KAKA MICHUZI, HABARI KAZI ZA UJENZI WA TAIFA.
KWA JINA NAOMBA TU NIITE ZENA. MIE NIMEKUWA NA MCHUMBA AMBAYE WOTE TUMEKUWA HIV POSITIVE. YEYE KWAO BOTSWANA, NASI TULIKUTANIA ENGLAND NA TULIANZA URAFIKI BILA KUJUWA HALI ZETU WOTE.
TUKIWA MASOMONI TULIKUWA NA TUNASHIRIKIANA TUKIISHI PAMOJA.MIMI NILKUKWA MWAJIRIWA NA MUDA WANGU UKAISHA WA KUSOMA NJE YA NCHI NIKARUDI TZ. YEYE AKAENDELEA KUISHI KULE MPAKA ALIPOPATA KESI AKAFUNGWA JELA NA BAADA YA MWAKA AKATOKA.
MIMI NIKIWA NAMSUBIRI ARUDI ILI TUISHI PAMOJA KWA NDOA, LAKINI ALIPORUDI AFRIKA, HUSUSAN HAPA DAR, NDUGU ZAKE WAKAMKATAZA ASIOANE NA MIMI. TENA WAKAMWAMBIA AREJEE KWAO GABERONE, NAYE AKAWASIKILIZA. WAKATI HUO NILIISHAMSAIDIA MAMBO MENGI SANA, ADA ZA WATOTO ALIOZAA NA MWANAMKE WALIYEACHANA MIAKA MINGI ILOPITA, NA AMBAYE ALIISHI NAYE HAPA DAR.
BASI BAADA YA MANENO KUTOKA KWA NDUGU ZAKE AMBAYO HAYAKUNIFURAHISHA NAMI NDUGU ZANGU WAKAONA NI WATU WASIOKUWA NA SHUKRANI. KWA HIYO HUYU BWANA ALIRUDI KWAO NAMI NIKO HAPA DAR NAISHI KWA UPWEKE NA SONONEKO KWAMBA KUPATA TENA MTU AMBAYE ANAFANANA NA MIMI NI NGUMU.
KWA UFUPI NAOMBA MRAFIKI AMBAO NITAWASILIANA NAO KWA EMAIL ILI IKIWEZEKANA NIPATE MWANDANI WA MOYONI MWENYE HALI KAMA YANGU:
na simu yangu ni
0774 68 96 65
Pole sana dada yangu kwa matatizo.Ninaamini kuwa utapata marafiki wengi wenye hali kama yako na hatimaye kufikia ndoto yako ya ndoa kama moyo wako unavyotaka kuridhia.Lakini jambo moja la muhimu ninachotaka kukuambia ni kuwa,NDOA NI MPANGO WA MUNGU,kwa maana nyingine NDOA NI BAHATI hii ina maana kuwa kama hutaolewa hautakuwa umetenda dhambi yeyote ile,cha msingi uiangalie na kuitunza vema afya yako ndilo jambo la muhimu kwa sasa.Jitahidi kuhudhuria ibada na maombi kama wewe ni mkristo amini Yesu mtenda miujiza kuwa yupo hata leo ipo siku iliyopangwa na Mungu (siku ya bahati) utapona kwa imani! Ninakupenda sana japo sikufahamu na kamwe usijisike mpweke,mimi ni binti kama wewe,single,HIV Negative!! Mungu akutie nguvu!!! by makiromaro@yahoo.com
ReplyDeletekazi kwelikweli
ReplyDeletepole sana sister zena kwa majaribio uliyopata,ila ukumbuke kuwa mitihani ndiyo inayokufanya uwe strong na makini zaidi katika next relation na katika future yako as a whole.
ReplyDeleteNa pia nakushauri katika kutafuta rafiki wale ambao ni HIV positive jaribu kuwapa uzito zaidi,na ndio katika hao utakuja pata mwandani wa moyo wako.
Dada Zena wala usijali. Inaonekana kama wewe ni mwanamke mwenye busara na upendo kwa jinsi ulivyoweza kumsaidia huyo bwana ambaye hakuwa na shukhrani. Wapo wengi sana wa namna hiyo hivyo jichunge ili wengine wasije dandia boti. Nina imani mwenyezi Mungu atakupa atakaekufaa zaidi. Nakutakia kila la kheri.
ReplyDeletePole sana da Zena. ushauri wangu ni surrander your life to jesus mwachie matatizo yako yote. sasa hivi sio mda wa kuanza kutafuta mwenzi mwingine wakati huja heal yaliyokupata. simama na mungu katika sala na tafuta marafiki watakaokusupport especially now you need them. then wait and see God at work. pole dada,yatapita haya. Mungu akupe nguvu.
ReplyDeletePole dada zena.unaonekana na busara ya kuzaliwa na huruma ya moyoni.hakika utaingia mbinguni.ingekuwa ni mtu mwingine wala asingejali.
ReplyDeleteDada i am so proud of u...kumbuka mungu yupo na kamwe hawezi kukuacha.are u a christian???kama sio naomba nisamehe ila sote tunamuomba yule yule kama ni mkristo soma kutoka 34.10,matendo 10.38,yohana 15.7,isaya 43.19 na uone jinsi mungu anavyotenda miujiza.kama utapata muda njoo kwenye mkesha sinza christian centre kila jumamosi usiku kucha tunakesha tukimlilia mungu,,,mungu hatakuacha ukeshe bure lazima takutendea muujiza na nina imani upone.nimeshuhudia wengi wakipona dada,hakuna tatizo mungu asilotatua.baada ya hapo atakupa mume kwa muda wake.Gods time is the best rafiki,be patient and wait for Gods promises,he said the trials we endure shall never overwhelm us.be blessed
ReplyDeleteHii kesi tumeisikiliza upande mmoja hivyo ni vigumu kutoa hukumu/ushauri sahihi.
ReplyDeleteHata hivyo nakupa pole sana Zena. Mrudie mola wako, fanya mazoezi ya kila mara, punguza sana kushiriki tendo la ndoa, tumia muda mwingi kujipumzisha nafsi yako, ondoa tamaa za kimapenzi,kama CD4s zako ziko chini sana tumia ARVs na kufuata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa ugonjwa huo.
Naelewa kuwa hukuutumia vibaya ujana wako, lakini usiwe na majuto kwa yaliyokukuta na gangamala na strong na hatimaye utaishi kwa matumaini kwa muda mrefu tu.
Nakupa pole sana dada yangu na nakutakia kila la heri katika kumpata mtu ambae utaishi nae for the rest of your life. Unaonyesha ni mdada mwenye roho nzuri na pia umejiweka wazi katika tatizo lako.Mungu akulinde na akujalie ndoto zako zitimizwe.
ReplyDeletejitahidi usome makala mbalimbali katika internet, unaweza kukutana na watu ambao wanahitaji mtu kama wewe pia. usikate tamaa.
God bless you
je ukimwi ulikuwa nao hata kabla au huyo bwana ndo amekuambukiza?
ReplyDeletePole sana Zena!! Hakika tabia za watu wa kusini mwa Africa zipo tofauti sana na zile za Afrika Mashariki na kati. Katika maswala ya familia (ndoa) huku kusini watu wachache sana wenye ndoa wengi wao wamelelewa na mzazi mmoja (wa kike). Hii inaonyesha kabisa kwamba labda dada Zena hukupata sana undani wa hizi tabia za huku kusini.. All in all you have your life now to take care of na nina hakika utapata mtu sawia kwako na hata kwa ndugu zako.
ReplyDeleteMuombe mungu utapata tu rafiki umpendae achana na kusononeka hiyo ni hari ya kawaida kwa maisha ya sasa hakuna mwenye uhakika wa kuiona kesho uwe HIV +Ve au -Ve na kujiona wewe ndio mkosefu. Mungu ndio anaye jua yote, wewe ni binadamu kama walivyo binadamu wengine na nina uhakika mungu atakupa tu umpendae yeye ndio dira ya maisha yetu.
ReplyDeleteNondo
Ars
STRONG WOMAN KUMBUKA WEWE NI WASHOKA USITATIZWE KATU PIGA MOYO KONDE MAMBO YATAKUWA KAMA UNAVYOTARAJIA
ReplyDeletePole sana. Bado Mungu anakupenda. Salimisha maisha yako kwa Yesu Kristo uokoke. Nenda kanisa wanakofanya maombi. Nina hakika kama unaamini basi virusi vitapotea kwa jina la Yesu
ReplyDeleteWEWA NE LAZIMA UNAMATATIZO YA SELF ESTEEM . YOU CAN BE SINGLE AND HAPPY HIZO NDOA UNAZOLILIA WENZIO WANATAKA KUTOKA . NDOA SASA HIVI NI DRAMA NA HASAHASA UNAUMWA UTAPUNGUZA SIKU ZAIDI ZA KUISHI MAANA STRESS .NDOA NI ZINAHITAJI MOYO NA KAMA HUNA IMMUNE SYSTEM NZURI UTAONDOKA . OK
ReplyDeletePole dada,
ReplyDeleteLakini sijajua kwanini unataka rafiki ambaye ameathirika tu?Mbona kwa uelewa wangu mdogo siku hizi hata watu ambao si waathirika una unaweza kuishi nao bila shida na mkapata hata mtoto ambaye hajaathirika.
Ahsante,
KT
Pole kwa yaliyokusibu ndugu yetu, but the most, nakupongeza. Kuna watu wengi sana wake kwa waume (ila wanaume wanaongoza) ambao ni HIV+ na wanaambukiza kwa makusudi kabisa. Mungu akupe kheri daima.
ReplyDeletePili, usione umetengwa, bali jione miongoni mwa tulio wengi. HERI YAKO WEWE UNAJUA HALI YAKO, WENGI HATUJAPIMA NA TUNAPETA kipuuzi. Wenza wapo, na utawapata kwa njia tofauti.
ILA KUWA MAKINI kwa sababu kwa njia hii tutakuja wengi, sasa wenda ikakuwia vigumu kuchagua the right one. Whether you believe or not, being HIV+ positive doesn't remove humanity, thus requiring you to be extra careful...in selecting a partner. Othewise, you will end up dropping your CD4 counts more rapidly than when singly living.
Morever, if you like or wish, anzisha au jiunge na kundi (shirika, say) la watu waishio au walio katika mapambano. Au pia jiingize kwenye haya mapambano, kuwa mdau (kama ulivyo) kwa kupambana na kusaidia wengine. Makundi haya yapo mengi hapa nchini, na ya kimataifa pia. Is a great opportunity.
>> Labda nikupe ushuhuda tu kwamba binafsi nimepata fursa ya kufahamu watu wengi, mbalimbali, ndani na nje ya nchi kwa kujihusisha na vikundi hivi. Najisikia fahari kuwa mmoja wa wanaoleta mabadiliko chanya kwa taifa langu na dunia kwa ujumla.
Ninaokutana nao na niliowahi kukutana nao kwenye hizi organizations, ambao nao ni wanawake wanaoishi na VVU (mimi sio mwanamke, bali nimejihusisha zaidi na mambo ya jinsia) hawana upweke. They have lots of friends, HIV+ na HIV- nikiwemo nami, and I feel blessed to share views with them cos "they know what to be done, how and why" more than others (HIV-) do.
Tafadhali, tembelea tovuti mbalimbali ujionee zaidi ni namna gani wanawake waishio na VVU 'wanapeta' bila tatizo. Upweke ulionao unatokana na mwenzako kukuacha katika mazingira kama hayo, and never because of your HIV sero-status.
Ukitaka kuwasiliana nami please usisite.
Ubarikiwe sana,
tgirlsnetwork@gmail.com
Dada jipe moyo, usikate tamaa na maisha. God is GOd of love, peace and healing. So trust in Him with all your heart and leave the rest to Him, expect Him to work miracles in your life every single day. God is madly in love with you, remember that He takes pleasure in His creatures, Us. And trust me, right now He is holding you in the palms of His Hands, watching you very closely. Dada, GOD LOVE YOU!, and love Him back with all your heart and you'll see His salvation everyday. You're so strong, keep it up!, na Mungu Akuponye na kukupa faraja.
ReplyDeleteIN JESUS NAME!
NIMEPENDA SANA JINSI WABONGO WALIVYOCHANGIA KUHUSU HUYU DADA SABABU MTU WA KWANZA KUTOA MAWAZO ANAONEKANA MLOKOLE BASI WOTE WALIOFUATIA WAKAOKOKA,SAFI SANA MANAKE HUWA COMMENT ZA HUMU ZINAKUWAGA ZA AJABU AJABU SAAANA,HONGERENI!!
ReplyDeletemh!!!!!!!! wizi mtupu!
ReplyDeletepole da zena!! usijali sana thats not the end of world dear as life will always go on.kaa chini tulia mwombe mola azidi kukupa afya njema ndio kikubwa. haijaandikwa ktk misaafu au biblia kama umeukwaa basi lazima uwe na jamaa alionao,never!! you sound so understanding&innocent too. usijali ninayo email yako,i will keep in touch privately and we will take it frm there.mi mwenyewe japo sinao ila im looking 4 someone 2 be the mum of my kids. niko uk pia ila nakuja tz b4 the end of the yr,may be we will meet and talk in details. MEANWHILE STAY HEALTH AND LOOK AFTER YOURSELF!!!!!!
ReplyDeletedada zena, pole lakini ndio maisha. ninachokwambia ni kuwa kama ni rafiki wa kalamu na mtu wa kuongea naye ukiwa umepata upweke ndio unatafuta poa na tumaini utampata. lakini kama ni mtu wa kukuoa wala usihangaike yote ni mipango ya mungu. Take it ieasy and enjoy your life. Hawa wanaume especially wa kiafrica watakuengezea tu pressure ufe siku sio zako. really u don't miss anything. mimi nimeolewa lakini nakwambia if I knew then what I know now or if I could turn back time nooooo way I would do it over. Nimesoma nje nikarudi kuolewa nyumbani (traditiona way)...sasa hivi nina watoto na wakwe. Wenzangu ambao niliwaacha nje wanaonekana wadogo kuliko mimi mara kumi. Don't you dare to involve with any african man wakati wanajua hali yako. Watakuuse. Mie hapa mzima lakini mume ni wa part time. Kila akitoka kazini yupo na wenzake kwenye club zao mpaka usiku. kazi kuniletea nyama za kuku tu hapa. Who needs nyama za kuku kila siku? I could go on and ond and on but what I am trying to tell you ni kuwa enjoy your single life to the fullest
ReplyDeleteJAMANI WAPENDWA WOTE AMBAO MMECHANGIA KUTOA COMMENTS ZENU NASEMA ASANTENI SANA SANA. NIMEKUWA NASOMA COMMNTS ZA WATU MBALI MBALI WANAPOTOA ISSUES KAMA MIMI KIASI AMBACHO WAMEKUWA WANAKATISHWA TAMAA HATA MIMI NILIJIANDAA KUYAPATA MANENO HAUO LAKINI KWANGU IT WAS VERY DIFFERENT?. WATU NADHANI SASA WAMESTAARABIKA NA YAWEZEKANA WENGI WANAMPENDA MUNGU AMBAPO HATA KAMA NI MUISLAMU AU MKRISTO ANAPOKUWA NA HOFU YA MUNGU BASI ATATOA MANENO YA KUTIA MOYO KWA MUHITAJI KAMA MIMI ZENA. KWA KWELI NIMEZIHIFADHI COMMENTS ZOTE KWA UKUMBUSHO WANGU MAANA NINA IMANI KUBWA KWAMBA MUNGU ANAJUWA KUMSOMA BINADAMU ALIYEMUUMBA KWA MIKONO YAKE. HIVYO KILA HITAJI AMBALO LIKO SAMBAMBA NA MAPENZI YAKE MUNGU BASI ATALIJIBU KWA WAKATI ANAOTAKA YEYE. MAMA ULIYEKUWA ULAYA UAKARUDI UKAOLEWA KWA NDOA HUKU HOME UMESEMA KWELI SANA. YAANI NDOA NYINGI HAZINA FURAHA. WATU WAPO TU NA WANAOLUPENDA WATAKUAMBIA HALI NA UKWELI. ILA MAMA SHIDA INAKUJA, SI AFDHALI MUME WA PART TIME LAKINI AWE WAKO KULIKO KUCHUKUWA PART TIME WA WENZAKO?. HII NDIO SHIDA KUBWA. MWILI ALIVYOUMBA MUNGU NA KAMA UNA AFYA NJEMA UNAHITAJI UPATE UHUSIANO NA MWENZA WAKO SASA KAMA MWILI UNATAKA NA UNACHUKUWA WA WENZAKO SI UNACHUKUWA DHAMBI MBAYA HAPA DUNIANI?. BORA KUWA NA WAKO NA HATA UKIFANYA SALA NA MAOMBI MUNGU ANAPOKEA. KULIKO KUCHUKUWA WA WENZAKO. HILO NDILO HITAJI LA KUWA NA WAKO LINAPOKUJA. GOD BLESS YOU ALL,......
ReplyDeleteDuuu poleeee
ReplyDelete