HABARI ZILIZOPATIKANA JIONI YA LEO NI KWAMBA KIPA WA ZAMANI WA TAIFA STARS ALIYEWAHI KUCHEZEA SIMBA, YANGA, SIGARA NA PAN AFRICA JOSEPH KATUBA, AMEFARIKI DUNIA LEO KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA KUTOKANA NA MARADHI YA KIFUA.
KWA MUJIBU WA KIPA WA ZAMANI WA TAIFA STARS NA PAN AFRICAN AMBAYE SASA NI KOCHA WA MAKIPA WA TIMU YA TAIFA, JUMA PONDAMALI MENSAH, MSIBA WA MAREHEMU KATUBA UPO MAGOMENI MAPIPA MTAA WA MPILIPILI AMBAKO MIPANGO YA MAZISHI INAFANYWA.
KATUBA ATAKUMBUKWA KWA UHODARI WAKE AKIWA LANGONI AMBAPO ALIKUWA MMOJA WA MAKIPA WACHACHE AMBAO WALIKUWA KAMA WANA MIKONO YA NTA KWA JINSI MPIRA ULIVYOKUWA UNANATA MOKONONI HATA KWA MKWAJU MKALI SANA. PIA ALIKUWA AKICHEZA VYEMA NDANI YA 18 KIASI HATA ALIZIMUDU VYEMA KONA NA MAJALO.
MOLA AIWEKE MAHALI PEMA ROHO YA MAREHEMU KATUBA
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2009

    Nadhani kifo cha Joseph Katuba kimewaumiza wengi. Alikuwa goalkeeper hodari na alikuwa na mengi ya kujifunza kutoka kwake. Binafsi sikuwahi kufuatilia maisha yake baada ya yeye kustaafu soka, lakini nahisi alikuwa na mchango mkubwa katika soka la tz. Atakumbukwa kwa uhodari wake akiwa golini. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.

    Mdau. Kigali

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2009

    dah, RIP jose. kijiweni mwananyamala tutakaaje sasa?

    poa mzee tutaonana asubuhi njema!......

    mdau,

    komakoma....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2009

    MUNGU AMSAMEHE MAKOSA YAKE R.P.I JOSE

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2009

    Tusiwasahau Omar Mahadhi bin Jabir na Athumani 'Mehalla' Mambosasa...mashujaaa wa net forever!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2009

    R.I.P Joseph Katuba, alikuwa ni moja ya makipa bora Tanzania waliotia fora langoni kwa umahili wao wa kudaka mipira Katuba anaingia kwenye orodha ya makipa bora waliowahi kutokea katika medali ya soka,makipa wengine bora ni pamoja na:
    1.Athumani Juma Mambosasa (Simba)
    2.Omar jabir Mahadhi (Simba)
    3.Mohamed Mwameja. (Costal,simba)
    4.Idd Pazi father (simba, plisner)
    5.Ally Bushir (small simba)
    6.Rifat Said (malindi,yanga)
    7.Khamis Kinye (yanga)
    8.Juma Ponadamali (pan,yanga)
    9.Ramadhan Korosheni (KMKM)
    10.Juma Kaseja (simba,yanga)
    11.Juma Muhina (pamba)
    12.Sahau Said Kambi (Yanga)
    13.Mohamed Nyarusi (sigara,simba)
    14.Often Martin (ushirika,Simba)
    15.Ivo Mapunda (Yanga)
    16.Ali Salehe(Nyotanyekundu,Malind

    ReplyDelete
  6. napenda kutuma salamu zangu za rambirambi kwa familia ya marehemu joseph katuba nimepokea habari kifo chake kwa masikitiko makubwa haswa ukizingatia nipo mbali na KIJIJINI KWETU MWANANYAMALA-A.mungu ailaze roho yake mahali pema,amin.ni mimi S.J.TUNGU

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 08, 2009

    jama uliyetuma orodha ya makipa umenikumbusha mbali sana nakupa hongera pia salamu zangu za rambirambi ziwafikie familia ya joseph katuba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...