumia vionjo vya midundo ya dansi ya kibongo.
Kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Ras makunja ataliongoza kundi hilo jukwaani kwa kazi moja tu, nayo ni kuwadatisha na kuwapa shangwe mashabiki! hebu wasikilize hapa mdau upate uhondo wa kazi yao nzuri
pia wasiliana nao kwa
pia unaweza kupata habari zaidi bofya hapa
the-ngoma-africa-band-continues-to-thrill-fans.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2009

    vichaa hawa wanakubalika! wao hakuna kulemba ni mdundo tu!
    kazi yao ni tishio la kimataifa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2009

    najua vichaa lazima mtawasha moto mkali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...