Dear michuzi tunafurahi kukutumia picha hizi ambazo tulikuwa tunasherekea kuagana Da' Vicky Kamata (mwenye nyekundu) mara baada ya kumaliza masomo yake vizuri hapa Southampton UK na anarejea nyumbani Tanzanai wakati wowote kuanzia sasa. Tutafurahi kaka kama utazirusha katika mtandao wetu wa jamii ambao haubagui wala hauchagui.
Home
Unlabelled
kamnuso ka kumuaga da' viky kamata southampton
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
we mwenye afro kuuuubwa na t-shirrt nyeusi inaelekea ardhi ya malkia imekukubali vilivyo. ndo UK hiyo kama una kazi basi hakuna sehemu kama UK duniani humu. hela iko juu kinoma kama una kazi inalipa kishenzi. mi nimeishi marekani miaka mitano baadae nikazamia hapa UK kwakweli naona kuna tofauti kubwa sana hapa UK mambo mswano Pound inalipa ile mbaya yani sahivi US dola naiona kama toileti pepa flani hivi.
ReplyDeleteyah sister vicky,hongera sana kwa kupata uamuzi huo wa kurudi nyumbani baada ya masomo,ningependa pia wabongo wengine waige mfano huo,na inaniuma zaidi kuona wabongo wenzangu tena wasomi wanafanya kazi za kusafisha vyoo au barabara ambapo angerudi bongo angekuwa ni mtu muhimu sana kijamii,wabongoeeh tuachane na kasumba ya ulaya,mimi pia nipo mbioni kurudiii
ReplyDeleteShimboni shafo papa MREMA, we miss you H-TOWN
ReplyDeletemdau weye unaesema wabongo turudi zetu bongo umetugusa kwenye ikulu zetu, jua kuna makundi matatu wanaokuja ulaya la kwanza kwa ajili ya kusoma na kurudi,la pili kutafuta mitaji na kurudi la tatu wamefika hawataki kurudi Bongo wala kusikia habari hiyo. kwa hiyo uheshimu uhuru wa watu hata kama umeona wamepotea waelimishe tu kiduchu.
ReplyDeletemjomba wa kwanza, kama unatathmini maendeleo ya kipesa kwa ukubwa mwili au wingi wa nywele kalaghabaho...
ReplyDeleteNB: waafrica tutajifunza lini kama mafuta mengi mwilini yana madhara kiafya??
We anonymous kwenu Masaki, kwetu Tandale halafu unaniambia nirudi, una wazimu eeh! kila mtu alikuja na kiroba chake, mnaotaka kurudi rudini na tunaotaka kubaki tuacheni tubaki. kazi bongo hadi uwe na connection, na mie hiyo connection sina, unataka nikale kwa balozi eeh! unajuaje kama mie si-enjoy kusafisha vyoo?
ReplyDeletemzee wa early times,stake country represent..
ReplyDeleteWewe ujui watoto wa mafisadi kazi ziko tayari!! Wewe ukijitia kurudi nyumbani na hakuna mtu unayemjua jikoni kiama chako na litakuchwea. Sisi tuko USA tunaendelea kubeba ma-boxes na yanalipa kama kawaida. Huyu dada kazi ipo tayari.
ReplyDeleteJamani kifua cha huyo Da'Vicky kimetulia na kimekwenda shule kubwa. Ukimpelekea mpira anautuliza kifuani kwanza halafu ndio anapiga shuti, GOOOOOOOOAL!!!!!!!!!
ReplyDeletewewe anoymous 1:41 am, umeulizwa hayo yote?au shobo tu, ndo nyie nyie mnabeba mabox huko unajifanaya $ kwako kama toilet pepa, Tz ndugu zako umewaachia nini?ala, kila m2 akianza kujishembendua kama hivyo 2tafika?pamoja na kukaa nje miaka yote hiyo bado una ushamba wa kutozoea vitu na kujitangaza,..Hongera Vicky karibu home.
ReplyDeleteMtoto wa mkulima Tz
wewe anonymous acha kumwatanganya wabongo kuwa warudi nyumbani, Bongo hakuna kitu vumbi tu na shida kibao haziishi, wewe daaa vick wala usirudi bongo hakika utaijutia hiyo nafasi yako ya kutoka kwa malkia haya bwana yetu macho karibu tule vumbi Bongo.
ReplyDeletemie mdau niko kijiweni Bongo
Aliahidi ubalozini akimaliza masomo atarudi kwao, ndio maana wakampa visa, Na sasa Anarudi...Hongera kwa uadilifu.
ReplyDeleteSijawahi kusikia Mtu ana British Passport au indefinite leave to remain na ana kazi nzuri (professional) karudi bongo kabla ya mid 30's to late 40's...All the best mama.
hongera sana madame V.
ReplyDeleteKila la kheri katika mchakato wa maisha urudipo nyumbani.
Edo aka ISHI
wadau naomba kusema kidogo hivi sis wtz hatuna kazi hata wale wa ulaya yalele.kwanini mtu abaki ulaya wakati uku tayari ana jina kubwa kama yeye na nafanya kazi nzuri Bot Mshara mzuri wewe unataka tena ubebe taulo za wazungu kwa $2000.00 kwa mwezi wakati pango $ 800.00 na pia heshima hakuna mitoto haina heshima kama nyumbani bongo watch out men. wewe unayebaki uko una kazi ya maana bongo ndoo maana
ReplyDeleteunaangaika. bongo tamu saaaaana
viela lakini unafanya mambo ya maana kama kiwanja,wazaziwako nk.
weee annon apo ukue akili na mwili pia
ReplyDeletebongo michingo miiiingi sana,yan km huna mtu kwishnei kbs
madame uyu ana wake tena vibosile kwisha habari yenu
ni ayo tu
Duh! Mwana mwenye fulana kama ya Michuzi tulikuwa tunakula wote vumbi TTCL sasa naona mambo yake si mabaya!! Nakusalimia Mkuu!
ReplyDeleteNyie jidanganyeni krudi bongo. Mwenzenu alikuwa na "leave of absence" kutoka BOT, sasa anarudi kazini. Nyie fuateni asali mliwe na nyuki. Kurudi bongo ni mpaka uwe na kazi tayari si kwenda kutafuta kazi bongo, majungu mengi sana. Afisa mwajiri akiona una degree ya abroad anakwambia kazi hakuna ili usichukue nafasi yake huko mbele.
ReplyDeleteBongo ni mpaka uwe na godfather au upo kwenye payroll tayari ndiyo fikiria kurudi. Vinginevyo kama hujajilipua katembelee ndugu na jamaa wiki moja geuza ukikaa sana utaishiwa nauli na kujikuta umekwama.
Karibu, karibu, karibu!
ReplyDeletewewe dogo wa June 23, 2009 5:33 AM una matatizo kweli, yaani picha zote hukuona cha kusema ila kifua cha huyo kimwana! you are pervert! big time pervert, you need help! ha ha ha ha
ReplyDeleteNakubaliana na ndugu zangu wabeba mabox wadanganyika! Lakini jamani naoma angalau mkipata hizo hela tafuteni watu waaminifu angalau mjenge vibanda maana naamini kabisa tuela twa kubeba mabox na kusafisha vyoo ukitunza asilimia fulani na kujenga nyumbani inaleta raha! Kumbukeni TZ ardhi ipo!
ReplyDeleteDa!!! wangu umesema, anon wa 4:25 am, kwao masaki wewe tandale wapi na wapi, nani? atakuona huko tandalae karibia na uwanja wa fisi,wewe ni jilani yangu ulikua na mimi maeneo ya manzese, karibia na uwanja wa fisi, wangu achana nao hao watoto wa vibosi, mafisadi, tandale,manzese, uwanja wa fisi, hakuna hata kibosire anaekaa mitaa ya huko,
ReplyDeleteHa jamani kwani ilikuwa lazima mjitoe katka blog? Any ways hongereni
ReplyDeleteJamani, huyo Vicky Kamata anafanya kazi BOT, so angekuwa chini kamaangebaki huko UK, hivyo nyie wabeba mabox msifuatishe huyu dada, na ni kada mzuri wa ccm, mwache arudi kula pipi,
ReplyDeleteAh papaaa Lukwaro Jacob kumbe ndo mana umepotea sana mjini..... Mama yuko wapi kaka?
ReplyDeleteSafari njema, da vick, ukifika home bongo utasikia heee!!!! katoka ulaya, katoka uk. Hizo ndio zetu, labda kama unatoka masaki, lakini huko uswahilini kwetu, katoka ulaya, hiyo ndio Tz yetu na wa Tz ndio sisi
ReplyDeleteHUYO ANNON WA KWANZA KAMA KAJITILIA UJIKSI MWENYEWE? HALAFU BADO MSHAMBAZ WAA PHOTO. CHEKI ALIVYOKODOLEA MACHO CAM IKAMKOSA....NIPIGE PICHA BASI WATU WANIONE NILIVYOKWIVYA NA NGANO ZA UK...TEHTEHTEHTEHEEEEE
ReplyDeletedah ila unajua watoto wa southampton wanakaushamba fulani hivi watu wengi wamekuwa wakija kusoma na wanaondoka na phd ila hawajitoi humu ila hii group ni wale watu wanaolazimisha kujulikana anyway naona wamefurahi kuwekwa kwenye blog but hakuna cha maana wengi tumemaliza shule na tunarudi kimya kimya sasa yote haya ya nini?
ReplyDeleteSafari njema wasalimie bongo.Madau uliyeponda Marekani inategemea ulikuwa wapi na unafanya kazi gani,Hapa mbona ni kila kitu!
ReplyDeleteMwakani narudi bongo kula bata kidogo.
Big up da Vick.