Balozi wa Denmark nchini Mh. Bjarne Sorensen akimtunuku mtunza bustani Mzee Peter Namkwata medali maalumu toka kwa Malkia Margrethe II wa Denmark kwa kuwa mfanyakazi wa muda mrefu katika ubalozi wa nchi hiyo Dar. Mzee Namwkata amepiga mzigo ubalozini hapo kwa zaidi ya miaka 20

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2009

    Mwenyezi Mungu akupe heri na akujalie afya njema Mzee Peter Namkwata!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2009

    hii tuzo/chuma huambatana na dollarzzz au ndo kuchorana na ilo chuma???

    sii mchezo mzee kapiga kizigo!!anastahili dollarzzz thr that tuzo

    nieleweshwe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2009

    Inapendeza sana kuona Malkia wa Denmark kamkumbuka mtunza bustani wa Tanzania. Hii ni challenge kwa viongozi wetu ambao mara nyingi wanakumbukana wao kwa wao na kusahau wafanyakazi wa chini.

    ReplyDelete
  4. John MashakaJune 24, 2009

    Mara Nyingi sitei maoni, lakini nimeguswa sana na unyenyekevu wa mzee wetu na kulazimika kuandika !

    It is heart touching to see how humility can push humans to greater hights;

    A gardener being honored by a royal family is something so uncommon in most of African countries

    May this simple but powerful picture of humility captures the attention of our rullers who see the voiceless as their stooges to glory.

    Mzee wangu Mungu na Akubariki na uendelee na kazi yako inayokupa mkate wako wa kila siku
    Amen

    John Mashaka

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2009

    mzee peter wajanja wataanza kukutafuta sasa hivi kwa ajili ya reference za viza ya denmark kama siyo shengein,anyway congratulation mzee,ni wachache sana ambao wanaweza kukaa kwenye kazi kwa muda mrefu na katika ufanisi wa kuweza kupewa tuzo,wabongo fundisho

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2009

    Wampe na mengine ya ziada basi zaidi ya medali....he has spent his energy throughout his life for Denmark! Potelea mbali hata kama alikuwa analipwa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2009

    Kila la heri mzee namkwata. God bless u forever!
    I wish i could work for those yrs. Maana siku hizi ni ngumu kufikisha miaka mingi kiasi hicho makazini mwetu.
    Zawadi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2009

    hongera sana. lakini nahisi mzee hakuanzia kazi hapo kwani 20 is not much, ukilinganisha na jinsi umri wake unavyoonekana kuwa juu.

    ReplyDelete
  9. Pamoja na kumpongeza huyu mzee kwa uwajibikaji, nimevutiwa na kitendo cha Malkia na falsafa inayojitokeza humo, na ndio mtazamo wangu kuhusu umuhimu wa watu kama wafagiaji, wavuta mkokoteni, wapishi, na kadhalika, kama nilivyoeleza kwenye makala hii hapa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 24, 2009

    We anonymous wa 2.58... Duh! Unadhani hatuoni hilo? But thats not the issue here

    Hongera mzee

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 24, 2009

    Hicho kitu huyo mzee anaweza badilisha in terms of $$$$$?Kama haiwezekani basi haina dili.watoto home hawana chakula eti wewe una heshima kutoka kwa malkia make no sense.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 24, 2009

    sahihisho kidogo mkuu wa nanihii. Nipo huku Denmark. Na Habari zilizopo huku ni kwamba huyu mzee amefanya kazi ya kutunza bustani za huo ubalozi kwa miaka 40 sasa na sio 20.
    Hongera sana mzee. Mungu akupe nguvu tele na maisha marefu zaidi mpaka ufike miaka 100

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 24, 2009

    Sipendi kabisa ninaposikia eti anapewa medali toka kwa queen. Yaani ni hilo tu!!! nothing else. Mzee kama huyu-loyal like him angestahili kitita kikubwa cha kumstaafisha na mahangaiko ya kutumia kemikali katika bustani za ubalozi for all these years.

    Pole Sana mzee wetu- God bless you richly.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 24, 2009

    jamani angekuwa serikalini angekuwa ameshaastaafu mumgu akubariki baba wa watu.aliyesema huyu babu wa bustanini ni nani

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 25, 2009

    Nafanya kazi katika ubalozi wa Marekani Nairobi. Baada ya miaka 15 tu, wanakupa haki ya kuishi Marekani kama unaitaka (Green Card) Si wewe tu, bali na familia yako yote. Nasubiri miaka 2 nifunge virago vyangu. Texas here I come baby!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 25, 2009

    Jamani sio medali tuu. Kwa hakika wafanyakazi wa huo ubalozi wana angaliwa vizuri sana kimaslahi huyo hapoa hakosi kibanda pamoja na ada ada za wajukuu hazipigi chenga.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 26, 2009

    mmh jamani babu hongera saana, lakini medali sio ya maana saana angalao wangemjengea nyumba nzuuri ambayo inamahitaji ya muhimu kama maji,na vinginevyo. Maana hata wakimpa pesa kweli jamaa hawataacha kumvamia wakidhani pesa kalala nazo kwenye godoro,mimi naona kwa upeo wangu wangempa kitu cha kumbukumbu kwa maisha yetu ya kibongo kama kumjengea nyumba akiamua kuipangisha ajipatie pesa hilo ni lakwake maana nguvu ndo zinaisha na anahitaji saana kipato cha kumsukuma mbeleni.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 27, 2009

    mi naona wazungu wanamzingua tu mzee wetu, mpeni life inayoeleweka yeye na familia yake, medari ndo nini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...