Mahakama Kuu ya Tanzania inatarajia kuanza kusikiliza jumla ya kesi tano za mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) katika miji ya Kahama na Shinyanga kuanzia jumatatu ijayo (Juni 8, 2009).
Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu Bw. John Utamwa, amesema leo kwamba kesi tatu zitasikilizwa mjini Kahama na Jaji Gabriel Rwakibarila kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza na zimepangwa kusikilizwa kwa muda wa siku 35 hadi kumalizika.
Bw. Utamwa amesema Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Kanda ya Dodoma, Bw. Gadi Mjemas, anatarajiwa kusikiliza kesi nyingine mbili katika Mahakama Kuu mjini Shinyanga ambazo zimepangwa kusikilizwa kwa muda wa siku 21.
“Taratibu zote kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hizo zimekamilika,” alisema Bw. Utamwa leo (Juni 5, 2009).
Naye msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Omega Ngole, amethibitisha leo kwamba tayari Mawakili wa Serikali wameshawasili katika miji ya Kahama na Shinyanga kwa ajili ya kuendesha kesi hizo ambazo upelelezi wake umekamilika.
Kuanza kusikilizwa kwa kesi hizo, kunaifanya Tanzania kuungana na nchi za Rwanda na Burundi ambazo zimeanza kusikiliza kesi za aina hiyo hivi karibuni.

Kwa kweli inabidi wakati mwengine mupitie picha munazotumiwa, si vizuri kuweka picha kama hizi ambazo hazina faida yeyote kwa msomaji, ni kuidhalilisha maiti tu, au munaweza kutumia utaalamu kuifanya ionekane vizuri kidogo au kuandika habari zake tu.
ReplyDeleteLazima tujifunze kuziheshimu maiti.
Miongoni mwa suluhisho ni kupiga marufuku kikweli uganga wa kienyeji/jadi/asili bila kujali ni mmasai au mfipa.
ReplyDeleteMisupuu me natoa ushauri wa bure...I believe work ethics zako zanamandate utoe warning whenever unaweka graphics ambazo zinaweza kua disturbing. that way readers anaweza kuopen link at their own discretion maana kama mtu unafungua blog na mtoto yuko next to u unakumbana na hii picha haitakua jambo la busara.
ReplyDeleteagain huo no mtazamo wangu
mdau
Houston,TX
Bwana michizi habari ya saa hizi, pole kwa mihangaiko ndugu yangu. mimi mdau kutoka Uk, napenda kuanza kwa kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya, pili napenda kutoa maoni yangu kuhusiana na habari ambayo umeitoa kuhusiana na mauaji ya kikatili yanayofanywa na watu ambao huwezi kuwa "describe" kwa namna yeyote ile.
ReplyDeleteHawa jamaa wanaofanya haya mambo natumaini wanahitaji kufanyiwa uchunguzi wa akili, kama sikosei inasemekana haya mambo yanafanyika ili waweze kufanya ushirikina na kupata utajiri, swala la kujiuliza ni kua kama huyo mganga (sangoma) anaweza kukupatia mtu utajiri kwa njia hii ya kinyama kwa nini asianze kujitajirisha kwanza yeye?? hii inashangaza na kusikitisha sana kuona kuna watu bado wanaishi maisha ya namna hii katika karne hii ya "Science & Technology".
Hawa watu wanahitaji kupigwa vita na kutokomezwa, hii inasikitisha sana ndo maana hata "primeminister" wetu alitoa kauli na hata kufikia kutokwa machozi pale bungeni Dodoma ambazo baadhi ya watu na wabunge walizipigia kelele. Lakini hii inaonyesha ni kiasi gani unyama huu ulivyo mgusa kiongozi wetu kama binaadamu wa kawaida.
Jamii inapaswa kutambua ya kua hii si vita ya serikali pekee, tunapaswa kushirikiana kulitokomeza jambo hili. Jambo hili linatia aibu Taifa letu mbele ya ulimwengu. Nitumaini nchi yetu ina sheria ambayo inaruhusu adhabu ya kifo!! hivyo ningeshauri adhabu hii ichukue mkondo japo watu watadai ni kinyume na "human rights"
Mwisho bwana michuzi ningependa kukuomba na kutoa ushauri wangu ya kua wakati mwingine jaribu kutokutoa picha hizi "live" namna hii kwani Blog hii ni ya jamii kama inavyo julikana hivyo kuna watoto wanaipitia na picha hizi nitatisha hata kwa watu wazima, pia tujaribu kustiri aibu za wafiwa na marehemu. Asante sana Mdau UK
HAPA HAKUNA CHA KUSIKILIZA AS LONGER AS WAMEUA NA KUNA USHAHIDI WA KUTOSHA KINACHOBAKIA MUHESHIMIWA HAKIMU WAHUKUMU TU SAWA SAWA NA MAKOSA YAO,KESI KAMA HIZI HAZITAKIWI KUCHUKUA SIKU NYINGI KAMA UMEJULIKANA WEWE NI MUUAJI HAKUNA CHA KUSUBIRI HAPO.TUNAOMBA HAKI ITENDEKE HAPA BILA UPENDELEO WA NAMNA YEYOTE.WATU KAMA HAWA CHINA HUKO AU LAO NI KUCHEZEA KITANZI TU.
ReplyDeleteNachotaka kusema hao wauwaji kama wakipatikana na hatia basi hukumu ya KIFO ichukue mkondo wake na Rais asione huruma a sign haraka iwezekanavyo ili iwe mfango kwa wauaji wengine
ReplyDeletekaka michuzi sijui nianzie wapi ?
ReplyDeletehata salamu nimesahau this is too graphic !
inauma sana pia isingefaa kuwekwa hadharani
watu waliofanya kitendo hiki wanastahili laana kubwa. yaani unamuua mtoto mdogo maskini wa watu kisa tu unataka viungo vyake ukafanyie ushirikina wa kutajirika.
ReplyDeleteserikali ihakikishe kuwa wahusika ni wahusika haswa na hawaja singiziwa,kisha wapate hukumu ya kifungo cha maisha jela,na ikiwezekana wawe wanapigwa bakora wakiwa uchi kilasiku asubuhi,mchana na jioni,dozi ya bakora 5 huku matakoni wanabandikwa kitambaa kililowanishwa ktk maji ya pilipili na chunvi,ikiwezekana ziwe zinachukuliwa picha za vidio kisha wanaonyeshwa watu ktk TV hii itasaidia kukomesha wengine wanaofikiria kujiunga ktk ushenzi huu wa tabia!huu ni unyama ,uhayawani kuliko hayawani yeyote yule aendaye kwa miguu,mabawa ,au kwa tumbo,maana hakuna hayawani amtendaye hayawani wa aina yake kwa ukatili wa jinsi hii.na ikiwezekana wanipe mimi kazi ya kuwatandika mijeledi hiyo hata kama watataka niwe nalipia fedha nitalipia ilimradi hawa jamaa waliofanya ushenzi huu wakome na liwefundisho.NYAMBAFFFFFFF. vima kabisa mbwa hawa. chodo kabisa hana maana ktk jamii.xwyz****#%@~ yao
Uganga wa jadi nivigumu kuhuzuia, Sababu wagombea UBUNGE na nafasi nyingine kutwa ushinda kwa waganga,na ndio wao utumwa vingo vya walemavu wa ngozi.
ReplyDeleteBwana michizi habari ya saa hizi, pole kwa mihangaiko ndugu yangu. mimi mdau kutoka Uk, napenda kuanza kwa kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya, pili napenda kutoa maoni yangu kuhusiana na habari ambayo umeitoa kuhusiana na mauaji ya kikatili yanayofanywa na watu ambao huwezi kuwa "describe" kwa namna yeyote ile.
ReplyDeleteHawa jamaa wanaofanya haya mambo natumaini wanahitaji kufanyiwa uchunguzi wa akili, kama sikosei inasemekana haya mambo yanafanyika ili waweze kufanya ushirikina na kupata utajiri, swala la kujiuliza ni kua kama huyo mganga (sangoma) anaweza kukupatia mtu utajiri kwa njia hii ya kinyama kwa nini asianze kujitajirisha kwanza yeye?? hii inashangaza na kusikitisha sana kuona kuna watu bado wanaishi maisha ya namna hii katika karne hii ya "Science & Technology".
Hawa watu wanahitaji kupigwa vita na kutokomezwa, hii inasikitisha sana ndo maana hata "primeminister" wetu alitoa kauli na hata kufikia kutokwa machozi pale bungeni Dodoma ambazo baadhi ya watu na wabunge walizipigia kelele. Lakini hii inaonyesha ni kiasi gani unyama huu ulivyo mgusa kiongozi wetu kama binaadamu wa kawaida.
Jamii inapaswa kutambua ya kua hii si vita ya serikali pekee, tunapaswa kushirikiana kulitokomeza jambo hili. Jambo hili linatia aibu Taifa letu mbele ya ulimwengu. Nitumaini nchi yetu ina sheria ambayo inaruhusu adhabu ya kifo!! hivyo ningeshauri adhabu hii ichukue mkondo japo watu watadai ni kinyume na "human rights"
Mwisho bwana michuzi ningependa kukuomba na kutoa ushauri wangu ya kua wakati mwingine jaribu kutokutoa picha hizi "live" namna hii kwani Blog hii ni ya jamii kama inavyo julikana hivyo kuna watoto wanaipitia na picha hizi zinatatisha hata kwa watu wazima, pia tujaribu kustiri aibu za wafiwa na marehemu. Asante sana Mdau UK
Tafadhali sana Nd. Michuzi tunaomba utoe hizi picha ni kinyume na haki za binadamu. Kuna watoto ambao wanaangalia hii blgo.
ReplyDeleteAsante Sana.
No Michuzi usitoe hizi picha kwani this is what is going on in our country so maybe if we see them as they are it might help us to walk in their shoes and push us to fight for our fellow humanbeings who are the victims.
ReplyDeletePicha ziko so graphic Michuzi na sio sawa kutuonyesha bila warning!
ReplyDeleteHata CNN hawawezi kufanya hivi....Ujumbe ni mzuri sana na mauaji haya ni ya kupigwa vita kwa kila hali lakini sio kuweka picha kama hizi hapa.
Sio kujali watoto bali mtu yeyote...this is just not right.
J.
Toronto
hi michuzi,am so imbarased wt ma country man ,4 real yani,kunasiku nipo mwenyewe kazini najishauaa nikaulizwa nimetokea wapi mwenyewe nikajibu na mbwe mbwe zote TANZANIA SI nikaambiwa wanakoua maalbino,nikachoka kabsaa yani.this is so serious jamani hadi twatambulika lol.serikali ingilieni kati jambo hili si dogo litatupeleka kubaya jama.
ReplyDeletenyinyi mnaosema asiweke hizo picha mnakosea ilikusudi jamii iwaone hawa watu ni wabaya inabidi watu tuone ukatili huu ilikusudi tuwachukie na wale waliokuwa wanasema kumhuku kifo mtu aliyeua ni vibaya hapo mnaonaje aliyeua naye anyongwe mpaka kufa tena hata ukimkuta anamfupa wa zeruzeru.mkikamata mkonokwamkono mnaua hapohapo.hawawatu ni washenzi.lakini sio kwamba waganga wajadi wote wanafanyahivyo niwatu na tamaazao wameinglia fani.mbona hata madaktari wa hospital nao wanatoa mimba za wanawake naule nao ni uuaji.poleni wafiwa wote nawote mliotishwa na hiipicha
ReplyDeleteMICHUZI I BEG YOU PLEASE REMOVE THESE PICTURES .PLEASEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteShukrani kwa kuondoa picha hizi za ajabu Michuzi! So disturbing duh :( Maelezo yalitosha kwa kweli!
ReplyDeleteMichu,
ReplyDeleteShukran kwa kuondoa those disturbing photos! Respect the Dead!
Heshima kwako Kaka.
ReplyDeleteShukrani kwa kuondoa taswira hizo.
Amani kwako