


Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
good work first lady.natumaini michango hii itawafikia walengwa.
ReplyDeleteHongera mama kikwete kwa kulitumikia taifa.
ReplyDeleteinapendeza kwani unajenga afya pia shavu dodo.
ReplyDeleteNi jambo la kusikitisha sana kwamba Wazazi wanajifanya hawana habari na lishe ya watoto wao hususan wale wadogo kabisa wenye umri chini ya miaka kumi na mbili watakapo shinda shuleni kutwa nzima wakihudhuria masomo yao!Tatizo hili ni la nchi nzima.Mwaka 2005 mimi binafsi nililazimika kutoka Dar es Salaam kwenda Iringa kusaidiana na Kiwanda cha kusindika Maziwa Fresh ya Ng'ombe kilichopo eneo la Ipogolo au Ruaha Bondeni kijulikanacho kwa jina la ASAS DAIRIES LIMITED, ambacho kinasimamiwa chini ya uangalizi makini sana wa Wakurugenzi kina Salim Abri na nduguye Fayaz Abri.Tuliendesha Kampeni Kabambe kabisa ambayo ni mfano wa kuigwa Kitaifa ,kampeni ya unywaji maziwa mashuleni,hususan katika shule za msingi.Kauli mbiu ya Kampeni hiyo ilikuwa ni "Unywaji wa Glasi moja tu ya Maziwa Fresh kila siku kwa kila mwanafunzi kutazidisha Ubunifu na Afya ya Akili kwa manufaa ya Taifa".Taasisi zote za Manispaa ya Iringa zilishirikishwa pamoja na shule zote za msingi.Na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya Kimataifa ya Unywaji wa Maziwa Mashuleni ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati huo
ReplyDelete,Mh.Generali Msataafu Luhanga,alisisitiza sana kuhusu umuhimu wa "Uendelevu wa Mradi huo katika MANISPAA YA IRINGA na katika mkoa mzima".Lakini cha ajabu kuanzia mwaka huo wa 2005 hadi leo hii hakuna hata Kiongozi mmoja aliye lichukulia suala hilo kwa umakini uliostahili.Na hadi hii leo licha ya kuwepo kwa iwanda hicho cha Maziwa ya Ng'ombe mjini Iringa hakuna hata shule moja ya msingi yenye utaratibu wa kutoa maziwa ya ng'ombe kwa wanafunzi wake japo kwa glasi moja tu kwa kila mwanafunzi kwa siku!Nilipata bahati ya kuzungumza na wawakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam ya WFP-World Food Programme na walikuwa tayari kabisa kusaidia jitihada hizo za kiwanda cha ASAS DAIRIES LIMITED kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa wa Iringa,lakini hadi hii leo inasikitisha sana kusema kwamba hakuna hata Kiongozi mmoja wa MKOA WA IRNGA aliyelichukulia suala hilo kwa umuhimu uliostahili!Ni aibu sana na fedheha kubwa!Nimelazimika kuyasema haya baada ya kuona jitihada za Mama Salma Kikwete kuhusu suala hilo ambalo hivi sasa lilitakiwa liwe limesha onyesha mafanikio makubwa katika baadhi ya mikoa kama Iringa ambako wawekezaji binafsi walipata ujasiri wa kutaka kutoa huduma hiyo kwa gharama nafuu zaidi kwa kushirikiana na serikali za mitaa lakini hakuna aliyeona umuhimu wake.Matokeo yake ni UTORO zaidi mashuleni na matokeo duni zaidi ya wanafunzi katika mitihani yao.NAFIKIRI WAKATI SASA UMEFIKA KWA KILA MHUSIKA KUTIMIZA WAJIBU WAKE KWA MANUFAA YA KIZAZI KIJACHO NA TAIFA LETU KWA UJUMLA!-tonny-
Noma sana. Salma anapiga mzigo kuliko nyomi la mawaziri na manaibu waziri tulilonalo.
ReplyDeleteanony wa june8 saa:549 unachosema ni kweli kwamba viongozi hawako serious na majukumu yao,lakini mimi pia nalitazama kuamzia kwa kiongozi huyu namba moja ktk ngazi ya mwanzo ya maendeleo yaani familia. kiongozi huyu aitwaye mzazi anapaswa aelimishwe hadi atambue kuwa anawajibu wa kwanza kabisa yeye kupanga namna ya kuvikimu viumbe anavyotarajia kuvileta hapa duniani mapema.sasa ndio wakati muafaka wa kuwandaa wazizi wa baadaye ktk hili,na kuwakumbusha ambao tayari ni wazazi kuhusu wajibu wao.
ReplyDeletetunajuwa kwamba jukumu la serikali ni kuwafanya watu wake wawe na maisha bora,lakini kama mlengwa[mwananchi] hajui jukumu kae ni nini itakuwa kazi sana kufikia kile tunachokusudia.
maana hii inakuwa sawakabisa na kuwa na madaktari wazuri,vifaa vya kisasa,mdawa,n.k lakini ukawa na wanachi walengwa wa huduma ambao hata jukumu lake la wali kwa afya yake halifahamu. mfano-hawezi kuchemsha maji ya kunywa,hawezi kunawa mikono kabla ya kula,hawezi kutengeneza choo na kuzuia kutawanyika kinyesi,hawezi kufyeka majani na kufukia madimbwi ya maji karibu na nyumbani kuzuia kuzaliana mbu,analewea pesa pombe badala ya kununua chandarua au viatu virefu vya kuzuia kung'atwa na luba anapokwenda kulima mpunga.
mtu huyu ataugua tu hata kama mazingira ya kutibiwa yapo lakini bado atazidi kuugua tena na tena.
nadhani ni wakati muafaka wa kuifanya jamii yetu sasa itambue majukumu yake ya awali,kisha serikali ibanwe kutengeneza miundo mbinu ya kurahusisha maendeleo.
hebu fikiria kuna mtu yuko ktk kijiji fulani hukoo!mtu huyo anaoa kila baada ya miaka miwili au mitatu hivi na ana wake zake 6-9,na kila mke ana watoto sio chini ya 5,jumla ana watoto kati ya 30-45, je kama ni mkulima na mfugaji wa kawaida unategemea watoto hao atamudu kuwatunza? matokeo yake atajifanya jukumu la kutunza watoto ni la mama pekee na yeye kazi yake ni kuwazungukia wakezake anapata huduma zake.
hapa nieleweke,si challenge tamaduni za watu wala dini,lakini lazima tufike wakati tutambue kwamba ili tuendelee lazima watu wawekwe tayari kwa ajili ya kufikia malengo ikibidi hata kwa kulazimishwa na baadaye wataiona faida.
itakuwa ni aibu na fedheha kama mzazi anazaa watoto anashindwa kuwapa glass ya maziwa,akisubiri WFP wampatie mtoto wake maziwa wakati yeye si mlemavu ni mtu mzima kiafya.hapa tatizo linakuwa liko kichwani tu,kumfanya aelewe wajibu wake. mtu huyohuyo ukimpa elimu ya kiwango cha degree nadhani itakuwa vigumu sana kumshawishi afanye kitendo alicho kifanya awali(cha kuowa wake6-9,kuzaa watoto 30-45,na kuitegemea WFP wawape watoto wake maziwa. ataona ni fedheha kwake na kujidhalilisha).
UWEZO WA KUBADILIKA TUNAO,ILA NIA BADO HATUNA.
ELIMU NI UFUNGUO KWA MABADILIKO YA MAISHA NA MAENDELEO KWA UJUMLA.
ningefurahi sana kama hizi juhudi zitaenda sambamba na mchakato wa kuhamasisha umma[kuuelimisha majukumu yao na ikbidi kuwalazimisha wale wabishi]
kwa mfano: waambiwe wazae watoto wanao weza kuwatunza,atakaye shindwa kumpa mtoto basic needs zake atakamatwa na kupelekwa ktk makambi ya kuzalisha kwa kutumia nguvu usiku na mchana,na serikali badala ya kuagiza chakula nje ita nunua chakula ktk makambi hayo na kweka ktk maghala ya taifa,au watafanya kazi nyingine za kimaendeleo iliwemo kushiriki ujenzi wa barabara,kufyatua matofali na kuwatumia wanavyuo vya uhandisi kufanyia practical kwa kuwajengea watu nyumba bora vijijini kwa kuchangia gharama za saruji na bei nafuu] na mapato yatakayo patikana yatapelekwa kwa familia husika ambayo mzazi alishindwa kujipanga kwa hiari yake.
hii itwafanya watu wasiwe tayari kufanya vitu visivyo na mpangilio.hata vibaka wa mitaani pia watapotea,maana wanazagaa kwa kuwa hawasakwi ili watumiwe ktk production. WE CAN IF WE WANT THE CHANGES,IS NOT EASY TO WORK OUT FREEDOM,especially uhuru wa kiuchumi na maendeleo.
Wangewashirikisha MAFISADI kwenye michango tungekua mbali sana.
ReplyDeleteI`m just say.
Salma Hongera mama In-Shallah na Mola akuzidishie Iman
ReplyDelete...kwa ufupi tu na ushauri...
ReplyDeletenyie annons wawili mlioandika MAGAZETI MAREEEFU apa,hakuna ata mtu atayesoma/au laa kusoma kwa makini izo maelezo
mmepoteza nguvu tu apo na inaboa
ni hayo tu