Mzee Michuzi mimi nina kero,
Ninafanya kazi nje ya Tanzania na mara nyingi nikija nyumbani Tanzania nafikia (on transit) hoteli ya Kilimanjaro kempiski ambayo inafahamika kama (five star) kabla ya kwenda nyumbani kwetu kuwaona wazazi kijijini.
Kinachonikera ni kwamba katika hoteli hi ambayo ipo Tanzania kwene moyo wa jiji la Dar Es Salaam- katika Luninga zoote hapa hotelini- kuna channel 26- channel zoote ni za nje na channel moja tu ndiyo ya Tanzania (TBC- Tanzania Broadcasting Corporation). Pia nayo mara zoote haipaikani.
Cha misingi pia ni kwamba Watanzania wengi san pia niwateja katika hoteli hii. Nilijaribu kuongea kwa kirefu na moja wa wafanyakazi hapa hotelini - waanambia kwamba mimi si Mtanzania wa kwanza ku- lalamikia swala hili lakini hakuna ufumbuzi wowote.
Nimekuwa nikizungukia hoteli nyingi pia nchi nyingine, katika Luninga zao- lazima utapata si chini ya channel tatu hadi tano ambazo ni local channel.
Mh. Michuzi, wadau wanalionaje hili?
Asante sana
Mdau Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2009

    Tatizo liko kwa DSTV wanatoa channels za nje nyingi na kuacha za kiafrika hususan za kibongo,mimi mwenyewe nimelipia DSTV easy chanells unapewa chanels 10 kati ya hizo 9 ni za kihindi na 1 tbc,hamuwezi kuamini TBC inaonekana kwa kwikwi na sauti inakatakata,nilijaribu kuwafuata ofisini angalau wabadilishe hizo selections walizotuwekea sis wateja wa easy channels nikaambiwa eti hizo easy chanells ni default channels kwenye system yao kama naona sifaidi basi nilipie channels 26 kwa mwezi,kwa kifupi nilichoka na majibu yale.Naomba DSTV na mamlaka husika ya mawasiliano TCRA ifuatilie kwa ukaribu suala hili!! yaani bora ya iliyokuwa GTV!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2009

    na wewe ni fisadi...yan unafikia 5starzz???

    hii nchi ni ya wenyewe wee ujui tu?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2009

    Msilete za kuleta hapa hoteli inatoa package ya facility kwa kuzingatia yao kichwani ukitaka unapangisha hutaki amia kwingine au jenga nyumba yako uweke unachotaka. Huku kwetu Uwnja wa fisi hata TV hatuhitaji mambo yoye laivu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2009

    SASA WEWE ULIENDA KUTAZAMA TV WENZAKO WANAKUJA KUTALII.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2009

    JAMANI ALIKUWA KWENYE HONEY MOON, ANY WAY USIHOFU,WAAMBIE WAWEKE OPTION YA KUTUMIA TV PEKE YAKE BADALA YA KUTUMIA DECODER ILI KUKAMATA CHANNEL ZA HAPO HAPO BONGO.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2009

    Mimi nakushauri uwe unafikia gesti moja maarufu kule Tandale Uzuri, jina limenitoka kidogo. Huko, Kila TV ina antenna ya ke (tubelight Technology), na unapata Chanel zaidi ya 7 za kibongo!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2009

    KWANI TELEVISION SI KAMA RADIO TU UNA-TONE UNACHOTAKA. WENYE HOTEL WANATAKA HIZO CHANNEL WANAZOONYESHA, CONTROL WA HIZO TV NDO ANACOWAWEKEA WATEJA WAKE, SASA UNAPOSEMA TV ZINGINE HAZIPATIKANI SIELEWI, UNAMAANA HATA KAMA UKIZITAFUTA KATIKA TV ZA HOTEL HIYO HAZIPATIKANI AU HOTEL HIYO HUPENDA HIZO ZA NJE TU. BUT YOU HAVE TO UNDERSTAND THAT MAYBE IS THEIR POLICY SO YOU AS AN OUSIDER YOU CAN'T CHANGE IT.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2009

    Hapa haupati hata wazo 1 la kusadia manake watu wana wivu, Jamaa wamesikia umefikia nyota 5, huenda mtu hajalala hata ile ya nusu nyota si rahisi kutoa mchango wa kuboresha! Kempinski Wanapaswa kulitambua hilo local channel zinasaidia kuitangaza nchi, Mmamarekani akiona jamaa wanaflow bongo fleva hapo lazima akasimulie kwao! Kwanza hao watalii hawataki hiyo Michale manake kila siku wanayaona kwao!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2009

    Hapa haupati hata wazo 1 la kusadia manake watu wana wivu, Jamaa wamesikia umefikia nyota 5, huenda mtu hajalala hata ile ya nusu nyota si rahisi kutoa mchango wa kuboresha! Kempinski Wanapaswa kulitambua hilo local channel zinasaidia kuitangaza nchi, Mmamarekani akiona jamaa wanaflow bongo fleva hapo lazima akasimulie kwao! Kwanza hao watalii hawataki hiyo Michale manake kila siku wanayaona kwao!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2009

    nakuunga mkono mdau wa mwisho 1:48pm hapo ni wivu kwanini kalala 5 star hotel ndio maana wengine wanaongea ushuzi.kuwa na local channel katika hotel kubwa inasaidia kutangaza nchi hasa kwa wageni ambao si watanzania,hizo channel za majuu wanaziona kila mara wakiwa huku kwao hakuna wa kuitangaza nchi yetu zaidi ya sisi wenyewe "aidharauae nchi yake anajidharau mwenyewe".
    Mungu ibariki Tanzania.
    mdau scandinavia.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2009

    rafiki yangu hio ndio lack of pride in self ambayo na kaugonjwa tumekuwa nako Tanzania kwa miaka mingi sana. Hapo nakuambia hata channel za Burkina Faso au Somalia zingepatikana zingeonyeshwa badala ya channel za bongo!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 19, 2009

    Hilo nimekumbana nalo Movenpick,walidai wanatumia cable TV ambayo inasababisha tusione local channels.Mbali na hapo nilishangaa hotel kubwa kama hizo hawana vyakula halisi vya kitanzania.Unaambia ni indian dishes nk,ushamba mtupu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 19, 2009

    Kwa kweli sio Kempinski tuu haionyeshi Channel za Kitanzania hata City Garden, Chef Pride, etc. Hoteli nyingi za Tanzania ambazo zinahadhi na hata Restaurant huwa hazionyeshi channel zetu. Kwa hakika sielewi kwanini hivi? Kwa upande wangu naona sio sawa sababu pia kuonyesha vipindi vya Kitanzania ni njia mojawapo ya kuonyesha tamaduni zetu hasa pia kupitia michezo mbali mbali inayoonyeshwa, pia kujua maendeleo ya nchi yetu mfano kwa njia ya habari.

    Siamini kama BBC, CNN, DW kunamtu ameshawahi kuona habari za kitanzania labda iwe tuu zile kubwa hasaa ndio wanazionyesha.

    Hii inaonyesha pia jinsi gani watanzania tunavyokuwa hatuithamini nchi yetu na kutukuza Umagharibi kwa sana. Hatupendi kuitangaza nchi yetu.

    Tungependa waweke hata channel kama tatu Zakitanzania ili Wageni wote na hata Wazawa waweze kufaidi na wageni waweze kuona au kusikia zaidi kuhusu nchi yetu Maendeleo ktk habari, Bunge, Maigizo, nk.

    ReplyDelete
  14. Elly Mbotto Jr., IdodomyaJune 19, 2009

    Mara nyingine fikia huku NAMNAANI iliyoko Sinza huku bondeni, utapata channells zote na hassa zile maalum kwa ajili ya watu wazima zinazowaonyesha wabongo tu na jinsi walivyo mahiri katika fani.
    BONGO RAHA TUPU JAMANI

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 19, 2009

    WENGI WALIOONGEA HUMU KUMPONDA MDAU WANA MAPUNGUFU MAKUBWA MAWILI: KWANZA HAWAJUI THAMANI YA NCHI YAO NA JINSI ILIVYO MUHIMU KWA WAGENI. PILI, HAWAJAWAHI KUSAFIRI DUNIANI, UKISAFIRI KINACHOKUVUTIA SANA HOTELINI NI LOCAL CHANNELS AMBAZO ZINAKUONYESHA MAMBAO YA NCHI ULIYOTEMBELEA AMBAYO YANAVUTIA SANA KWASABABU HUJAWAHI KUYAONA!. HATA KWA MBONGO UKITOKA NJE LEO, TV ZA BONGO ZINAKUWA KIVUTIO SANA KWASABABU HUJUI KITU. NI KAMA UNAVUMBUA UPYA! ZAIDI YA HAPO WALIOPONDA WANA UPEO MDOGO...UGONJWA MAMBAO NI MKUBWA TANZANIA!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 19, 2009

    Jamani watanzania tuna wivu!!!!!!! Na inasikitisha sana tena sana pale mtu anapouliza kitu anategemea maoni mazuri, badala yake unakutana na maoni hayana kichwa wala miguu na ujui uanzie wapi? Naomba tubadirishe hii tabia ya mtu kuuliza kitu cha maana unatoa maoni ambayo hayana msingi. Inasikitisha na inauma sana. Tukibarilika nina imani kuwa tunaendelea kimawazo katika jamii husika. Nawashukuru sana wote mnaojitahidi kutoa maoni mazuri pale mtu anapouliza kitu chake ili kupata ufafanuzi zaidi.

    Ahsante sana.
    Mdau-USA

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 19, 2009

    HUYU ATAKUWA MHAYA AU MGANDA.

    ReplyDelete
  18. Jamani kuna watu humu wanatoa mawazo ambayo yanaonyesha ni jinsi gani baadhi ya watanzania walivyo lala usingizi, hivi kweli kila siku lazima tutegemee watu toka nje kutuletea maendeleo? Tuamke jamani, ndugu yetu anajaribu kutafuta ufumbuzi ni kitu gani kifanyike ili tuweze kulitangaza Taifa.
    Mtu unatoa ushauri eti afikie mnamnani, tatizo ni kua hatujui ya kua watu wenye kuitembelea nchi yetu hawawezi kulala huko bondeni kama unavyotaka wewe, kwa namna yeyote watalala hizo hoteli kubwa ambazo ndiko tunatakiwa tuwaonyeshe nini kinaendelea nchini. sina maana ninadharau huko bondeni haya ni maoni yangu, anyway naweza kuandika mpaka nikawachosha wasomaji lakini ukweli ni kua tunapochangia mawazo tujaribu kutumia "reflective thinking" tusikurupuke tu nakuongea utumbo, ops samahani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 20, 2009

    Wewe ANONY.June 19 @ 7:53AM. Hakuna cha mhaya, cha mkanda au mkenya hapa. Kama hauna cha uchangia kaa kimya. Watu mnakalia mambo ya ukabila kamwe hamtaendelea. Mtu akitoa wazo zuri kwa ajili ya ufafanuzi zaidi, nyie mnakalia mhaya, msukuma, mnyamwezi, kaishie huko na ukabila wako.

    Mdau-Chanika

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 20, 2009

    mdau Elly Mbotto wewe ziro kabisa... but burudani tu ha hahaa

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 22, 2009

    mdau elly mbotto....

    hahahahaaaaahahahaaaa tih tih

    kumbe na wewe zako??

    yan jamen iyo hotel sijui danguro limejificha hata huwezi jua kuna huduma

    pale wanakutana wooote wanaowashwa

    hahahahaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...