msanii Gabriel The King a.k.a GTK anajitambulisha kwa video ya mojawapo ya singo zake sita kati ya vyake 12 anazotarajia kuvimwaga hewani hivi karibuni na baadaye albamu nzima yenye vibao 12 kabla ya mwaka huu kumalizika, huku akidai kiti cha enzi cha ufalme wa Hip Hop.

Singo hii inaenda kwa jina la Ju' kama Obama na imetengenezwa Mawingu studios kwa Dj Bonny Luv na FishCrab, wakati kazi ya video ni yake Adam Juma wa Visual Lab.

Anasema baada ya majuma matatu atafyatua singo ingine itayokwenda kwa jina la 'Barua ya wazi kwa JK' na kuendelea kumwaga singo moja moja kwa muda huo hadi zitimie sita, ndipo atoa albamu nzima ya vibao 12.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    KWELI HUYU BWANA YUKO JUU. NAMKUBALI 100%. UZURI UNASIKIA MISTARI MINGI NDANI YA KIBAO CHAKE. WENGINE HUWA ZAIDI NA MBWEMBWE ZA MAPIGO YA VYOMBO KULIKO UIMBAJI. KAZI YAKO IMETULIA.

    SEMA TU SWALI LANGU NI -KWANINI WAIMBAJI 'STAA' WA BONGO HUVAA JEZI ZA MICHEZO ZA USA?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2009

    Kutokana na umri sisikilizi sana maneno ila video imetulia.
    Wanawake is the best flavor kwa music video na mandhari nzuri pamoja na nice cars na beautiful places. Video is good.

    Tuondokane na ugonjwa wa video za kuoensha matatizo na majumba ya udongo kama tunashawishi misaada. Hazitii hamu kuangalia.

    Sometimes dirty ladies and ugly some. No bueno amigoz

    Modernisation is very important hasa kwa villagelization and globalisation.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2009

    ohooooooo..
    ni kweli yupo juu kama mzee Barack Hussein Obama ??

    linganisha basi

    http://www.daylife.com/topic/Barack_Obama/photos

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2009

    Nyie watu mmesikiliza beats tu! Mmesikia maneno anayosema? Eti Marekani hakulipi. Thubutu! Labda wa watu ambao hawajaenda shule na pengine wewe ni mmoja wapo na mwanakijiji. Kama marekani hakulipi kwa nini sasa Obama yuko juu? Marekani unaweza kujenga nyumba kwa box, niembie nchi gani unaweza kufanya hivyo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2009

    Nina madeni uku usa kama nina hakili nzuri vile.Nakubari ujumbe.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2009

    hahaha Unafurahia madeni? kazi kweli ipo..

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2009

    Ohhhh puleeeeeeees

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2009

    teheteheh umenichekesha hapo juu wee uliyempa link alinganishe....

    bongo bwana....mtu chakula kikijaa kwenye fridge ndani basi anajiona tajiri its more than that guys

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2009

    Singo nyingine baada ya wiki tatu?
    Namna hiyo hutaendelea. Tengeneza pesa na hiyo kwanza

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2009

    Video - good
    Beats - good
    lyrics and storyline - very poor...

    Mimi sikujui mshkaji sijui ulikuwa majuu lakini kiswahili cha mziki kimekupita mbali na mistari yako haijapangika kabisa kama unai-force vile?

    ni hayo tu....

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 06, 2009

    NAMFURAHIA MWIMBAJI KUWAPA WATU PICHA HALISI YA MAISHA WANAYOWEZA KUKUMBANA NAYO WAKIFIKA USA AU "MAJUU". NI ONYO ZURI MTU ASIFIKIRI TU KUWA USA ATABADILI MAISHA KUWA MAZURI. WANGAPI WAMEZAMA USA NA HAWANA UBAVU HATA WA NAULI YA KWENDA NYUMBANI? LAKINI HAPOHAPOKUMBUKA WAPO WENGI SANA WANAOTENGENEZA PESA NZURI. PROFESA ANAYEFUNDISHA UDSM KWA MFANO HAWEZA KUWA NA KIPATO HALALI CHAKULINGANA NA PROFESA WA USA. AU MBEBA BOKSI WA USA HAWEZA KUWA SAWA NA MBEBA LUMBESA WA KARIAKOO.

    UNAYEOGOPA MADENI SHAURI YAKO. MAISHA NI WAKATI UPO DUNIANI. SASA BORA UISHI BILA DENI NA UFE? CHAGUO LAKO.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 06, 2009

    Track iko bomba tu video iko poa pia au siyo kaza buti mazee kama kweli unataka kuwa juu kama obama inahitaji moyo na uvumilivu na siyo kukata tamaa hahahah umeogopa kushindia mikate USA?Uko na kibarua kigumu mazee game yeyote ile huwa ni ngumu tu jitahidi utafika huko juu ni hayo tu!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 08, 2009

    kwanini tanzania tunataka kuwa kama wamarekani????!!!! sitakaa ni support miziki hiyi ya kibongo,ni uchizi mtupu.I hate the video contents, it's just crap!! what the hell, champagne glasses,taking video with a range rover.to me,bongo this kind of bongo flava doesnt have originality,oh my God,tanzanians,they love being americans.I am so sick of this.

    ReplyDelete
  14. Naipenda Video na Lyrics zake..i think its pretty hot'' stop hating haters!
    Anayosema is nothing but the truth..about life in America & Tanzania....nimeishi Bongo na nimeishi USA...the difference though is nikuwa America ajira zipo..wakati Bongo mpaka uwe na Degree...au uwe na Refa ndio upate kazi..na ukiwa Juu ka Obama U Hustle Mo'..so GTK Tell e'm''let"Em know what time it is Baby!! You Rock''...we are rocking this your video in CT...Representin''

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 23, 2009

    Ladies and Gents,i read yo comments,some of you are haters,mwenzenu kasema ukweli,US maisha ni magumu,that's reality accept it,we u hapo juu unasema,US unaweza jenga nyumba,kwa pesa gani uliyonayo? we all know about 30 year mortgages,kwa hiyo usitudanganye hapa,na hako ka associate kako,let the boy do his thing,that's his choice and story line.GTK you do you,forget about HATERS,CONNECTICUT loves the MUSIC VIDEO and yo story.DON'T GIVE UP,PEACE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...